BREAKING

Thursday, 5 July 2018

MULTICHOICE TANZANIA YAIBUKA KIDEDEA SABASABA


1

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (Kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana cheti na kombe baada ya banda la DStv kuibuka kidedea katika kundi la waonyeshaji wa huduma na bidhaa za teknolojia ya Mawasiliano.

2

Wafanyakazi na mawakala wa MultiChoice Tanzania wakishangilia ushindi mara baada ya banda lao la DStv kuibuka banda bora katika kundi la waonyeshaji wa huduma na bidhaa za teknolojia ya Mawasiliano katika maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam

3

Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania akiwa na balozi maalum wa DStv Nancy Sumari wakionyesha cheti na Kombe walivyokabidhiwa kampuni ya MultiChoice Tanzania baada ya kuibuka banda bora katika kundi la waonyeshaji wa huduma na bidhaa za teknolojia ya Mawasiliano katika maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam

DKT TIZEBA AKABIDHIWA MATREKTA 500 YA URSUS NA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim M. Majaliwa (Mb) akimkabidhi hati ya makabidhiano Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba  ya matrekta 500 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe  ikiwa ni ishara ya kukabidhi matrekta 560 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018.  Watatu kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji, Charles Mwijage, Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Naibu Waziri wake, Dkt, Mary Mwanjelwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba Kitabu cha Mwongozo wa Taratibu za Kujenga Kiwanda Nchini Tanzania baada ya kufungua Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. 


Waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba (Mwenye maiki) akizungumza kabla ya kukabidhiwa matrekta 500 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018.  
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe  ikiwa ni ishra ya kukabidhi matrekta 560 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018.  Watatu kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji, Charles Mwijage na kushoto ni Naibu Waziri wake, Mhandishi Stella Manyanya. Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Naibu Waziri wake, Dkt, Mary Mwanjelwa


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) leo 4 Julai 2018 amemkabidhi Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba jumla ya matrekta 500 yatakayopelekwa kwa vyama vya ushirika vya msingi ili wakulima kunufaika na tija katika kilimo hususani zao la Pamba.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 42 ya sabasaba katika viwanja vya Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam, Mhe. Dkt Tizeba alisema kuwa sekta ya kilimo nchini bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tija ndogo inayosababishwa na matumizi madogo ya pembejeo, huduma duni za ugani na matumizi ya zana duni za kilimo ambapo wakulima wengi wanatumia majembe ya mkono au kutumia maksai wakati wa kulima.

“Katika kilimo cha Pamba msimu wa mwaka 2017/2018 ushahidi unaonyesha kwamba wakulima walichelewa kuanza kuandaa mashamba yao kwa sababu Maksai wakati wa kiangazi wanadhoofu sana, na mara mvua inaponyesha hawawezi kulima mpaka majani yawe mengi ndio wapate nguvu za kuanza kulima, hali hii inaondoa uwezekano wa wakulima kutumia teknolojia mpya katika kilimo kama vile kilimo hifadhi ambacho kimedhihirika kuongeza tija zaidi ya mara mbili” Alikaririwa Mhe Dkt. Tizeba

Aliitaja mikoa itakayoanza kunufaika na mpango huo katika awamu hii ya kwanza kuwa ni pamoja na Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Tabora na Geita, awamu ya pili ikijumuisha mikoa ya Singida, Kagera, na Kigoma huku awamu ya tatu ikitarajiwa kuhusisha mikoa ya Kanda ya Mashariki kwa kuzingatia ongezeko la uzalishaji wa pamba katika maeneo hayo.

Mhe Tizeba alisema mtazamo wa mpango huo ni kuunganisha nguvu za mkulima mmoja mmoja ili kuharakisha kuleta maendeleo yao ambapo utatekelezwa kwa kutumia sehemu ya fedha zinazolipwa AMCOS kama kamisheni ya kusimamia ununuzi wa pamba ambapo matarajio ni kukusanya Bilioni 6 kama uzalishaji wa pamba utafika kilo milioni 400 kwa mwaka.

Mhe. Dkt Tizeba alimuhakikishia Waziri Mkuu kuwa Wizara ya kilimo itatekeleza mpango huo kupitia kwa Mrajis na Bodi ya Pamba ambapo kutakuwa na vituo vinane (8) vya kusimamia Trekta hizo huku kituo kimoja kikiwa ni kwa kila mkoa na viwili kwa mikoa mikubwa inayozalisha pamba kwa wingi.

Aidha, alisema kuwa vituo vitatoa mafunzo kwa madereva na vitafuatilia matengenezo na ushauri wa kitaalamu kuhusu usimamizi wa zana hizo ambapo hadi sasa wizara ya kilimo imepeleka wahandisi wanne (4) na wengine wawili (2) watapelekwa hivi karibuni katika kituo cha kuunganisha matrekta kilichopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ambapo lengo ni kuwapa uzoezfu na uelewa mpana wa kitaalamu wa usimamizi wa matrekta hayo.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha azma hiyo ya kimapinduzi itafanya kazi kwa ufasaha na wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri ili utekelezaji uweze kupata mafanikio na kufanikisha mtazamo wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli katika hatua anazozichukua za kuboresha kilimo nchini ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika sherehe hizo Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa amemkabidhi  waziri wa kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba matrekta 500 ya Ursus kwa ajili ya wateja wa mwanzo katika awamu ya kwanza ya uunganishaji wa matrekta maalumu kwa ajili ya shughuli za kilimo vijijini huku Jeshi la Magereza likikabidhiwa matrekta 50 na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Matrekta 10.

Monday, 2 July 2018

MAMBO MUHIMU YANAYOPATIKANA KATIKA RIPOTI YA UTAFITI WA UHISANI NCHINI ILIYOANDALIWA NA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY CODE


Mchambuzi na mwandishi wa ripoti ya utafiti wa Uhisania Tanzania Bw. Tom Were akiichambua ripoti hiyo mapema jana jiji Dar es salaam.

Watanzania wametakiwa kuwa na moyo wa kutoa kwa kusaidiana wenyewe ndani ya jamii na hata katika kuendeleza huduma mbalimbali za kijamii ili kuweza kusaidia taifa kusonga mbele.


Hayo yamesemwa mapema jana jijini Dar es salaam na Mwanachama wa Bodi ya wakurugenzi ya Foundation for Civil Society Bi. Nesia Mahenge wakati wa uzinduzi wa riporti ya utafiti maalum kuhusu uhisani na utamaduni wa kujitolea ndani ya Tanzania.

Ripoti hiyo iliyohusisha utafiti uliofanywa kati ya mwezi februari hadi mwezi aprili na kuhusisha mashirika ya Foundation for Civil Society (FCS) kwa kushirikiana na Jukwaa la Uhisani Tanzania (Tanzania Philanthropy Forum) kwa lengo la kupata taarifa muhimu kuhusu hali ya uhisani au hali ya kujitolea kwa jamii nchini Tanzania.
Mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi ya Foundation for Civil Society Nesia Mahenge akielezea kwa undani mambo yanayopatikana katika ripoti hiyo ya Utafiti wa Uhisani nchini Tanzania.

Mwanachama wa bodi huyo alisisitiza umuhimu wa mtu mmoja mmoja  pamoja na taasisi mbalimbali binafsi hususani zinazofanya kazi za kijamii kuendelea kujitolea katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kuacha tabia ya kuisubiri serikali kufanya kila kitu.

Aliendelea kusisitiza kuwa ni vema kushiriki katika shughuli mbalimbali za kuleta maendeleo ikiwa ni moja wapo ya njia nzuri ya kuisaidia serikali katika kuinua miradi kadhaa ikiwemo Elimu, Afya, Ujenzi na sio kwa kuwezesha kifedha tu lakini hata katika kusaidia kuleta wahisani watakao fanikisha zoezi hilo pia ni hatua kubwa.

“Lakini pia katika hali ya kujitolea kwa Tanzania uelekeo wake sio mbaya sana kwani watanzania wanaonyesha kuwa wana moyo wa kutoa kwa kusaidiana, lakini pia hata katika juhudi za kujiletea maendeleo kwa kusaidia huduma mbalimbali za kijamii hali inaonyesha bado tupo vizuri” alisema Nesia
Wachambuzi wakiichambua Ripoti ya Utafiti wa Uhisani Tanzania 

Aliongezea kwamba tatizo moja linalojitokeza katika nchi yetu ni kwamba kunakosekana takwimu/taarifa sahihi za watu wanaojitolea lakini zingekuwepo ingesaidia kujua kiwango husika cha watu wanaojitolea katika miradi ndani ya jamii yao na hii inatokana na sharia na mifumo iliyowekwa ndani ya nchi yetu.

Na mwisho alipenda kuwashauri wadau kutumia matokeo ya utafiti huu kama sehemu ya kubadilishana uzoefu katika tasnia nzima ya uhisani na kujitolea katika jamii na kuhamasisha umuhimu wa uhisani miongoni mwa jamii ya watoaji pia kuweka muongozo wa kuendeleza uhisani Tanzania.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini uchambuzi wa Ripoti ya uhisani Tanzania iliyozindiliwa na Foundation for Civil Society mapama jana jijini Dar es salaam.

Thursday, 28 June 2018

MULTICHOICE TANZANIA YAWEKA NGUVU KWENYE RIADHA


Mkuu wa mawasiliano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (wapili kushoto) na Kocha wa riadha Meta Petro (kulia) ambaye pia ni mlezi wa mwanariadha Francis Damiano wakisaini mkataba maalum wa udhamini wa mwanariadha huyo jijini Dar es Salaam. Multichoice imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa kumdhamini mwanariadha huyo mchanga na pia kudhamini kambi ya mafunzo kwa wanariadha. Kushoto ni Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Wilhelm Gida Buday na wa pili kushoto ni mwanariadha Fracis Damas Damiano.

 

 Mkuu wa mawasiliano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (wapili kushoto) na Kocha wa riadha Meta Petro (kulia) ambaye pia ni mlezi wa mwanariadha Francis Damiano wakiwa Tayari kubadilishana nyaraka punde baada ya kusaini  mkataba maalum wa udhamini wa mwanariadha huyo jijini Dar es Salaam. Multichoice imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa kumdhamini mwanariadha huyo mchanga na pia kudhamini kambi ya mafunzo kwa wanariadha. Kushoto ni Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Wilhelm Gida Buday.


Mkuu wa mawasiliano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (kushoto) akimkabidhi nakala ya mkataba mwanariadha chipukizi Francis Damiano mara tu baada ya kusainia mkataba wa udhamini kwa mwanariadha huyo. Kulia ni Kocha wa riadha Meta Petro  ambaye pia ni mlezi wa mwanariadha Francis Damiano.  Multichoice imeingia mkataba wa mwaka mmoja wa kumdhamini mwanariadha huyo mchanga na pia kudhamini kambi ya mafunzo kwa wanariadha.

MultiChoice Tanzania imetangaza kuendelea kudhamini mchezo wa riadha hapa nchini huku ikisaini makubaliano maalum ya kumdhamini mwanariadha kinda Francis Damiano Damasi. Udhamini huo unahusisha fedha ya kujikimu kwa mawanariadha huyo na mafunzo yake na wanariadha wengine katika kambi maalum ya mafunzo inayotarajiwa kuwa wilayani Mbulu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa udhamini kwa mwanariadha huyo, Mkuu wa Mawasiliano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana, amesema kuwa dhamira kubwa ya MultiChoice ni kuhakikisha kuwa mchezo wa riadha unakuwa na mchango mkubwa katika kuliletea taifa sifa, kutoa ajira kwa vijana wengi na kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi.
“Tunataka taifa hili lijulikane ulimwengu mzima kama chimbuko la mabingwa, na tumeanza na riadha. Tumedhamiria kukuza mchezo huu na kuufanya kama chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana wetu, lakini pia riadha ni mchezo, ni burudani, na ni sekta nyeti kiuchumi kama ikiendelezwa” alisema Mshana na kuongeza “Tunataka kuusikia wimbo wetu wa taifa katika mashindano makubwa ya kimataifa, tunataka kuiona bendera yetu ikipepea juu katika kila mashindano makubwa ya riadha ya kimataifa, tunataka mamia ya vijana wetu wenye uwezo mkubwa katika riadha washiriki kwenye mashindano makubwa, waweze kujipatia kipato, kuwekeza na kuwa chanzo cha maelfu ya ajira na hatimaye kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu”
Amefafanua kuwa udhamini huo utakuwa wa mwaka mmoja na utaendelezwa na kuboreshwa kulingana na hali itakavyokuwa pamoja na mafanikio yatakayopatiokana. “ Huu ni mkakati wetu endelevu, ni mpango wetu maalum unaojulikana kama ‘Ni Zamu Yetu’! ambao umejikita katika kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana wetu katika riadha.” Amesema Mshana.
Mbali na kumdhamini Damiano, MultiChoice pia itadhamini kambi maalum ya mafunzo itakayokuwa wilayani Mbulu ambayo inatarajiwa kuanza mafunzo rasmi hivi karibuni. Amebainisha kuwa taratibu za kuanza kwa kambi hiyo zipo katika hatua nzuri na kambi inatarajiwa kuanza rasmi Agosti mwaka huu na itakuwa na wanariadha kinda wasiopungua sita – wasichana na wavulana.
Kwa upande wake mwanariadha Damiano ambaye ni mshindi wa medali ya shaba katika mashindano ya vijana ya Jumuia ya Madola yaliyofanyika visiwa vya Bahamas, amesema udhamini huo utamfanya aweze kufanya mazoezi yake vizuri kwani sasa hyo ndiyo itakuwa kazi yake ya kudumu. Amesema kilicho mbele yake ni ushindi tu. “Nashukuru sana kwa udhamini wa MultiChoice, na mimi naahidi kuwa nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kuwa siwaangushi MultiChoice na siwaangushi watanzania.”
Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania Wilhelm Gida-Buday, amesema wamefarijika sana kuona kuwa MUltiChoice inaendelea kudhamini riadha na akasema udhamini huo siyo tu utamsaidia mwanariadha husika, bali pia ni chachu hata kwa wanariadha chipukizi kuwa na moyo na ari ya kushiriki katika mchezo huo.
Amesema Shirikisho la Riadha Tanzania litahakikisha kuwa udhamini huo unakuwa wa manufaa na unazaa matunda yaliyotarajiwa ya kuleta medali zaidi kutaka katika mashindano ya kimataifa. “Ufadhili wa aina hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya mchezo wa riadha. Tunaahidi ushirikiano wetu wa hali na mali ili kufanikisha malengo na tutahakikisha kuwa tunatoa ushirikiano unaostahili kwa wadhamini wetu” alisema Gida.
Mwanariadha Francis Damiano Damasi, anatarajiwa kushiriki mashindano makubwa ikiwemo Mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki yanayofanyika mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam, Mashindano ya vijana ya Dunia (World Junior Championship) mwezi Julai nchini Finland, Mashindao ya vijana ya Olympic kanda ya Afrika mwezi Julai nchini Algeria, Mashindano ya vijan ya Olympic (Youth Olympic Games) mwezi Oktoba nchini Argentina, na mashindano ya nyika ya vijana (World Junior Cross-country) mapema mwakani nchini Denmark.


