Balozi wa uingereza nchini Tanzania David Concar amekipongeza kiwanda cha Mkwawa cha uzalishaji wa bidhaa ya maji yenye ubora kwa matumizi ya binadam yeyeto yule wa ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
Monday, 25 January 2021
BALOZI WA UINGEREZA APONGEZA UBORA WA MAJI YA MKWAWA MKOANI IRINGA
Wednesday, 20 January 2021
ZLATAN APIGA ZOTE AC MILAN YASHINDA 2-0 NA KUPAA KILELENI
Zlatan Ibrahimovic jana amefunga mabao yote mawili dakika ya saba kwa penalti na 52, AC Milan ikiichapa Cagliari 2-0 katika mchezo wa Serie A Uwanja wa Sardegna Arena, Cagliari.
Sasa AC Milan inafikisha pointi 43 na kuendelea kuongoza Serie A kwa pointi tatu zaidi ya mahasimu wao wa Jiji, Inter Milan (43-40) baada ya wote kuchezsa mechi 18
OZIL ANA KWA ANA NA MTANZANIANIA MBWANA SAMATTA - UTURUKI
Mesut Ozil amesaini kujiunga na klabu ya soka ya Fenerbahce, akiondoka ndani ya washika mitutu wa London Arsenal baada ya kudumu ndani ya Arsenal kwa mika saba na nusu.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu tangu kuwasili kwa kocha wa Arsenal Mikel Arteta ambaye alionekana kutokwenda sawa na kocha huyo ambaye pia aliwahi kucheza naye kabla ya kustaafu kandanda.
Ozil
Mesut Ozil aliposafiri na familia yake kujiunga na klabu yake mpya ya Fenerbahce Istanbul -Uturuki
Kiungo Mahiri Ozil akiwasili Uwasili Uturuki
Picha mojawapo aliyopiga na kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger baada ya kusaini kuichezea timu hiyo mwaka 2013 akitokea Real Madrid
Tuesday, 19 January 2021
MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MAADHIMISHO YA SIKU YA KISWAHILI-DODOMA
Monday, 18 January 2021
RAIS MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MULEBA -MKOANI KAGERA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Muleba wakati akiwa njiani kuelekea Bukoba mkoani Kagera leo tarehe 17 Januari 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Kemondo wakati akieleka Bukoba mjini mkoani Kagera leo tarehe 17 Januari 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Kemondo wakati akieleka Bukoba mjini mkoani Kagera leo tarehe 17 Januari 2021
RAIS MAGUFULI KUZINDUA SHULE YA SEKONDARI YA WAVULANA YA IHUNGO...
Huu ndio muonekano wa Shule ya Sekondari ya wavulana Ihungo iliyoko Bukoba Mkoani Kagera inayotarajiwa kuzinduliwa na Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli Januari 18 mwaka huu wa 2020. kufuatiwa ukarabati kukamilika ambao umegharimu shilingi Bilioni 10.9
Saturday, 16 January 2021
DSTV YAMWAGA OFA KWA WATEJA WAKE YATAJA PROMOSHENI KABAMBE YA 'PANDA TUKUPANDISHE'
MultiChoice Tanzania imetangaza promosheni maalum kwa wateja wa DStv ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu itakuwa ikiwapandisha vifurushi wateja wake.
Hii ni promosheni inayowawezesha wateja wa DStv wanaokidhi vigezo (wateja waliokatika, wateja wanaoendelea na wateja wapya) kupata fursa ya kulipia kifurushi kinachofuatia cha juu yake na kupandishwa kwa kupatiwa kifurushi cha juu ya kile walicholipia kwa muda maalum. Hii itategemea na kifurushi ambacho mteja alikuwa amelipia hadi kufikia tarehe 8 Januari 2021 au kifurushi alichojiunga nacho baada ya tarehe 8, Janurai 2021. Mathalan,
Mteja wa kifurushi cha Bomba, akilipia kifurushi cha Family, atapandishwa hadi kifurushi cha Compact bila malipo ya ziada kwa mwezi mmoja.
“MultiChoice Tanzania inafurahi kuzindua rasmi promosheni yake maalum ya ‘Panda tukupandishe’ hii ikiwa ni njia mojawapo ya kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kuwa nasi na pia njia ya kuwahakikishia kuwa tumejipanga vema kuendelea kuwapatia burudani isiyo na kifani” amesema Ronald Shelukindo, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania wakati wa uzinduzi rasmi wa promosheni hiyo jijini Dar es Salaam.
Amesema kampuni hiyo inaendelea kuwapatia wateja wake burudani ya kina bila kusahau maudhui mengine kama Habari na elimu, huku ikihakikisha kuwa wateja wake wanapata maudhui kemkem na ya kusisimua ya ndani na nje.
Kaimu meneja wa thamani kwa wateja Lucy Kisasa amesema kama zilivyo promosheni nyingine, kuna vigezo na masharti ambavyo vitafuatwa ili mteja aweze kunufaika na promosheni hii. Amesema promosheni hii ni kwa wateja wa DStv waliopo Tanzania, wale ambao akaunti zao ziko hai na wale ambao akaunti zao zimekatika. Pia inawahusu wateja wapya wa DStv wanaojiunga sasa na huduma hizo.
Amesema mteja wa DStv anayelipia kifurushi cha juu ya kile anachotumia au cha mwisho kutumia atapandishwa kifurushi kwa muda wa mwezi mmoja bila malipo ya ziada na pia mteja mpya wa DStv aliyejiunga siku ya, au baada ya tarehe 8 Januari 2021 ambaye atalipia kifurushi cha juu ya kile alichojiunga nacho naye pia atanufaika na ofa hii.
Hata hivyo, wateja wa DStv ambao wamelipia kifurushi chao kwa mwaka mzima hawahusiki na promosheni hii kwani hawa tayari wana ofa yao ambapo hupata mwezi mmoja wa kifurushi chao bila malipo ya ziada.
Amefafanua kwamba Mteja atakayetaka kulipia kifurushi cha juu yake kabla kifurushi alichonacho hakijaisha naye atanufaika na ofa hii na pia salio lake la kifurushi cha awali litaendelea kubaki kwenye akaunti yake na hivyo kuwaza kulitumia tena punde ofa aliyopata itakapokamilika kulingana na vigezo na masharti.
Wednesday, 13 January 2021
RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE -KULA CHAKULA NA WATOTO YATIMA UKUMBI WA KIBADA GARDEN -KIGAMBONI MUFTI WA TANZANIA ALI KIBA , KUJUMUIKA...
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete anatarajiwa kushiriki chakula cha Mchana na watoto yatima wa kituo cha Amani Foundation For ORPHANAGES -Kigamboni January 16 mwaka huu..
Wageni wengine ambao wanatarajiwa kushiriki katika Chakula cha Mchana katika tukio ambalo litaambatana na uchangiaji Uimarishaji wa Kituo hicho ni pamoja na Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Bin Zubeiry Ally, Sheikh Mkuu wa Mkoa Alhad Mussa Salum ,Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.Faustine Ndugulile sambamba na Mwanamuziki wa kizazi kipya Ali Kiba....
Thursday, 7 January 2021
LAMECKY NYAMBAYA KIONGOZI MPOLE USONI! MWENYE HAIBA YA UANA MICHEZO...MUUMINI WA SOKA LA VIJANA.
Na Said makala
Nelson Mandela, rais wa kwanza wa Afrika Kusini kuchaguliwa kidemokrasia na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, , alifariki Desemba 5, mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 95, Mandela aliwahi kutumikia kifungo kwa miaka 27 kwa sababu ya mapambano yake dhidi ya mfumo wa kibaguzi wa Afrika Kusini unaofahamika kama Ukaburu, Aliachiwa huru kutoka gerezani mwaka 1990, na kuwa rais miaka minne baadae, na kuachia madaraka baada ya kutumikia kwa kipindi kimoja tu, kitendo adimu kufanywa na wenye madaraka barani Afrika.
Ni Mpambanaji aliyeonyesha uwezo wa kuongoza kwa vitendo, yes! alikuwa mtu mhimu sana katika Ulimwengu wa siasa , wacha nisiseme ya kisiasa hapa nataka kumzungumzia mtu mmoja anaitwa Lamecky Nyambaya Mwenyekiti Mpya wa Chama cha soka Mkoa wa Dar es Salaam, mtu jasiri hususani kuhamasisha soka nchini ambaye alianza kujiimarisha kwenye uongozi wa soka la Vijana
Mwaka Jana Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) siku ya Jumapili,ya Novemba 29,mwaka 2020 Ulifanyika uchaguzi na kupata viongozi wapya ambao wataongoza chama hicho kwa miaka minne, nafasi hiyo ya Mwenyekiti iliyokuwa imeachwa wazi na Almasi Kasongo ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi (TPLB) tayari ina mtu sahihi mwenye haiba ya aina yake mtu mwenye moyo wa kusaidia soka popote anapokwenda, Huyoni Lamecky Nyambaya...
Lameck Nyambaya aliyekuwa mgombea pekee na kupata kura 27 aliaminiwa zaidi na hiyo inatokana na utendaji wake wa kazi uliotukuka akiwa Mjumbe wa soka ndani ya Shirikisho la soka tanzania TFF, akiwakilisha Mkoa wa Dar es salaam , hivi sasa bila shaka kupewa mikoba ya kuwa Mwenyekiti DRFA mengi mazuri yanakuja , katika mwaka wa 2021 Nyambaya anatakiwa kuzingatia mambo mengi lakini machache nitayataja na ni haya yafuatayo ili haiba yake iweze kutimia zaidi na kuendelea kupata sifa za kiongozi...
Kwanza.. .Nyambaya anapaswa kuendeleza pale Almas Kasongo alipoachia na kupiga mbizi ndefu kuleta maendeleo ya soka kwa kuwa tayari ana uzoezfu wa kuongoza,
Pili.. .Azungumze na wadau kupata kilio cha wanamichezo kwani wapo wazazi ambao wanaaminiu kuwa vijana wao kudidimia katika soka ni kupoteza mwekeo sawa na wale wanaoingia katika shindano la Miss Tanzania wakiamini kule ni kujidhalilisha bila kujua kuwa huko kuna vipaji vinavyokufa kutokana na imani hizo potofu, hivyo anapaswa kuwa mshawishi zaidi kwa wazazi kupata vipaji.
Tatu...Nyambaya asijifungie Ofisni asiwe na Umangi Meza hayo yote akiepuka tunamuona Nyambaya mkubwa katika uendelezaji wa soka Tanzania kwa miaka ijayo
Hizo ni nguzo chache ambazo zinanishawishi kuamini Lamecky Nyambaya ni mtu mwenye malengo ya haki na maamuzi ya busara kila mara anapoamua kusaidia soka, naamini amekuwa karibu na familia ya soka amekuwa mwenye huruma na familia ya soka kama alivyo na huruma kwa familia yake hivyo wadau washikamane naye katika kuhakikisha soka linakuwa zaidi kwani yupo katika jiko bora la Dar es salaam, ambalo limejaa viungo vya kila aina , nikimanisha Mkoa wa Dar es salaam, ndio wenye vipaji vya kila aina....mimi nashawishika kumwita Lamecky Nyambaya ni Kiongozi wa mfano kwa kuwa hana Mbwembwe anatekeleza mambo yake kwa vitendo.
WAZIRI MWIGULU APONGEZA UONGOZI WA MAHAKAMA KWA KUTOA USHIRIKIANO NA KUWAPA NGUVU TAWJA KUFANIKISHA KAZI ZAO
Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake (TAWJA) Mhe Jaji Joaquuine De-Mello akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.
Na Mathias Canal, Wizara ya Katiba na Sheria-Mwanza
Serikali imefurahishwa kwa kazi zinazofanywa na Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake TAWJA katika kupigania haki za wananchi.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba akimuwakilisha Mhe Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) uliofanyika tarehe 7 Januari 2021 katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT) Jijini Mwanza.
Amewataka majaji hao kuendelea kuongeza na kuimarisha Haki za Wanawake katika suala la Haki Sawa kwa wote; Kukuza Upatikanaji wa Haki kwa Wanawake, Kukuza/Kuendeleza Uongozi wa Mahakama; Kufanya tafiti za kisheria katika Usawa wa Kijinsia na Haki za Binadamu; Kubadilishana taarifa katika masuala tata yanayowahusu Wanawake na kuondoa Upendeleo wa Kijinsia na Ubaguzi wa aina yeyote.
Amesema kuwa mtazamo mkubwa wa TAWJA ni kuhakikisha Majaji Wanawake na Mahakimu pamoja na Maafisa wengine wa Mahakama na Washirika wanaandaliwa kwa kuwapatia nyenzo sahihi na muhimu zinazohitajika katika kukuza Haki Sawa kwa Wote (‘Equal Justice for All’)
“Ninafahamu kuwa mmekuwa mkifanya hivyo bila kuchoka kwa kipindi cha miaka ishirini (20) mfululizo tokea TAWJA kuanzishwa kwake mwaka 2000. Kwa hili niwapongeze sana Wanachama wote, mnatakiwa kujivunia na kutembea kifua mbele kwa kazi nzuri mnazofanya. Naamini kuwa hili lisingewezekana bila msaada mkubwa kutoka kwa Mahakama ya Tanzania Bara na Zanzibar” Alikaririwa Dkt Mwigulu
Dkt Mwigulu amesema ni wazi kuwa sauti zao Majaji na Mahakimu Wanawake ikijumuisha na zile za Wadau wengine nchini zimepelekea utayari, uwazi na hamasa katika kulaani ubaguzi na ukiukwaji wa Haki za Binadamu unaofanywa na wanajamii katika maeneo yetu.
Waziri Mwigulu amesem akuwa kaulimbiu ya Mkutano huo ni; “Weledi na Ustawi wa Majaji Na Mahakimu Wanawake: Chachu ya Mabadiliko”, imekuja wakati muafaka na mahali sahihi kwani mara nyingi Wanawake Wataalamu hawatilii maanani ustawi wao, na hasa Maafisa wa Mahakama ambao muda wote hutingwa zaidi na majukumu yao ya msingi.
Kutokana na Kaulimbiu hiyo, mtaibua vitu vingine vilivyojificha na vinayowakabili Maafisa wa Mahakama amesisitiza katika mkutano huo kujadiliwa kwa kina kuhusu masuala yahusuyo afya za akili na mwili na kudadavua kuhusu uchumi, masuala ya kisaikolojia sambamba na kuangalia ukuaji katika maeneo ya utoaji haki.
“Maendeleo ya Mwanamke ni maendeleo ya wote. Hivyo ni lazima kumpa mwanamke kipa umbele. Ni muhimu sana kumpa mwanamke nafasi nyingi bila kujali kuwa ni haki yake ya msingi kwani pia ni kuonyesha matumizi mazuri ya uelewa wa uchumi.” Amesisitiza