BREAKING

Monday 25 November 2019

OKWI ,KAGERE WATAJWA TUZO ZA MWANASOKA BORA AFRIKA.....



Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imeingiza wachezaji wawili kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Klabu Afrika ambayo itatolewa Jumanne ya Januari 7 mwakani katika kilele cha Tuzo ya Mwasoka Bora barani ukumbi wa Citadel Azure, Hurghada nchini Misri.

Hao ni washambuliaji Mnyarwanda Meddi Kagere na Mganda Emmnaule Okwi ambaye hata hivyo amehamia Al Ittihad ya Misri.
Wachezaji hao wameingizwa kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kuiwezesha Simba SC kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita ambako walitolewa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 


Ikiwa chini ya kocha Mbelgiji, Simba SC ilizipiku JS Saoura ya Algeria na AS Vita ya DRC baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi D, ikizidiwa pointi moja na mabingwa wa kihistoria Afrika, Al Ahly ya Misri iliyoongoza kwa pointi zake 10.

Na hiyo ni baada ya kuzitoa Mbabane Swallows ya Swaziland kwa jumla ya mabao 8-1, ikishinda 4-1 nyumbani na 4-0 ugenini na Nkana FC ya Zambia kwa jumla ya mabao 4-3, ikishinda 3-1 Dar es Salaam baada ya kufungwa 2-1 Zambia katika hatua ya mchujo.

Esperance waliopewa ubingwa baada ya Wydad Casablanca kugomea mechi ya marudiano ya fainali dakika ya 59 baada ya refa kukataa bao lao, imetoa wachezaji watano kwenye kinyang’anyiro hicho ambao ni Anice Badri, Taha Yassine Khenissi wote Watunisia, Fousseny Coulibaly wa Ivory Coast, Franck Kom wa Cameroon, Youcef Belaili wa Algeria ambaye amehamia Ahli ya Jeddah.

Zamalek ya Misri imetoa wachezaji watatu, Ferjani Sassi wa Tunisia na watoto wa nyumbani, Mahmoud Alaa na Tarek Hamed, wakati wapinzani wao wa jadi, Al Ahly wametoa mchezaji mmoja, Mtunisia Ali Maaloul.

Wydad Casablanca imetoa wachezaji wawili pia Ismail El Haddad na Walid El Karti wote wa Morocco, sawa na TP Mazembe Meschack Elia  na Tresor Mputu wote wa Kongo na Mamelodi Sundowns, Mganda Denis Onyango na Themba Zwane wa Afrika Kusini. Wengine ni Herenilson wa Petro de Luanda ya nyumbani, Angola, Jean Marc Makusu wa AS Vita ya nyumbani Kongo na Mtogo Kodjo Fo Doh Laba wa RS Berkane ya Morocco aliyehamia Al Ain ya Abu Dhabi.

KLOPP PRESHA YASHUKA KWA MO SALAH NI KUELEKEA MCHEZO WA LIGI YA MABINGWA JUMATANO



Kocha mkuu wa Liverpool Klopp,  amethibitisha kuwa mshambuliaji wake Mohamed Salah atarejea uwanjani Jumatano kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napol.

Salah raia wa Misri alikosa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace ambao Liverpool ilishinda mabao 2-1 na kuifanya izidi kujikita kileleni ikiwa na pointi 37 kwenye msimamo  kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
.
Klopp amesema kuwa Salah alikuwa fiti kuivaa Crysytal Palace kutokana na hali yake kuimarika ila aliamua kumpumzisha kwa ajili ya kazi nzito ya jumatano dhidi ya Napol.

“Salah yupo vizuri na ilibidi aanze kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace niliamua nimpe mapumziko ila mwisho wa siku mchezo wetu tulishinda kwani hakuwa na timu kwa muda wa siku nane alikuwa nchini Misri na mabao yalifungwa na Robert Firmino na Sadio Mane.
“Tulipaswa kufanya changuo la kumuanzisha ama kumuacha apumzike tukakubaliana tumpumzishe atarejea uwanjani Jumatano kukabiliana na Napol,” amesema Klopp.

BITEKO AUNGA MKONO JUHUDI ZA WANANCHI BUKOMBE...

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM) ameendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo katika jimbo hilo ambapo Novemba 23, 2019 ametoa ahadi ya mbao 700 zenye thamani ya shilingi milioni 4.2 kwa ajili ya upauaji wa Zahanati ya Kijiji cha Imalanguza.

Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara huku pia akitoa ahadi nyingine ya mifuko 100 ya simenti kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Imalanguza.
Na George Binagi-GB Pazzo, Geita
 Mbunge wa Bukombe, Doto Biteko akizungumza kwenye mkutano huo.
 Wakazi wa Kata ya Bukombe wakimsikiliza mbunge Doto Biteko kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Imalanguza.
 Mwonekano wa Zahanati ya Imalanguza ambayo pia mbunge Doto Biteko amekabidhi mabati 250 kwa ajili ya upauaji.
Diwani wa Kata ya Bukombe, Rozalia Masokola akitoa salamu zake kwenye mkutano huo.
Tazama Video hapa chini

FAINALI YA KIBABE KOMBE LA CECAFA KILIMANJARO QUEENS VS HARAMBEE STARLETS...CHAMAZI

Uwanja wa Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Jioni time ya Kilimanjaro Queens  itakuwa na kazi ya kuhimili miguu ya Wanawake wenzao kutoka Kenya ambao wanahaha kubeba kombe kwenye fainali ya Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na hakuna timu hata moja inayojua utamu wa kufungwa zaidi ya kufunga tu.

Kilimanjaro Queens ya Tanzania iliyo chini ya kocha mkuu Bakari Shime ambao ni mabingwa watetezi kwenye mechi zao zote za kundi A wanaongoza wakiwa na pointi tisa sawa na Harambee Starlets wenye pointi tisa.

Shime amesema kuwa mtihani utakuwa mgumu leo ila ana matumaini na vijana wake watapambana kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa.

"Kufika fainali sio kubeba kombe ni lazima tupambane ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea kwa sasa, kuna kazi ngumu ila lazima tujue kwamba tunahitaji kushinda mashabiki watupe sapoti," amesema.

Timu ya Wanawake ya Kenya ni miongoni mwa timu ambazo zinawania tuzo ya timu bora Afrika kwa timu za Wanawake hivyo sio timu nyepesi kwenye ushindani.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube