Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko amekerwa na utendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akitoa maagizo uongozi wa kituo cha miito ya simu (call centre) ufumuliwe.
Maagizo ya Dk Biteko kwa Tenesco ni kufuatia kutotekelezwa kwa maagizo yake ya aliyoyatoa mwaka jana ya kuwepo kwa namba ya mawasiliano ya wateja isiyolipiwa ambapo itamwezesha mteja kupiga simu bila kukatwa salio agizo ambalo halijatekelezwa.
Dkt Biteko ameyatoa maagizo hayo baada ya kutembelea kituo cha miito ya simu Tanesco ambapo amesema watendaji wa shirika hilo wamezoea kazi.
No comments:
Post a Comment