BREAKING

Wednesday, 11 October 2023

MAONYESHO YA BIDHAA ZA KUKU KUFANYIKA DAR....



Chama cha wafuga kuku Tanzania (The Poultry Association of Tanzania) kimeandaa maonesho ya siku mbili ya bidhaa za kuku yatakayofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam tarehe 13 na 14 Oktoba 2023.

Maonesho hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya 8 hapa nchini yanatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega na yatahudhuriwa na washiriki wapatao 40 wa Ndani nan je ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maandalizi, mratibu wa maonesho hayo Sufian Zuberi amesema maandalizi yote yamekamilika na wameshasajili washiriki 40 kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo Afrika Kusini, Uholanzi, China na nchi nyingine.

“Tumepata muitikio mzuri wa washiriki na tunaamimi maonesho ya mwaka huu yatawawezesha watembeleaji kujifunza mambo mengi yanayohusiana na ufugaji bora wa kuku. Tunawashauri wakazi wa Dar waje kwa wingi kwenye maonesho haya ili wajifunze ufugaji bora wa kuku na pia wapate uelewa wa bidhaa za kuku.” Alisema Sufiani na

Kwa mujibu wa takwimu rasmi, kuku hutoa 18% ya lishe ya Protini hapa nchini na ni moja ya vyanzo vya kipato kwa kaya Zaidi ya milioni 4 hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube