BREAKING

Tuesday, 25 September 2018

CHELSEA NA LIVERPOOL JUMAMOSI WIKI HII NDANI YA SUPERSPORT MAMBO NI MOTOOOOO! Supe


Jumamosi hii kwenye Premier League, Wana wa darajani aka the Blues - Chelsea ambao wanashikilia nafasi ya 3 katika msimamo wa Ligi watakuwa wakiwakaribisha vinara wa Ligi wanaoshikilia namba 1, Liverpool. 

Hii ndio mechi nadhani raia wote tunaisubiri kwa hamu. Mechi itapigwa saa 1 na nusu usiku ndani ya Supersport 3 kupitia kifurushi cha Compact kwa sh.69, 000 tu.

Mechi nyingine ni kwenye premier league Jumamosi ni

·      West Ham United vs Manchester United saa 8:30 mchana SuperSport 3 kwenye kifurushi DStvCompact

·      Manchester City vs Brighton saa 10:30 jioni Supersport 10 ya kifurushi DStv Bomb ash.19, 000 tu!
·      Arsenal vs Watford saa 11 jioni kwenye Supersport 5 ya kifurushi DStv Compact Plus

Mteja wa DStv, Lipia kabla akaunti yako kukatika upate ofa ya chaneli za ziada za supersport za kifurushi cha juu kwa kipindi cha siku 7 ufurahie soka kabambe msimu huu bila gharama ya ziada.

Hii ni sababu nyingine ya kufurahia ukilipia kifurushi chako mapema.

Na kumbuka ukiwa na Application ya DStv Now utaweza kuangalia mechi zote kupitia simu yako ya mkononi, Tablets, Laptop na hata Desktop ukiwa mahali popote wakati wowote bila gharama ya ziada.

Monday, 24 September 2018

HUSSEIN TUWA :MTUNZI WA VITABU VYA HADHITHI MWENYE 'UKWASI' WA UANDISHI BOBEZI WA VITABU VYA HADITHI

 Picha Mbalimbali zikimuonyesha Mtunzi mahiri wa Vitabu vya Hadithi Hussein Tuwa akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kitabu chake kipya cha MTAFITI,Kitabu hicho kinaelezea baadhi ya matukio halisia zikiwepo vurugu zilizotokea Mtwara wakati wa Mchakato wa mafuta ya  Gesi.



Friday, 21 September 2018

M-BET WAENDELEA KUMWAGA PESA KWA MASHABIKI WA SOKA ...

 Mshindi wa ubashiri wa Perfect 12 Given Nasson akikabidhiwa mfano wa hundi na Mwakilishi wa kampuni ya kubeti ya M-Bet David Malley


Thursday, 20 September 2018

ASDP II ITALETA MAGEUZI KATIKA SEKTA YA KILIMO NCHINI-DKT TIZEBA

Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), Waziri wa kilimo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa utafiti na kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania hafla iliyofanyika katika ukumbi wa ESRF Jijini Dar es salaam Leo tarehe 19 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa uzinduzi wa Mradi wa utafiti na kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania hafla iliyofanyika katika ukumbi wa ESRF Jijini Dar es salaam Leo tarehe 19 Septemba 2018 wakifatilia kwa umakini mkubwa hotuba ya Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), Waziri wa kilimo.
Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), Waziri wa kilimo (kulia) akikata utepe ishara ya kuzindua Mradi wa utafiti na kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania hafla iliyofanyika katika ukumbi wa ESRF Jijini Dar es salaam Leo tarehe 19 Septemba 2018. Mwingine pichani ni Dkt Tausi Mbaga Kida, Mkurugenzi wa Taasisi ya tafiti za kiuchumi na kijamii ESRF.
Picha ya pamoja Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) Waziri wa kilimo akiwa na washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa utafiti na kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania hafla iliyofanyika katika ukumbi wa ESRF Jijini Dar es salaam Leo tarehe 19 Septemba 2018.

Na Mathias Canal-WK, Dar es salaam

Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) Waziri wa kilimo, ameitaja Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (Agricultural sector Development Programme ASDP II) kwamba italeta mageuzi makubwa katika sekta hiyo zikiwemo sekta zingine ya Mifugo na Uvuvi kwa kuongeza uzalishaji, tija na kufanya kuwa na matokeo makubwa yatakayopelekea kupungua kwa madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

Dkt Tizeba ameyasema hayo Leo tarehe 19 Septemba 2018 wakati wa uzinduzi wa Mradi wa utafiti na kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania hafla iliyofanyika katika ukumbi wa ESRF Jijini Dar es salaam.

Alisema kuwa ASDP II ni Programu ya miaka 10 itakayotekelezwa kuanzia mwaka wa 2017/2018 hadi 2027/2028 katika vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Awamu ya kwanza itaanza kutekelezwa 2017/2018 hadi 2022/2023 ambayo ni muendelezo wa awamu ya kwanza ya ASDP 1 iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2006/2007 hadi 2013/2014.

Alieleza kuwa Programu hiyo imezingatia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Mpango wa Maendeleo wa muda mrefu 2012-2021, Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano 2016-2021, Mkakati wa kuendeleza sekta ya kilimo 2015 na Mpango wa uwekezaji katika kilimo na lishe (Tanzania Agriculture and Food Security Investment Plan -TAFSIP 2011). 

Pia alisema kuwa Wizara ya kilimo inaendelea kukuza na kulinda Maendeleo ya sekta ya kilimo yaliyo endleevu kwa kuongeza uzalishaji, kubiresha mifumo inayokwenda sambamba na tabia nchi kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia ya nchi kwa umakini mkubwa sana kwani Tanzania ni miongoni mwa nchi chache ambazo zimefanikiwa kuendeleza Mpango mkakati wa kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi ili kwenda sambamba na Dira ya maendeleo ya Taifa 2025. 

Alisema kuwa serikali inatambua juhudi zitakazotolewa na mradi wa utafiti wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi katika nyanja za kilimo na Mfumo wa chakula nchini Tanzania CCRF-AFRICAP katika kuelewa mustakabali wa sekta ya kilimo.
Mradi huo wa CCRF-AFRICAP ni mradi wa kikanda utakaojumuisha nchi nne Barani Afrika ambazo ni Tanzania, Malawi, Afrika kusini, na Zambia ambapo kwa upande wa Tanzania Mradi huo utasimamiwa na ESRF ambazo ni wawakilishi wa mtandao wa Taasisi zinazojihusisha na uchambuzi wa sera katika nyanja za chakula, kilimo, na maliasili Barani Afrika (FANRPAN) ukijumuisha watafiti katika nyanja za mifumo ya kilimo ikiwemo sayansi ya udongo, sayansi ya mimea, sayansi ya Mifugo na ikolojia, kisiasa na sayansi ya jamii.
Kwa mujibu wa Dkt Tausi Mbaga Kida, Mkurugenzi wa Taasisi ya tafiti za kiuchumi na kijamii ESRF, alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuainisha na kutekeleza Sera zinazotokana na uthibitisho wa kisayansi kupitia utafiti katika kuendeleza Maendeleo endelevu, uzalishaji, mifumo ya kilimo inayozingatia mabadiliko ya tabia nchi ili kuwezesha kufikia usalama wa chakula na Maendeleo ya kiuchumi.
Mabadiliko ya tabia nchi ni miongoni mwa changamoto inayoikabili mataifa ya Afrika katika karne ya 21 kwani inakadiriwa kuwa idadi ya watu watakaokuwa hatarini kwa njaa itaongezeka maradufu Barani Afrika pia kupelekea ongezeko la ukame , kupungua kwa uzalishaji na kubadilika kwa Nyakati za hali ya hewa yatakayopelekea kupungua kwa uzalishaji wa Mazao mengi ya chakula yanayostawi sana.

Tuesday, 18 September 2018

UEFA CHAMPIONS LEAGUE is baack!


DStv wamewasha tena Moto Jumanne hii ambapo msimu mpya wa UEFA Champions league unaanza rasmi, Na ni kwenye Supersport pekee ndipo utaweza kuipata Ligi hii ya Mabingwa wa Ulaya Mubashara!

Barcelona watatufungulia pazia kwa mechi kali dhidi ya PSV itakayochezwa saa 2 usiku na kuruka LIVE kwenye DStv kupitia Supersport 5. Inter Milan itacheza dhidi ya Tottenham Hotspur saa 2 usiku na utaipata mechi hii LIVE kwenye Supersport 6 kifurushi Compact Plus.

Borussia Dortmund wataenda Jan Breydel Stadium kukutana na Club Brugge mechi itakayorushwa LIVE kwenye Supersport 8 ya kifurushi Bomba kwa sh.19, 000 saa 12 jioni.

Mechi nyingine kali Jumanne hii ni kati ya Liverpool dhidi ya PSG itakayochezwa saa 4 usiku kwenye Supersport 5 kifurushi Compact Plus.

Mteja wa DStv, Hakikisha unalipia kifurushi chako kabla hakijakatika ili upate ofa ya kuongezewa chaneli za supersport za kifurushi cha juu kwa kipindi cha siku 7 buree na utaweza kufurahia msimu mpya wa UEFA Champions League.

Kumbuka ukiwa na Application ya DStv Now utaweza kuangalia mechi zote kupitia simu yako ya mkononi, Tablets, Laptop na hata Desktop ukiwa mahali popote wakati wowote bila gharama ya ziada.

DStv sasa inapatikana kwa sh.79, 000 tu unapewa na kifurushi cha mwezi mmoja Bomba buree, Kujiunga piga 0659 070707!
DStv Moto Hauzimi!




Tuesday, 11 September 2018

M-BET WAENDELEA KUWANUFAISHA WATANZANIA ,WAMWAGA ZAIDI YA MILIONI 239 KWA MSHINDI WA PERFECT 12

Mshindi wa ubashiri wa Perfect 12 Ibrahim Pius Mbwilo akikabidhiwa mfano wa hundi na Meneja Masoko wa M-Bet Allen Mushi

 Mshindi wa M-Bet Ibrahim Mbwilo akionyesha Hundi yake ya Milioni 239,4178,00

Meneja Masoko wa M-Bet Allen Mush akizungumza wakati wa kukabidhi hundiya Milioni 239,4178,00 kwa mshindi Ibrahim Bwilo Mkazi wa Iringa

Friday, 7 September 2018

RC HAPI: MARUFUKU KUWANYANYASA MACHINGA KATIKA MAENEO WANAYOFANYIA YA KAZI ZAO


Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga wa manispaa ya Iringa kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto ambazo wanakabiliana katika kuleta maendeleo ya mkoa wa Iringa na kuhakikisha wanaijenga Iringa mpya ambayo inatakiwa na wanairinga 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea wakati wa kikao cha wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga na mkuu wa mkoa wa Iringa
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga walijitokeza kumsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi na kama ambavyo unawaona walivyokuwa makini kumsikiliza hapo

 NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa mkoa wa Iringa amepiga marufuku wafanyabiashara wadogo wadogo kunyanyaswa katika mahali ambazo wanafanyia biashara kwa kuwa wanatoa kodi ambayo inachochea kuleta maendeleo ya watanzania hususani mkoani iringa tukielekea kuijenga Iringa mpya.

Akizungumza kwenye mkutano na wafanyabiasha wadogodogo wa manispaa ya Iringa mkuu wa mkoa Ally Hapi alisema kuwa wafanyabiasha wadogo wadogo maarufu kama machinga wanatakiwa kufanya biashara zao kwa kufuta taratibu na sheria za nchi huku viongozi wakiancha kuwanyanyasa kwa kuwa nao ni wafanyabiashara.

“Toka nikiwa mkuu wa wilaya najua umuhimu wafanyabiasha wadogo wadogo kwa kuchangia katika kukuza uchumi wa eneo husika hivyo natangaza rasmi ni marufuku kuwanyanyasa wafanyabiasha wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa” alisema Hapi

Hapi aliwataka polisi wanasimamia eneo lastand kuu kuacha mara moja kunyanyasa wafanyabiasha wadogo wadogo wanaofanyia biashara katika eneo hilo.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya katibu na mwenyekiti wa chama cha wafanyabiasha wadogo wadogo (machinga) kutoa kilio hicho mbele ya mkuu ya mkoa kwa kusema wamekuwa wakinyanyaswa na askari ambao wanafanya kazi katika stand kuu.

Katibu wa wafanyabiasha wadogo wadogo manispaa ya Iringa Joseph Kilyenyi alisema kuwa baadhi ya viongozi wa halimashauri ya manispaa ya Iringa pamoja na baadhi ya polisi wamekuwa kikwazo cha kufanya biasha kwa uhuru na kuongeza pato la manispaa ya Iringa.

“wafanyabiasha wadogo wadogo tupo zaidi ya elfu moja tukiwekewa mfumo sahihi kwa wakati sahihi tunaweza kutoa kodi zaidi ya shilingi milioni tisa ambapo hapo tunatoa shilingi mia tatu  na ikiwa shilingi mia tano halmashauri itaingiza mapato mengi ambayo yatachangia maendeeleo ya manispaa” alisema Kilyenyi

Kilyenyi alisema kuwa wafanyabiasha wadogo wadogo wa manispaa ya Iringa wapo tayari kulipa kodi kama ambavyo Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo na kuwapa nafasi wafanyabiasha wadogo wadogo kufanya kazi kwa uhuru na kuchochoe maendeleo.

“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania DR John Pombe Magufuli amekuwa akitupelea na kuthamini hivyo hata sisi tunawajibu wa kuhakikisha tunalipa ushuru na kodi pale inapotakiwa ili kukuza juhudi za kuleta maendeleo ya nchi yetu” alisema Kilyenyi

Kilyenyi alimpongeza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela pamoja na MNEC wa mkoa wa Iringa Salim Asas kwa kuwasaidia kutatua migogoro mbalimbali ambayo imekuwa ikiwakabili wafanyabiasha wadogo wadogo

“Baada ya kupokea kero za wafanyabiasha wadogo wadogo mkuu wa mkoa wa Iringa Hapi alimtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya Iringa ndani ya mwezi mmoja kuhakikisha wanatengeza mfumo rafiki ambao utakuwa utasidia kukusanya kodi kwa wafanyabiasha hao.

Nimetoa siku thelathini kwa viongozi wa halmashauri kuhakikisha wanatengeza mfumo rafiki ambao hausababisha wafanyabiasha wadogo wadogo kulipa kodi katika maeneo wanayofanyia kazi ili kuwaondolea usumbufu wa kuwafuta mliko” alisema Hapi

Aidha hapi alisema kuwa hatawavumia viongozi wowote wale ambao watakwamisha kuijenga Iringa mya ambayo inatakiwa kuwa kama kituvu cha utalii nyanda za juu kusini

Naye afisa biashara wa manispaa ya Iringa kassim majariwa alisema kuwa ameyapogea maagizo yote ambayo mkuu wa mkoa ameagiza kuhakikisha kunakuwa na ongezeko la ukusanyaji wa kodi katika halmashauri ya Iringa.

WILFRIEDY ZAHA ROHO YAKE SAAFI....


Wilfried Zaha anatarajiwa kutoa mchango mkubwa kusaidia wanadada wa klabu ya Crystal palace.

Hatua hiyo ya winga wa Crystal Palace inafuatia ripoti kwamba kikosi cha pili cha klabu hiyo kimeambiwa kulipoa £250 kila mmoja wao la sivyo waondoke katika klabu hiyo.

Timu ya wanawake ya Crystal Palace ambayo inacheza katika ligi ya wanawake amesema kuwa ripoti hiyo ya Guardian sio ya kweli.

Klabu hiyo imesema kuwa inamshukuru Zaha mwenye umri wa miaka 25, ambaye mwezi Agosti alisaini kandarasi mpya yenye thamani ya £130,000 kwa wiki.

TAIFA STARS WAWASILI KIBABE KAMPALA ,UGANDA KESHO KUUMANA NA TIMU YA TAIFA YA UGANDA UWANJA WA NAMBOOLE

Kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars' kikiwa tayari kuwakabili The Cranes,'Uganda

Wednesday, 5 September 2018

USIWACHUKULIE POA DSTV SIO WA MCHEZO MCHEZO WIKI HII UGANDA DHIDI YA TAIFA STARS MAMBO NI MBASHARAAAAAAA SUPER SPORT 8






WIKI HII NDANI YA DStv!!

Mashindano mapya kabisa ya UEFA Nations League yanaanza kutimua vumbi wiki hii huku pazia likifunguliwa na magwiji wawili wa Soka siku ya Alhamisi. 

Ambapo Ufaransa (Mabingwa wa Dunia) watacheza dhidi ya Ujerumani (Mabingwa wa Dunia waliopita). Kisha kuendelea na Albania dhidi ya Israel siku ya Ijumaa, huku Italy ikiikaribisha Poland siku hiyo hiyo ya Ijumaa na kumaliziwa na Turkey vs Russia.


Jumamosi Switzerland itacheza dhidi ya Iceland, Finland vs Hungary wakati England wakicheza dhidi ya Spain. Na siku ya Jumapili Germany itacheza dhidi ya Peru, France itacheza dhidi ya Netherlands, Bulgaria vs Norway Na Denmark vs Wales!


Mechi hizi zote utazipata ndani ya DStv kuanzia kifurushi chako cha Bomba kwa sh.19, 000 tu!


Bila kusahau Jumamosi hii, DStv inakuletea mtanange wa kukata na shoka pale Uganda (The Cranes) watakapozichapa na timu yetu ya Taifa Tanzania yaani Taifa Stars. Macho Na masikio tutayaelekeza Uganda, tarehe 8/9/18 ndani ya Supersport 8 ya kifurushi Bomba kwa sh.19, 000 tu ndani ya DStv pekee!


Moto Hauzimi na kama Sio DStv Potezea!
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube