Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeeleza kuridhishwa na oparesheni zilizofanyika mwaka jana 2024 kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola ambapo ilifanikiwa kukamata dawa za kulevya Kilogramu 673.2 za Methamphetamine na heroin, miongoni mwa hizo, kilogram 448.3 ziliwahusisha raia wanane wa Pakistani.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretas Lyimo amesema sehemu kubwa ya dawa hizo zikikamatwa katika bahari ya Hindi katika harakati za kuingizwa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema Serikali ya awamu ya sita kuputia mamlaka ya kudhibiti Dawa za Kulevya DCEA kwa mwaka 2024 ilifanya mapinduzi makubwa katika kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya na kwamba katika dawa zilizokamatwa zipo zilizokutwa zimefichwa ndani ya jahazi la raia hao wa Pakistan.
Aidha katika hatua nyingine Kamishna huyo amesema Serikali inaendelea kuweka mkazo katika kuhakikisha inaikinga jamii dhidi ya Madhara yatokanayo na dawa za kulevya akieleza pia jinsi watumiaji wanavyotumia vibaya bahari ya Hindi kufikisha madawa hayo nchini.
No comments:
Post a Comment