BREAKING

Thursday, 28 December 2017

MAN CITY ACHA MIGUUU IONGEE....YAZIDI KUCHANJA MBUGA...



Raheem Sterling celebrates scoring the opening goal of the game after a brilliant chipped pass from Kevin De Bruyne

Raheem Sterling akishangilia bao alilofunga na kuipa ushindi wa bao 1-0 timu yake ya Manchester City.KWA PICHA ZAIDI GONGA HAP>>>>>>>

Manchester City imeendelea kuonyesha kandanda la kuvutia na kuwaacha wapinzani wao wa karibu Manchester United kwa pointi 14 sasa na kuonyesha msimu huu wanadhamiria kutwaa ubingwa.

Mchezo wa usiku wa kuamkia leo ilichapa bao 1-0 Newcastle 
na kufanya kujiimarisha kileleni mwa ligi Kuu ya EPL.

LIVERPOOL YAMNYAKUA VIRGIL KUTOKA SOUTHAMPTON...

Liverpool wanaendelea kujiimarisha katika kikosi chao baada ya kumsajili Virgil van Dijk kwa pauni milion 75.

Wednesday, 27 December 2017

SIMBA NI FIMBO AMA KIBOKO, WANAJIANDAA KUWAKABILI DANDA FC JUMAMOSI



KANE AFUNGA MWAKA 2017 KWA KUWAPIGA BAO MESSI, RONALDO SASA ANATAKA KUANDIKA MPYA



Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane ameonyesha kuwa kweli amepania baada ya kumpiga mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi kwa mabao yaliyofungwa mwaka 2017.

Kane amefunga mabao matatu au hat trick katika mechi  Southampton ambayo imeisha kwa Tottenham kushinda kwa mabao 5-2.

Mabao hayo matatu yamemfanya Cane kufikisha mabao 56 mbele ya Messi ambaye sasa ana mabao 54 aliyofunga msimu wa 2017.


Baada ya Kane, Messi, wanaofuatia ni Cristiano Ronaldo, Edinson Cavani na Robert Lewandowski na ambao kila mmoja wanamaliza mwaka kila mmoja akiwa na mabao 53.

TAKWIMU:

  • Kane, 56 goals (49 with Tottenham, 7  England)
  • Messi, 54 goals (50 with Barcelona, 4  Argentina)
  • Cavani, 53 goals (50 with PSG, 3 Uruguay)
  • Lewandowski, 53 goals (44 with Bayern, 9 Poland)
  • Cristiano Ronaldo, 53 goals (42 with Real Madrid, 11 Ureno)

TANESCO YAFURAHISHWA NA HATUA ZA SERIKALI KULINDA VYANZO VYA MAJI YA KUFUA UMEME


  
INAELEZWA kuwa umeme wa maji, (Hydro power) ndio umeme wenye bei nafuu zaidi ukilinganisha na umeme unaotokana na vyanzo vingine.
Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa TANESCO anayeshughulikia uzalishaji (Power Generation), Mhandisi Abdallah Ikwasa, matumizi ya juu ya umeme nchini kwa sasa ni Megawati 1,060, kati ya hizo, TANESCO kwa kutumia mitambo yake, huzalisha Megawati zaidi ya 1,000, na kati ya hizo, Megawati 381 zinatokana na umeme unaozalishwa kutokana na maji, (Hydro powere) kutoka vituo vinne vya umeme wa maji vya Kidatu, Mtera, New Pangani Falls, Hale na Nyumba ya Mungu.
Hata hivyo katika siku za karibuni shughuli za kibinadamu zimekuwa zikiongezeka kwenye vyanzo vya maji yanayoelekea kwenye vituo vya kufua umeme, na hivyo kutishia shuhghuli za uzalishaji umeme kwenye vituo hivyo.
Mhandisi Ikwasa alitoa mfano Mto Pangani ambapo yapo maeno ambayo shughuli za kilimo zinaendelea karibu na mto, na madhara yatokanayo na shughuli hizo hupelekea kingo za mto kuwa dhaifu na wakati wa mvua maji yanachukua udongo na kuingiza kwenye mto na hivyo kina cha mto kinakuwa kifupi.
“Sasa kipindi ambacho mvua zinanyesha unatarajia maji mengi yatiririke kwenye mto lakini kwa sababu kina kimepungua mto hauwezi kubeba yale maji na badala yake maji yanasambaa na kusababisha mafuriko na mbaya zaidi hayafiki kwenye mabwawa kwa kiwango kinachohitajika.” Alisema Mhandisi Ikwasa.
Alisema TANESCO kama wadau wakubwa wa maji wamekuwa wakishirikiana na mamlaka zinazosimamia mabonde, ili kuelimisha watumiaji wengine wa  maji.
“Tunataka kuhakikisha kwamba, kunakuwepo na matumizi endelevu ya maji, tunatambua wananchi wanahitaji maji kwa kilimo na sisi tunayahitaji kwa uzalishaji umeme kwa hivyo yakitumika vizuri yanaweza kufanya kazi zote.” Alisema.
Mhandisi Ikwasa aliipongeza Serikali kwa juhudi kubwa inazochukua kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa.
“Makamu wa Rais aliunda kikosi kazi cha kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa na juhudi hizo zimeanza kuzaa matunda.” Alisema.
Ili kuhakikisha wananchi wanajenga dhana ya umiliki wa miundombinu ya TANESCO, Shirika limekuwa likishirikiana na wananchi katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kusaidia kutoa huduma za afya, elimu ya awali na usafiri katika maeneo yanayozunguka vituo vya kuzalisha umeme.

“Tunataka wananchi wafahamu kuwa pamoja na kwamba kazi yetu ni kuzalisha umeme, lakini tunataka tuwe sehemu ya maisha yao, kwa kusaidia mambo ya kijamii kama vile kutoa elimu bure ya awali, zahanati, na usafiri wa basi unaosaidia wananchi kusafiri kuelekea kwenye shughuli zao, tunadhani kwa ushirikiano huu, wananchi watakuwa wakwanza kulinda miundombinu yetu na pia kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwenye vyanzo vya maji.” Alisema Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji.
Ili kuhakikisha ujumbe huo pia unawafikia wananchi wote kupitia vyombo vya habari, wahariri wa vyombo vya habari walipata fursa ya kutembelea vituo vya kufua umeme wa maji vya Hale, New Pangani na Nyumba ya Mungu, vilivyoko mikoa ya Tanga na Kilimanjaro, kituo cha Mtera kilichoko mkoani Iringa na Kidatu mkoani Morogoro ili hatimaye watoe elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ya vyanzo vya mito ambayo maji yake ndio huelekea kwenye vituo vya kufua umeme.

 Meneja wa kituo cha kufua umeme wa maji cha Kidatu, Mhandisi Anthony Mbushi, (kushoto), akizungumza kuhusu jinsi mageti ya kuruhusu maji kwenye mabwawa kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme yanavyofanya kazi. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme. Mhandsisi Abdallah Ikwasa.
 Wananchi wa Kidatu, wakisub iri usafiri wa basi la Shirika la Umeme TANESCO, kuwapeleka kwenye mnada ili kuuza mazao yao. Usafiri huo hutolewa bure na Shirika katika mpango wake wa Corporate Social Responsibility (CSR) ili kujenga uhusiano mwema.
 Moja ya mashine za kufua umeme wa maji, (turbine), kituo cha Hale.
 Wasimamizi wa kituo cha kudhibiti mfumo wa umeme cha Mtera.
 Bwawa la New Pangani Water Falls.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza jambo.
Mhandisi Mahenda S.Mahenda, Meneja vituo vya kufua umeme vya Pangani Hydro Systems, akifafanua jambo.

WANANCHI JIJINI DAR ES SALAAM WAIPONGEZA KAMPUNI YA ABACUS PHARMA (A) LTD


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu (kulia), Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga  na Dk. Mohamed Mohamed wa ugonjwa wa Kisukari katika hospitali hiyo wakikata keki maalumu iliyotengenezwa kwa bidhaa za Sugar Free zisizo na sukari wakati wa uzinduzi  wa bidhaa hizo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

 Muonekano wa keki hiyo iliyotengenezwa kwa bidhaa hizo zisizo na sukari.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu, akizungumza bidhaa hizo.
Hii ndiyo timu ya maofisa masoko wa kampuni hiyo.

Na Dotto Mwaibale



WANANCHI jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake wameipongeza  Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD kwa kuwaletea bidhaa za Sugar Free ambazo zinasaidia kupunguza  matumizi makubwa ya sukari kwenye vyakula.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam walisema kampuni hiyo haina budi kupongezwa kwa kuzileta bidhaa hizo katika soko la Tanzania ili kukabiliana na changamoto ya matumizi kupitia vyakula.

"Hivi sasa kila pembe ya nchi yetu kumekuwa na changamoto ya ugonjwa wa kisukari ambao kwa kiasi kikubwa unatokana na mfumo wa ulaji na unywaji wa vyakula vyenye sukari kupita kiasi kwa bidhaa hizi mpya zinazosambazwa na Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD hakika itasaidia sana" alisema Frank Erasto mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam.

Erasto alisema yeye ni mihongoni mwa waathirika wa ugonjwa wa kisukari lakini tangu bidhaa hizo ziingie katika soko la Tanzania amekuwa akitumia bidhaa hizo ili asiongeze sukari mwilini mwake baada ya kupata matibabu.

Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina moaja la Reuben alisema familia yake imeanza kutumia bidhaa hizo ambazo hazina gharama kubwa.

"Familia yangu na marafiki zangu tumeanza kutumia bidhaa hizi za Sugar Free kusema kweli ni nzuri na zina radha kama ile zilizopo kwenye chakula halisi" alisema Reuben.


Mkazi wa Kariakoo Happyness Kimaro alisema kwake anaona bidhaa hizo ni mkombozi kwani ameanza kuzitumia baada ya kuathiriwa na ugonjwa wa kisukari na hapendi kuongeza sukari mwilini mwake.

"Sisi wagonjwa wa kisukari tumekuwa na changamoto kubwa ya ulaji wa vyakula mara tunaambiwa tusile hiki na kile tule vyakula ambavyo havina sukari ambavyo havina ladha sasa kwa kuletewa bidhaa hizi tunasema ni nafuu kwetu" alisema Kimaro.

Akizungumza bidhaa hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu alisema bidhaa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi makubwa ya sukari katika vyakula. 


Alisema bidhaa hizo zimetengenezwa mahususi ili kukabiliana na ongezeko la sukari mwilini na hivi sasa zinapatikana kwa bei ya chini katika soko la nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na kuwa bei hizo zipo kuanzia shilingi,4200, 4,500, 5,700, 8,850 na za bei ya juu ni shilingi 13,000 na kuwa zinategemea bidhaa husika.

"Bidhaa hizi zipo za aina mbili za sugar free gold  ambazo hutumika katika chai, uji, na vinywaji baridi tu  na sugar free natura hutumika katika baking, kupikia vyakula vinavyohitaji sukari katika upishi na pia hutumika katika chai, uji na vinywaji baridi na matumizi yake ni rahisi sana," alisema Babu.

Alisema kwa Tanzania bidhaa hizo zimeanza kuchukua soko kubwa baada ya wananchi kuona umuhimu wake na hivyo wanategemea muitikio utaendelea kuwa mkubwa.

Aliongeza kuwa, lengo kubwa la kampuni hiyo kusambaza bidhaa hizo ni kusaidia jamii kuelewa matumizi ya bidhaa hizo ambazo hazina sukari ingawa zina ladha ya sukari kama ile ya kawaida  na kwamba bidhaa hizo zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).


Akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga alisema ugonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni nchi ya tano Barani Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi.


Alisema hali hiyo inatokana na watu wengi hasa vijijini kutojijua mapema kama wameathiriwa na ugonjwa huo ambapo baadhi yao huanza kugundua baada ya kupata upofu, kukatwa miguu na kadhalika. 


Aliongeza kuwa, matibabu ya mgonjwa mmoja wa kisukari yanafikia asilimia 25 ya pato la familia fedha ambazo ni nyingi jambo linalowafanya wauguzaji kukata tamaa ya kumtibu mgonjwa na kuamua fedha hizo kuzielekeza katika matumizi mengine.


Dk.Chiwanga alitoa mwito kwa kusema ni vizuri kuzuia kupata kisukari kuliko kutibu.

Akizungumzia bidhaa za sugar free alisema hazitibu ugonjwa wa kisukari isipo kuwa zinamsaidia mgonjwa au mtu mwenye kisukari anapokula vyakula vingine visivyo na sukari kupata radha ile ile.

Alisema mtu mwenye ugonjwa wa kisukari hatakiwi kabisa kuvuta sigara ingawa vitu vingine kama vinywaji na pombe anatakiwa kutumia kwa uangalifu.

Tuesday, 12 December 2017

MAMIA WAMUAGA MWANAHABARI JOYCE MMASI JIJINI DAR ES


 Marehemu Joyce Mmasi enzi za uhai wake.
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mwanahabari Joyce wakati ukiwasili viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo kwa ibada ya kuuaga kabla ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.
 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Wanahabari wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Mchungaji Kulwa wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, akiongoza ibada hiyo.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando akizungumza kwenye ibada hiyo.
 Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo akizungumza. Lyimo na marehemu Mmasi wanatoka kijiji kimoja.
 Familia ya marehemu ikiwa katika ibada hiyo. Kulia ni mtoto wa kwanza wa marehemu, Lawrence Nicky Mayella.
 Mume wa marehemu Joyce Mmasi, Andrew Kamugisha akizungumza kwenye ibada hiyo.

Rafiki wa marehemu Mashaka Mgeta, akizungumzia maisha ya Joyce na jinsi alivyomfahamu.


 Waandishi wa habari wanawake wanaounda kikundi cha Wawata wakitoa neno katika ibada hiyo.
 Mwanahabari Hellen Mwango akisaidiwa baada ya kupoteza fahamu.
 Mtoto mkubwa wa marehemu,  Lawrence Nicky Mayella, akisoma Historia ya mama yake.
 Mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Thomson, akizungumza katika ibada hiyo.
 Waombolezaji wakiwa katika foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu.
Foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho.

VILIO Majonzi na simanzi vilitawala   wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa mwanahabari nguri Joyce Mmasi iliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Katika ibada hiyo mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wanahabari na wadau wengine walijitokeza katika viwanja hivyo kwa ajili ya kumuaga mpendwa wao Joyce Mmasi ambaye alikuwa akifanyia kazi katika gazeti la Mwananchi.

Mchungaji Kulwa kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambaye aliongoza ibada hiyo aliwaambia watu waliokuwepo kwenye ibada hiyo kuwa wanapaswa kujitayarisha wakati wote kwani hawajui ni lini wataondoka hapa duniani.

"Mwenzetu Joyce ametutangulia tulikuwa naye pamoja lakini wewe uliye hai leo hii umejiandaeje katika maisha ya kiroho?" alisema Mchungajia Kulwa.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando alisema kifo cha Mmasi kimemshitua kila mtu na wanahabari wamepata pigo la kumpoteza mwenzao.

Mhando alihimiza kudumisha upendo kwa watu wote pamoja na wanahabari.

Katika ibada hiyo makundi mbalimbali yalijitokeza kutoa salamu za rambirambi na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, siasa, serikali na wadau wengine.

Mwili wa marehemu Joyce umesafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro nyumbani kwao kwa mazishi.

Marehemu ameacha mume na watoto watatu, Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu.

VIJANA WA ZANZIBARA NA TANZANIA BARA WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM KUANGALIA FURSA ZILIZOPO NCHINI


 Vijana kutoka Zanzibar na Tanzania Bara wakiwa katika mkutano wa majadiliano ya kuangalia fursa zilizopo nchini ili kuzifanyia kazi kwa ajili ya kulitetea taifa maendeleo. Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki Makao Makuu ya Kampuni ya Trumark jijini Dar es Salaam.
 Majadiliano yakiendelea.
 Msisitizo katika majadiliano hayo.
 Fursa mbalimbali zikiandikwa katika makundi.
Picha ya pamoja ya vijana hao.

VIJANA wa Zanzibar na Tanzania Bara wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia fursa zilizopo nchini ili kuliletea taifa maendeleo.

Katika mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki Makao Makuu ya Kampuni ya Trumark vijana hao wapatao 14 kwa niaba ya wenzao walijadiliana mambo mbalimbali na kuangalia fursa za maendeleo zilizopo nchini.

Kwa ujumla fursa zilizokuwa zimeangaliwa katika maeneo mbalimbali na wazo hilo limekuja baada ya baadhi yao kutembea nchi nzima Tanzania Visiwani na Tanzania Bara na kuziona hivyo wakaona ni vema kuunganisha nguvu ya pamoja kwa kuwashirikisha wenzao na kuona waanzie wapi.

"Tumetembea nchi nzima na kuona fursa mbalimbali tukaona ni vizuri vijana wa Zanzibar na Tanzania Bara tukutane tujadiliane na tuone ni fursa zipi tuzifanyie kazi kwa manufaa yetu kama vijana na taifa kwa ujumla" alisema mmoja wa vijana hao ambaye hakupenda kuingia kiundani zaidi kwa kuwa mchakato wa jambo hilo ndio kwanza upo jikoni.

Alisema hivi sasa vijana wasitegemee kuajiriwa badala yake waziangalie fursa zilizopo nchini na hizo ndizo zitakazo waondoa katika mawazo ya kutegemea kuajiriwa.

Alisema kuna fursa za kuanzisha viwanda vidogo vidogo, ufugaji, ufundi mbalimbali, kilimo na mambo mengine hivyo ni vema vijana wakaangalia huko zaidi.

Alisema wamekutana katika mkutano huo kuangalia fursa hizo na wapi pa kuanzia na mchakato huo ukikamilika wataweka mambo hadharani na kukamilisha mambo yote lengo likiwa ni kuwaunganisha vijana wa nchi nzima.

=

Thursday, 7 December 2017

NI KIAMA UEFA LIVERPOOL WAIGEUZA ANFIELD MACHINJIO WAKIICHAPA SPARTAK BAO 7-0 LIGI YA MABINGWA ULAYA





















 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube