BREAKING

Wednesday, 6 December 2017

MHANDISI KAMWELWE ATEMBELEA MRADI WA UPANUZI WA MFUMO WA UZALISHAJI NA UGAWAJI MAJI CHALINZE UNAOTEKELEZWA NA SERIKALI KUPITIA DAWASA


WAZIRI WA Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi Mradi wa maji awamu ya tatu ya upanuzi wa chanzo na mtandao wa maji wa Chalinze mkoani Pwani leo Desemba 6, 2017.

Mradi huo unaotekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, (DAWASA), upanuzi wa chanzo cha maji, ujenzi wa matenki na ulazaji wa mabomba, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji pamoja na ujenzi wa Ofisi mpya za Mradi.
“Mradi huu unahusisha  upanuzi wa mtambo wa kusafishia maji wa Chalinze ambao chanzo chake ni Mto Wami na lengo ni kuongeza uzalishaji kufikia mita za ujazo Elfu Tisa (9000) kwa saa kutoka mita za ujazo Mia Tano (500) kwa saa.” Amefafanua Mhandisi Kamwelwe.
Akifafanua zaidi Mhandisi Kamwelwe amesema, Mradi pia unahusisha ujenzi wa Matrenki 19, ulazaji wa mabomba ya ukubwa tofauti wenye urefu wa kilomita 1,022, ujenzi wa vizimba vya kuchotea maji 351 katika  vijiji na vitongoji vya Halmashauri za Chalinze na Bagamoyo Mkoani Pwani.
“Mradi huu ni Mkubwa na unahusisha pia baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Tanga na Morogoro katika wilaya za Handeni na Ngerengere.” Ameongeza Waziri huyo.
Aidha Mheshimiwa Waziri, alisema Wananchi wa maeneo yatakayofaidika na Mradi huo ambao ni Mkubwa ni pamoja na wakazi wa Manga hadi Tengwe katika Mkoa wa Tanga, mji na vitongoji vya Chalinze, na baadhio ya maeneo ya Bagamoyo na Kibaha Mkoani Pwani, wakazi wa maeneo ya Kizuka A na B, Tukamisasa, Lulenge, Visakazi hadi Bwawani  pamoja na Sangasanga A na B Mkoani Morogoro.
Maeneo mengine yatakayojengwa matenki ni pamoja na Pera, Pingo, Bwilingu, Msoga, Diozile, Lugoba, Mindutulieni, Saleni, Mazizi, Msata, Kihangaiko, Kilemera, Hondogo, Miono North 3, Kimange, Rupungwi na Manga.
Kati ya matenki hayo 19 mojawapo ni tenki kuu la Mazizi lenye uwezo wa kuhifadhi lita Milioni 2, kukamilika kwa ujenzi wa tenki hiulo kutafanya kuwa tenki kubwa zaidi kuliko yote Mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa Mhandisi Kmwelwe, Mradi utrakapokamilika utagharimu dola za KImarekani Milioni 41.36 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim yta nchini humo. Hata hivyo Waziri ameonyesha kukerwa kwake na kusuasua kwa mkandarasi kumalizia kazi hiyo kwa muda uliopangwa na kwamba kama asingefuata ushauri wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Wataalamu wa Wizara yake, basi leo Desemba 6, 2017 ilikuwa siku ya kuvunja mkataba wa Mkandarasi huyo. "Hata hivyo Mkandarasi baada ya kuahidi kukamilisha mradi Februari 8, 2017, tumeona tumuache hadi muda huo, lakini akishindwa hatuna njia nyingine ni kuvunja mkataba na kutafuta Mkandarasi mwingine." Alionya Waziri Kamwele wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwenye chanzo cha maji Mto Wami.
Kwa upande wake Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete, amemshukuru Waziri Kamwele na Serikali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa nia yake ya dhati ya kuwaondolea kero ya maji wakazi wa Chalinze, na kwamba ana imani kubwa ya kukamilika kwa mradi huo baada ya kuulalamikia kwa muda mrefu bungeni kuwa umechelewa sana. "Mheshimiwa Waziri napenda nikushukuru sana na hasa Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa Dkt. John Magufuli, kwa kazi nzuri ambayo Serikali inafanya katika kutatua kero za wananchi na hasa wapiga kura wa jimbo la Chalinze." Alisema Mhe. Kikwete.

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isaack Kamwelwe, (wane kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe.Majid Mwanga, Watatu kulia, Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete, (watatu kushoto),Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo, (wapili kulia), Mkandarasi wa Mradi wa uboreshaji miundombinu ya maji kutoka kampuni ya WAPCOS Limited ya India, Mhandisi  P.G. Rajani na maafisa wengine, wamiwa mbele ya tenki la kusafishia maji linalojengwa chini ya mradi huo unaoendeshwa na Sewrikali kupitia DAWASA, kwenye chanzo cha Maji Mto Wami, Mkoa wa Pwani, Desemba 6, 2017


 Mhe. Mhandisi Kamwelwe, akizungumza jambo na Mhe. Ridhiwani Kikwete, walipotembelea chanzo cha Maji Mto Wami.
 Mbunge wa Bagamoyo, Mhandisi, Dkt.Shukuru Kawambwa, akimsikiliza Mhe. Waziri Kamwelwe, wakati wa ziara ya Waziri wilayani Bagamoyo kukagua ujenzi wa tenki la kuhifadhia Maji, Desemba 6, 2017. Tenkji hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi lita milioni 6.
 Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo, akitumia mchoro kuelezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa tenki la Maji Bagamoyo Mkoani Pwani, Desemba 6, 2017
 Mhe.Waziri Kamwelwe, akisalimiana na mmoja wa mafundi wanaojenga tenki la kuhifadhia maji Bagamoyo.

 Mkandarasi wa Mradi wa uboreshaji miundombinu ya maji kutoka kampuni ya WAPCOS Limited ya India, Mhandisi  P.G. Rajani, akitumia mchoro kumueleza Waziri Kamwelwe, (wapili kuhsoto) na Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mwang'ingo, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi huo

 Taswira ya ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji lita milioni 6, Bagamoyo Mkoani Pwani kama inavyoonekana Desemba 6, 2017

 Mhbe., Kamwelwe, (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe.Majid Mwanga, (wapiili kulia) na Wakandarasi kutoka kampuni ya India ya WAPCOS.

ALIYEWAHI KUWA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA 'TAIFA STARS' NA MKUU WA MKOA WA MANYARA JOEL BENDERA AFARIKI DUNI


Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).Kwa habari zaidi endelea kufutilia mtandao wako pendwa wa Shamakala360.blogsport.com

Monday, 4 December 2017

MHE MWANJELWA AIPONGEZA NFRA KUANZISHA MRADI WA KUONGEZA UWEZO WA KUHIFADHI MAZAO KUPITIA UJENZI WA VIHENGE NA MAGHALA NCHINI



Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na Wakulima wa Mji wa Makambako, Mkoani Njombe katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mahindi yaliyohifadhiwa kwenye Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba ya namna ya ununuzi na uhifadhi wa mahindi kwenye Ghala la Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Makambako, Mkoani Njombe wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja, Leo Novemba 1, 2017.


Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amesifu juhudi za uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa utendaji kazi kwa ubunifu kwa kuanzisha Mradi Wa kuongeza uwezo Wa kuhifadhi Mazao.

Mradi huo utahusisha ujenzi Wa Vihenge vya kisasa, Mghala ya kisasa pamoja na ukarabati Wa Ofisi ambapo baada ya mradi huo kukamilika wakala utakuwa umeongeza uwezo Wa kuhifadhi Shehena ya mahindi ya uzito Wa zaidi ya Tani 250,000 ambapo Vihenge vya kisasa ni 190,000 MT na Maghala 60,000 MT.

Mradi huo unataraji kutekelezwa na kampuni mbili za kandarasi kutoka serikali ya Poland (Feerum na Unia Arab) kwa usimamizi Wa Wakala Wa Majengo Tanzania (TBA) ambapo unataraji kugharimu zaidi ya Bilioni 150 za Kitanzania.

Tayari maandalizi ya awali yameshakamilika ikiwemo Utiwaji saini mikataba, Uchunguzi Wa udongo, Tathmini ya athari ya Mazingira, Pamoja na kutembelea eneo la mpango kazi.

Akizungumza wakati akikagua Ghala la Kuhifadhia mahindi Kanda ya Makambako Mkoani Njombe, Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alisema kuwa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umefanya kazi kubwa ya ubunifu na kujiongeza kwa ajili ya kuwanufaisha wakulima katika Kanda zote saba ikiwemo ya Makambako-Njombe, Kipawa-Dar es salaam, Dodoma, Shinyanga, Arusha, Songea na Sumbawanga.

Alisema kuwa pamoja na Kanda ya Makambako kupangiwa kununua jumla ya Tani 6500 katika msimu Wa mwaka 2017/2018 ambapo baada ya lengo kukamilika ziliongezwa fedha za ununuzi hivyo kununua jumla ya Tani 8,961.530

Akisoma taarifa ya Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba alisema kuwa Kanda ya Makambako ni miongoni kwa Kanda itakayoongezewa uwezo Wa kuhifadhi ambapo tayari kuna kiwanja chenye ukubwa Wa Hekari 2,9965 kilichopo Makambako na Mbozi chenye ukubwa Wa Hekari 53.691.

Alisema Wakala umefanikiwa kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kununua baadhi ya Mazao ya Chakula cha ziada kutoka kwa wakulima, Kutoa Chakula cha ziada kwa waathirika, Kutekeleza mkakati Wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUKUTA) kwa kutoa bei nzuri kwa wakulima wanaouza Mazao yao kwa NFRA sambamba na utekelezaji Wa malengo ya milenia 2025.

Katika ziara hiyo ya kikazi ya Siku Moja katika Mji Wa Makambako Mkoani Njombe, Naibu Waziri Wa Kilimo pia amekutana na kufanya kikao cha kazi na wafanyakazi Wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya chakula Kanda ya Makambako ambapo pamoja na mambo mengine amewasihi kufanya kazi kwa Nidhamu, Weledi, Kujituma, Uvumilivu, Bidii na mshikamano.

Wakati huo huo amefanya mazungumzo na wakulima kutoka Kanda ya Makambako ambapo wakulima hao wamesifu Juhudi za serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwajali ikiwa ni pamoja na kupunguza Tozo na Ushuru.

Wakulima hao kwa nyakati tofauti wameupongeza Uongozi Wa Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Makambako kwa kuwashirikisha na kuwajali wakulima katika kila hatua ya ununuzi Wa mazao.

WANACHAMA WA SIMBA WAMPA TIMU MO KIULAINIIII...AHAIDI MAKUBWA KATIKA KLABU HIYO


  
Baada ya Mfanyabiashara bilionea kijana zaidi Afrika, Mohammed 
Dewji kushinda zabuni ya kuchukua hisa hadi 50 asilimia katika klabu ya Simba, Mohammed Dewji aliingia ukumbini akiwa anasubiriwa kwa hamu na wanachama wa Simba.

Wanachama hao ndiyo waliopitisha uamuzi huo na kusubiri tume iliyokuwa inasimamia kupitia jaji mstaafu Mohayo kupitia mchakato na baadaye kutangaza.

Baada ya kutangazwa walishangilia kwa nguvu na baadaye Mo Dewji aliingia huku akishangiliwa kwa nguvu na baadaye akapewa nafasi ya kuzungumza na wanachama hao aliowashukuru na baadaye kuwaeleza nia yake na mipango yake ya uwekezaji.

TANZANIA NA LIBYA NGOMA NGUMU ZATOKA SARE YA BILA KUFUNGANA CECAFA..



MHE MWANJELWA AWATAKA WAJUNBE MKUTANO MKUU CCM MKOA WA MBEYA KUCHAGUA VIONGOZI MAKINI


 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza  na wajumbe wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya, Leo Disemba 3, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana  na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akifatilia Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.
 Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akitoa salamu za wabunge wa Mkoa wa Mbeya wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe Jijini Mbeya, Leo Disemba 3, 2017.


Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Leo Disemba 3, 2017 amewasihi Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kuchagua viongozi makini, weledi, wenye nidhamu na kipawa cha uongozi.

Mhe Mwanjelwa ameyasema hayo wakati akitoa salamu za wabunge Wa Mkoa Wa Mbeya kwenye Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi Wa Tughimbe uliopo katikati ya Viunga vya Jiji la Mbeya.

Alisema kuwa wajumbe hao hawapaswi kuchagua viongozi kwa sababu ya kufahamiana, Urafiki, Ujamaa au Undugu badala yake wanapaswa kuchagua viongozi wenye maono na mtazamo chanya ili wawe mfano bora katika kukiimarisha na kukijenga Chama Cha Mapinduzi.

Mbele ya wajumbe hao Mhe Mwanjelwa kwa ushirikiano na wabunge wote Wa Mkoa Wa Mbeya wamempatia zawadi ya Pawatila Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi kwa ajili ya Kilimo cha kisasa ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi na ufanisi Wa uongozi wake kama Mwenyekiti katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2012-2017.

Alisema kuwa Zawadi hiyo inayogharimu fedha za kitanzania takribani Shilingi Milioni Tano ni michango ya wabunge hao kwa Mwenyekiti huyo kutokana na uhodari wake katika kuimarisha Chama katika Mkoa Wa Mbeya sambamba na kuyavunja makundi yote yaliyokuwepo wakati Wa uchaguzi Mkuu Wa mwaka 2015.

Akifungua Mkutano huo Mwenyekiti Wa CCM Mkoa Wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu Wa Mkoa Wa Lindi Mhe Godfrey Zambi alimpongeza Naibu Waziri Wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa kwa kusafiri usiku wa manane kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano huo pamoja na kuwa na majukumu mengi ya kiserikali Wilayani Songea Mkoani Ruvuma.

Zambi alisema Kuwa kitendo cha Mhe Mwanjelwa kushiriki katika Mkutano huo kimeonyesha mfano bora na umakini katika kuheshimu Chama Cha Mapinduzi kinachoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.

Kwa upande wake Msimamizi Mkuu katika Mkutano huo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe Antony Peter Mavunde aliwataka wajumbe hao kuchagua viongozi wenye uwezo Wa kuwasaidia wanachama na wananchi katika kuchagiza shughuli za maendeleo.

Aidha, alisema uchaguzi huo unapaswa kufuata kanuni na taratibu za uchaguzi.

Mkutano huo utamalizika kwa kuchagua Mwenyekiti Wa CCM Mkoa Wa Mbeya na Mjumbe Wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa.

WAFANYAAKAZI MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB), WAJIPANGA KUBORESHA ZAIDI HUDUMA MWAKA 2018



WAKATI Mwaka 2017 ukifikia ukingoni taasisi mbaliombali nchini zimeanza kuwakusanya watumishi wake na kufanya tathmini ya utendaji na kujadili namna ya kuzikabili changamoto walizokutana nazo ili hatimaye kuongeza ufanisi mwaka ujao 2018.
Miongoni mwa taasisi hizo ni Mwalimu Commercial Bank, (MCB), ambao wamekutana jijini Dar es Salaam, ili kufanya tathmini ya kiutendaji na kuweka mikakati mipya waingiapo mwaka 2018.
Wafanyakazi hao kutoka idara mbalimbali wakiongozwa na Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi pia walipatiwa semina kuhusu masuala mbalimbali ya kiuwajibikaji katika maeneo tofauti kutoka kwa mtaalamu wa kujenga umoja kwa wafanyakazi ili kupata matokeo bora, (Team building consultant), Elizabeth Wachuka.
Ili kuonyesha ushirikiano wafanyakazi hao walibadilishana zawadi mbalimbali ambapo kila mfanyakazi alimuandalia zawadi mfanyakazi anayemvutia zaidi kiutendaji.

 Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, akizunumza wakati wa semina hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 2, 2017
 Wafanyakazi kwa utulizvu kabisa wakisikiliza kilichokuwa kikizunhgumzwa.
  Wafanyakazi kwa utulizvu kabisa wakisikiliza kilichokuwa kikizunhgumzwa.
  Wafanyakazi kwa utulizvu kabisa wakisikiliza kilichokuwa kikizunhgumzwa.

 Meneja Msoko, Bi. Rahma Ngassa

Wafanyakazi kwa utulizvu kabisa wakisikiliza kilichokuwa kikizunhgumzwa.

 Msaidizi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Furaha Johnson, akisaini kwenye makubaliano ya kimkakati ambayo kila mfanyakazi atawajibika
 Mtaalamu wa kujenga umoja kwa wafanyakazi ili kupata matokeo bora, (Team building consultant), Elizabeth Wachuka. akitoa mada.
 Wafanyakazi wakiwa kwenye kikundi wakijadiliana.
Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi, (mwenye t-shirt ya mistari, akiungana na wafanyakazi wenzake katika majadiliano ya vikundi.
 Mtaalamu wa kujenga umoja kwa wafanyakazi ili kupata matokeo bora, (Team building consultant), Elizabeth Wachuka. akitoa mada.

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube