BREAKING

Sunday, 24 March 2024

MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI IKULU - DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Dar es Salaam tarehe 24 Machi, 2024.



Baadhi ya Mawaziri wakipitia makabrasha na nyaraka mbalimbali wakati wa Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Machi, 24.

IBADA YA SHUKRANI :KINANA AUNGANA NA FAMILIA YA HAYATI EDWARD LOWASSA- MONDULI

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndg. Abdulrahman Kinana, ameungana na wanafamilia, viongozi wa chama, Serikali na wananchi katika ibada ya Shukrani ya Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Monduli Mjini Mkoani Arusha, Leo marchi 24, 2024.





 








ROTARY YAPANDA MITI 1,000 KAZIMZUMBWI




Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam imeanza kampeni ya kupanda miti ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuhifadhi mazingira sambamba na mradi wake wa kutoa madawati kwa shule za umma hapa nchini.


Wanachama wa klabu hiyo kwa kushirikiana na Africa Asia Youth Foundation mwishoni mwa wiki walipanda miti 1,000 katika msitu wa Kazimzumbwi. Klabu hiyo inatarajia kupanda miti 2,500 kabla ya mwisho wa mwezi April 2024.


Mpango wetu huu wa kupanda miti unaenda sambamba na mradi wetu wa kutoa madawati kwa shule za umma ambapo hadi sasa tumeshatoa madawati takriban 4,000 yenye thamani ya takriban shilingi miliono mia tano na bado tunaendelea alisema Rais wa klabu hiyo Nikki Aggarwal. 


Madawati haya yatatumiwa na wanafunzi zaidi ya 10,000 WA while mbalimbali za msingi mkoani Dar es Salaam Amesema kuwa kwakuwa moja ya malighafi za kutengenezea madawati ni mbao, klabu hiyo imeamua kupanda miti ili kutunza mazingira. Tunathamini sana mazingira na tunajuamazingira ni uhai, hivyo chochote tunachofanya tunahakikisha tunatoa kipaumbele kwenye uhifadhi wa mazingira alisisitiza Nikki.


Mbali na kutoa madawati na kupanda miti, klabu hiyo pia kwa kushrikiana na serikali imeandaa mafunzo maalum ya teknohama kwa waalimu wa shule za msingi jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yatafanyika mwezi Apriili katika Chuo Cha Ufundi Dar es Salaam ambapo walimu 80 kutoka shule mbalimbali za Dar es Salaam watashiriki Miradi hii ni ushirikiano wa klabu ya Rotary ikishirikiana na klabu ya Rotary ya Vancouver ya nchini Canada


Thursday, 1 February 2024

DSTV 'HAWAPOI HAWABOI' WAZINDUA KAMPENI YA PANDA TUKUPANDISHE






Hilda Nakajumo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Pandatukupandishe...

Ronald Selukindo ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko multchoice Tanzania ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Pandatukupandishe...

Kampuni ya Multchoice Tanzania DSTV imezinduzia kampeni yake mpya ya  #PandaTukupandishe, ambapo wameeleza hiyo yote ni kuwapa burudani wateja wao katika nyanja mbalimbali kama Soka, Tamthiliya, Filam na Michezo ya watoto.

Ronald Selukindo ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko multchoice Tanzania anasema kwamba kama ilivyo kawaida ya DStv inaendelea kuwapa furaha mashabiki wake kupitia ving'amuzi vyao na kuongeza channel zenye burudani..

Amesema wakati Michuano ya Mataifa ya Afrika AFCON ikiendelea nchini Ivory Coast wameendelea kuwapa burudani nyingine watanzania kwa kuhakikisha wasanii mbalimbali nao wanapata furusa ya kuwapa burudani watanzania, ikiwa ni njia mojawapo ya kumuunga mkono Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukuza tasnia ya michezo.

Katika uzinduzi huo Shelukindo amesema DSTV inawaletea burudani nyingine kama  Show ya Kijanja Wana wa Town pamoja Tamthilia ya Nuru zitakazoanza mwezi huu wa Februari ulifanyika.


Wednesday, 31 January 2024

WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA MATAIFA 8 KUSHIRIKI TAMASHA LA PASAKA 2024



Kuelekea Tamasha la Pasaka mwaka 2024 Alex Msama Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion waandaaji wa Tamasha hilo amethibitisha waimbaji wa muziki wa injili kutoka mataifa  zaidi ya 8 watakuwepo kwenye Tamasha la Pasaka la mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Alex Msama kuwa maandalizi makubwa kuelekea Tamasha hilo yamekwisha fanyika kwa asilimia kubwa na watu wakae mkao wa kula kwani Tamasha la mwaka huu litakuwa na zuri na lenye shangwe kubwa sana kwa wakazi wa mkoa wa Dar es salaam.

Tamasha la mwaka huu litafanyika siku ya Jumapili ya Pasaka, huku kauli mbiu ikiwa ni ASANTE MUNGU KWA KUTUPA RAIS SAMIA S HASSAN MCHAPA KAZI



Thursday, 25 January 2024

TAMASHA LA PASAKA 2024 KUANZIA JIJINI DAR ES SALAAM,MACHI 31


Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Alex Msama ametangaza Tamasha la Pasaka mwaka 2024  linatarajia kuanza kufanyika katika mkoa wa Dar es Salaam siku ya Pasaka tarehe 31 mwezi 3 mwaka 2024

Waimbaji mbali mbali wa muziki wa Injili watashiriki katika  Tamasha hili kubwa la Pasaka kwa mwaka 2024.

Maandalizi makubwa yanaendelea kufanyika, na Tamasha la mwaka huu limekuja na kauli mbiu inayosema "

 ASANTE MUNGU KWA KUTUPA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN MCHAPA KAZI.....

Monday, 22 January 2024

SPORTPESA WAIUNGA MKONO TAIFA STARS AFCON KWA PROMOSHEN


 Afisa wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano SportPesa Lydia Solomon, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya Sportpesa AFCON

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube