BREAKING

Friday, 7 September 2018

WILFRIEDY ZAHA ROHO YAKE SAAFI....


Wilfried Zaha anatarajiwa kutoa mchango mkubwa kusaidia wanadada wa klabu ya Crystal palace.

Hatua hiyo ya winga wa Crystal Palace inafuatia ripoti kwamba kikosi cha pili cha klabu hiyo kimeambiwa kulipoa £250 kila mmoja wao la sivyo waondoke katika klabu hiyo.

Timu ya wanawake ya Crystal Palace ambayo inacheza katika ligi ya wanawake amesema kuwa ripoti hiyo ya Guardian sio ya kweli.

Klabu hiyo imesema kuwa inamshukuru Zaha mwenye umri wa miaka 25, ambaye mwezi Agosti alisaini kandarasi mpya yenye thamani ya £130,000 kwa wiki.

TAIFA STARS WAWASILI KIBABE KAMPALA ,UGANDA KESHO KUUMANA NA TIMU YA TAIFA YA UGANDA UWANJA WA NAMBOOLE

Kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kikiwa tayari kuwakabili The Cranes,'Uganda

Wednesday, 5 September 2018

USIWACHUKULIE POA DSTV SIO WA MCHEZO MCHEZO WIKI HII UGANDA DHIDI YA TAIFA STARS MAMBO NI MBASHARAAAAAAA SUPER SPORT 8






WIKI HII NDANI YA DStv!!

Mashindano mapya kabisa ya UEFA Nations League yanaanza kutimua vumbi wiki hii huku pazia likifunguliwa na magwiji wawili wa Soka siku ya Alhamisi. 

Ambapo Ufaransa (Mabingwa wa Dunia) watacheza dhidi ya Ujerumani (Mabingwa wa Dunia waliopita). Kisha kuendelea na Albania dhidi ya Israel siku ya Ijumaa, huku Italy ikiikaribisha Poland siku hiyo hiyo ya Ijumaa na kumaliziwa na Turkey vs Russia.


Jumamosi Switzerland itacheza dhidi ya Iceland, Finland vs Hungary wakati England wakicheza dhidi ya Spain. Na siku ya Jumapili Germany itacheza dhidi ya Peru, France itacheza dhidi ya Netherlands, Bulgaria vs Norway Na Denmark vs Wales!


Mechi hizi zote utazipata ndani ya DStv kuanzia kifurushi chako cha Bomba kwa sh.19, 000 tu!


Bila kusahau Jumamosi hii, DStv inakuletea mtanange wa kukata na shoka pale Uganda (The Cranes) watakapozichapa na timu yetu ya Taifa Tanzania yaani Taifa Stars. Macho Na masikio tutayaelekeza Uganda, tarehe 8/9/18 ndani ya Supersport 8 ya kifurushi Bomba kwa sh.19, 000 tu ndani ya DStv pekee!


Moto Hauzimi na kama Sio DStv Potezea!

Thursday, 30 August 2018

MULTCHOICE TANZANIA YATANGAZA WASHINDI WATAKAOPATA FURSA YA MAFUNZO YA FILAMU NAIROBI....



image.png
  
MultiChoice Tanzania, Imetangaza  washindi  wanne waliokidhi vigezo katika shindano la MultiChoice Talent Factory lilizinduliwa rasmi mapema mwezi Mei mwaka huu . Programu hii itawezesha jumla ya vijana 60 kutoka katika nchi mbalimbali barani Afrika kuweza kupata mafunzo ya filamu kwa kipindi cha mwaka mmoja katika vituo vitatu tofauti, kimojawapo kikiwa nchini Kenya (Nairobi) ambapo vijana hawa watakuwapo ifikapo tarehe 01 Oktoba mwaka huu.

Mchakato mzima  wa kupatakana kwa washindi hawa ulichukua takribani muda wa miezi miwili ambapo kwa hapa nyumbani Tanzania tulipokea maombi kutoka kwa vijana zaidi ya 160, yaliyofuatiwa na mchujo ulifanyika tarehe 20 Julai Mwaka huu hapa Dar es Salaam Tanzania.Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania, ndugu Alpha Mria akielezea kwa undani namna mchakato huu wa kupata vijana wenye vipaji na mapenzi kwenye sekta ya Filamu na mwisho kupatikana washindi hawa wane ambao mnamo Octoba 2018 wataenda kuiwakilisha Tanzania kwenye ya Mafunzo Maalum ya Tasnia ya Filamu MultiChoice Talent Fatory,  huko Jijini Nairobi Kenya kwa kipindi cha mwaka mzima.

“Maendeleo ya nchi yetu kwa muda mrefu yamekuwa yakitambuliwa kwa uwekezaji katika maliasili nyingi tulizonazo kama vile madini, kilimo, mifugo, wanyamapori, na kadhalika huku sekta ya ubunifu ikiwa haijapewa kipaumbele kikubwa na hivyo sekta ya sanaa na ubunifu kuwa na mchango mdogo katika ukuaji wa uchumi wetu. Ili kuhakikisha kuwa tunasaidiana na serikali katika mkakati wake wa kuifanya sekta ya ubunifu na sanaa kuwa moja ya mihimili ya uchumi wetu, MultiChoice imeanzisha program hii na tumeanza na sekta ya filamu. Vijana wa kitanzania waliofanikiwa kufudhu katika mchakato huu ni Sarah Kimario  kutokea Dar es Salaam, Wilson  Nkya kutoka Kigoma, Jamal Kishuli kutoka Arusha na Jane Moshi kutoka mkoa wa Kilimanjaro, alisema Alpha Mria  Meneja Masoko MultiChoice Tanzania.

image.png

Picha ya Pamoja ya Uongozi wa Multichoice Tanzania wakiwa na Vijana walioibuka kidededea watakao kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye Mafunzo Maalum ya Filamu Multichoice Talet Factory, jijini Nairobi Kenya, kutoka kusho ni Jamal Kishuri kutokea Arusha, Jane Moshi kutoka mkoa wa Kilimanjaro, katikati ni Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo akifuatiwa na mshindi Sarah Kimario  kutokea Dar es Salaam, pembeni ni Menejea Masoko MultiChoice Tanzania Alpha Mria na mwisho kulia ni mshindi wetu mwingine Wilson  Nkya kutoka Kigoma wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa halfa hiyo.

Tumebarikiwa kwa vipaji vingi katika fani mbalimbali na bila shaka tukiwekeza katika vipaji vya vijana wetu bila shaka tutafanikiwa kupanua wigo wa ajira na uchumi wetu na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. Amesema mafunzo hayo yataanza rasmi mwezi Oktoba mwaka huu itawawezesha vijana hawa wanne kutoka Tanzania kuungana na vijana wengine kutoka nchi mbali mbali za Afrika katika vyuo maalum vya mafunzo ya utengenezaji wa filamu ambavyo vitakuwa nchini Nigeria, Kenya na Zambia. Kwa upande wao, washindi waliotangazwa kufudhu katika program hii wametoa shukrani zao za dhati hususani kwa kampuni ya MultiChoice sambamba na serikali ya Tanzania kwa ujumla. Akiongea katika hafla nhiyo, Wilson Nkya mmoja kati ya vijana waliopata fursa hiyo alisema kuwa “ Kipekee hii ni fursa tuliyokuwa tukiisubiri kwa muda mrefu na tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa Kampuni ya MultiChoice, serikali na jamii yote kwa ujumla.  Tunaahidi kufanya kila liwezekanalo na mtegemee matokeo chanya kutoka kwetu’, alimalizia Wilson.
image.png
Meneja Uendeshaji MultiChoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo pamoja na Meneja Masoko MultiChoice Tanzania Alpha Mria wakiwapongeza vijana hawa wakitanzania walioibuka washindi wa mpango huu wa kukuza tasnia ya Filamu Afrika unaotambulika kama Multichoice Talent Factory, vijana hawa wataliwakilisha Taifa kwenye mauzo haya maalum ya mwaka mzima yatakayofanyika Jijini Nairobi Kenya, kwa ukanda wa Afrika Mashariki yakiwa yameandaliwa na kugharamiwa na MultiChoice Afrika.

Wednesday, 29 August 2018

RWANDA-YANGA KUSHUKA DIMBANI LEO KUIVAA RAYON SPORTS


Yanga itashuka dimbani kucheza mchezo wa kukamilisha ratiba na Rayon huku ikiwa haina nafasi yoyote ya kusonga mbele.

Kwa mujibu wa Mratibu wa timu, Hafidh Saleh, amesema wachezaji wote wako vizuri kiafya na hakuna yoyote ambaye yuko majeruhi.

Saleh ameeleza lengo lao kubwa kwenye kipute hicho ni kuweka heshima ya kuhakikisha wanapata matokeo licha ya kuwa hawana nafasi ya kusonga mbele.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki ambapo itachezwa kwenye Uwanja wa Nyamirambo uliopo jijini Kigali.

Yanga ilianza michuano hiyo kwa kusua sua baada ya kukubali vipigo vikubwa viwili, wakati ilipokutana na USM Alger ya Algeria nchini Algeria na kuchapwa mabao 4-0 na Gor Mahia kuwachapa idadi kama hiyo.


Timu hiyo ilijitutumua ilipocheza Dar es Salaam, na USM Alger baada ya kuifunga timu hiyo mabao 2-1

DROO YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA KUPANGWA LEO SAA MOJA





  • Klabu nne za England watatambua wapinzani wao katika awamu ya makundi ya mashindano ya kuwania ligi ya mabingwa Ulaya wakati droo itakapofanyika leo Alhamisi.

  • Manchester City itakuwa katika chungu cha kwanza na Manchester United na Tottenham Hotspur katika chungu cha pili huku Liverpool ikiwekwa kwenye chungu cha pili au cha tatu.
Droo inatarajiwa kufanyika Grimaldi Forum huko Monaco mwendo wa saa moja usiku saa za Afrika Mashariki.

Mabingwa kombe hilo ni Real Madrid ambao waliwafunga Liverpool katika fainali


MTOTO WA JINSIA MBILI YA KIKE NA KIUME AZALIWA MULEBA MKOANI KAGERA



Mtoto wa Jinsia mbili ya kike na kiume amezaliwa katika Hospitali Teule ya Rubya iliyopo wilayani Muleba mkoani Kagera.

Kuzaliwa kwa mtoto huyo kumethibitishwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Geore Kasibante (pichani),  ambaye alisema hali ya mtoto huyo kuwa inaendelea vizuri na kuwa wakati wowote atapelekwa hospitali kubwa kwa ajili ya uchunguzi ili afanyiwe upasuaji kwa vile katika hospila hiyo hawana madaktari bingwa wa kuweza kufanya upasuaji huo.

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube