BREAKING

Monday, 25 November 2019

FAINALI YA KIBABE KOMBE LA CECAFA KILIMANJARO QUEENS VS HARAMBEE STARLETS...CHAMAZI

Uwanja wa Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Jioni time ya Kilimanjaro Queens  itakuwa na kazi ya kuhimili miguu ya Wanawake wenzao kutoka Kenya ambao wanahaha kubeba kombe kwenye fainali ya Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na hakuna timu hata moja inayojua utamu wa kufungwa zaidi ya kufunga tu.

Kilimanjaro Queens ya Tanzania iliyo chini ya kocha mkuu Bakari Shime ambao ni mabingwa watetezi kwenye mechi zao zote za kundi A wanaongoza wakiwa na pointi tisa sawa na Harambee Starlets wenye pointi tisa.

Shime amesema kuwa mtihani utakuwa mgumu leo ila ana matumaini na vijana wake watapambana kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa.

"Kufika fainali sio kubeba kombe ni lazima tupambane ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea kwa sasa, kuna kazi ngumu ila lazima tujue kwamba tunahitaji kushinda mashabiki watupe sapoti," amesema.

Timu ya Wanawake ya Kenya ni miongoni mwa timu ambazo zinawania tuzo ya timu bora Afrika kwa timu za Wanawake hivyo sio timu nyepesi kwenye ushindani.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube