BREAKING

Thursday, 14 March 2019

ZANA COULIBALY BEKI WA SIMBA ASIYEISHA VITUKO....


SIMBA HAITANII!! YAAPA JUMAMOSI ITAKUWA VITA YA KISASI....


Timu ya Simba itakuwa uwanjani kuvaana na AS Vita kwenye mchezo mgumu wa kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika siku ya Jumamosi katika Dimba la kisasa la Taifa. 

Kama Simba watashinda mechi hii basi ni asilimia 100 watakuwa wamefuzu kwa lakini pia ni heshima kubwa kwa Tanzania na ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa kuwa ndiyo timu pekee iliyobaki.

Kutokana na hali hiyo ni vyema sasa tukabadilika kidogo na kuziunga mkono timu zetu zinazoshiriki
hatua hiyo na hii itakuwa heshima ya pekee kwenye soka la nchi hii. 

Kufuzu kwa Simba ni faida pia kwa Yanga kwa kuwa timu hizo ndiyo kubwa ambazo zinashiriki michuano ya kimataifa mara kwa mara michuano ya kimataifa.

Mashabiki wa Yanga Jumamosi wanatakiwa kuingia uwanjani kwa ajili ya kuiunga mkono Simba ili kuliletea taifa sifa kubwa. 

Kwenda na kuishangilia Vita haliwezi kuwa jambo zuri kwa
kuwa wote ni Watanzania na tunatakiwa kuhakikisha tunaweka uzalendo mbele zaidi ya mambo mengine yote kama ambavyo yamekuwa yakifanya mataifa mengine ambayo yameendelea kisoka.

UWANJA WA SOKA WA KISASA ULIVYOINUA DODOMA ....


Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wataalamu wa Tanzania na Misri wanaoshughulikia ujenzi wa uwanja wa michezo katika Jiji la Dodoma, unaotarajiwa kujengwa kwa msaada wa Mfalme wa Morocco, Mtukufu Mohammed VI.

Balozi wa Morocco hapa nchini aliyeongoza ujumbe wa wataalamu kutoka Morocco Abdelilah Benryane amesema pamoja na kuzungumzia uhusiano mzuri wa Tanzania na Morocoo wamejadiliana kuhusu utekelezaji wa miradi iliyokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco hapa nchini mwaka 2016 ikiwemo ujenzi wa Msikiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Jijini DSM na kuanza kwa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu Jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amesema uwanja huo utajengwa eneo la Nanenane kando ya barabara ya Dodoma – Morogoro, utajengwa kwa mfano wa mlima Kilimanjaro na utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji kati ya 85,000 na 100,005.

Wednesday, 6 March 2019

TANZANIA YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA KIMATAIFATA


Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (Kulia) na Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo Grace Mgaya (kushoto) wakikabidhi seti ya DStv kwa mkuu wa shule ya sekondari St Mary Goretti Sr. Lucrecia Njau na mshindi wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle wakati wa mahafali ya kidato cha sita katika shule ya St Mary Goretti hivi karibuni. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg wakati shule yake imepata cheti na zawadi ya kufungiwa huduma ya DStv.




Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana akimkabidhi mshindi wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle cheti cha ushindi wakati wa mahafali ya kidato cha sita katika shule ya St Mary Goretti hivi karibuni. Kulia ni Afisa Uhusiano  wa MultiChoice Tanzania. Grace Mgaya. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg. 
 Mkuu wa shule ya  St Mary Goretti Sr. Lucrecia Njau akifurahi baada ya kupokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana mara baada ya shule hiyo kufanikiwa kutoa mshindi wa jumla wa wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg
 
 Mshindi wa Jumla wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle akikabidhiwa kikombe cha ushindi na Mkuu wa shule ya St Mary Goretti Sr. Lucrecia Njau baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa jumla wa wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg.
 

Mshindi wa Jumla wa tuzo za kimataifa za DStv Eutelsat Star Awards Pricilla Marealle akifurahi na wazazi wake Calvin Marealle  na Jamila Marealle mara baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi. Pricilla aliibuka mshindi wa kwanza katika tuzo hizo na kuwashinda wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. Mbali na kutunukiwa cheti maalum, Pricilla atapata fursa ya kutembelea kituo cha Anga cha Afrika Kusini na makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg.



Kwa mara nyingine tena Tanzania imeibuka kinara  katika tuzo za kimataifa za wanafunzi zijulikanazo kama DStv Eutelsat Star Awards ambapo mwanafunzi Priscilla Marealle kutoka shule ya sekondari ya St. Mary Goreti mkoani Kilimanjaro ameweza kuipeperusha bendera ya Tanzania kwa kunyakua nafasi ya kwanza katika kipengele cha uchoraji bango  ikiwa ni baada ya mchuano mkali baina ya mamia ya wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. 
Kwa upande wa uandishi wa insha kijana Tanaka Chonyera kutoka  nchini Botswana aliweza kujinyakulia ushindi wa kwanza.

Tuzo hizi ambazo huhusisha uandishi wa insha maalum au kuandaa bango yenye ujumbe kuhusiana na elimu ya anga hususan Setelait ni za wazi kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wenye umri kati ya miaka 14 – 19 kote barani Afrika ambapo kampuni ya MultiChoice inaendesha shughuli zake.

Katika msimu huu wa nane, washindani walitakiwa kuandika insha au kubuni bango litakaloelezea licha ya Satelait kutumika katika shughuli mbalimbali, ni namna gani zitaweza kutumika zaidi ili kuleta maendeleo chanya ulimwenguni.

Priscilla ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha sita wa mchepuo wa Sayansi katika shule ya Mtakatifu Maria Goreti alitangazwa rasmi kuwa mshindi mjini Accra nchini Ghana ambapo ndipo jopo la watahini liliongozwa na Paolo Nespoli, mwanaanga nguli kutoka European Space Agency (ESA) lilikaa kupitia kazi kutoka kwa wanafunzi walioshinda katika nchi mbalimbali. 

Akiongea baada ya kukabidhiwa cheti cha uthibitisho wa ushindi wakati wa mahafali ya kidato cha sita ya shule ya Mtakatifu Mary Goreti iliyopo Moshi Kilimanjaro, Priscilla amesema amefurahi sana kwa ushindi huo mkubwa ambao umemletea yeye, shule yake na taifa zima kwa ujumla sifa kubwa. “Nimefurahi sana kupokea taarifa hizi nzuri. Naamini ushindi wangu utakuwa ni chachu kubwa kwa wanafunzi wenzangu kote nchini kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika tuzo kama hizi na mashindano mengine ya kitaaluma ya ndani na nje ya nchi, na kusisitiza  kuwa Ndoto huanza kufanya kazi pale unapojiamini” alisema Priscilla.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo ya Mtakatifu Maria Goreti Sister Lucresia Njau alisema kuwa anaishukuru sana kampuni ya MultiChoice Tanzania kwa kuwapatia nafasi ya kushiriki katika Mashindano hayo na hatimaye kuweza kunyakua tuzo hiyo kupitia mwanafunzi wao Priscilla.

“Huyu kijana ana jitahidi sana katika chochote kile anachokifanya, iwe ni darasani au hata katika majukumu mengine nje ya darasani. Ni msikivu mtiifu lakini zaidi ya yote ni mbunifu sana. Naamini haya ndiyo yaliyomfanya aweze kushinda tuzo hizi” alisema Sr. Lucrecia Njau.

Naye, Mkuu wa Uhusiano MultiChoice Tanzania Johnson Mshana alisema,” Huu ni msimu wa tatu mfululizo kwa Tanzania kuendelea kung’ara katika tuzo hizi za DStv Star Awards. Tulianza kupeperusha bendera yetu na kijana Davids Bwana msimu wa sita baada ya kushika nafasi ya pili Afrika katika kipengele cha uandishi wa insha, kisha tukaibuka kidedea baada ya kupokea taarifa za ushindi wa kwanza wa kijana Taheer Rashid katika msimu wa saba mwaka jana na leo hii tunayofuraha kubwa kuona kuwa tumeendeleza wimbi la ushindi.”

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya Pricilla kutangazwa kuwa mshindi, walimu na wazazi wa mwanafunzi huyo wa kidato cha sita mwenye umri wa miaka 19, wamesema kuwa wanamfahamu vyoma Pricilla kuwa ni kijana mwenye kupenda kujibidisha sana katika masuala ya kitaaluma na kijamii hivyo ushindi wake ni kitu kilichotarajiwa na kwamba wanaamini kuwa anastahili ushindi huo.
Pamoja na kupata cheti maalum cha ushindi, Pricilla atapata fursa (Yeye na Mzazi au mlezi) ya kutembelea kitua cha Anga cha Afrika Kusini na pia kutembelea makao makuu ya MultiChoice jijini Johannesburg kama mgeni maalum wa DStv  huku shule aliyotoka ikipata zawadi ya cheti pamoja na kufungiwa huduma ya DStv.

Tuesday, 26 February 2019

BENKI YA STANDARD CHARTERED KUWEZESHA HUDUMA ZA KIBENKI ZAIDI YA 70 KIDIGITALI

 Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dk. Bernard Kibesse,akihutubia wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa programu ya Standard Chartered Tanzania Digital App.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani akihutubia wageni waalikwa katika hafla ya uzi nduzi wa programu ya Standard Chartered Tanzania Digital App uliofanyika katika hoteli ya Hyatt.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bernard Kibesse (Kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani,Balozi wa Programu mpya ilizozinduliwa,Vanessa Mdee na Mkuu wa huduma za kibenki wa wateja wadogo wa Benki hiyo, Ajmair Riaz ,wakionyesha miondoko ya UNSTOPABLE wakati wa hafla ya uzinduzi

REPSSI YAENDELEA NA KAMPENI KUTOKOMEZA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI

Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala akiongea na vijana kijiweni kuhusu athali za mimbaMkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala akiongea na vijana kijiweni kuhusu athali za mimba
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala 

Mwandishi wetu, Pwani.

Shirika linalojihusisha na masuala ya kijamii na kisaikolojia kwa watoto (REPPSI) limeendelea kufanya kampeni ya kutokomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni mkoani Pwani.

Kampeni hiyo inafanyika ili kuhakikisha watoto wa kike wanatimiza ndoto zao za kielimu ili kushiriki katika mkakati wa Serikali wa Tanzania ya viwanda.

Akizungumza na wakazi wa Kibiti Mkoani Pwani, Mkurugenzi Mkazi wa REPSI Tanzania, Edwick Mapalala alisema tatizo la mimba na ndoa za utotoni bado kubwa na kwamba linahitaji jitihada za pamoja kupambana nalo.

“Mfano ni hizi kampeni za kutoa elimu na kuihamasisha jamii kumthamini mtoto wa kike zinasaidia kwa hiyo kama tutaendelea nazo jamii itaelewa, watoto watatimiza ndoto zao,” alisema.

Mapalala alisema katika kampeni hizo wanazoshirikiana na Shirika la Pasada linalojihusisha na masuala ya Ukimwi chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Pwani, vijana hasa madereva bodaboda wamefikishiwa elimu kuhusu thamani ya mtoto wa kike.

Baadhi ya viongozi wa vijiji na kata walikiri kuwa ndoa za utotoni ni changamoto kubwa lakini wanaendelea kupambana nayo.

Mratibu wa Elimu Kata ya Salala, Wilayani Kibiti Erasmus Assenga alisema kwa mwaka huu tu wanafunzi wawili wa Sekondari katika kata hiyo wameacha masomo kwa mimba.

“Kwa hiyo kampeni hii ni muhimu kwa sababu watoto wa kike wenyewe wanafikishiwa elimu, jamii hasa wanaume wanaelezwa na wanajua umuhimu wa kuwathamini,” alisisitiza.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Pasada Ester Mbwana alisema anaamini kuwa baada ya kampeni hizo kutakuwa na mafanikio makubwa kwa sababu, jamii inaelewa na imekubali kusaidia katika ulinzi wa mtoto.

Wednesday, 6 February 2019

TRC YAWAPA SHAVU WASANII KUTEMBELEA MRADI WA RELI YA KISASA YA STARDARD GAUGE

Kiongozi wa Wasanii, Steve Nyerere akuongea na wanahabari kuwaelezea madhumuni ya Safari ya wasanii wote katika wote Februari 7, 2019 kutembelea mradi wa Reli ya Kisasa ya reli ya Kisasa ya Standard Gauge inayoanzia Dar es Salaam na kuelekea Morogoro. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Kaimu Mtendaji Mkuu wa shirika la reli nchini (TRC) Jamila Mbarouk (kulia) akiongea na wanahabari jinsi walivyoweza kudhamini wasanii hao kutembelea Mradi wa mradi wa Reli ya Kisasa ya reli ya kisasa ya Standard Gauge inayoanzia Dar es Salaam na kuelekea Morogoro ambapo amesema kuwa wametoa nafasi hiyo ili wasanii wakienda, warudi na watoe ushuhuda wa kweli kwa wananchi maana wao ni kioo cha jamii.
Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka ambaye ni mwakilishi wa wamiliki na wasanii wa bendi za muziki wa Dance akitoa machache mbele ya wanahabari.

Msanii wa Muziki wa Taarabu Khadija Kopa akitoa msisitizo wa wasanii kuendelea kumuunga mkono rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutangaza yale mazuri ambayo amekuwa akiyafanya katika kusukuma kurudumu la maendeleo Tanzania.

 *Wasanii wapewa fursa adhim kutembelea mradi wa standard garge Na Khadija Seif, Globu ya Jamii. Shirika la reli nchini (TRC) limetoa nafasi kwa wasanii kutembelea mradi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge ili kujionea unavyoendelea. Mradi huo wa reli ya Kisasa ya Standard Gauge umeanzia jijini Dar es Salaam na kuelekea Morogoro utarahishisha usafiri wa abiria na mizigo, pia inatarajia kukuza biashara kati ya Tanzania na nchi Jirani kama vile Burundi, Rwanda na DRC kwa kuwa baadaye itaendelezwa kwenda hadi nchi zote zilizoko mpakani mwa Tanzania. 

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mtendaji Mkuu wa shirika la reli nchini (TRC) Jamila Mbarouk amesema ni fursa adhimu kwa wasanii pamoja na waandishi wa habari kwa pamoja kupanda treni hiyo kwa lengo la kuangalia mradi huo uliweza kujengwa kwa awamu mbali mbali. Mbarouk amesema Safari hiyo itasaidia kutangaza utalii uliopo ndani hasa kuwepo kwa treni hiyo ya umeme ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo ya tani elfu 10 huku iikiwa na spidi ya kilomita 160 kwa saa. "Shirika la reli (TRC) limewapa kipaumbele wasanii, wachoraji, wacheza mpira, Washehereshaji (MC), Waimbaji watakuwa mabalozi wazuri katika kuutangazia umma treni hiyo kukagua Standard Garge mpya itakayotoka Dar es salaam hadi Morogoro" alisema Mbarouk.

 Aidha ameeleza treni hiyo imeitengeneza kwa pesa za watanzania kutokana na kodi zilizokusanywa. Mbarouk ametoa wito kwa wananchi na wafanyabiashara kulipa kodi ili iweze kusaidia uchumi wa Tanzania maana bila kodi hakuna maendeleo. Kwa upande wake Msanii wa filamu nchini Steve Nyerere amepongeza uongozi wa Shirika la Reli (TRC) kwa kuwapa fursa wasanii na kutambua mchango wao katika jamii. "Mkuu wa mkoa Paul Makonda anakaribisha kwa wote wanaohitaji mikopo aliyohaidi wakati wa Mkutano wa wasanii wote nchini kuweza kupata mkopo huo utakaowezesha kufanya kazi kwa weledi mzuri ili kukuza tasnia zote nchini." alisema Nyerere. 

 Ameongeza kuwa ni vyema wasanii kuendelea kutangaza mema yote yanayofanywa na rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo Watanzania kwa kuwa wao ni vioo vya jamii na wananguvu kweli kuleta mabadiriko.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube