BREAKING

Friday, 26 July 2019

KATIKA MAKOCHA 100 WANAOOMBA KUINOA TAIFA STARS HAKUNA KOCHA HATA MMOJA MZAWA, JE NI UOGA AMA MASILAHI KIDUCHU?



Wilfredy Kidao, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa mpaka sasa tayari wamepokea maombi ya makocha 100 wanaotaka nafasi ya kuinoa timu ya Taifa.

Katika orodha hiyo hakuna hata jina moja la mzawa ambaye ameomba kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania baada ya 
Kocha Mkuu Emmanuel Ammunike  kusitishiwa mkataba wake baada ya kuboronga kwenye michuano ya Afcon 2019 nchini Misri.

 "Tumepokea maombi ya makocha zaidi ya 100 wakitaka kazi ya kuifundisha timu ya Taifa, maombi ni mengi na tunayafanyia kazi.

 "Kwa sasa nguvu zeru tunazielekeza kwenye michuano ya Chan na kwenye maombi hayo 100 hakuna mzawa hata mmoja," amesema.

TAHA WATAKIWA KUFANYA TAFITI ZA KUWAKOMBOA WAKULIMA NCHINI TANZANIA

 Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akiongea na wakulima na wageni waalikwa wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA) iliyofanyika katika mjini Morogoro. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro. Meneja miradi Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA) Bi. Elianchea Shanga akiongea na wakulima na wageni waalikwa wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa taasisi ya TAHA iliyofanyika katika mjini humo. Wakulima wa Mboga Mboga akinyoosha mikono kujitambulisha.
 Meneja mradi Naimana akizungumza wakati akitambulisha mradi huo huku wakulima na wageni waalikwa wakifuatilia.
 Mmiliki wa shamba la nyanya la kisasa akiongea machache.
Meneja miradi TAHA Bi. Elianchea Shanga akiwatambulisha mabwana shamba wanaosaidia kufundisha wakulima.
 Wafanyakazi wa TAHA wakitoa elimu kwa wakulima.
 Kilima cha kisasa cha nyanya.
 Mgeni rasmi Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akipewa maelezo juu ya kilimo cha kisasa cha nyanya kutoka kwa Meneja mradi huo Naimana.
 Vingozi wa kijiji wakiwa na Mgeni rasmi.
Wakulima wakiwa na mgeni rasmi.

CHATO WAITAMANI DHAHABU YA KIJANI ILIYOPO WILAYA YA MUFINDI

Mkuu wa msafara huo Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo jinsi gani wanavyoweza kuzalisha miche ya miti ambayo inakuwa kwa muda mfupi sana
Mkuu wa msafara huo Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri akiwa na baadhi ya viongozi wa kutoka mkoa wa Geita walipokuwa kwenye ziara ya kutembelea shamba la miti ya kupandwa la Sao Hill lililopo mkoani Iringa
Moja kati ya maeneo ambayo yanatumika kuzalia miche ya miti

Uchumi wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa umetajwa kutegemea zao la miti katika kukuza uchumi na kuongeza pato la taifa tofauti ya wilaya nyingine kama Chato ambao wamekuwa wakitegemea ufugaji,uchimbaji wa dhahabu,uvuvi na kilimo

Hiyo imebainika wakati wa ziara ya baadhi ya viongozi wa wilaya ya Chato,Mkoa wa Geita na viongozi wa vijiji vinavyolizunguka Shamba la Miti la Biharamulo lililopo mkoani Geita baada ya kutembelea Shamba la Miti Sao Hill linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji katika shamba hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa msafara huo Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Eng. Mtemi Msafiri alisema kuwa kwa mara ya kwanza amejifunza faida kubwa inayotokana na zao la miti katika kukuza uchumi wa nchi na kujionea jinsi gani wananchi wa wilaya ya Mufindi wanavyonufaika na dhahabu ya kijani

“Leo ndio nimegundua kuwa zao la miti ni dhahabu ya kijani kwa namna inavyosaidia kukuza uchumi tofauti na walivyodhani hapo awali kwa namna ambavyo wao wamekuwa wakitegemea kuchimba dhahabu ambazo hazionekani tofauti na zao la miti ambavyo limekuwa linaonekana” alisema Eng Msafiri



Eng Msafiri alisema kuwa shamba la Miti Sao Hill ndilo shamba kubwa zaidi kati ya mashamba yote ya Serikali na ni nguzo ya maendeleo, na mkombozi wa mazingira wa Wilaya ya Mufindi na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini nasi tumeona ni vema tujifunze kutoka kwa wenzetu.

“Tumejionea jinsi shamba hili lilivyo kuwa dhahabu ya ukuaji wa sekta ya viwanda vidogo na vikubwa vya uchakataji wa mbao,  linavyosaidia kuongezeka kwa ari ya upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira kwa wananchi wanaozunguka shamba na wananchi wa Wilaya za Mufindi, Kilombero na jamii jirani wamekuwa wakipatiwa gawio la asilimia 5 ya mrahaba kila mwaka”alisema Eng. Msafiri.

Eng. Msafiri anasema ziara hiyo imeweza kuwafumbua macho na kuona jinsi gani shamba hilo lilivyo toa  fursa ya ajira zinazotokana na kazi za msimu za mashambani na viwanda tegemezi vya mazao ya misitu, fursa za uwekezaji,  na ufugaji wa nyuki unaotokana na na uwepo wa misitu ya asili na ile  ya kupandwa pamoja na vyanzo mbalimbali vya maji.

Awali akitoa ufafanuzi wa shamba la Sao Hill mkurugenzi wa Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo alisema shamba hilo ni miongoni mwa mashamba 23 ya miti ya kupandwa ya serikali ambayo yanasimamiwa na wizara ya maliasili na utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).


“Shamba la Sao Hill lililopo hapa Mufindi lilianzishwa kwa majaribio mnamo mwaka 1939 hadi mwaka 1951 na upandaji kwa kiasi kikubwa ulianza rasmi mwaka 1960  hadi 1980 na shamba hilo linaukubwa wa hekta 135,903 ambazo zimehifadhiwa kwa ajili ya upandaji wa miti  na uhifadhi wa mazingira” alisema Mbwambo



Mbwambo alisema shamba hilo limehamasisha kwa kiwango kikubwa upandaji wa miti kwa jamii inayolizunguka ambapo pia hutoa msaada wa mafunzo na miche ya miti kwa ajili ya kupandwa ili kupambana na uharibifu mkubwa wa misitu unaoendelea nchini.

 “Takribani hekta 372,000 ya misitu inapotea kila mwaka na ili misitu hii isiweze kupotea tunatakiwa tuendelee kupanda angalau hekta 185,000 kwa mwaka kwa hapa Mufundi na Ukanda wote wa Nyanda za Juuu Kusini hamasa ya kupanda miti imekuwa kubwa kutokana na thamani inayoonekana Sao Hill kiasi kwamba imefikia hatua sasa Serikali inawaelimisha watu waache baadhi ya maeneo kwa ajili ya kilimo cha mazao mengine ya chakula na biashara” Alisema Mbwambo.

Kwa upande wake meneja wa Shamba la Miti la Biharamulo Thadeus Shirima alisema kupitia ziara hiyo ya siku mbili anaamini sasa kutakuwa na uelewa wa pamoja wa umuhimu wa shamba hilo katika kuleta maendeleo katika Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla.

Thadeus alitoa shukurani kwa Mkuu wa Wilaya ya Chato, kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Chato na Mkoa wa Geita, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Bukombe kwa msaada na maelekezo yao muhimu yaliyosaidia kuhakikisha uanzishwaji wa Shamba la Miti la Biharamulo unafanikiwa kwa kufanikisha kuwaondoa wananchi waliovamia msitu wa hifadhi Biharamulo ili kuanzishwa shamba hilo la miti.

Ziara hiyo ina wajumbe 45 ambao vingozi wa Wilaya na Mkoa wa Geita, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mkurugenzi wa halmashauri,Wenyeviti wa Vijiji, Madiwani, Maafisa tarafa, Jeshi la Zima moto na uokoaji, Mwenyekiti na katibu wa Chama cha Mapinduzi, baadhi ya Wakuu wa Vitengo na Idara za Halmashauri ya Wilaya, baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ,  Katibu Tawala wa Wilaya na Wataalamu kutoka Shamba la miti Biharamulo.

Tuesday, 11 June 2019

POLEPOLE AWAFUNDA MAKATIBU WA ITIKADI NA UENEZI MKOA WA IRINGA



Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole akitoa semina kwa makatibu wa idara ya Itikadi na uenezi wa mkoa wa Iringa iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo

Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa (MNEC) Salim Asas akiwahutubia makatibu wa idara ya Itikadi na uenezi wa mkoa wa Iringa walikuwa wakipewa semina na Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole juu ya Idara hiyo,semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
 Baadhi ya makatibu wa Idara ya Itikadi,siasa na uenezi mkoa wa Iringa wakiwa makini kumsikiza Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole alipokuwa anawafunda.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole Amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia chama hicho kutokuwa chanzo cha migogoro na majungu bali wawe suluhisho kwa kuwa lengo la chama ni kusimamia serikali na kuwaletea watanzania Maendeleo.

ameyasema hayo kwenye semina ya kuwafunda katibu wa Idtikadi na uenzi wa ngazi zote mkoani Iringa, Polepole amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wamekuwa chanzo cha migogoro hata kufanya kurudisha nyuma maendeleo ya chama.

Amesema kuwa chama hicho kimejengwa kwenye misingi bora kwa lengo la kutumikia wananchi na kusikiliza watu pamoja na kujua shida zao lakini kuna baadhi yao wanaleta majungu wao kwa wao jambo linalofanya kutowavumilia.

“Sasa hivi hii ni ccm mpya chini ya mwenyekiti Dr John Pombe Magufuli na hana utani anataka kazi tu na wale ambao wanaona wameshindwa watupishe maana unapoacha sumu ndani si ya siku itakudhuru tunapogombana wanaoumia ni watanzania waliotupa dhamana ya kusimamia serikali”Alisema Polepole

Polepole ameongeza kuwa kwasasa mlango uko wazi endapo mtu anaona atashindwa kupelekana na kasi ya CCM mpya chini ya mwenyekiti wao John Pombe Magufuli ni vyema akapisha na kuacha wanaojua kufanya kazi.
 
Hata hivyo Polepole amewataka viongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa huku akimtaka katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza kuunganishi vizuri na kuendelea kuwatumikia wananchi vizuri kwa kueleza mambo mazuri yanayofanywa na serikalia ya CCM.

Vile vile Polepole amewasifu viongozi katika ngazi zote kwasababu wameibadilisha ccm na wananchi wameelewa dhamira ya Chama katika kuisimamia serikali.

Aidha Polepole alisema kuwa chama cha mapinduzi kikifanya vibaya kwa wananchi ujue kuwa idara ya Itikadi na uenezi haijafanya kazi yake ipasavyo,hivyo ni lazima kila kiongozi awajibike ipasavyo ili kutimiza malengo ya chama.

“Tunatakiwa kushughulikia matatizo ya wananchi kwa kuwapa mafunzo mbalimbali viongozi wa ngazi za chini ili kueneza vilivyo cha hicho ambacho kipo madarakani muda mrefu sasa” alisema Polepole

Polepole aliwaambia viongozi hao kuwa uongozi ni kujitolea na sio kutegemea kupata maslai furani kwenye chama wakati unagombea nafasi mbalimbali lazima uwe unasehemu ya kuingiza kipato kingine na usitegemee kuvuna kutoka kwenye chama.

Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa (MNEC) Salim Asas alimtaka katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza kuratibu namna nyingine tena ya kuwawezesha makatibu hao kuanzia ngazi ya chini hadi juu kupata fedha za kufanyia kazi mafunzo walipata kutoka kwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole.

“Ramadhani Baraza nakuomba uratibu zoezi hilo ili tuone jinsi ya kuwasaidia makatibu hao ili waweze kukieneza vilivyo cha chetu kwa wananchi wote huko waliko” alisema Asas

Naye katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza alisema ameyapokea maagizo yote na atayafanyia kazi ili idara hiyo mkoa wa Iringa iwe mfano kwa mikoa mingine hapa nchini.

BWALYA SIMBA HACHOMOI.....


Mshambuliaji namba moja wa Nkana ya Zambia, Walter Bwalya ameweka wazi kwamba amepokea ofa ya Simba na Sportif Sfaxien ya Tunisia.

Mchezaji huyo mwenye asili ya DR Congo amesema kwamba bado wako kwenye majadiliano ambayo yanakwenda vizuri na huenda wakakamilishana muda wowote.

Friday, 10 May 2019

WAZIRI BITEKO AZINDUA SOKO KUU LA MADINI MWANZA

Waziri wa Madini, Doto Biteko (pichani) amefanya uzinduzi wa Soko Kuu la Madini Mwanza na kutumia fursa hiyo kuwahimiza wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kutumia soko hilo kuuzia madini yao na kuachana na tabia ya utoroshaji wa madini.

Uzinduzi wa soko hilo unganishi Kanda ya Ziwa umefanyika Mei 08, 2019 katika jengo la Rock City Mall ambapo Biteko amebainisha kwamba uanzishwaji wa masoko ya madini nchini umesaidia ongezeko la kiwango cha uuzaji madini tofauti na hapo awali ambapo yalikuwa yakiuzwa kiholela na hivyo kuikosesha Serikali mapato.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akitoa salamu za tume kwenye uzinduzi huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akitoa taarifa ya hali ya uanzishwaji masoko ya madini nchini ambapo amebainisha kwamba zaidi ya mikoa 10 tayari imeanzisha masoko hayo.
Mfanyabiashara wa madini, Kakono Kaniki akitoa salamu kwa niaba ya wafanyabiashara wa madini mkoani Mwanza.

Mongella ajivunia Soko Kuu la Madini Mwanza "tunataka nchi ifaidike"

DC KASESELA: MARUFUKU KUFANYA BIASHARA IRINGA KAMA HULIPI KODI AU HUNA KITAMBULISHO CHA MACHINGA

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizunguza na wafanyabiashara wa bidha za kusindika walikuwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali
 Wafanyabiashara wa bidha za kusindika wakiwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali na wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa bidhaa za kusindika

 NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Wafanyabiashara wa wilaya ya Iringa wametakiwa kufanya biashara wakiwa wamelipa kodi au wanatakiwa kuwa na kitambulisho cha wafanyabishara wadogo wadogo maarufu kama kitambulisho cha machinga.

Akizungumza na wajasiliamali waliokuwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa,mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema ni marufuku kwa sasa kufanya biashara yoyote wilaya ya Iringa bila kulipa kodi na zile ambazo hazijafikia hatua kodi zitalipa tozo

“Sasa tunaanza kufanya mchakato wa kuchunguza kujua wafanyabiashara wangapi wanafanya kazi hizo bila kulipa kodi na tutawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za nchi zinavyosema” alisema Kasesela

Kasesela aliwataka wafanyabiashara wadogowadogo wote wa wilaya ya Iringa kuhakikisha wanapata kitambulisho cha kwa shilling elfu ishirini ambacho kinatamruhusu kufanya biashara sehemu yoyote hapa nchini kwa mujibu wa Rais

“Jamani ili ufanye biashara kwa uhuru katika wilaya ya Iringa ni lazima uwe na kitambusho cha wafanyabisahara wadogo au uwe umelipia leseni kutoka katika mamlaka husika la sivyo huwezi kufanya biashara hiyo wilaya ya Iringa” alisema Kasesela

Kasesela aliwataka wananchi wote wanaopenda kufanya biashara kuhakikisha wanafanyabiashara kwa kufuata taratibu zilizowekwa na nchi ili wasipate usumbufu wowote ule kutoka kwa mamlaka za wilaya ya Iringa.

“Jamani wananchi wa Iringa changamkieni kuchukua vitambulisho vya wafanyabishara wadogo wadogo ili kufanya biashara zenu mkiwa na uhuru wa kutosha ila mkikahidi mkono wa sheria utawahusu” alisema Kasesela

Aidha Kasesela aliwashauri wafanyabishara ya bidhaa za kusindika kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kufuata kanuni za kisheria kwa kuhakikisha wanalipa kodi kama inavyostahili.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo walimuadi mkuu wa wilaya hiyo kuwa watahamasishana kuhakikisha wote wanakuwa na vitambulisho hivyo ili wafanye biashara kwa uhuru na haki.

“Mkuu tunakuhakikishia kuwa tutafanyabiashara huku tukiwa tumevaa vitambulisho hivi kwa kuwa Rais wetu katupa uhuru wa kufanya biashara zetu mahali popote pale bora mradi tuwe na vitambulisho hivyo” walisema wafanyabiashara hao

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube