Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mawaziri wa Kenya Musalia Mudavadi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 29 Aprili, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA.
Monday, 29 April 2024
RAIS SAMIA NCHINI KENYA-ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mawaziri wa Kenya Musalia Mudavadi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 29 Aprili, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA.
RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA-KENYA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 29 Aprili, 2024. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia ambao unatoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea.
Sunday, 7 April 2024
RAIS DK.MWINYI AONGOZA DUA KUMBUKUMBU YA KARUME
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameongoza kisomo cha Dua na Hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, iliyofanyika Afisi Kuu CCM Kisiwandui Zanzibar tarehe 07 Aprili 2024.
Viongozi mbalimbali wameshiriki wakiwemo wa Serikali, Dini , Vyombo vya ulinzi na usalama na Vyama vya siasa.
Thursday, 4 April 2024
RAIS SAMIA AWAAGIZA VIONGOZI WATEULE KUHESHIMIANA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wateule kuwa nguzo kubwa katika kutatua migogoro iliyopo kwenye jamii na sio kuisababisha migogoro.
RAIS SAMIA: MAKONDA UMENIKOSHA UMETUCHANGAMSHA WANACCM
IKULU-Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuapisha aliyekuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Paul Makonda leo Aprili 4, 2024 Ikulu, Dar es Salaam kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Makonda anachukua nafasi ya John Mongella Hafla ya uapisho huo inahusisha viongozi mbalimbali
Wednesday, 3 April 2024
HAPI AULA U-KATIBU MKUU JUMUIYA YA WAZAZI CCM
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano, Aprili 3, 2024 imemteua aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa ya Iringa na Mara, Ally Hapi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa chama hicho.
Hapi anachukua nafasi ya Gilbert Kalima ambaye ameteuliwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.
NI JOKATE TENA UVCCM VIJANA..
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imemteua Jokate Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) akichukua nafasi ya Fakii Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
MWENYEKITI SAMIA AONGOZA KIKAO KAMATI KUU CCM
RAIS SAMIA AZINDUA TUME YA ULINZI TAARIFA BINAFSI NA MIFUMO YA USAJILI...
Tuesday, 2 April 2024
DSTV WAZINDUA KAMPENI YA MFALME WA BOMA YAWEKA KIHISTORIA ...
Afisa maendeleo bodi ya Filam nchini Simon Peter, amewaka watunzi wa Filam nchini kuwa wabunifu ili kuendelea kutengeneza soko kubwa la ajira kwa wasanii huku akiwakumbusha wasanii kuendelea kusajili kazi zao za sanaa katika Bodi ya filam
ROTARY CLUB WATOA MAFUNZO KWA WALIMU 80 YA KIDIGITAL
Hamza kasongo Mwanachama Rotary Club akizungumza na walimu washiriki wa Mafunzo ya Kidigital
Ili kuendana na kasi ya kidigital ya ukuajia wa teknolojia duniani Taasisi ya Rotary Klabu imetoa mafunzu ya Teknohama kwa walimu wa Shule tano za msingi katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam,.