BREAKING

Tuesday, 8 November 2016

TFF YAMLILIA MZEE SAID MOHAMED WA AZAM FC


MZEE SAID WAKATI WA UHAI WAKE, AKIZUNGUMZA MBELE YA RAIS WA AWAMU YA NNE, JAKAYA MRISHO KIKWETE

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa Azam FC na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Sheikh Said Muhammad aliyefariki dunia leo Novemba 7, 2016 katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.

Taarifa za kufariki dunia kwa Mzee Said Muhammad ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi zimethibitishwa na Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba aliyesema kwamba alifariki dunia katika wodi ya Wagonjwa mahututi (ICU) hospitalini hapo baada ya kuzidiwa ghafla nyumbani kwake.

Kutokana na kifo hicho, Rais wa TFF Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Yahya Mohammed, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, Uongozi wa Klabu ya Azam, familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki. Amewataka kuwa watulivu wakati huu mgumu wa kumpoteza Mzee Said Muhammad.

Katika salamu zake, Malinzi amemwelezea marehemu Said Muhammad kuwa alikuwa hazina katika mpira wa miguu nchini kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutoa mchango ya mawazo na miongozo katika Kamati ya Utendaji ya TFF. 

Aliongoza Klabu ya Azam kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) kwa mara ya kwanza tangu klabu hiyo ianzishwe.

“Ndani ya Kamati ya Utendaji ya TFF, Mzee Muhammad ndiye aliyekuwa na umri mkubwa ukilinganisha na wajumbe wengine, lakini alikuwa hakosi vikao muhimu. Mchango wake wa mawazo ulikuwa nguzo kwetu. Nimepokea taarifa hizi za kifo chake kwa masikitiko makubwa,” amesema Rais Malinzi leo mara baada ya kupokea taarifa za kifo hicho.

Taratibu za mazishi zinafanywa nyumbani kwa marehemu. Sheikh Said Muhammad atazikwa kesho Jumanne alasiri  katika makaburi ya Kisutu baada ya mwili wake kuswaliwa msikiti wa Maamur ulioko Upanga, jijini Dar es Salaam.


Inna lillah wainn ilayh  Rajiuun.

Monday, 7 November 2016

KIFO CHA SAMWEL SITTA: CCM YATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI

Marehem Samwel Sitta
Dar es Salaam
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, Samuel John Sitta, kilichotokea usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akitibiwa.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka, imesema,  Samuel John Sitta, amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Katibu wa CCM na Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha uwekezaji, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mjumbe wa Kamati Kuu, Mbunge, Waziri na Spika.


Taarifa hiyo imesema, Sitta alikuwa ni Kiongozi mchapakazi, mwadilifu na aliyejitambulisha kwa utendaji wenye kufuata falsafa yake ya “kasi na viwango”. Ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Chama na Serikali.


Kufuatia kifo hicho, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Spika wa Bunge la Job Ndugai, familia  na Wananchi wa Jimbo la Urambo. "Tunaungana nao katika msiba huu ambao pia ni msiba wetu, Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Ameni", Amesema Kinana akikaririwa na taarifa hiyo.

LWANDAMINA RASMI AACHIA NGAZI ZESCO, ANATUA RASMI YANGA KESHO





Hatimaye Kocha George Lwandamina amemalizana na klabu ya Zesco ambayo ameipa mafanikio makubwa tangu ajiunge nayo .

Kocha huyo ambaye siku chache alikuwa nchini na kuleta mtikisiko kwa kocha aliyepo Han  ameachia ngazi rasmi kuinoa Zesco ambayo mkataba wake ulikuwa unaisha Januari 2017.

 Lwandamina amethibitisha kuachia ngazi katika klabu hiyo, kwa taarifa yake mwenyewe .

"Ni kweli, tumemalizana vizuri kabisa na mambo yamekwenda kitaalamu," alisema.

Kuhusiana na kutua Yanga, Lwandamina amekubali kuwa anakuja nchini lakini hakutana kuweka wazi.

"Baada ya hapa Zesco, sasa naelekea katika nchi nyingine ya Afrika. Nipe siku moja nikupe jibu," alisema.

Lakini taarifa za uhakika zinaeleza kwamba kocha huyo atafika nchini kesho usiku kwa ajili ya kumalizana na Yanga.

"Tunajua anakuja huko Tanzania kesho usiku, ndege yake inaonyesha hivyo," alisema wakala wake.

LIVERPOOL YAIBAMIZA 6-1 WATFORD





Wachezaji wa Liverpool wakishangilia ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Watford leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield. Mabao ya Liverpool yamefungwa na Sadio Mane dakika ya 27 na 60, Philippe Coutinho dakika ya 30, Emre Can dakika ya 43, Roberto Firmino dakika ya 57 na Georginio Wijnaldum dakika ya 91, wakati la Watford lilifungwa na Daryl Janmaat dakika ya 75,kwa PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

PINDA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA

 Wazuri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipotembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, jana.  Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.
 Wazuri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipotembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam
Wazuri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipotembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka, na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chana. 

Tuesday, 1 November 2016

MKUU WA MKOA WA SINGIDA MHANDISI MATHEW MTIGUMWE AKUTANA NA WADAU WA KILIMO CHA PAMBA KUJADILI MAENDELEO YA KILIMO CHA PAMBA KATIKA MKOA HUO

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akifungua Mkutano wa wadau wa pamba wenye dhamira ya kujadili maendeleo ya kilimo cha zao la Pamba katika mkoa wa Singida.
 Wadaau wa kilimo cha Pamba Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini Mkutano wa kujadili namna bora ya kuimarisha kilimo cha zao hilo katika Mkoa wa Singida
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa pamba Mkoa wa Singida
 Wadaau wa kilimo cha Pamba Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini Mkutano wa kujadili namna bora ya kuimarisha kilimo cha zao hilo katika Mkoa wa Singida

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa wadau wa kilimo cha Pamba Mkoa wa Singida
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe Elias Choro Tarimo akisisitiza jambo wakati wa Mkutano huo
 Moja ya wakulima wa Kilimo cha pamba Wilayani Ikungi Timoth S. Nkulu akimuomba Mkuu wa Wilaya kuzisimamia Wilaya zote kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa uzalishaji wa kilimo hicho.
 Wadau wa kilimo cha pamba wakihakiki maazimio waliyoyapitisha

Na Mathias Canal, Singida

Zao la Pamba ni miongoni mwa mazao ya kipaombele ya biashara yanayozaliswa Mkoani Singida kwa kuwa linastahimili hali ya hewa ya Mkoa ya uwepo wa mvua zenye mtawanyiko usioridhisha kwa baadhi ya maeneo ambapo kutokana na hali hiyo Mkoa unaendelea kuhimiza wakulima kuzalisha zao hilo kwa kiasi kikubwa ili waweze kuongeza kipato na usalama wa chakula.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Mkutano wa wadau wa kilimo cha pamba Mkoa wa Singida ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe wakati akifungua Mkutano huo iliokuwa na dhamira ya kujadili maendeleo ya kilimo cha zao la Pamba katika mkoa huo.

Mhe Mtigumwe amesema kuwa Katika Mkoa wa Singida Kampuni ya Biosustain Ltd inayojishughulisha na Kilimo cha Mkataba imeweza kusaidia zao la Pamba kwa kuanzisha kiwanda cha kuchambua Pamba chenye uwezo wa kuchambua Tani 16,000 kwa mwaka ambapo kupitia kilimo cha mkataba wakulima wa Mkoa wa Singida wamepata pembejeo, Mafunzo ya kilimo bora na soko la uhakika ambapo katika utekelezaji wa kilimo cha mkataba msimu wa mwaka 2015/2016 wakulima 4,204 wamepatiwa mafunzo.

Kwa msimu huu wa Mwaka 2016/2017 Mkoa umepata mgao wa mbegu za Pamba kutoka Bodi ya Pamba jumla ya Tani 120 (Wilaya ya Iramba na Mkalama Tani 80, Wilaya ya Manyoni Tani20 na Wilaya Ikungi na Singida Tano 20) ambazo zinaendelea kusambazwa kwa wakulima.

Imeelezwa kuwa zao la Pamba linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo tija ndogo katika uzalishaji (200 kg/ekari) kutokana na wakulima kutozingatia kanuni bora za kilimo cha pamba, matumizi ya viuatilifu ambavyo havina uwezo wa kudhibiti wadudu waharibifu wa zao la pamba (Feki), Matumizi ya mbegu zisizoota vizuri (Feki), Kubadilika kwa bei ya pamba mwaka hadi mwaka, Mvua zenye mtawanyiko usioridhisha kwa baadhi ya maeneo kwa mfano maeneo ya Bonde la Ufa ya Iramba, Mkalama na Manyoni.

Rc Mtigumwe amesema kuwa Mkutano wa wadau wa kilimo cha Pamba ni fursa nzuri ya kuwakutanisha wadau muhimu wa zao la pamba na kujadiliana mafaniko, Changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya kufanikisha kuongeza kwa tija na faida katika uzalishaji wa zao la pamba.
Ameeleza malengo ya kimkoa kulima zao hilo kwa kiwango  kikubwa cha Hekta 8,510 kwa Mwaka 2016/2017 na matarajio ni kuzalisha Tani 8,075.

Katika Mkutano huo kwa umoja wao wadau wa kilimo cha Pamba wamepitisha maazimio 17 kama ifuatavyo:

  1. Wataalamu wa kilimo wa ofisi ya mkuu wa Mkoa na halmashauri za wilaya  watafute ufafanuzi wa deni kwakushilikiana na Biosustain kumpatia Katibu Tawala wa Mkoa ndani ya mwezi mmoja.
  1. Katibu Tawala wa Mkoa awaandikie barua uongozi wa Kampuni ya Quton kuitwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuja kutoa maelezo kwanini hawahudhurii vikao na walete ufafanuzi wa deni wanalodaiwa na namna ya kulilipa.
  1. Halmashauri ya Wilaya ya Singida inatakiwa ilejeshe fedha za ushuru  wa Pamba  kwa halmashauri ya Ikungi iliyolipwa kwao kwa makosa ndani ya miezi sita (6). 
  1. Elimu juu ya Matumizi ya mizani iendelee kutolewa ili kuongeza uelewa na ufanisi kwa wakulima.
  1. Kila halmashauri itoe taarifa ya maendeleo ya zao la Pamba kwenye eneo lake kwenye vikao vya wadau wa Pamba.
  1. Bodi ya Pamba ilete wakaguzi wa Pamba wasiopungua  wawili kwa Mkoa wa Singida ndani ya miezi miwili kuanzia sasa.
  1. Wakurugenzi wapitie na wasimamie mikataba inayoingiwa kati ya Makampuni na wakulima ili kuepuka malalamiko yasiyo yalazima wakati wa utekelezaji.
  1. CDTF wawe ni wajumbe kwenye kikao hiki  na waalikwe kuanzia kikao kijacho ili watoe mchango wao kwa maendeleo ya Pamba katika Mkoa wa Singida.
9)      Bodi ya Pamba iangalie uwezekano wa kuwahusisha watafiti watoe mbegu bora inayostahimili ukame na kutoa mazao mengi.
 
10)   Katibu Tawala wa Mkoa aiandikie Wizara ya Kilimo kuikumbusha kuimarisha udhibiti wa ubora wa viuatilifu.
 
11)   Wakurugenzi wa halmashauri, Bodi ya Pamba na kampuni ya Biosustain waendelee kutoa Elimu stahiki ili kukuza uzalishaji wa Pamba.
 
12)   Kila kaya lazima ilime ekari mbili za Pamba ili tupate Pamba yakutosha kuanzisha kiwanda cha nguo. 
 
13)   Kila shule ya msingi na sekondari lazima iwe na ekari mbili (2) za zao la Pamba ili zitumike kama shamba darasa kwa wanafunzi na wananchi wanaoishi maeneo ya jirani. 
 
14)   Wakurugenzi wahakikishe vitabu vya mwongozo wa kilimo na mifugo vinapatikana na kuwafikia wakulima, kila kijiji kipate nakala tano (5) kabla ya Januari, 2017.
 
      15) Jalada la usajili lenye orodha ya wakulima na ekari zao kiujumla na mazao wanayoyalima
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube