TIMU za Zambia, Zesco na Nkana FC zimepangwa pamoja katika Kundi C Kombe la Shirikisho Afrika baada ya droo iliyofanyika leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri.
Pamoja na Zesco na Nkana FC, klabu anayochezea beki Mtanzania, Hassan Ramadhani Kessy, timu nyingine katika kundi hilo ni Al Hilal ya Sudan na Asante Kotoko ya Ghana.
Mabingwa watetezi, Raja Club Athletic wamepangwa pamoja na wapinzani wao wa Morocco, RS Berkane na Hassania Agadir kwenye Kundi A, huku timu nyingine katika kundi hilo wakiwa ni mabingwa wa Kongo, AS Otoho.
Kukutana kwa timu tatu za Morocco kwenye hilo, kunakumbushia michuano ya mwaka 2012, wakati timu tatu za Sudan; Al Merreikh, Al Hilal na Ahly Shendi zilipopangwa kundi moja pai, huku timu nyingine kwenye kundi lao ikiwa ni Interclube ya Angola.
Hassan Kessy, wa kwanza kushoto walioinama amepangwa kundi moja na Zesco, Al Hilal na Asante Kotoko
Katika droo hiyo ambayo mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, Patrick Mboma alisaidiana na Katibu Msaidizi wa CAF, Anthony Baffoe kupanga makundi, timu mbili za Tunisia, Etoile du Sahel na CS Sfaxien zimekutanishwa Kundi B pamoja na Enugu Rangers ya Nigeria na Salitas ya Burkina Faso.
Mabingwa mara tano Afrika, Zamalek ya Misri wamepangwa Kundi D pamoja na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia, Petro Atletico ya Angola na NA Hussein Dey ya Algeria.
MAKUNDI YOTE KOMBE LA SHIRIKISHO:
Kundi A – Hassania Agadir (Morocco), AS Otoho (Kongo), RS Berkane (Morocco), Raja (Morocco)
Kundi B – Etoile du Sahel (Tunisia), Rangers (Nigeria), Salitas (Burkina Faso), CS Sfaxien (Tunisia)
Kundi C – Zesco (Zambia), Al Hilal (Sudan), Asante Kotoko (Ghana), Nkana (Zambia)
Kundi D – Gor Mahia (Kenya), NA Hussein Dey (Algeria), Petro Atletico (Angola), Zamalek (Misri)
KWA MSAADA WA MTANDAO WA BIN ZUBEIRY....
No comments:
Post a Comment