Wilfried Zaha anatarajiwa kutoa mchango mkubwa kusaidia wanadada wa klabu ya Crystal palace.
Hatua hiyo ya winga wa Crystal Palace inafuatia ripoti kwamba kikosi cha pili cha klabu hiyo kimeambiwa kulipoa £250 kila mmoja wao la sivyo waondoke katika klabu hiyo.
Timu ya wanawake ya Crystal Palace ambayo inacheza katika ligi ya wanawake amesema kuwa ripoti hiyo ya Guardian sio ya kweli.
Klabu hiyo imesema kuwa inamshukuru Zaha mwenye umri wa miaka 25, ambaye mwezi Agosti alisaini kandarasi mpya yenye thamani ya £130,000 kwa wiki.
No comments:
Post a Comment