BREAKING

Wednesday 30 September 2015

MAMA SAMIA SULUHU ,MGOMBEA MWENZA WA URAIS CCM ALIYEPANGA KUWAPIGANIA KIMAENDELEO WANAWAKE TANZANIA

Mama Samia Suluhu; Mgombea Mwenza Aliyepanga Kuwapigania Wanawake

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.
[/caption] MCHUANO wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajia kufanyika Oktoba 25, 2015 unaendelea maeneo mbalimbali ya nchini, huku vyama anuai vilivyofanikiwa kuingia katika ushindani huo wa kisiasa vikinadi ilani na sera zao kwa Watanzania ili kuwashawishi wachaguliwe. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mara ya kwanza kimemsimamisha mwanamke katika ngazi ya juu ya uongozi. Kimemteuwa mwanamama, Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wa mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama hicho, John Pombe Magufuli. Kwa mantiki hiyo endapo kitafanikiwa kushinda urais Tanzania kwa mara ya kwanza mwanamke atashika nafasi ya juu ya madaraka ndani ya Serikali. Bi. Suluhu ambaye amewahi kufanya kazi kama kiongozi katika Serikali zote mbili yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar (Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar-SMZ) anauzoevu wa kutosha na elimu nzuri inayomuongeze sifa ya kuimudu nafasi aliyopewa kwa sasa. Ki historia, Bi. Suluhu alizaliwa Januari 27, mwaka 1960 nchini na kupata elimu yake ya msingi na sekondari Zanzibar, kabla ya kuendelea na elimu ya juu kwa kozi mbalimbali katika vyuo vikuu vya Mzumbe nchini Tanzania, Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza kwa ushirikiano na Chuo Kikuu Huri cha Tanzania (OUT). [caption id="attachment_62370" align="aligncenter" width="741"]Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kulia) akimjulia hali mmoja wa akinamama katika moja ya wodi za wazazi nchini. Kiongozi huyo anaahidi endapo atashinda uchaguzi kupitia chama chake ataziangalia zaidi huduma za afya ya uzazi ili kuboresha zaidi. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kulia) akimjulia hali mmoja wa akinamama katika moja ya wodi za wazazi nchini. Kiongozi huyo anaahidi endapo atashinda uchaguzi kupitia chama chake ataziangalia zaidi huduma za afya ya uzazi ili kuboresha zaidi.[/caption] Mwanamama huyu pia amefanikiwa kuchukua kozi ndogo ndogo anuai katika vyuo vya ndani na nje ya Tanzania, vikiwemo vya; 'Institute of Management for Leaders, Hyderabad, India', Zanzibar Institute of Financial Administration, ZIFA, pamoja na National Institute of Public Administration, Lahore Pakistan. Mgombea huyo mwanamama amekuwa waziri na mbunge kwa zaidi ya miaka mitano mfululizo na pia kufanikiwa kushika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, nafasi ambazo kwa kiasi kikubwa zinamuongezea sifa ya kuweza kuimudu nafasi aliyopewa kwa sasa anasema hii ni nafasi pekee kwa akinamama wote bila kujali itikadi zao kumuunga mkono ili aweze kushinda na kuweka historia nchini ya mwanamke kushika nafasi ya juu kuliko zote nchini. Kwa sasa kiongozi huyu anazunguka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Visiwani kuinadi ilani ya CCM. Bi. Suluhu anasema ilani ya CCM imepanga kufanya mengi mazuri kwa Watanzania, lakini pamoja na hayo amejitolea kuhakikisha anawapigania akinamama endapo atafanikiwa kushinda nafasi hiyo ili kuweza kukabiliana na changamoto anuai ambazo zimekuwa kero na kikwazo kwao. Anazitaja changamoto hizo ni pamoja na huduma za afya ya uzazi ambapo akinamama wengi na watoto wachanga wamekuwa wakipoteza maisha katika eneo hilo. Anasema licha ya ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kufafanua zaidi itakavyo boresha huduma za afya kiujumla, lakini atalisimamia na kuongeza nguvu za ziada kuhakikisha akinamama wanapata huduma za kuridhisha maeneo wanapopata huduma za afya ya uzazi. Akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Jimbo la Mbulu Mjini anasema endapo CCM itashinda uchaguzi huu imepanga kuajiri watumishi 15,000 wa sekta ya afya wakiwemo madaktari 2020 ndani ya kipindi kifupi ili kuhakikisha inaboresha zaidi huduma za afya maeneo mbalimbali nchini hasa huduma za akinamama na watoto. Bi. Suluhu anasema hatua hiyo ni mpango maalumu wa kuboresha huduma za afya kiujumla na hasa huduma za akinamama wajawazito na watoto ambapo wamekuwa na changamoto katika huduma hizo. [caption id="attachment_62371" align="aligncenter" width="800"]Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akiinadi ilani mpya ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kwa wananchi (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akiinadi ilani mpya ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kwa wananchi (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake.[/caption] Aidha anaongeza kuwa mpango mwingine ni kuwawezesha akinamama na vijana kiuchumi kupitia vikundi vyao. Anabainisha kuwa eneo hili Serikali ya CCM kupitia ilani yake imetenga shilimi milioni 50 kwa kila kijiji fedha ambazo zitakuwa zikikopeshwa makundi hayo kwa masharti nafuu ili waweze kujikwamua kiuchumi. Anasema eneo hilo pia halmashauri zitasimamiwa kutoa asilimia tano ya mapato kuwaunga mkono akinamama na vijana ili kuchochea maendeleo yao. Ili kukuza biashara zao Bi. Suluhu anasema Serikali itasimamia kuhakikisha asilimia 30 ya tenda ndogondogo za halmashauri mbalimbali zipewe vikundi vya akinamama na vijana. Anaeleza kuwa ili kuongeza thamani kwa mazao yatakaokuwa yakizalishwa na vikundi hivyo kupitia miradi ya kilimo imepanga kujenga viwanda vingi maeneo mbalimbali ya nchi ambavyo vitayaongezea thamani mazao na pia kuzalisha ajira kwa asilimia 40, jambo ambalo pia litakuza uchumia wa akinamama na vijana. Mwanamama huyo shupavu anabainisha kuwa kutokana na suala la kero ya maji pia kuwaumiza zaidi akinamama ilani ya chama chake imedhamiria kumalizia miradi ya maji na kuanzisha mingine anuai ili kukabiliana na changamoto ya kero ya maji safi na salama iliyopo maeneo mbalimbali ya nchini vijijini ama mjini. Bi. Suluhu anasema Serikali watakayoiunda itaendelea kushughulikia kero ya maji katika vijiji vyenye ukame na kuhakikisha kila kijiji kinapata maji safi na salama kwa matumizi. Lakini ili kumaliza kabisa kero hiyo anasema Serikali itaunda mfuko wa maji ambao utashughulikia kero za huduma za maji safi na salama. Anasema migogoro yoyote inayosababisha mapigano idadi kuwa inayoathirika ni wanawake na watoto, hivyo Serikali itakayoundwa na CCM itahakikisha inapima ardhi yote ya vijiji pamoja na Wilaya na kuainisha mipaka ili kukomesha migogoro ya ardhi inayochangia mapigano ya wakulima na wafugaji baadhi ya maeneo ya Tanzania mara kwa mara. [caption id="attachment_62372" align="aligncenter" width="800"]Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya akinamama na wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (mwenye miwani) akisalimiana na baadhi ya akinamama na wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni.[/caption][caption id="attachment_62373" align="aligncenter" width="800"]Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM. Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.[/caption] Anasema mara baada ya kupima ardhi na kuweka mipaka kati ya maeneo ya wakulima na wafugaji watahakikisha mipaka hiyo inatambulika na kuheshimiwa na jamii zote mbili ili kuzuia migogoro na mapigano ambayo yamekuwa na uhasama mkubwa na kupoteza uhai na mali za raia wasio kuwa na hatia katika maeneo yenye mgogoro. Hata hivyo katika kampeni zake mara zote amemalizia kwa kuwaomba wananchi kutunza amani iliyoasisiwa na viongozi wetu wa taifa kwa kutokubali kuyumbishwa na kushawishia kuvuruga amani ya nchi. "...Tusikubali kuchokozwa na kuchokoseka na kuvuruga amani...bila amani hakuna maendeleo," alisema Bi. Suluhu. Anawataka viongozi wa siasa kuacha kutoa vitisho kwa wapiga kura kwani hali hiyo ni kuibaka demokrasia hivyo CCM na vijana wake hawatakuwa tayari kuona demokrasia inabakwa nchini na wapuuzi wachahe. "...Vijana wa CCM naomba mkikamata kibaka wa demokrasia shughulikeni naye kidogo kabla ya kumpeleka polisi...CCM itashinda kwa kishindo," alisema Nape Nnauye. Miongoni mwa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo kulingana na taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni pamoja na CCM, CUF, CHADEMA, UMD, NCCR- Mageuzi, NLD, UPDP, NRA, TADEA, TLP, UDP, DEMOKRASIA MAKINI, CHAUSTA, DP, APPT-Maendeleo, Jahazi Asilia, SAU, AFP, CCK, ADC, CHAUMMA na ACT-Wazalendo.

MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AENDELEA NA KAMPENI ZAKE MKOANI MARA, ASEMA NCHI HII NI YA VIONGOZI WAADILIFU, AWAHAIDI WANANCHI WA SIRARI NEEMA YA UMEME

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Musoma, leo asubuhi,  kuendelea na ziara ya kufanya mikutano ya kampeni katika maeneo mbalimbali mkoani Mara. Mama Samia leo anatarajiwa kuhutubia mikutano ya kampeni Sirari,  Mwisenge,  na Sirori Simba.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Damia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenykiti wa CCM mkoa wa Mara Christopher Sanya baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Musoma, asubuhi hii.


 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan, akisalimia na Mgombea Ubunge jimbo la Musoma Vijijini, Sospeter Muhongo, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Musoma leo
 Mamam Samia akisalimia baadhi ya viongozi wa CCm, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege mjini Musoma le
 
 Mama Samia akiwa na Ofisa Mwandamizi kutoka Makao makuu ya CCM Juliana Chitinka baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Musoma


Mdau akijaribu kupata picha za Mama Samia
 Msafara wa Mama Samia ukiwa njiani kwenda Sirari, Tarime mkoa wa Mara leo
Msanii wa Bongo Movie, maarufu kwa jina la Bi Mwenda, akihamasisha wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo, Sirari mkoani Mara.
 Wananchi wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Sirari, mkoani Mara
 Wananchi wakiwa na bango kuomba Mamlaka ya Mji Mdogo wa Sirari, Tarime mkoani Mara
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akimwelekeza jambo, Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini, Michael Kimbaki, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo Sirari mkoani Mara. Kulia ni Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Vijijini, Chrisopher Kangoye.
 Wananchi wakimshangilia Mama Samia kwenye mkutano wa Sirari mkaoni Mara
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akiwanadi wagombea Ubunge, wa majimbo ya Tarime, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo Sirari mkoani Mara. Kulia ni Chrisopher Kangoye (Tarime Vijijini) na kushoto ni Michael Kimbaki (Tarime Mjini).
 Wananchi wakipiga 'Push Up' kumuunga mkono Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassa, uliofanyika Sirari mkoani Mara.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi y CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwaaga baadhi ya viongozi, baada ya mkutano wa kampeni aliofanya leo, Sirari mkoani Mara. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Saturday 26 September 2015

VIONGOZI WA CHADEMA GAIRO,MIKUMI WAKIMBILIA CCM, BI SAMIA SULUHU AWAPOKEA KWA MOYO MMOJA...!

Msafara wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan ukiwasili Gairo mkoani Morogoro.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwashukuru baadhi ya wananchi waliofika kumpokea mpakani mwa Mkoa wa Dodoma na Morogoro alipokuwa akiwasili kuanza ziara ya kampeni mkoani Morogoro leo.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais CCM, Bi. Suluhu (kushoto) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Morogoro walipofika kupokea akitokea mkoani Dodoma. Mgombea huyo ameanza ziara ya kampeni Mkoa wa Morogoro leo.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili Mkoa wa Morogoro tayari kwa ziara ya kampeni.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili katika mkutano mdogo wa kwanza kuinadi ilani ya CCM Jimbo la Gairo leo Morogoro.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili katika mkutano mdogo wa kwanza kuinadi ilani ya CCM Jimbo la Gairo leo Morogoro.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili katika mkutano mdogo wa kwanza kuinadi ilani ya CCM Jimbo la Gairo leo Morogoro.
WanaCCM na wananchi wengine wakiwa katika mkutano wa kwanza wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Suluhu (hayupo pichani) katika Jimbo la Gairo.
WanaCCM na wananchi wengine wakiwa katika mkutano wa kwanza wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Suluhu (hayupo pichani) katika Jimbo la Gairo.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby akizungumza na wanaCCM na wananchi waliofika katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby (kulia) akizungumza jambo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais CCM, Bi. Suluhu katika mkutano wa kampeni Gairo.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili katika mkutano mdogo wa kwanza kuinadi ilani ya CCM Jimbo la Gairo leo Morogoro.
Mbunge wa Afrika Mashariki, Angela Kiziga akizungumza katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika Jimbo la Gairo.
Baadhi ya vijana wakiwa wamepanda juu ya gari lililoegeswa ili kumuona mgombea mwenza wa CCM, alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni Gairo.
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akiwahutubia wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Gairo Mkoani Morogoro.
Baadhi ya wanachama wa CCM na wapenzi wa chama hicho wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu alipowasili katika Jimbo la Mvomero leo ambapo alifanya mkutano wa kampeni.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby akiwahutubia wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Gairo Mkoani Morogoro.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa mgombea mwenza wa CCM, alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni Gairo.
CCM Oyeeeeeeee....! Mkutano Jimboni Gairo.
Baadhi ya viongozi wa CCM (kulia) wakimpa zawadi ya sare kada mkogwe wa CCM Jimbo la Gairo.

Wakereketwa na wanaCCM wakimpokea mgombea mwenza wa CCM Jimbo la Gairo.
Wakereketwa na wanaCCM wakimpokea mgombea mwenza wa CCM Jimbo la Gairo.

Mmoja wa viongozi na makada wa Chadema wilaya ya Gairo (kushoto) akitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu. 
Katibu wa Chadema Wilaya ya Gairo, Yona Senyagwa (kushoto) akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katibu huyo pamoja na makada wenzake wametangaza kukihama chama cha Chadema na kujiunga na CCM leo.
Bi. Samia Suluhu akiwa amesimamishwa na wananchi njiani alipokuwa akielekea Wilayani Kilosa kufanya mikutano ya kampeni.
Kada mkongwe wa Chadema Kata ya Dumila, Tegemea Mnhambo akitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais, Bi. Suluhu.
WanaCCM na wananchi wakifuatilia mkutano wa kampeni juu ya gari lililoegeshwa.
Wananchi na wapenzi wa CCM wakiwa wamemsimamisha mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu.
WanaCCM na Wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM.
Wakitumia mbinu mbadala kumlaki mgombea mwenza wa CCM
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Inspecta Harun akihamasisha wanaCCM na wananchi mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi.  
Mmoja wa makada wa Chadema waliojiunga na CCM, katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi akisalimia wananchi.
Mgombea mwenza Bi. Suluhu akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi. 
Mmoja wa makada wa Chadema waliojiunga na CCM, katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi akionesha kadi yake kabla ya kumkabidhi mgombea mwenza.

Mgombea mwenza Bi. Suluhu akimkabidhi kadi mmoja wa makada wa Chadema waliojiunga na CCM, katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi.

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube