BREAKING

Monday, 9 November 2015

SHAMAKALA360 BLOG YAMTEMBELEA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE DK JAKAYA KIKWETE KIJIJINI KWAKE MSOGA,ASEMA UFUGAJI UNALIPA AJIVUNIA NG'OMBE WAKE.

 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete,wakati wa mazungumzo na mahojiano mafupi nyumbani kwake Msoga

 Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitoka ndani kuelekea ilipo mifugo yake
 Rais Kikwete akisikiliza jambo kwa makini
 Hapa aneleza jambo kwa msisitizo
 Rais Mstaafu Kikwete akiwa na Mkewe Mama Salma Kikwete, hapa ni kwenye zizi kubwa la Ng'ombe wake






DK Kikwete  Akimshika Ng'ombe wake

 Akifurahia jambo

 Kikwete akisisitiza jambo kwa Mfanyakazi anayehudumia Ng'ombe

 Dume likiwa linakula majani yaliyotengenezwa kisasa

 Baadhi ya Ng'ombe wa Rais Mstaafu Kikwete

 Rais Kikwete na Mkewe wakiangalia Ng'ombe wao
 Ng'ombe akiwa anakunywa maji

 Mfanyakazi akifanya usafi katika zizi la Ng'ombe

 Baadhi ya Ng'ombe wakiwa mapumzikoni 



Rais Mstaafu DK.Kikwete akionyesha  Baadhi ya mabaki ya Chakula cha Ng'ombe

Rais mstaafu Dk.Jakaya Kikwete akieleza jinsi ufugaji wa Ng'ombe wake

Na Said Makala

Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk.Jakaya Mrisho Kikiwete, sasa ni mfugaji halisi baada ya kustaafu na kumkabidhi kijiti Dk John Pombe Magufuli, ambapo Kikwete amesema kuwa sasa anajikita katika ufugaji wa Ng'ombe pamoja na Kilimo.

Shamakala360 imemtembelea rais huyo mstaafu nyumbani kwake kijiji cha Msoga,Chalinze na kufanya naye mazungumzo kwa kina, kabla ya kutembezwa katika himaya yake ya ufugaji wa Ng'ombe.

Katika maswali kadhaa ambayo aliulizwa na mtandao huu, Rais Kikwete anaeleza amekuwa akifarijika zaidi kuona maendeleo mazuri ya ufugaji hivyo kustaafu kwake sasa nguvu anaelekeza katika Kilimo na ufugaji.

"Napenda Ufugaji kumbuka nimestaafu nimeamua kurejea Kijijini kwetu hapa Msoga kama unavyoona sasa nina Ng'ombe wengi sana nitaendelea kuwatunza na pia nitajikita kwenye Kilimo"Alisema

Katika mazungumzo hayo marefu pia Kiongozi huyo ambaye aliongoza Tanzania kwa Miaka 10, ameeleza kuridhishwa na kiwango kizuri cha Soka kinachoonyeshwa na nyota wanaosakata kandanda la kulipwa kunako klabu ya soka ya TP mazembe ya Kongo ambapo amesema ni wachezaji wenye nidhamu na ndio sababu inayowapa matumaini.

Kauli ya Kikwete imekuja baada ya nyota hao kufanikiwa kutwaa kombe la Klabu Bingwa Afrika dhidi ya timu ya USM ya Algeria na Samatta kutwaa kiatu cha dhahabu.

Aidha Rais huyo Mstaafu ameitakia kila la kheri timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa stars'inayotarajiwa kucheza mchezo wa kuwania kufuzu hatua za makundi ya kombe la Duni dhidi ya Algeria.

"Naitakia kila la kheri timu ya Taifa Stars,katika mchezo wao Jumamosi naamini wanaweza kuifunga Algeria,na wakasonga mbele hivyo nina imani kubwa kwao wanaweza kufika mbali hata mimi nilipokuwa rais nilikuwa na nia dhabiti kufikisha mbali soka, nashukuru hata hapa nilipofikia najua rais aliyenipokea kijiti Dk John Magufuli ni mpenda michezo naye ataendeleza yale niliyoyaacha" Alisema Kikwete.

Rais Kikwete atakumbukwa kwa mengi na wanamichezo kufuatia mikakati yake mbalimbali ya kuhakikisha soka linakua Tanzania ikiwepo kuleta makocha ambapo alilipa mishahara yake kama ilivyokuwa kwa kocha Mbrazili Marcio Maximo,si hilo tu bali hata sasa ameacha kumbukumbu baada ya kujenga kituo cha kuendeleza vipaji cha Kidongo chekundu Jijini Dar es Salaam.


Friday, 6 November 2015

MULTICHOICE TANZANIA WAMTANGAZA RASMI DIAMOND PLATNUMZ KUWA 'OFFICIAL DSTV BRAND AMBASSADOR'

DSC_0168
Mwanamuiki nyota nchini Tanzania, Nassib Abdul ama Diamond Platnumz akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani). (Picha na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Adndrew Chale, Modewji
[DAR ES SALAAM-TANZANIA]
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania mapema jana imezindua ofa kabambe za msimu wa siku kuu huku ikimtambulisha rasmi Mwanamuziki Diamond Platnumz kuwa balozi maalum wa bidhaa za kampuni hiyo ikiwemo kifurushi cha DSTV BOMBA chenye chaneli zaidi ya 65 ikiwemo huduma ya vituo kadhaa vya televisheni za hapa nchini.
Akimtambulusha rasmi Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Furaha Samalu, amemtambulisha Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa balozi wa king’amuzi hicho na kutaja gharama zake kuwa ni shilingi 23,500/= kwa malipo ya mwezi na king’amuzi chenyewe kinapatikana kwa shilingi 79,000/= na kuwataka wananchi kuchangamkia huduma hiyo muhimu katika msimu huu wa ofa za sikukuu.
Meneja masoko huyo ameongeza kuwa, kifurushi hicho kimesambaa nchini mbalimbali barani Afrika hivyo wasanii wa filamu, muziki na wengineo ambao watang’aa kwenye vipindi hivyo watakuwa wakionekana pande mbalimbali barani Afrika na hivyo kuwapatia umaarufu na kuwaongezea soko la kazi zao.
DSC_0151
Mwanamuziki Diamond Platinumz akisoma kipeperushi chenye maelezo juu ya ofa mbalimbali za DStv wakati wa utambulisho wa ofa za sikukuu pamoja na kutangazwa kwa balozi huyo wa bidhaa za DSTV. Katikati Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
DSC_0233
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua jambo katika mkutano huo na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo na upande wa kulia ni msanii Diamond Platnumz balozi wa bidhaa za DSTV.
DSC_0159
Meneja mauzo wa DSTV, Bw. Salum Salum akifafanua jambo juu ya ofa hiyo mpya na mahaala wanapopatikana nchini kwa mawakala wote ambapo amewaomba watanzania kuchangamkia ofa ya kuunganishwa haraka huduma bora zaidi za chaneli za kisasa kupitia DSTV.
DSC_0174
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo wa DSTV..
DSC_0176
Mwandishi wa gazeti la Raia Tanzania akiuliza swali juu ya bidhaa za DSTV..
DSC_0171
Mpiga picha wa Magazeti ya Habari leo, Fadhili Akida akiuliza swali katika mkutano huo wa DSTV..
DSC_0185
Ilifika wakati wa zawadi.. Diamond akisoma jina la mwandishi wa habari aliyeshinda zawadi hiyo..
DSC_0190
Diamond Platnumz akimkabidhi mwandishi wa habari, Sangu Joseph king'amuzi alichojishindia katika droo iliyochezeshwa wakati wa mkutano huo.
DSC_0196
Diamond akikabidhi zawadi ya King'amuzi cha DSTV kwa mwandishi wa habari Rajab Musa baada ya kushinda..
DSC_0204
Diamond akikabidhi zawadi ya king'amuzi kwa mwandishi wa habari, Joseph Mchekadone baada ya kushinda..
DSC_0205
Diamond Platnumz akimkabidhi king'amuzi mwanahabari wa ITV, Ester Sangai baada ya kuibuka mshindi..
DSC_0165
Meneja mauzo wa DSTV, Bw. Salum akisisitiza juu ya ofa hiyo ambapo ameeleza kuwa wateja watapa kujionea chaneli mbalimbali zenye mvuto na picha za kuvutia huku bidhaa zake zikiwa ni tofauti kabisa na zingine.
KAWAIDA DSC_0168 Mwanamuiki nyota nchini Tanzania, Nassib Abdul ama Diamond Platnumz akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani). (Picha na Andrew Chale, Modewjiblog). Na Adndrew Chale, Modewji [DAR ES SALAAM-TANZANIA] KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania mapema jana imezindua ofa kabambe za msimu wa siku kuu huku ikimtambulisha rasmi Mwanamuziki Diamond Platnumz kuwa balozi maalum wa bidhaa za kampuni hiyo ikiwemo kifurushi cha DSTV BOMBA chenye chaneli zaidi ya 65 ikiwemo huduma ya vituo kadhaa vya televisheni za hapa nchini. Akimtambulusha rasmi Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Furaha Samalu, amemtambulisha Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa balozi wa king’amuzi hicho na kutaja gharama zake kuwa ni shilingi 23,500/= kwa malipo ya mwezi na king’amuzi chenyewe kinapatikana kwa shilingi 79,000/= na kuwataka wananchi kuchangamkia huduma hiyo muhimu katika msimu huu wa ofa za sikukuu. Meneja masoko huyo ameongeza kuwa, kifurushi hicho kimesambaa nchini mbalimbali barani Afrika hivyo wasanii wa filamu, muziki na wengineo ambao watang’aa kwenye vipindi hivyo watakuwa wakionekana pande mbalimbali barani Afrika na hivyo kuwapatia umaarufu na kuwaongezea soko la kazi zao. DSC_0151 Mwanamuziki Diamond Platinumz akisoma kipeperushi chenye maelezo juu ya ofa mbalimbali za DStv wakati wa utambulisho wa ofa za sikukuu pamoja na kutangazwa kwa balozi huyo wa bidhaa za DSTV. Katikati Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo. DSC_0233 Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua jambo katika mkutano huo na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo na upande wa kulia ni msanii Diamond Platnumz balozi wa bidhaa za DSTV. DSC_0159 Meneja mauzo wa DSTV, Bw. Salum Salum akifafanua jambo juu ya ofa hiyo mpya na mahaala wanapopatikana nchini kwa mawakala wote ambapo amewaomba watanzania kuchangamkia ofa ya kuunganishwa haraka huduma bora zaidi za chaneli za kisasa kupitia DSTV. DSC_0174 Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo wa DSTV.. DSC_0176 Mwandishi wa gazeti la Raia Tanzania akiuliza swali juu ya bidhaa za DSTV.. DSC_0171 Mpiga picha wa Magazeti ya Habari leo, Fadhili Akida akiuliza swali katika mkutano huo wa DSTV.. DSC_0185 Ilifika wakati wa zawadi.. Diamond akisoma jina la mwandishi wa habari aliyeshinda zawadi hiyo.. DSC_0190 Diamond Platnumz akimkabidhi mwandishi wa habari, Sangu Joseph king'amuzi alichojishindia katika droo iliyochezeshwa wakati wa mkutano huo. DSC_0196 Diamond akikabidhi zawadi ya King'amuzi cha DSTV kwa mwandishi wa habari Rajab Musa baada ya kushinda.. DSC_0204 Diamond akikabidhi zawadi ya king'amuzi kwa mwandishi wa habari, Joseph Mchekadone baada ya kushinda.. DSC_0205 Diamond Platnumz akimkabidhi king'amuzi mwanahabari wa ITV, Ester Sangai baada ya kuibuka mshindi.. DSC_0165 Meneja mauzo wa DSTV, Bw. Salum akisisitiza juu ya ofa hiyo ambapo ameeleza kuwa wateja watapa kujionea chaneli mbalimbali zenye mvuto na picha za kuvutia huku bidhaa zake zikiwa ni tofauti kabisa na zingine.

JEFF AACHIA VIDEO YA WIMBO WAKE MPYA WA "MAMA AFRIKA" UNAOTANGAZA UTALII WA TANZANIA

jeff
Mwanamuziki aliyewahi ishi nchini Tanzania na pia mwenye asili ya Congo, Jeff Maximum ambaye anaishi Ughaibuni katika shughuli zake za Muziki katika pozi ambapo kwa sasa ameachia video ya wimbo wake mpya wa "Mama Afrika" ambao wimbo huo unatangaza Utalii wa Tanzania.
Na Mwandishi Wetu
Mwanamuziki anayefanya kazi zake nchini Marekani na Dubai, Jeff Maximum tayari ameshaachia video ya wimbo wake mpya uitwao “Mama Afrika” ambao umetayarishwa Bagamoyo Nchini Tanzania hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Jeff anaweka wazi kuwa, kuwa video hiyo iliyoachiwa Novemba 2 mwaka huu, tayari imeshaanza kuonekana katika vituo mbalimbali vya televisheni Bara la Afrika ikiwemo nchini, pia katika nchi za Nigeria, Afrika Kusini, Kongo, Ghana, Kenya na kwingineko.
Pia video hiyo inaonekana katika vituo vya televisheni vya nchini Uingereza, Dubai, Amerika na kwingineko huku ikitangaza utalii wa Tanzania kwa asilimia kubwa.
Jeff anaweka wazi kuwa, aliamua kuitayarishia video hiyo nchini Tanzania kwa kuwa ni kati ya nchi nyingi anazozipenda zaidi Barani Afrika.
Na kuongeza kuwa, video hiyo imetengenezwa na mwongozaji anayechipukia kutoka Tanzania Hanscana (Wanene Films), huku audio yake ikiwa imetayarishwa katika studio yake iliyopo nchini Dubai (One Vision Records).
Tazama video hiyo hapa chini.
Attachments area Preview YouTube video Jeff Maximum - Mama Africa (Official Music Video)

VOTE SHERIA NGOWI FOR BEST EAST AFRICAN FASHION DESIGNER OF THE YEAR

IMG-20151104-WA0027
To cast your vote click this link www.abryanzstyleandfashionawards.com/vote

Thursday, 5 November 2015

BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUAPISHWA KWA RAIS MPYA WA AWAMU YA TANO,JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI PAMOJA NA MAKAMU WA RAIS BI. SAMIA SULUHU HASSAN,LEO SHEREHE ZILIZOFANYIKA KATIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM,JAKAYA NAYE AWAAGA WANANCHI KWA FURAHA ...

 Rais mpya wa awamu ya tano Dk.John Pombe Magufuli, akionyesha ngao pamoja na Mkuki mara baada ya kuapishwa


 Rais Mpya wa Tanzania awamu ya Tano DK John Pombe Magufuli akikagua Gwaride baada ya kula kiapo cha kulitumikia taifa.


 Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu Hassan, akisubiri kula kiapo 


 Rais wa awamu ya tano DK John Pombe Magufuli akisaini mara baada ya kula kiapo cha kulitumikia taifa wanaoshuhudia ni Jaji Mkuu Othuman Chende pamoja na ,Katibu Mkuu kiongozi Balozi. Ombeni Sefue, na kushoto mwishoni ni Rais Mstaafu anayemaliza muda wake Dk. Jakaya Kikwete akionyesha nyuso ya furaha 


 Rais mpya wa awamu ya tano DK John Pmbe Magufuli akiapa 


 Makamu wa Rais awamu ya Tano Bi Samia Suluhu Hassan akiapishwa na Jaji Mkuu Othman Chande



 Rais Mpya wa Tanzania awamu yaTano DK John Pombe Magufuli akikagua Gwaride baada ya kula kiapo cha kulitumikia taifa.


 Rais wa awamu ya nne, anayemaliza muda wake wa uongozi akiwa na makamu wake wa Urais Mohamed Ghalib Bilal, wakiwapungia wananchi mikono ya kwa heri baada ya kuwatumikia kwa miaka 10.


 Rais Mstaafu DK Jakaya Kikwete akifurahia jambo pamoja na Makamu wake DK Bilal
 Rais Mstaafu DK Jakaya Kikwete akiwapungia wananchi mkono kabla ya kumkabidhi kijiti rais wa awamu ya tano Dk John Pombe Magufuli



 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube