BREAKING

Thursday, 3 January 2019

JAMHURI YAIGOMBEA AZAM FC ,KOMBE LA MAPINDUZI


Michuano ya Mapinduzi imenza kutimua vumbi huku kigogo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bar azam FC akianza kwa sare na timu ya Zanzibar ya Jamhuri

Mechi hiyo iliyokuwa na upinzani kwa pande zote mbili, ilishuhudiwa Azam FC ikianza kuandika bao la uongozi dakika ya 28, lililofungwa na kiungo mshambuliaji, Tafadzwa Kutinyu, kwa mkwaju wa penalti uliotokana na Emmanuel Balele, kuunawa mpira wakati akiokoa shuti la mfungaji wa bao hilo.

Jamhuri iliyocheza kwa nidhamu kubwa kwenye eneo la ulinzi hadi kufanikiwa kuwabana washambuliaji wa Azam FC, ilipata bao la kusawazisha dakika ya 66 lililofungwa na Abdul Ramadhan, bao lililowafanya kuambulia pointi hiyo moja.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC kuhitaji matokeo mazuri kwenye mechi zake tatu zilizobakia za hatua ya makundi, ikianza na Yanga Jumamosi hii, mchezo unaofuatia utakaofanyika Uwanja wa Amaan saa 2.15 usiku.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube