BREAKING

Saturday 30 April 2016

CHAMA CHA WAKUNGA TANZANIA (TAMA) WATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI


DSC_2376Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari (kushoto) akieleza jambo kwa wanahabari na watu mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo kwa waandishi wa habari juu ya kufahamishwa shughuli za Wakunga. Kulia ni Bi. Felister Bwana kutoka UNPFA, Nchini Tanzania.
DSC_2381Mkutano huo ukiendelea...
DSC_2383 DSC_2389Baadhi ya maafisa kutoka taasisi za Wakunga na mambo ya Afya wakifuatilia mkutano huo.
DSC_2391Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari akito mada katika mkutano huo..
DSC_2397DSC_2402Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo
DSC_2408Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huoDSC_2409Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari akitoa mada katika mkutano huo kwa wanahabari..
DSC_2436Mratibu wa TAMA, Bi. Martha Rimoy akitoa mada maalum kwa waandishi wa habari namna kazi na shughuli za Wakunga wanazofanya hapa nchini
DSC_2432
Afisa Mipango wa UNFPA, hapa nchini, Bi.Felista Bwana akitoa maelezo mafupi juu ya wakunga hapa nchini
DSC_2448Mratibu wa TAMA, Bi. Martha Rimoy akitoa mafunzo hayo katika mkutano huo kwa wanahabari
DSC_2464Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo
DSC_2479Bi. Felista Bwana akitoa mada katika mkutano huo
DSC_2467Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari akifafanua maswali kwa wanahabari wakati mkutano huo..
DSC_2481
DSC_2426Picha ya pamoja baadhi ya wanahabari na wandaaji wa mkutano huo maaalum kwa wanahabari kuelekea siku ya Wakunga Duniani ambayo kilele chake ni hapo Mei 5 mwaka huu huku kwa Tanzania ikitarajiwa kufanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. 


Chama cha Wakunga Tanzania(TAMA) watoa mafunzo kwa wanahabari Nchini
Chama cha Wakunga Tanzania (Tanzania Midwives Association-TAMA) imefanya mkutano maalum wa kuhamasisha waandishi wa Habari kuhusu kazi za wakunga katika kuelekea siku ya Wakunga Dunia ifikapo hapo Mei 5 mwaka huu.
Katika mkutano huo uliofanyika jana Aprili 28, TAMA ilibainisha kuwa, wanahabari wengi wamekuwa wakichanganya habari za wakunga wataalam ambao wapo chini ya Chama hicho na wale wakunga wa jadi ambao hawana taalum pamoja na kiapo cha kufanya kazi hiyo kitu ambacho kinaleta usumbufu mkubwa kwa jamii.
Mratibu wa TAMA, Bi. Martha Rimoy katika mkutano huo, ameeleza kuwa, shughuli za Wakunga wataalam ni wale tu ambao wamesomea taaluma hiyo pamoja na kula kiapo katika kumsaidia Mama na Mtoto na na huyo ndiyo anaitwa Mkunga na si wale ambao hawajapata mafunzo wala kula kiapo.
Aidha, aliomba wanahabari na vyombo vya habari kuzipatia nafasi/Kipaumbele habari za Wakunga kwani zitaondoa woga kwa jamii iliyojenga Imani potofu kwa wakunga.
“Jamii imekuwa ikijenga Imani potofu namna ya Wakunga buka kujua mkunga huyo ni yupi. Tunaomba ifahamike Mkunga ni yule aliyepata mafunzo yake kitaalam na pia kula kiapo pamoja na kusajiliwa na taasisi husika kama ilivyo taratibu za Nchi.
Tuondoe Imani zingine kwa Wakunga pia tunawaomba wanahabari kuweza kutoa elumu ya kutosha kuhusiana na mambo ya Wakunga hasa wakunga wataalam ambao wamepatiwa mafunzo yote ya kuhakikisha wanamuokoa Mama na mtoto wakati wa uzazi” alieleza Bi. Martha Rimoy.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, ameeleza kuwa, Wakunga wataalam wanao wajibu
wa kumsaidia Mwanamke na mtoto katika kukabiliana na vifo vitokanavyo na Masuala ya Uzazi vinavyozidi kuwatesa akina mama wengi, hasa inapokuja wakati wa tendo la kujifungua.
Aidha, Dkt. Sebalda amebainisha kuwa, pamoja na Changamoto mbalimbali, vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5, imepungua kwa asilimia 81, huku akitaka muendelezo wa elimu utolewe kwa Jamii.
Kwa upande wake, Afisa Mipango wa Afya ya Mama na Uzazi wa Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA)nchini, Bi. Felista Bwana ameelezea kuwa, upo umuhimu wa Mkunga mtalaam katika kuokoa Uhai wa Mama na mtoto kwani bila wao Dunia ingekuwa kwenye matatizo makubwa.
Siku ya Ukunga Duniani Inatarajiwa kuadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam, Mei 5 mwaka huu huku ikibeba ujumbe wa kauli mbinu ya “Wanawake na Watoto wachanga ni muhimili wa Ukunga”.
Aidha, mkutano huo ulieza changamoto wanazokabiliana nazo wakunga ni nyingi hivyo wameimba Serikali kuangalia namna ya kukabiliana nayo ili kila Mkunga kufanya kazi yake kwa uhuru na haki kwa dhama za sasa huku wakiomba jamii kuondoa dhana potofu dhidi yao pindi wawaonapo katika vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali zote.
Mkutano huo maalum wa TAMA, ulihusisha wanahabari mbalimbali kutoka katika vyombo vya Habari nchini ikiemo, Magazeti, Radio, Televisheni na magazeti ya mtandaoni.


Wednesday 27 April 2016

BUNGE SPORTS CLUB NA BARAZA LA WAWAKILISHI HAKUNA MBABE,ZATOKA SARE YA BAO 1-1

 
DSC_2098 DSC_2099Kapteni mpya wa timu ya Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, Mh. Sixtus Mapunda akitoa maelezo kwa kikosi hicho cha Bunge muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wao huo dhidi ya timu ya Baraza la Wawakilishi mchezo uliochezwa katika uwanja wa Amaan,
DSC_2285Waziri wa Kilimo, Mfugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba akipata picha ya pamoja na mmoja wa wachezaji wa Baraza la Wawakilishi
DSC_2282
Mchezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi ambaye pia analiwakilisha Jimbo la Tunguu, Mh. Simai Mohamed Said akijadiliana jambo na ,Mwakilishi wa Rahaleo (CCM), Mh. Nasasor Salum Al Jazeera wakati wa mchezo huo maalum dhidi ya timu ya Bunge.
DSC_2150
Timu zikiingia uwanjani
DSC_2151 DSC_2157 DSC_2160 DSC_2162
Wachezaji wakisalimiana kabla ya mechi
DSC_2169 DSC_2187
DSC_2190 DSC_2197
Kikosi cha timu ya Bunge kabla ya mchezo huo kuanza..
DSC_2197
Kikosi cha timu ya Bunge kabla ya mchezo huo kuanza..
DSC_2202 DSC_2206
Kikosi cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar kabla ya mchezo huo kuanza...
DSC_2247
Mchezo ukiendelea katika uwanja huo wa Amaan
DSC_2253 DSC_2255
Mashabiki wakifuatilia mchezo huo
DSC_2258 DSC_2259Viongozi wakiwa katikajukwaa maalum la wageni waalikwa.
DSC_2261 DSC_2267 DSC_2271 DSC_2273
Kikosi cha Bunge kikitoka katika vyumba vya kupumzikia kuendelea na kipindi cha pili
DSC_2294 DSC_2296
Viongozi wa timu wakihamasisha timu yao hiyo ya Bunge...
DSC_2305
Viongozi wa timu wakiwa hawaamini baada ya Baraza la Wawakilishi kusawazisha bao hilo na kuwa 1-1...
DSC_2307
Kikosi cha Baraza la Wawakilishi waliokuwa wapo mapumziko wakifurahia baada ya kusawazisha bao hilo
DSC_2326 DSC_2339Kikosi cha Bunge mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo
nightofhope17DSC_2345DSC_2348 DSC_2352
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid akizungumza baada ya mchezo huo
DSC_2357
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais Mazingira na Muungano Mh. January Makamba akizungumza mara baada ya mchezo huo
maxresdefault
Kikosi cha Bunge kikiomba dua mara baaa ya mchezo huo...
DSC_2360Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Bunge (wa pili aliyesimama nyuma) akipata picha ya pamoja na baadhi ya vijana waliojitokeza katika mchezo huo wa kuimalisha Muungano.
DSC_2371Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Bunge na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba wakipata picha pamoja na Vijana wa Visiwani Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Bunge na Baraza la Wawakilishi ambao uliisha kwa sare ya bao 1-1. 



Timu ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania, Bunge Sports Club usiku wa leo Aprili 26.2016 imeweza kutoka sare ya bao 1-1, dhidi ya timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mchezo uliochezwa uwanja wa Amaan, Unguja na kushuhudiwa na watu mbalimbali.
Mchezo huo wa aina yake na wa kipekee kwa kikosi hicho cha Bunge Sports Club kiliweza kucheza kandanda safi na la kuvutia wakati wote ambapo waliweza kupata bao lao la kuongoza ndani ya dakika 22 ya mchezo katika kipindi cha kwanza bao safi lililofungwa kwa kushuti la nje ya 18 na kuwaacha Wachezaji wa Baraza la Wawakilishi wasijue la kufanya.
Bao hilo la Bunge Sports Club ambalo lilikuwa la ushindi lilidumu hadi kipindi cha pili ambapo katika dakika ya 67, Timu ya Baraza la Wawakilishi ilifanikiwa kusawazisha bao hilo na kufanya mchezo kuwa 1-1. Bao hilo lilipachikwa kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya hasa mvua kiasi cha kuwapoteza vibaya wachezaji wa timu ya Bunge ambao walicheza katika mazingira magumu sana.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika, Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamoto alibainisha kuwa kikosi chake kilicheza soka safi na wataendelea kukiimalisha kwani wanaamini mpira ni ajira ambapo pia alieleza kuwa bila washindani wao ‘kuwachomekea’ wanahakika wangefanya vizuri zaidi n ahata kuibuka na mabao mengi.
Kwa upande wake, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid alizipongeza timu zote mbili na kuzitaka kuendelea kudumisha michezo na suala la Muungano kwa ujumla kwani wanahakika kupitia michezo suala hilo litaenziwa kwa miaka yote.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais Mazingira na Muungano Mh. January Makamba alibainisha kuwa wataendelea kuulinda Muungano huku akiwataka Watanzania kuishi kwa misingi ya Amani na utulivu kwa kipindi chote ambapo pia alieleza kuwa suala la Michezo litaendelea kuwapo ilikuongeza mshikamano kwa watu wote.


 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube