BREAKING

Tuesday, 22 January 2019

BODI YA WAKUREGENZI DAWASA YAWATAKA WAFANYAKAZI DAWASA WAWE WAADILIFU

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi wakipewa maelezo juu ya mfumo wa usambazaji wa maji kutoka katika tanki la Makongo jijini Dar es Salaam. Bodi hiyo inafanya ziara ya siku tatu ili kuweza kujifunza na kujionea jinsi mifumo ya usambazaji wa maji kwa jiji la Dar es Salaam na Pwani. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
 Mashine zilizofungwa katika tanki la makongo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi wakionyeshwa mtambo wa kuendeshea maji. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wakiangalia mfumo wa Tenki la SalaSala jijini Dar es Salaam ikiwa ni ziara yao ya kujifunza masual mbali mbali ya maji.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi  wakiwa wamewasili kituo cha mtambo wa Ruvu chini- eneo la Bagamoyo - Pwani. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi wakiongea na wafanyakazi wa DAWASA kituo cha mtambo wa Ruvu chini- eneo la Bagamoyo - Pwani. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi wakiongea wakiangalia zoezi la kutandika mabomba ili kuwagawia maji wakazi wa Goba -Kizudi jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange jinsi maji yanavyovunwa katika Mtambo wa Ruvu Chini - eneo la Bagamoyo - Pwani.
Wakikagua eneo la mto Ruvu chini...
Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa DAWASA, Injinia Aron Joseph akiwaonyesha Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (kwanza kulia) pampu za kuvuta maji.
Meneja wa DAWASA ofisi ya Bagamoyo, Alexander Ng'wandu akitoa maelezo machache mbele ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange mara baada ya kutembelea ofisi hizo zilizopo mjini Bagamoyo - Pwani.
Meneja wa DAWASA ofisi ya Bagamoyo, Alexander Ng'wandu akitoa maelezo machache mbele ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA iliyoongozwa na Mwenyekiti wao Jenerali Mstaafu Davis mara baada ya kutembelea tenki  la maji la Bagamoyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi wakiongea na wanahabari mara baada ya kumaliza kutembelea kituo cha mtambo wa Ruvu chini- eneo la Bagamoyo - Pwani.
JENERALI MWAMUNYANGE ATEMBELEA MTAMBO WA RUVU CHINI NaCathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imewataka wafanyakazi wa DAWASA kuendelea kuwa waadilifu katika kazi zao ili kuweza kuwapa huduma bora wananchi wa Dar es Salaam na Pwani. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi mara baada ya kutembelea mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini na kuongea na wafanyakazi wa DAWASA wa kituo hicho. Jenerali Mstaafu Mwamunyange amefurahishwa na utunzaji wa mazingira katika eneo la mto Ruvu ikiwa ndio chanzo kikubwa kinachozalisha maji kwa asilimia 88 katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Akiwa katika ziara yake ya siku ya pili, Jenerali mstaafu Mwamunyange ametembelea mtambo huo ikiwa ni mara ya kwanza toka achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo. "Nimejifunza mambo mengi hata wenzangu wamekili kuna mambo mengi tulikuwa hatuyafahamu hakika sasa tutakuwa watendaji wazuri kwa kutambua kile tunachokisimamia," Amesema Jenerali Mstaafu Mwamunyange. Amesema jitihada kubwa za serikali zinafanyika kuhakikisha wananchi wote wanapata maji hususani kwenye maeneo yaliyokuwa hayana maji kwa kipindi chote kikubwa wananchi wawe wavumilivu kwakuwa DAWASA wanafanya kazi kuwapelekea maji. Baada ya kuwasili katika mtambo huo walipata fursa ya kuzungumza na wafanyakazi wa mtambo huo na kuwataka wafanye kazi kwa juhudi kubwa ili kutimiza adhma ya serikali ya kufikia asilimia 95 ya wananchi wote ifikapo 2020. Amesema, anafahamu kuna changamoto mbalimbali za wafanyakazi ila amewaahidi atazifanyia kazi atakapokutana na Sekretarieti ya DAWASA. Mbali na kutembelea mtambo wa Ruvu Chini, Bodi hiyo ilitembelea Tenki la maji la Changanyikeni, Busta pampu zilizofungwa Makongo kwa ajili kusukuma maji na maunganisho mapya Salasala. Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi itaendelea kwenye maeneo mengine tofauti kwa ajili ya kujifunza na kuona namna DAWASA wanavyotoa huduma ya maji kwa wananchi wa Dar esSalaam na Pwani.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube