BREAKING

Sunday, 11 July 2021

ARGENTINA MABINGWA WA COPA AMERICA....MESSI AZOA TUZO....



TIMU ya taifa ya Argentina imetwaa taji la Copa America baada ya ushindi wa bao 1-0 mbele ya Brazil katika mchezo wa fainali uliochezwa usiku wa kuamkia leo. 

Ni Angel Di Maria alipachika bao la ushindi dk 22 ambalo lilidumu mpaka dakika ya 90. Argentina pia ilipiga jumla ya mashuti 6 huku mawili yakilenga lango na Brazil wao walipiga 13 na mawili yalilenga lango.

Licha ya uwepo wa staa wa Brazil Neymar Jr ndani ya kikosi hicho bado alishindwa kuipa ushindi timu hiyo ambayo ilikuwa inapambana na staa wa Argentina,  Lionel Messi.

Ilikuwa ni fainali ya kibabe Uwanja wa Maracana ambayo ilishuhudia jumla ya kadi 9 za njano zikitolewa ambapo Argentina wao walionyeshwa 5 na Brazil 4

RAIS SAMIA AKUTANA NA NAIBU MKURUGENZI WA UNEP


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Bibi Joyce Msuya, Ikulu Jijini Dodoma leo Julai 09,2021.(picha na Ikulu)



 

Wednesday, 30 June 2021

MAGAZETI YA TANZANIA BARA, ZANZIBAR, KENYA, UGANDA NA UCHINA, LEO J5, JUNI 30, 2021












ENGLAND WANA JAMBO LAO EURO 2020....WAICHAPA UJERUMAN 2-0


Nyota wa England Raheem Sterling usiku wa jana alikuwa mwiba katika mchezo uliowakutanisha Engeland na Ujeruman hatua ya 16 bora ya michuano ya Euro akifunga bao dakika ya 75, katika mchezo uliofanyika kwenye dimba laWembley 

Nahodha wa EnglandHarry Kane alishindilia mwiba wa mwisho kwa kufunga bao maridadi kwa kichwa dakika ya 86 na kuzamisha kabisa jahazi la wajeruman 

EURO 2020- UKRAINE HIYOOO ! ROBO FAINALI



 Michuano ya EURO 2020 imeendelea kutikisa katika hatua ya robo fainali ambapo katika mchezo wa hatua ya 16 bora Ukraine imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sweden.

Nyota wa mchezo huo Oleksandr Zinchenko alifunga bao dakika ya 27 bao ambalo baadae ililisawazishwa na mchezaji Emil Forsberg.

Dakika 90 za mchezo wa kawaida ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Baadae ziliongezwa dakika 30 na nyota Artem Dovbyk alipachika bao dk 120 na kuifanya timu yake ya Taifa ya Ukraine kutinga hatua ya robo fainali.

Timu ya Sweden ilipata pigo baada ya mchezaji wao Marcus Danielson katika dakika ya 99 alionyeshwa kadi nyekundu na kuwafanya Sweden kumaliza mchezo huo wakiwa pungufu.


RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA FEDHA DUNIANI



 

Tuesday, 29 June 2021

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCMA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KAMATI KUU YA TAIFA -DODOMA


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi NEC, kilichokutana leo Juni 29,2021 katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Jijini Dodoma


 

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube