BREAKING

Wednesday 25 October 2023

RAIS DKT .SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI IKULU -ZAMBIA





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema mara baada ya kuwasili Ikulu ya Lusaka nchini Zambia tarehe 25 Oktoba, 2025









 

TAWA YAFADHILI MRADI WA UJENZI WA MADARASA KALIUA, WANAFUNZI WAELEZA HISIA ZAO.







SERIKALI kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imefadhili mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili, ofisi moja ya walimu na jumla ya madawati 30 katika shule ya msingi Usinge iliyopo wilaya ya kaliua Mkoani Tabora

Mradi huu ambao tayari umekwishakamilika na kuanza kutumika umegharimu kiasi cha Tsh. Millioni 50 (50,000,000/=) ambazo ni fedha zinazotokana na bajeti ya ndani ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA

Akiongea na waandishi wa habari katika ziara ya ukaguzi wa mradi huo wa maendeleo kwa jamii Oktoba 24, 2023 Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja ameeleza kuwa TAWA iliona adha wanazozipata wanafunzi wa Shule ya msingi Usinge kwa kukosa madarasa ya kutosha, ofisi ya walimu pamoja na madawati hivyo ikaona vyema kufadhili mradi huo ili kuwapunguzia adha hizo na kuwapa fursa wananchi kuona faida zitokanazo na shughuli za uhifadhi na  umuhimu wa uwepo wa Taasisi hiyo katika maeneo yao 

"Ifahamike kuwa changamoto  kubwa katika vijiji vinavyozunguka hifadhi ni kwamba shule nyingi zinakosa madarasa na madawati ya kutosha lakini pia wanakosa nyenzo mbalimbali za kuwawezesha wao kuweza kusoma katika mazingira bora" amesema

"..kwahiyo Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania iliona vyema kufadhili miradi hii ili kuwawezesha wananchi wanaozunguka maeneo haya kufaidi rasilimali hizi za Wanyamapori na uhifadhi kwa ujumla" ameongeza

Salma Madua Ally ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika shule hiyo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan na Taasisi ya TAWA kwa ufadhili huo  ambao ameuelezea kama ni msaada mkubwa kwao ambao hawakuutegemea kwani umepelekea kuongeza uwezo wao wa uelewa na ufaulu darasani

"Nawashukuru wasimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA pia tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea madarasa ambayo hatukutegemea kuwa nayo, pia madarasa haya yametufanya tuweze kuwa tunafaulu na kuwa tunaelewa vizuri" amesema

"...Kipindi cha nyuma tulikuwa tunakaa darasa moja watu wengi, tulikuwa hatuwezi kuelewa kwa urahisi lakini saizi tumegawanyishwa madarasa" ameongeza

Naye Joseph Paulo mwanafunzi wa Shule hiyo ameeleza kuwa kabla ya ujenzi wa madarasa  na kufadhiliwa madawati hayo walikuwa wakikaa chini huku wanafunzi wachache wakikalia madawati hali ambayo ilifanya  nguo zao zichafuke na kukosa umakini darasani, lakini kwa sasa wote wanakaa  kwenye madawati na kusomea kwenye vyumba vizuri vya madarasa

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bw. Ibrahimu Bakari Juma ameeleza kuwa shule ya Usinge ilikuwa na uhaba wa vyumba sita vya madarasa pamoja na madawati 90 hivyo ufadhili huo uliotolewa na Serikali kupitia TAWA umewezesha idadi ya wanafunzi 90 kukaa kwenye madawati

Aidha ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dr. Samia Suluhu Hassan lakini pia ameelekeza pongezi na shukrani zake kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA kwa ufadhili huo

Monday 16 October 2023

RAIS SAMIA AKIWA ZIARANI SINGIDA -APEWA HESHIMA YA MAMA WA TAIFA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Bombadia Mkoani Singida katika muendelezo wa ziara yake Mkoani humo tarehe 16 Oktoba, 2023


Kwaya ya Utumishi wa Umma ikitumbuiza kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mkoa wa Singida yaliyofanyika katika uwanja wa Bombadia tarehe 16 Oktoba, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye maadhimisho ya Miaka 60 ya Mkoa wa Singida yaliyofanyika katika uwanja wa Bombadia tarehe 16 Oktoba, 2023


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye viwanja vya Bombadia kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya Miaka 60 tarehe 16 Oktoba, 2023


Wednesday 11 October 2023

MAONYESHO YA BIDHAA ZA KUKU KUFANYIKA DAR....



Chama cha wafuga kuku Tanzania (The Poultry Association of Tanzania) kimeandaa maonesho ya siku mbili ya bidhaa za kuku yatakayofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam tarehe 13 na 14 Oktoba 2023.

Maonesho hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya 8 hapa nchini yanatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega na yatahudhuriwa na washiriki wapatao 40 wa Ndani nan je ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maandalizi, mratibu wa maonesho hayo Sufian Zuberi amesema maandalizi yote yamekamilika na wameshasajili washiriki 40 kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo Afrika Kusini, Uholanzi, China na nchi nyingine.

“Tumepata muitikio mzuri wa washiriki na tunaamimi maonesho ya mwaka huu yatawawezesha watembeleaji kujifunza mambo mengi yanayohusiana na ufugaji bora wa kuku. Tunawashauri wakazi wa Dar waje kwa wingi kwenye maonesho haya ili wajifunze ufugaji bora wa kuku na pia wapate uelewa wa bidhaa za kuku.” Alisema Sufiani na

Kwa mujibu wa takwimu rasmi, kuku hutoa 18% ya lishe ya Protini hapa nchini na ni moja ya vyanzo vya kipato kwa kaya Zaidi ya milioni 4 hapa nchini.

KINANA AKUTANA NA BALOZI WA NORWAY OFISI NDOGO ZA CCM, DAR ES SALAAM




Makamu Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu Abdurahman Kinana amekutana na kufanya mazungumzo na  Balozi wa Norway Nchini Tanzania Mhe. Tone Tinnes leo Jumatano, Oktoba 11, 2023, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es salaaam.

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube