BREAKING

Monday, 15 January 2024

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU CCM






Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu  ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Leo tarehe Januari  15, 2023 Unguja, Zanzibar

Thursday, 11 January 2024

MKAZI WA KAGERA OLIVIA PASTORI AKABIDHIWA MIL. 10 ZA MAJIFTI DABODABO KUTOKA TIGO


Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Joseph Mutalemwa(kulia) akimkabidhi mfano wa hundi Shilingi milioni kumi Mshindi wa Magifti Dabodabo mkazi wa kijiji cha Rushaka, Kitongoji cha Bweigilo kata ya Bwendangabo wilayani Bukoba mkoani Kagera Olivia Pastory baada ya kuibuka mshindi katika hafla iliyofanyika nyumbani kwao mshindi,katikati ni Meneja wa Tigo Mkoa wa Kagera Robert Paul akishuhudia.

Tuesday, 9 January 2024

MLOGANZILA WAZINDUA HUDUMA YA MAFUNZO YA WAGONJWA WA KIHARUSI








Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Taasisi ya Kiharusi Duniani (The World Stroke Organization) imezindua mafunzo maalumu kwa wataalamu wanaoshughulikia magonjwa ya kiharusi kwa lengo la kuendelea kuboresha huduma kwa wagonjwa hao.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya nje (OPD) Dkt. Elimeena Meda amesema mafunzo hayo ni muhimu kwani kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa kiharusi hivyo ni muhimu watoa huduma wote kujua namna bora ya kuwahudumia wagonjwa hao.

“Tumeona sababu ya kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa kiharusi, mafanzo haya yanahusu kada zote zinazoshiriki katika mnyororo wa kuwahudumia wagonjwa wa kiharusi ili kuboresha huduma wanapokuwa hospitalini hadi wanaporuhusiwa” ameongeza Dkt. Meda.

Kwa upande wake, muandaaji wa mafunzo hayo kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dkt. Sarah Matuja amebainisha kwamba ugonjwa wa kiharusi umekuwa tishio nchini na unawakumba watu wenye umri wa miaka kati ya miaka 40 hadi 60 na hivyo kuathiri nguvu kazi ya jamii.

Mafunzo hayo yanatolewa na wataalamu bingwa wa magonjwa ya kiharusi duniani kuanzia leo Januari 9 hadi Machi 19, 2024 ambapo yatahusisha wakufunzi ambao ni Madaktari Bingwa wa kiharusi duniani na yatafanyika kwa nadharia na vitendo.

TIGO WADHAMINI WA MAONYESHO YA KIBIASHARA ZANZIBAR


Mkurugenzi wa kanda Tigo Zantel, Aziz  Said Ali, akimuelezea Mshafanyabiashara wa Mwani,  Jaha Haji Khamis kuhusu huduma ya Mjasiriamali box katika maonesho ya kibiashara Zanzibar,ambapo Tigo zantel ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo.

Saturday, 6 January 2024

DKT. BITEKO- TUYAENZI NA KUYALINDA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kuyaenzi, kuyalinda na kuyaishi kwa dhamira ya dhati, Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwani Waasisi wa Nchi  walifanya mapinduzi hayo ili kuwa na Taifa huru ambalo kila mtu anakuwa na hadhi, kuondoa dhuluma iliyokuwepo na kufanya wananchi kuishi kwa amani na furaha.

Amesema hayo tarehe 6 Januari 2024 wakati akizungumza na Wananchi  katika Wilaya ya Mkoani, mkoani Kusini Pemba mara baada ya kuzindua Afisi ya Uhamiaji na Makaazi ya Askari wilayani humo.

“Sisi Wananchi tunawajibu wa kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kuyaishi, kuyaheshimu,  kukuza uchumi wa nchi na kukuza uzalendo ili baada ya muda mrefu hata baada ya miaka 100 mbele, watakaokuja kusherehekea Mapinduzi haya wakute Zanzibar iliyobora zaidi na waseme Mapinduzi haya yalitufaa.” Amesema Dkt. Biteko

Ameeleza kuwa, moja ya tunu tuliyonayo ni mshikamano hivyo watu wasiruhusu mtu yoyote kuwagawanya kwa misingi yoyote ile, bali maendeleo yaunganishe watu wote na kwamba tofauti za vyama, dini na  kabila visifanye watu wakae kwenye makundi bali kuunganisha watu kwa maslahi ya nchi na watanzania.

Amesema kuwa, nchi inapoenda kusherehekea Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari mwaka huu, watanzania wote waungane kuwaombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, ili waendelee kuongoza vyema, kuimarisha ustawi wa Taifa na kuwaunganisha Watanzania.

Kuhusu Jengo hilo jipya la Afisi ya Uhamiaji katika Wilaya ya Mkoani, mkoani Kusini Pemba, Dkt, Biteko amesema kuwa ni moja ya matunda ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kwani kabla ya Mapinduzi watu walinyimwa haki zao za kimsingi zikiwemo za uhamiaji kama vile kupata pasi ya kusafiria na hivyo Mapinduzi yamewezesha wananchi kupata uhuru wa kusafiri nje ya mipaka ya nchi.


Friday, 5 January 2024

MAGIFTI DABODABO YA TIGO -MUUZA MATUNDA ALAMBA MIL.5...



Kampeni ya Magifti Dabodabo inayoendeshwa na Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo, imewakabidhi mamilioni yao washindi wa kampeni hiyo waliopatikana wikiendi iliyopita.

Katika tukio hilo washindi watatu, Flazia Issa, Stephano Mgova, Shabani Juma walikabidhiwa shilingi milioni moja kila mmoja na Kiungi Juma alikabidhiwa shilingi milioni tano alizojishindia.

Akiwakabidhi mfano wa hundi ya fedha walizojishindia Semaji la Kampeni hiyo, Haji Manara aliwapongeza washindi hao na kuwataka wakawe mabalozi wazuri wa kampeni kwani wao ndiyo mashuhuda wakubwa wa ukweli na uwazi wa kampeni hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Bidhaa za Tigo, Ndevorael Eliakimu aliwataka watumiaji wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Tigo kwa huduma mbalimbali kama vile kufanya miamala, kulipa bili na malipo mengine, kununua vocha kwa kutumia Tigo Pesa au za kukwangua na huduma nyinginezo.

Eliakimu amesema kampeni bado inaendelea ambapo pamoja na pesa taslimu kuna zawadi za seti ya vifaa vya nyumbani vya kisasa kutoka Kampuni ya Hisense ikiwemo friji, runinga, microwave na seti ya muziki (sound bar).

Sambamba na zawadi hizo, Eliakimu amesema kuna zawadi kubwa za magari mapya kabisa ya kisasa ambapo zawadi zote hizo zitatolewa mara mbili kwa kila mshindi na mpendwa wake kama inavyoitwa kampeni hiyo Magifti Dabo dabo.

Wednesday, 3 January 2024

SERIKALI YANUFAIKA NA ZAIDI YA BILIONI 600.…




Serikali imesaini mikataba mitano ya uwekezaji Mahiri kwa wawekezaji wa wanyama pori nchini ambapo Serikali itanufaika na zaidi ya shilingi bilioni mia sita tisini za kitanzania  ikiwa na lengo la kuvutia na kuendeleza vivutio vilivyopo nchini vinavyomilikiwa na  mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania (TAWA) ikiwa ni jitihada za rais wa awamu ya sita Mh Rais Dkt Samia Suluu Hassan katika kukuza utalii wa ndani  na kuwanufaisha watanzania wote.....

Waziri wa maliasili na utalii Angela Kairuki amesema hii ni nafasi kwa serikali ya Tanzania kupitia Mhe Rais  samia kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji na kuendelea kuwavutia wawezekaji na kuongeza idadi ya wawekezaji nchini

Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi ya wakurugenzi ya (TAWA) Hamis Semfuko amesema lazima kuboresha miundombinu ambayo inamilikiwa na tawa ili kuvutia utalii wa ndani katika maeneo mbali mbali…

Mmoja kati ya wawekezaji katika hafla hiyo Taral Abood amesema kupitia uwekezaji huo wanaenda kutekeleza na kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya sita katika kupiga hatua za kimaendeleo…

Hafla hiyo ya utiaji wa saini ya mikataba sita umehudhuriwa na wakala wa misitu tanzania tfs, mamlaka ya usimamizi wa nyamapori tanzania tawa, na wawekezaji pamoja na wadau kutoka sehemu mbali mbali.

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube