BREAKING

Tuesday, 31 December 2019

MKULO ASEMA HANA MPANGO WA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KILOSA, MOROGORO 2020



Na Mwandishi Wetu, Morogoro.

Aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Morogoro Mustafa Mkulo (pichani) ameshangazwa na baadhi ya watu kudai anataka kugombea ubunge katika jimbo la Kilosa huku akikanusha hana mpango wowote wa kugombea nafasi hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Morogoro katika salamu za mwaka mpya wa 2020 ikiwa ni sehemu ya kawaida yake kufanya hivyo kila mwisho wa mwaka, Mkulo amesema ajabadilisha maamuzi yake ya kutogombea nafasi ya ubunge na kushangwazwa na baadhi ya watu kudai anataka kuombea tena nafasi hiyo.

“Kuna watu wamekuwa wakidai nataka kugombea tena ubunge Kilosa hizi ni habari za uongo sina mpango wa kugombea ubunge sehemu yoyote ile hapa nchini “ amesema Mkulo.

Mkulo amesema bado anajivunia katika miaka 10 ya ubunge jimbo la Kilosa kwa kutekeleza ilani ya chama kwa kipindi hicho na Wana-Kilosa kuridhika na utendaji wake.

Aidha Waziri waziri huyo mtaafu wa Fedha amesema ataendelea kuwa mwanachama na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hata hivyo amefafanua kuwa pamoja sio mbunge na wala hafikirii kugombea nafasi hiyo lakini ataendelea kutoa mawazo yake kwa CCM na hata kusaidia wasiojiweza kwa niaba ya CCM ili chama kiweze kutekeleza mipango yake ya kimaendeleo.

Katika salamu zake za mwaka 2020 Mkulo amesema anafurahishwa na utendaji kazi mzuri wa Rais wa awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli na anaunga na wanaCCM wengi kutomuingilia katika katika uchaguzi wa kipindi cha pili ya miaka mitano ijayo 2020 hadi 2025 ili aweze kutekeleza kwa ufasaha mipango ya kimaendeleo alioicha katika awamu ya kwanza.

“Huu ni utaratibu wangu wa kila mwaka kutoa salaumu za mwaka mpya tangu nikiwa mbunge na sasa ni wakati wa kusema ukweli Rais Magufuri kwa miaka minne amefanya mengi mazuri anahitaji pongezi kutoka kwa Watanzania hasa katika kupandisha uchumi na kuboresha miundombinu ya nchi hii” amesema Mkulo.

Mustafa Mkulo ni Mbunge Mstaafu ambaye aliongoza kwa miaka 10 katika jimbo la Kilosa ambapo pia katika kipindi hicho alishika nafasi ya Waziri wa Fedha na kuacha kugombea mwenyewe kwa hiari yake katika uchaguzi 2015 na nafasi yake ikachukuliwa na Mbunge wa sasa Mbaraka Bawaziri ambapo amesema maamuzi yake ya kuacha kugombea ni kutoa nafasi wa wanaCCM wengine kuchangia mawazo yao katika kuliletea maendeleo jimbo la Kilosa.

TCAA WAZINDUA MFUMO WA KIDIGITALI WA KUSAIDIA KUTUA NDEGE KATIKA KIWANJA CHA NDEGE CHA MPANDA - KATAVI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe na Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania,Mizengo Pinda kwa pamoja wakikata utepe kuasharia kuuzindua mfumo wa kidigitali utakaowezesha ndege kutua salama katika Kiwanja cha Ndege Mpanda, Mkoani Katavi. Afisa Muongoza Ndege Mwandamizi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA Sunday Walinda akimpatia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe maelezo ya kitaalamu kuhusu mfumo wa kidigitali utakaowezesha ndege kutua salama katika Kiwanja cha Ndege Mpanda, Mkoani Katavi. Rubani wa Shirika la ndege la Tanzania Rubani Hamza akielezea namna mfumo huo ulivyorahisisha hatua za utuaji ndege katika uwanja wa ndege wa Mpanda, Katavi. Viongozi walioketi meza kuu wakipungia ndege ya Shirika la ndege la Tanzania kama ishara ya kuitakia safari njema ilipokuwa ikipaa kutoka uwanja wa ndege wa Mpanda, Katavi. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari akielezea mchakato mzima ukinzia na tafiti na hatimaye kubuniwa kwa mfumo huu wa kidigitali wa kuziwezesha ndege kutua salama katika uwanja wa ndege wa Mpanda, Katavi. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe, akielezea kufurahishwa na jitihada zilizofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania kufanikisha mfumo huu kukamilika sambamba na kuipongeza mamlaka hiyo kwa kutumia wataalamu wazawa waliobuni mfumo huu katika Kiwanja cha Ndege Mpanda, Mkoani Katavi. Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh Juma Zuberi Homera ameipongeza TCAA kwa kubuni mfumo huu na kusisitiza kuwa wananchi wa Mpanda watumie fursa hii ya ujio wa ndege mara tatu kwa wiki kujiimarisha katika kuwekeza kwani milango ya biashara na wageni zaidi kufika mpanda kwa usafiri wa anga sasa imerahisishwa. Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda akiwachagiza wanaMpanda kuitumia fursa hii ya ujio wa ndege katika wilaya hiyo kujinufaisha kiuchumi.

Monday, 25 November 2019

OKWI ,KAGERE WATAJWA TUZO ZA MWANASOKA BORA AFRIKA.....



Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imeingiza wachezaji wawili kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Klabu Afrika ambayo itatolewa Jumanne ya Januari 7 mwakani katika kilele cha Tuzo ya Mwasoka Bora barani ukumbi wa Citadel Azure, Hurghada nchini Misri.

Hao ni washambuliaji Mnyarwanda Meddi Kagere na Mganda Emmnaule Okwi ambaye hata hivyo amehamia Al Ittihad ya Misri.
Wachezaji hao wameingizwa kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kuiwezesha Simba SC kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita ambako walitolewa na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 


Ikiwa chini ya kocha Mbelgiji, Simba SC ilizipiku JS Saoura ya Algeria na AS Vita ya DRC baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi D, ikizidiwa pointi moja na mabingwa wa kihistoria Afrika, Al Ahly ya Misri iliyoongoza kwa pointi zake 10.

Na hiyo ni baada ya kuzitoa Mbabane Swallows ya Swaziland kwa jumla ya mabao 8-1, ikishinda 4-1 nyumbani na 4-0 ugenini na Nkana FC ya Zambia kwa jumla ya mabao 4-3, ikishinda 3-1 Dar es Salaam baada ya kufungwa 2-1 Zambia katika hatua ya mchujo.

Esperance waliopewa ubingwa baada ya Wydad Casablanca kugomea mechi ya marudiano ya fainali dakika ya 59 baada ya refa kukataa bao lao, imetoa wachezaji watano kwenye kinyang’anyiro hicho ambao ni Anice Badri, Taha Yassine Khenissi wote Watunisia, Fousseny Coulibaly wa Ivory Coast, Franck Kom wa Cameroon, Youcef Belaili wa Algeria ambaye amehamia Ahli ya Jeddah.

Zamalek ya Misri imetoa wachezaji watatu, Ferjani Sassi wa Tunisia na watoto wa nyumbani, Mahmoud Alaa na Tarek Hamed, wakati wapinzani wao wa jadi, Al Ahly wametoa mchezaji mmoja, Mtunisia Ali Maaloul.

Wydad Casablanca imetoa wachezaji wawili pia Ismail El Haddad na Walid El Karti wote wa Morocco, sawa na TP Mazembe Meschack Elia  na Tresor Mputu wote wa Kongo na Mamelodi Sundowns, Mganda Denis Onyango na Themba Zwane wa Afrika Kusini. Wengine ni Herenilson wa Petro de Luanda ya nyumbani, Angola, Jean Marc Makusu wa AS Vita ya nyumbani Kongo na Mtogo Kodjo Fo Doh Laba wa RS Berkane ya Morocco aliyehamia Al Ain ya Abu Dhabi.

KLOPP PRESHA YASHUKA KWA MO SALAH NI KUELEKEA MCHEZO WA LIGI YA MABINGWA JUMATANO



Kocha mkuu wa Liverpool Klopp,  amethibitisha kuwa mshambuliaji wake Mohamed Salah atarejea uwanjani Jumatano kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napol.

Salah raia wa Misri alikosa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace ambao Liverpool ilishinda mabao 2-1 na kuifanya izidi kujikita kileleni ikiwa na pointi 37 kwenye msimamo  kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
.
Klopp amesema kuwa Salah alikuwa fiti kuivaa Crysytal Palace kutokana na hali yake kuimarika ila aliamua kumpumzisha kwa ajili ya kazi nzito ya jumatano dhidi ya Napol.

“Salah yupo vizuri na ilibidi aanze kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace niliamua nimpe mapumziko ila mwisho wa siku mchezo wetu tulishinda kwani hakuwa na timu kwa muda wa siku nane alikuwa nchini Misri na mabao yalifungwa na Robert Firmino na Sadio Mane.
“Tulipaswa kufanya changuo la kumuanzisha ama kumuacha apumzike tukakubaliana tumpumzishe atarejea uwanjani Jumatano kukabiliana na Napol,” amesema Klopp.

BITEKO AUNGA MKONO JUHUDI ZA WANANCHI BUKOMBE...

 Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM) ameendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo katika jimbo hilo ambapo Novemba 23, 2019 ametoa ahadi ya mbao 700 zenye thamani ya shilingi milioni 4.2 kwa ajili ya upauaji wa Zahanati ya Kijiji cha Imalanguza.

Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara huku pia akitoa ahadi nyingine ya mifuko 100 ya simenti kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Imalanguza.
Na George Binagi-GB Pazzo, Geita
 Mbunge wa Bukombe, Doto Biteko akizungumza kwenye mkutano huo.
 Wakazi wa Kata ya Bukombe wakimsikiliza mbunge Doto Biteko kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Imalanguza.
 Mwonekano wa Zahanati ya Imalanguza ambayo pia mbunge Doto Biteko amekabidhi mabati 250 kwa ajili ya upauaji.
Diwani wa Kata ya Bukombe, Rozalia Masokola akitoa salamu zake kwenye mkutano huo.
Tazama Video hapa chini

FAINALI YA KIBABE KOMBE LA CECAFA KILIMANJARO QUEENS VS HARAMBEE STARLETS...CHAMAZI

Uwanja wa Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Jioni time ya Kilimanjaro Queens  itakuwa na kazi ya kuhimili miguu ya Wanawake wenzao kutoka Kenya ambao wanahaha kubeba kombe kwenye fainali ya Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na hakuna timu hata moja inayojua utamu wa kufungwa zaidi ya kufunga tu.

Kilimanjaro Queens ya Tanzania iliyo chini ya kocha mkuu Bakari Shime ambao ni mabingwa watetezi kwenye mechi zao zote za kundi A wanaongoza wakiwa na pointi tisa sawa na Harambee Starlets wenye pointi tisa.

Shime amesema kuwa mtihani utakuwa mgumu leo ila ana matumaini na vijana wake watapambana kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa.

"Kufika fainali sio kubeba kombe ni lazima tupambane ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea kwa sasa, kuna kazi ngumu ila lazima tujue kwamba tunahitaji kushinda mashabiki watupe sapoti," amesema.

Timu ya Wanawake ya Kenya ni miongoni mwa timu ambazo zinawania tuzo ya timu bora Afrika kwa timu za Wanawake hivyo sio timu nyepesi kwenye ushindani.

Monday, 7 October 2019

MULTICHOICE TANZANIA YAANZA MAADHIMISHO YA WIKI KWA WATEJA

 Mkuu wa Huduma kwa Wateja wa MultiChoice Tanzania Ngwitika Mwakihesya  akimuelekeza mmoja wa wateja waliofika katika tawi la MultiChoice Mlimani City Aziz Makupa jinsi ya kupata huduma mbalimbali za DStv ikiwa ni sehemu ya maaadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Kushoto ni afisa wa huduma kwa wateja wa tawi hilo Vedastina Ishengoma. Katika maadhimisho hayo, MultiChoice itatoa zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi na wateja wake ikiwemo pia kuwatembelea wateja na kukusanya maoni yao ili kuweza kuboresha zaidi huduma zake.



Mkuu wa Huduma kwa wateja wa MultiChoice Tanzania Ngwitika Mwakihesya (kushoto) na Afisa Uhusiano Diana Ayo wakiwa na baadhi ya watoto waliofika na wazazi wao katika tawi la DStv Mlimani City mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali. MultiChoice inaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambapo pamoja na mambo mengine, itatoa zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi na wateja wake ikiwemo pia kuwatembelea wateja na kukusanya maoni yao ili kuweza kuboresha zaidi huduma zake.

Kampuni ya MultiChoice Tanzania imeanza maadhimisho ya wiki ya wateja ambapo itaendesha shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa zawadi kwa wafanyakazi na wateja kwa muda wa mwezi mzima.

Mkuu wa huduma kwa wateja Ngwitika Mwakihesya amesema kuwa katika kipindi hicho, MultiChoice Tanzania itakuwa na matukio mbalimbali yenye lengo la kuiwezesha kuwasogelea wateja karibu zaidi na kufahamu kwa kina uzoefu wao wa kupata huduma za DStv.

‘MultiChoice inaamini kuwa wafanyakazi na wateja wetu ndiyo nguzo ya ustawi wetu hivyo katika kipindi hiki tutahakikisha tunawafikia na kuwasikiliza maoni yao na hili tunalifanya ili tuweze kuboresha zaidi huduma zetu na kumfanya mteja ajisikie kuwa yeye kweli ni mfalme” alisema Ngwitika na kuongeza kuwa zoezi hilo litahusisha kuwazawadia wafanyakazi mbalimbali pamoja na wateja na pia kuwatembelea wateja wao maeneo mbalimblai ili kuwasikiliza na kupata maoni yao.

Amesisitiza kuwa kutokana na uzito huo, zoezi la kutembelea wateja litafanywa kwa kushirikiana na uogozi wa kampuni hiyo “Zoezi hili la kuwatembelea wateja litafanywa kwa kushirikiana na viongozi hivyo hata mkurugenzi mwenyewe na timu yake ya Menejimenti wataenda kuwatembelea wateja” alisisitiza Ngwitika.

Tuesday, 1 October 2019

WASANII WA TANZANIA 'WAJIUZA' KISANAA TAMASHA LA JAMAFEST...


Wasanii wa muziki wa Kizazi kipya wa kundi la TMK Wanaume Family wakiongozwa na Mhe. Temba akiogoza jahazi kutoa burudani ndani ya katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Msanii Country Boy akitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Msanii Country Boy akitoa burudani.
Msanii Barnaba akitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.


Msanii Nahreel wa kundi la Navy Kenzo akitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Aika wa Navy Kenzo akitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Nahreel na Aika wa kundi la Navy Kenzo wakitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Msanii Joh Makin akitoa burudani katika katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Dj D- Ommy kwenye mashine akiendelea kuwapagawisha wanajumuiya ya Afrika Mashariki waliofika katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.

Msanii Jux akitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.
Wasanii Jux (kushoto) na Joh Makin (kulia) wakitoa burudani. 
Aika, Nahreel na Jux wakitoa burudani kwa pamoja katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019.

Msanii Jux akimtambulisha mpenzi wake.



 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube