BREAKING

Thursday 12 September 2019

MSHINDI WA JACKPOT YA SPORTPESA AMEPOKELEWA NA WAZAZI WAKE, YEYE AELEZA FURAHA YAKE






Yule mshindi wa Jackpot ya Sh Mil. 825 Magabe Marwa amesema kuwa anajisikia furaha kurudi nyumbani kwao na kukutana na familia, wazee huku akiamini hicho alichoshinda kitamfanya aishi maisha ya kati tofauti na awali.


Marwa hivi karibuni alishinda mamilioni hayo pamoja na mwenzake Kingsley Simon mamilioni hayo kabla ya kugawana Sh Mil. 412 kila mmoja baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 13.


Marwa alisema kuwa mamilioni atayatumia kwa ajili ya matumizi ya familia yake pekee aliyoyaanzisha kwa maana ya mke na watoto, na familia aliyotoka kwa maana ya wazazi na wadogo zake,  hivyo ndio vitu vya msingi.


"Mimi ndio mtoto wa pili kwenye familia yetu, na tangu wazazi wangu wana nguvu mpaka wanafikia hatua hii, mimi ndio nimeyafaidi sana maisha. " "Sisi ni familia ambayo huwa tunafuraha hata kama kuna shida na inapendwa na watu wengi," alisema Marwa.


Neno la shukrani kwa SportPesa

"Naishukuru SportPesa kwakuwa wameweza kubadilisha maisha yangu, hivyo ningependa kuwashauri vijana wenzangu kuwa kama mtu anaweza basi aweze kucheza kama ambavyo mimi nimethubutu, maana cha msingi ni uthubutu.


Kuiamini SportPesa

"Mimi mara nyingi huwa nacheza Multibet kwa hiyo kama nikipata kidogo huwa napokea na mimi tayari ni mtu mwenye upeo kwamba hii michezo ipo kisheria.


"Najua nikishatengeneza mkeka wangu nikabet naletewa namba kwa hiyo kama wasiponilipa nina uwezo wa kwenda mahakamani kufungua kesi kwa hiyo nilikuwa najua kwamba nikishinda nitapata changu.


"Kwa watu ambao wanacheza na wale ambao bado hawajaingia kucheza, hii ni fursa ambayo haihitaji nguvu kubwa sana na haikuzuii kufanya shughuli nyingine.


"Ninaamini kama ukiitumi kama fursa, Mungu akikujalia na uwezo wako wa kutengeneza timu na kuzichambua basi mwisho wa siku utaibuka mshindi kama mimi


Marwa aliongeza kuwa yeye ni mtumishi na alikuwa na mipango yake  aliyoipanga lakini hamufikiri kwamba atakuja kupata fedha kama hiyo na kupanga mipango itakayomtoa hapo alipo hivi sasa ya kushinda mamilioni ilikuwa nafikiria kwamba nipange mipango itakayomtoa katika maisha yake ya hivi sasa.

WAHITIMU WA AKADEMI YA MULTCHOICE WATING BUNGEN


Wanafunzi wanne waliohitimu hivi karibuni mafunzo maalum ya uzalishaji filamu chini ya programu ya MultiChoice Talent Factory wamehudhuria kikao cha bunge la Tanzania kama wageni maalum wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Katika ziara hiyo pia wanafunzi hao walikutana na wadau mbalimbali akiwemo naibu spika Dr. Tulia Akson waziri Dr. Harrison Mwakyembe, naibu waziri Juliana Shonza, naibu waziri Anthony Mavunde na katibu mkuu wa wizara Suzan Mlawi.

1Mwakyembe
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe akisalimiana na wahitimu wa Akademi ya Filamu ya MultiChoice (MultiChoice Talent Factory Academy) katika viwanja vya bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika. Kutoka kulia ni Sarah Kimario, Jamal Mohamed, Wilson Nkya, Jane Moshi pampja na mkuu wa Mahusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na wahitimu hao katika viwanja vya bunge jijini Dodoma, viongozi hao waliwataka wahitimu hao kutumia mafunzo maalum waliyoyapata katika kuleta mapinduzi ya tasnia ya filamu hapa Tanzania. 
3 Juliana
Naibu waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza (kushoto) akizungumza na wahitimu wa Akademi ya Filamu ya MultiChoice (MultiChoice Talent Factory Academy) katika viwanja vya bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika. Kutoka kulia ni Wilson Nkya, Grace Mgaya, Jane Moshi, Sarah Kimario na Jamal Mohamed.

Kwa pamoja wamekiri kuwa tasnia ya filamu ni moja ya tasnia zinazokuwa kwa haraka hapa nchini hivyo ni muhimu wanatasnia wawe na mafunzo ya kutosha na yanayoendana na wakati ili iweze kupambana na nchi nyingine katika soko la filamu ulimwenguni huku tukihakikisha kuwa kazi zetu zinaakisi mila, desturi, utamaduni na uzalendo wetu.

4Tulia
Naibu Spika Dr. Tulia Ackson (katikati) akizungumza na wahitimu wa Akademi ya Filamu ya MultiChoice (MultiChoice Talent Factory Academy) nje ya ukumbi wa bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika. Kutoka kushoto ni Jane Moshi, Sarah Kimario, Jamal Mohamed na Wilson Nkya

Akizungumza na wanafunzi hao baada ya kumtembelea ofisini kwake, Katibu Mkuu Suzan Mlawi amesisitiza ahadi ya serikali kushirikiana na wadau wa tasnia mbalimbali ili kuharakisha ukuaji wa tasnia hizo. Amesema ushirikiano kati ya serikali na wadau ni muhimu na kwamba serikali itaendelea kuhakikisha kuwa sera na kanuni zinaboreshwa ili kuakisi hali halisi ya ukuaji wa tasnia ya filamu.
Wanafunzi hao wanne – Wilson Nkya, Jane Moshi, Jamal Mohamed na Sarah Kimario wamehitimu mafunzo maalum ya mwaka mmoja yanayofadhiliwa na MultiChoice ambapo vijana 60 kutoka kote barani Afrika huchaguliwa kwa mafunzo hayo kutoka nchi mbalimbali. Programu hiyo ina vituo vitatu vya mafunzo ambapo kwa upande wa kusini mwa Afrika kipo Lusaka Zambia, kwa Afrika Mashariki na kati kipo Nairobi Kenya na kwa Afrika Magharibi Lagos Nigeria.

2Mwakyembe
Mkuu wa Mahusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (wa pili kushoto) akiwatambulisha wahitimu wa mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe (Kushoto) mara baada ya wahitimu hao kuhudhuria kikao cha bunge kama wageni maalum wa waziri. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika kupitia program yake ya MultiChoice Talent Factory. Kutoka kulia ni Sarah Kimario, Jamal Mohamed, Wilson Nkya, Jane Moshi pampja na Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Grace Mgaya

Awamu ya pili ya program hii itaanza mwezi Octoba 2019 ambapo wanafunzi wengine 60 watapata mafunzo hayo. Tanzania kwa mara nyingine tena itapeleka wanafunzi wanne.

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube