Wednesday, 22 July 2015
Monday, 20 July 2015
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKATAA KUGOMBEA TENA UBUNGE

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekataa ombi la wananchi wa jimbo lake la uchaguzi la Katavi la kumtaka agombee tena ubunge katika jimbo hilo ili kuendeleza mipango mbalimbali ya maendeleo aliyoianzisha.
Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili katika kigango cha Kanisa Katoliki cha Kibaoni wilayani Mlele (Jumapili, Julai 19, 2015), Waziri Mkuu Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na anaamini wakati umefika wa yeye kuwaachia wengine nafasi ya ubunge wa jimbo la Katavi.
Amesema yeye ataendelea kuwa karibu na wananchi wa Katavi wakati wote na kwa vile atakuwa na muda wa kutosha atashiriki kikamilifu katika mikakati mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi ili waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini.
Mheshimiwa Pinda aliwaasa wananchi wa jimbo la Katavi wawe makini katika kuchagua mbunge na madiwani na kamwe watoa rushwa na wabadhirifu wasipewe nafasi katika uchaguzi ujao.
Akimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu, Paroko wa Parokia ya Usevya wilayani Mlele, Padri Aloyce Nchimbi aliwaasa wananchi wa Wilaya ya Mlele kumuenzi Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hata atakapokuwa amestaafu kwani bado watahitaji busara na uzoefu wake katika kujiletea maendeleo.
Waziri Mkuu yuko kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele kwa ajili ya mapumziko mafupi.
Leo saa 10 jioni ndiyo mwisho wa kurejesha fomu za ubunge ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JULAI 19, 2015.
18:31
DC WA KINONDONI, PAUL MAKONDA AZINDUA KISIMA CHA MAJI SAFI KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA WATOTO WETU TANZANIA
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (katikati), akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati akiwasili kwenye hafla ya kuzindua kisima cha maji safi katika Kituo cha Watoto Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana.
DC Makonda akisaini katika kitabu cha wageni katika kituo hicho.
18:30
THE STARS BAND YAZINDULIWA RASMI SIKU YA EID MOSI NDANI YA MZALENDO PUB HUKU IKISINDIKIZWA NA BENDI YA FM ACADEMIA PAMOJA NA BARNABA

Mkurugenzi wa The Stars Band, Aneth Kushaba akijitambulisha kwa mashabiki wakenm pamoja na azungumza na wapenzi wa bendi mpya ya The Stars Band wakati wa uzinduzi yeye binafsi alisema hawezi kusema yaliyopita bali wapenzi wa bendi hiyo wategemee makubwa kutoka kwenye bendi hiyo iliyozinduliwa siku ya Idd Mosi ndani ya kiota cha Mzalendo Pub
18:29
KOCHA WA ZAMANI WA SIMBA PATRICK LEWING ASAINI MIAKA Minne KUINOA STAND UNITED
Kocha Lewing akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba wa miaka minne kuinoa timu ya Stand United.
Mwenyekiti wa Stand United Amani Vincent akimtambulisha kocha Lewing kwa waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Stand United Amani Vincent akimtambulisha kocha Lewing kwa waandishi wa habari.
13:19
Sunday, 19 July 2015
AZAM FC YAANZA VYEMA MICHUANO YA KOMBE LA KAGAME YAIFUNGA KCC YA UGANDA BAO 1-0
Wachezaji wa Azam FC Didier Kavumbagu,Erasto Nyoni,Wawa na Himid Mao wakishangilia bao lao lililofungwa na mshambuliaji John Bocco.
Mfungaji wa bao la ushindi dhidi ya KCC ya Uganda John Bocco akishangilia
Na Said Makala
TIMU Azam FC imeanza vyema michuano ya kombe la Kagame baada ya kuifunga KCC ya Uganda bao 1-0.
Bao pekee la Azam fungwa na mshambuliaji John Bocco ambaye pia ni mchezaji wa Taifa Stars,bao ambalo lilizamisha jahazi la KCC, Bocco alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Shomari Kapombe ambaye aliambaa ambaa na mpira upande wa kulia na kumimina krosi safi iliofika katika miguu ya Bocco aliyewalima chenga mabeki wa KCC na kufunga kwa ulaini.
Azam waliendelea kulisakama lango la KCC, lakini umakini wa washambuliaji Didier Kavumbagu, na Bocco ulikuwa mdogo kwani walikosa mabao ya wazi, kipindi cha pili Bocco alishindwa kutumia kwa mara nyingine krosi safi ya Kipre Tcheche, baada ya kubaki yeye na nyavu huku kipa akiwa ameenda malikiti, lakini alipiga shuti kali lililoenda nje.
Hadi dakika 90 zinamalizika Azam waliibuka na ushindi huo na kujiweka vyema katika kinyang'anyiro cha michuano hiyo.

18:34
Subscribe to:
Posts (Atom)