NEYMAR ANG'ARA BRAZIL IKISHINDA 2-0 NA KUSONGA MBELE KOMBE LA DUNIA


Nyota wa Brazil, Neymar akimtoka kiufundi mchezaji wa Serbia katika mchezo wa Kundi E Kombe la Dunia Jumatano Uwanja wa Otkrytiye Arena mjini Moskow. Brazil ilishinda 2-0, mabao ya Paulinho dakika ya 36 na Thiago Silva dakika ya 68, hivyo kufuzu hatua ya 16 Bora na itakutana na Mexico Julai 2, wakati Serbia imetolewa. Uswisi iliyotoa sare ya 2-2 na Costa Rica nayo imefuzu pia 16 Bora na itamenyana na Sweden Julai 3 

UJERUMANI WATEMESHWA KOMBE LA DUNIA, WAPIGWA 2-0 NA KOREA KUSINI


UJERUMANI imevuliwa ubingwa wa dunia baada ya kufungwa mabao 2-0 na Korea Kusini leo katika mchezo wa Kundi F Kombe la Dunia Uwanja wa Kazan Arena nchini Urusi.
Mabao yaliyoizamisha Ujerumani waliobeba taji hilo mwaka 2014 nchini Brazil kwa kuifunga Argentina 1-0 katika fainali yamefungwa na Kim Young-Gwon dakika ya 90 (ongeza mbili za majeruhi) na Son Heung-Min dakika ya 90 ( (ongeza sita za majeruhi).
Ujerumani inatolewa mashindanoni baada ya kuambulia pointi tatu tu kutokana na ushindi wa 2-1 dhidi ya Saudi Arabia na kupoteza mechi mbili, kwani kabla ya leo walifungwa 1-0 na Mexico inayoungana na Sweden kwenda hatua ya 16 Bora.
Korea Kusini pamoja na ushindi wa leo imeaga pia mashindano, kwani imemaliza na pointi tatu sawa na Ujerumani ya kocha Joachim Low .
Hii ni mara ya kwanza ndani ya miaka 80 kwa Ujeruman kutolewa katika hatua ya makundi ya kombe la Dunia. Nayo Sweden imeichapa 3-0 Mexico, mabao ya Ludwig Augustinsson dakika ya  50, Andreas Granqvist kwa penalti dakika ya 62 na Edson Álvarez aliyejifunga dakika ya 74.  

Timo Werner wa Ujerumani akisikitika baada ya kupoteza nafasi nzuri ya kuwafunga Korea Kusini 

Wednesday, 27 June 2018

GERMANY OUT!......NI KOMBE LA DUNIA LA MAAJABU



KWA HABARI ZAIDI INGIA HAPA>>>>>>>>>>

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube