BREAKING

Monday, 9 January 2017

NI VITA NA VISASI NUSU FAINALI YA MAPINDUZI,ZANZIBAR KATI YA SIMBA NA YANGA....


Mavugo

MAPINDUZI


Na Mwandishi wetu Scolastica -Zanzibar

Ni simba na Yanga Jumanne zitachuana katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi, huko Visiwani Zanzibar kwenye Dimba la Aman.

Watani hao wa jadi watamenyana huk wakiwa na kumbukumbu ya sare ya kufungana mabao 1-1, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa kwanza.


simba imefika katika hatua hiyo baada ya kuifunga  Jang’ombe Boys, mabao 2-0 huku shujaa akiwana ni Mrundi Laudit Mavugo aliyefunga mabao yote.

Mchezo huo utafanyika Jumanne Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar timu hizo zinakutana kutokana na Simba kuongoza katika kundi lake la  A kwa pointi zake 10, ikifuatiwa na Jang’ombe Boys,huku Yanga wao wakishika nafasi ya pili katika kundi lake,lililoongozwa na Azam FC.

Friday, 6 January 2017

KIUNGO RIYAD MAHREZI ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA MWAKA 2016


Kiungo wa Leicester city Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka.
Mahrez mwenye miaka 25 raia wa Algeria aliyeisaidia Leicester kushinda taji la ligi kuu soka England msimu uliopita, tiyari ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa England sambamba na mchezaji bora wa BBC Afrika

Mshambuliaji wa Senegal na klabu ya Liverpool Sadio Mane na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon Pierre-Emerick Aubameyang walikuwa wakiwania tuzo hiyo pia.
Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Nigeria Alex Iwobi ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi.


Denis Onyango wa uganda na klabu ya Memelodi Sundowns akishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ligi za ndani.
Mchezaji bora kwa kina dada imeenda kwa Asisat Oshoala wa Liverpool na timu ya taifa ya Nigeria huku timu bora ya mwaka ikiwa ni Uganda.

KINANA AZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE DIMANI ZANZIBAR LEO

Katibu Mkuu wa CCM,Andulrahman Kinana akimnadi Mgombea wa Ubunge jimbo la Dimani Juma Ali Juma, katika uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo hilo, mjini Zanzibar, leo, Januari 5, 2017.
Katibu Mkuu wa CCM akihutubia wananchi katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Dimani, Zanzibar, leo
Katibu Mkuu wa CCMAbdulrahman Kinana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo wakiwasalimia wananchi wakati Kinana akimtambulisha Mpogolo, katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Dimani, Zanzibar, leo
Wananchi wakipokea kwa furaha salama za Kinaa na Mpogolo walipowasalimia wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akisalimia wananchi baada a kutambulishwa na Kinana kwenyeuzinduzi wa kampeni hizo leo mjini Zanzibar
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo leo mjini Zanzibar
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Ali Seif Idi, akizungumza na wananchi baada ya kukaribishwa a Kinana kwenye uzinduzi wa kampeni hizo,jibola Dimani Zanzibar, leo
Katibu wa NEC,Itkadina ueneziHumphrey Polepole akisalimia wananchi baada ya kukariishwa a Kinana kwenyeuzinduzi wa kampenihizo, jimbola Dmani Zanzibar leo
Polepole akionyesha furaha yake wakati akiwaslaimiawananchi baada ya kukaribishwa na Kinana kwenye uzinduzi wa kampeni hizo katika jimbo la Dimani, Zanzibar, leo
Plepole akizungumza baada ya kukaribishwa na Kinana kwenye uzinduzi wa kampeni hizo jimbo laDimani leo.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu, Ngemela Lubinga, akisalimia wananchi alipotambulishwa naKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani, Zanzibar, leo
Katibu wa NEC Oganaizesheni Muhammed Seif Khatib akizungumza na wananchi alipokaribishwana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani, Zanzibar, leo
Wananchi wakiwa na mabango kuonyesha walivyojitokeza katika uzinduzi wa kampeni hizoleo.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,PROF,JUMANNE MAGHEMBE AZINDUA BODI MPYA YA TANAPA.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof,Jumanne Maghembe akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Afrika jijini Arusha.
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof ,Jumanne Maghembe .
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu ,Jenerali George Waitara akifuatilia hotuba ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii ,Prof,Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa .
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa Dkt Chanasa Mpelumbe Ngeleja.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa Prof Wineaster Anderson
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa Prof,Alexander Songorwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akikabidhi vitendea kazi Devota Mdachi mjumbe wa bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) .
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu ,Jenerali George Waitara akitoa salam zake wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanika katika ukumbi wa Mhakama ya Afrika jijini Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini iliyomaliza muda wake Modestus Lilungulu walpkutana katika hafla fupi ya uzinduzi wa bodi mpya .
Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi ambaye pia ni mjumbe wa Bodi hiyo akifanya utamburisho wa wajumbe wa bodi ya Wadhamini wa shirika hilo.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Prof,Wineaster Anderson ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maliasili na Utalii endelevu Afrika (NARESTi Africa) akitamburishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Dkt Lucy Lugwisa kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira akitamburishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Prof,Alexander Songorwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Kamishna Marijani Nsato ambaye pia ni Mkuu wa Operesheni na Mafunzo Makao Makuu ya jeshi la Polisi akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Dkt Chanasa Mpalumbe Ngeleja ambaye pia ni Daktari Mkuu wa Mifugo ,Wizara ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,George Fumbuka ambaye pia ni Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Core Securities akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Devota  Mdachi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini akitamburishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyomaliza muda wake ,Modestus Lilungulu akitoa salam zake wakati wa uzinduzi rasmi wa Bodi mpya ya Wadhamini ya TANAPA.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Afrika jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali George Waitara (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof ,Jumanne Maghembe mara baada ya kuzinduliwa kwa Bodi hiyo.katikati ni Mkurugenzi wa TANAPA,Allan Kijazi.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) muda mfupi baada ya bodi hiyo kuzinduliwa.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa idara mbalimbali katika shirika hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja na mameneja katika shirika hilo. 

Thursday, 5 January 2017

TOTTENHAM YAISIMAMISHA CHELSEA IKIWA ANGANI 2-0

Tottenham imefutilia mbali ndoto ya Chelsea kutaka kuweka historia katika ligi kuu ya England kwa kushinda michezo 14 baada ya vinara hao kuchakazwa 2-0 White Hart Lane.
Spurs wamekwaa mpaka nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi baada ya Dele Alli kufunga magoli yote mawili kwa njia ya kichwa hii ikiwa ni mwishoni mwa kipindi cha kwanza na dakika ya 54.
Alli alifunga vyema kwa kupokea pasi safi kutoka kwa Christian Eriksen kwa magoli yote mawili.

 Eden Hazard alikuwa na nafasi mbili za kuiokoa Chelsea lakini Spurs waliweza kufanikiwa kupata alama tatu muhimu na kuwaondoa majirani zao Arsenal katika nafasi ya nne

KINANA AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM MONDULI, LEO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo ameongoza mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Jacob Nkomola, yaliyofanyika Mtoni Kijichi, Temeke Dar es Salaam.

Katika mazishi hayo walikuwepo piaa viongozi wengine wa ngazi ya juu wa CCM, wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu. Ngemela Lubinza.

Nkomola ambaye alifariki juzi jijini Dar es Salaam, mwili wake ulitangulia kuagwa nyumbani kwake, Mtoni Kijichi na baadaye kupelekwa katika Kanisa la Kianglikana, Mtoni Kijichi kabla ya kuzikwa katika makaburi yaliyopo Kijichi  saa kumi jioni. 

MAJALIWA AKAGUA MAGAHALA YA NFRA CHANG'OMBE DAR

 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mhahindi wakati alipotembelea magahala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) , Chang'ombe jijini Dar es salaam Januari  4, 2017.  Kulia kwake ni  Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi wakati alipotembelea  maghala ya NFRA, Chang'ombe jijini Dar es salaam Januari 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube