Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu leo katika uwanja wa Yombo Buza, Wilaya ya Temeke jijini Dares Salaam
Kikundi cha burudani ya kughani kwa semi cha FATAKI kikiburudisha wanaCCM na wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu leo katika uwanja wa Yombo Buza, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Temeke, Abass Mtemvu jijini Dar es Salaam akizungumza katika
mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu leo katika uwanja wa Yombo Buza,
Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu akiwapungia mkono wanaCCM na wananchi wengine waliohudhuria mkutano wake wa kampeni alipowasili uwanja wa Yombo Buza, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu amesema
ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imetenga kiasi cha fedha
kitakachotumika kama dhamana ili wajasiliamali mbalimbali wa jijini Dar
es Salaam waweze kudhaminiwa kwenye mabenki na kupewa mikopo ili
kuendeleza biashara zao.
Bi. Samia amesema hayo
leo jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa kampeni Yombo Buza, Wilaya
ya Temeke alipokuwa akiifafanua ilani ya Chama Cha Mapinduzi imepanga
kuwafanyia nini Watanzania endapo watashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,
2015 na kuunda Serikali ya CCM.
Mgombea huyo
mwenza alisema Serikali ya CCM imepanga kujenga mazingira bora ya
biashara kwa wajasiliamali ikiwa ni pamoja na kutenga fedha ambazo
zitatumika kama dhamana katika mabenki ili kuwadhamini wajasiliamali hao
kupewa mikopo ya kuendeleza na kuzikuza biashara zao.
Alisema
Serikali pia itaweka utaratibu wa kuzilazimisha halmashauri nchini
kuhakikisha asilimia 30 ya tenda zake zinafanywa na vikundi vya
kijasiliamali vya vijana pamoja na wanawake ikiwa ni mkakati wa kuwainua
vijana na akinamama kwenye biashara zao. Alisema halmashauri zimekuwa
zikitoa tenda nyingi kwa makampuni ya kati hata zile ndogondogo hivyo
utawekwa utaratibu tenda ndogo kwa sasa zifanye na vikundi hivyo.
Alisema
ili kuongeza maeneo ya kufanyia biashara Serikali ya CCM itawekwa
utaratibu mzuri ambao utakuwa ukifunga baadhi ya barabara na kuzitumia
kama masoko ya muda kwa siku maalum kisha baadaye kufunguliwa na
kuendelea na kazi zake. Kama hiyo aitoshi kodi ndogo ndogo zisizo na
msingi zitafutwa ili kumuondolea bughudha ba kero wajasiliamali.
Aidha
Bi. Suluhu aliongeza kuwa kwa Wilaya ya Temeke Serikali ya CCM imepanga
kujenga masoko kadhaa likiwemo lile la Kijichi ambalo litachukua
wafanyabiashara 580 kwa pamoja ili kuongeza fursa za biashara kwa
akinamama na vijana, ardha ambayo tayari imeshatengwa na ilichobaki ni
kuanza na ujenzi. Alibainisha kuwa Serikali itaanza kutenga asilimia 75
ya mapato ya halmashauri ili zirudi na kutumika kuzijenga barabara
ndogondogo ikiwa ni jitihada za kuboresha miundombinu.
Aliongeza
kuwa ili kuchochea ukuaji wa biashara kwa akinamama na vijana
wajasiliamali Serikali itaanza kuwabana mgambo ambao wamekuwa
wakiwabugudhi wafanyabiashara dogodogo ikiwa ni jitihada za kuondoa
usumbufu kwao.
Bi. Suluhu alisema miradi
mingine ambayo Serikali inayoundwa na CCM imepanga kuisimamia kwa karibu
ili kuboresha huduma hizo ni pamoja na uboreshaji huduma za afya, umeme
kwa vijiji vyote vya Mkoa wa Dar es Salaam, uboreshaji huduma za maji
safi na Salama, elimu pamoja na miundombinu ya barabara.
Mgombea
huyo wa urais anaendelea na mikutano ya kampeni jijini Dar es Salaam
baada ya jana kumaliza ziara ya kuinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi
katika Mkoa wa Singida na Dodoma.
No comments:
Post a Comment