BREAKING

Saturday 20 July 2024

MHE. RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MAZUNGUMZA NA RAIS WA CHINA MHE. XI JINPING




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping katika ukumbi wa The Great Hall of the People kabla ya kuanza mazungumzo jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake wakiwa kwenye kikao cha pamoja na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping na ujumbe wake katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing, tarehe 4 Septemba, 2024.






Friday 19 July 2024

MHE. RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA WATANZANIA WANAOISHI CHINA..


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na Watanzania wanaoishi nchini China (Diaspora) wakiwemo wafanyakazi, wanafunzi na wafanyabiashara,  Jijini Beijing tarehe 06 Septemba, 2024.







Monday 29 April 2024

RAIS SAMIA NCHINI KENYA-ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Kenya Mhe. Dkt. William Ruto mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 29 Aprili, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mawaziri wa Kenya Musalia Mudavadi mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 29 Aprili, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA.

RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA-KENYA






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya tarehe 29 Aprili, 2024. IDA ni Mfuko Maalum wa Benki ya Dunia ambao unatoa mikopo nafuu na misaada kwa nchi zinazoendelea.

Sunday 7 April 2024

RAIS DK.MWINYI AONGOZA DUA KUMBUKUMBU YA KARUME







RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi ameongoza kisomo cha Dua na Hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, iliyofanyika Afisi Kuu CCM Kisiwandui  Zanzibar tarehe 07 Aprili 2024.


Viongozi mbalimbali wameshiriki wakiwemo wa Serikali, Dini , Vyombo vya ulinzi na usalama na Vyama vya siasa.

Thursday 4 April 2024

RAIS SAMIA AWAAGIZA VIONGOZI WATEULE KUHESHIMIANA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wateule kuwa nguzo kubwa katika kutatua migogoro iliyopo kwenye jamii na sio kuisababisha migogoro.

Mhe. Rais Dkt. Samia amesema hayo kwenye uapisho wa viongozi wateule, Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo amesema mabadiliko ya viongozi ni mambo ya kawaida, ili kuimarisha ufanisi katika utendaji kazi kwa jamii na niwajibu wa viongozi kwenda kuwatumikia wananchi pindi wanapoteuliwa .

Aidha Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka  aliyekuwa Naibu Waziri wa Tamisemi, Deogratusi Ndejembi ambaye sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu akimsihi kwenda kufanya kazi kwa ukaribu na ushirikianio na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Patrobas Katambi, huku akitoa maagizo ya kuhakikisha vijana wanapata ajira na kuajiriwa.

Katika hatua nyingine amekemea migongano ya kimadaraka katika taasisi walizopo kwani watakapofanya hivyo hatosita kuwaondoa wote wawili…


RAIS SAMIA: MAKONDA UMENIKOSHA UMETUCHANGAMSHA WANACCM


IKULU-Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuapisha aliyekuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Paul Makonda leo Aprili 4, 2024 Ikulu, Dar es Salaam kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Makonda anachukua nafasi ya John Mongella Hafla ya uapisho huo inahusisha viongozi mbalimbali 

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube