Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam imeanza kampeni ya kupanda miti ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kuhifadhi mazingira sambamba na mradi wake wa kutoa madawati kwa shule za umma hapa nchini.
Wanachama wa klabu hiyo kwa kushirikiana na Africa Asia Youth Foundation mwishoni mwa wiki walipanda miti 1,000 katika msitu wa Kazimzumbwi. Klabu hiyo inatarajia kupanda miti 2,500 kabla ya mwisho wa mwezi April 2024.
Mpango wetu huu wa kupanda miti unaenda sambamba na mradi wetu wa kutoa madawati kwa shule za umma ambapo hadi sasa tumeshatoa madawati takriban 4,000 yenye thamani ya takriban shilingi miliono mia tano na bado tunaendelea alisema Rais wa klabu hiyo Nikki Aggarwal.
Madawati haya yatatumiwa na wanafunzi zaidi ya 10,000 WA while mbalimbali za msingi mkoani Dar es Salaam Amesema kuwa kwakuwa moja ya malighafi za kutengenezea madawati ni mbao, klabu hiyo imeamua kupanda miti ili kutunza mazingira. Tunathamini sana mazingira na tunajuamazingira ni uhai, hivyo chochote tunachofanya tunahakikisha tunatoa kipaumbele kwenye uhifadhi wa mazingira alisisitiza Nikki.
Mbali na kutoa madawati na kupanda miti, klabu hiyo pia kwa kushrikiana na serikali imeandaa mafunzo maalum ya teknohama kwa waalimu wa shule za msingi jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yatafanyika mwezi Apriili katika Chuo Cha Ufundi Dar es Salaam ambapo walimu 80 kutoka shule mbalimbali za Dar es Salaam watashiriki Miradi hii ni ushirikiano wa klabu ya Rotary ikishirikiana na klabu ya Rotary ya Vancouver ya nchini Canada
No comments:
Post a Comment