Katika kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita za kuboresha huduma za afya nchini Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imenza kambi maalum ya upasuaji wa upandikizaji wa meno bandia kwa njia ya kisasa kwa wagonjwa ambao wamepoteza meno yao kutokana na sababu mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kambi hiyo Daktari Bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno MNH.Mloganzila Dkt. Peter Shempemba amesema wagonjwa watakao hudumiwa katika kambi hiyo ni pamoja na wale ambao walifanyiwa upasuaji mwishoni mwa mwaka jana na wale ambao wanakuja kwa mara ya kwanza.
Ameongeza kuwa kundi la kwanza ni wale ambao walishawapandikiza mizizi ya meno katika awamu ya kwanza na kipindi hiki watapandikizwa meno na kundi lingine ni wale ambao wanapandikizwa mizizi kwa mara ya kwanza.
“Upandikizaji huu ni wa ubora wa hali ya juu, meno tunayoyapandikiza hayana tofauti na meno ya asili kwakuwa yanapandikizwa moja kwa moja kwenye mfupa wa taya na yanadumu kwa muda mrefu, hayawezi kutoka kirahisi, mtu ataweza kutafuna vizuri kama kawaida ” amesema Dkt. Shempemba.
Kambi hiyo inafanyika kwa kushirikiana wataalam wa ndani na Daktari Bingwa aliyebobea katika Upasuaji wa Taya kutoka Hospitali za Wochhardt Dkt. Chirag Desai ambapo itafanyika kwa kipindiki hiki cha siku saba kuanzia tarehe 20 hadi 26 Februari, 2025 ambapo takribani wagonjwa 45 watafanyiwa upandikizaji.
No comments:
Post a Comment