BREAKING

Tuesday, 11 June 2019

POLEPOLE AWAFUNDA MAKATIBU WA ITIKADI NA UENEZI MKOA WA IRINGA



Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole akitoa semina kwa makatibu wa idara ya Itikadi na uenezi wa mkoa wa Iringa iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo

Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa (MNEC) Salim Asas akiwahutubia makatibu wa idara ya Itikadi na uenezi wa mkoa wa Iringa walikuwa wakipewa semina na Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole juu ya Idara hiyo,semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
 Baadhi ya makatibu wa Idara ya Itikadi,siasa na uenezi mkoa wa Iringa wakiwa makini kumsikiza Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole alipokuwa anawafunda.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole Amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia chama hicho kutokuwa chanzo cha migogoro na majungu bali wawe suluhisho kwa kuwa lengo la chama ni kusimamia serikali na kuwaletea watanzania Maendeleo.

ameyasema hayo kwenye semina ya kuwafunda katibu wa Idtikadi na uenzi wa ngazi zote mkoani Iringa, Polepole amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wamekuwa chanzo cha migogoro hata kufanya kurudisha nyuma maendeleo ya chama.

Amesema kuwa chama hicho kimejengwa kwenye misingi bora kwa lengo la kutumikia wananchi na kusikiliza watu pamoja na kujua shida zao lakini kuna baadhi yao wanaleta majungu wao kwa wao jambo linalofanya kutowavumilia.

“Sasa hivi hii ni ccm mpya chini ya mwenyekiti Dr John Pombe Magufuli na hana utani anataka kazi tu na wale ambao wanaona wameshindwa watupishe maana unapoacha sumu ndani si ya siku itakudhuru tunapogombana wanaoumia ni watanzania waliotupa dhamana ya kusimamia serikali”Alisema Polepole

Polepole ameongeza kuwa kwasasa mlango uko wazi endapo mtu anaona atashindwa kupelekana na kasi ya CCM mpya chini ya mwenyekiti wao John Pombe Magufuli ni vyema akapisha na kuacha wanaojua kufanya kazi.
 
Hata hivyo Polepole amewataka viongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa huku akimtaka katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza kuunganishi vizuri na kuendelea kuwatumikia wananchi vizuri kwa kueleza mambo mazuri yanayofanywa na serikalia ya CCM.

Vile vile Polepole amewasifu viongozi katika ngazi zote kwasababu wameibadilisha ccm na wananchi wameelewa dhamira ya Chama katika kuisimamia serikali.

Aidha Polepole alisema kuwa chama cha mapinduzi kikifanya vibaya kwa wananchi ujue kuwa idara ya Itikadi na uenezi haijafanya kazi yake ipasavyo,hivyo ni lazima kila kiongozi awajibike ipasavyo ili kutimiza malengo ya chama.

“Tunatakiwa kushughulikia matatizo ya wananchi kwa kuwapa mafunzo mbalimbali viongozi wa ngazi za chini ili kueneza vilivyo cha hicho ambacho kipo madarakani muda mrefu sasa” alisema Polepole

Polepole aliwaambia viongozi hao kuwa uongozi ni kujitolea na sio kutegemea kupata maslai furani kwenye chama wakati unagombea nafasi mbalimbali lazima uwe unasehemu ya kuingiza kipato kingine na usitegemee kuvuna kutoka kwenye chama.

Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa (MNEC) Salim Asas alimtaka katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza kuratibu namna nyingine tena ya kuwawezesha makatibu hao kuanzia ngazi ya chini hadi juu kupata fedha za kufanyia kazi mafunzo walipata kutoka kwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole.

“Ramadhani Baraza nakuomba uratibu zoezi hilo ili tuone jinsi ya kuwasaidia makatibu hao ili waweze kukieneza vilivyo cha chetu kwa wananchi wote huko waliko” alisema Asas

Naye katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza alisema ameyapokea maagizo yote na atayafanyia kazi ili idara hiyo mkoa wa Iringa iwe mfano kwa mikoa mingine hapa nchini.

BWALYA SIMBA HACHOMOI.....


Mshambuliaji namba moja wa Nkana ya Zambia, Walter Bwalya ameweka wazi kwamba amepokea ofa ya Simba na Sportif Sfaxien ya Tunisia.

Mchezaji huyo mwenye asili ya DR Congo amesema kwamba bado wako kwenye majadiliano ambayo yanakwenda vizuri na huenda wakakamilishana muda wowote.

Friday, 10 May 2019

WAZIRI BITEKO AZINDUA SOKO KUU LA MADINI MWANZA

Waziri wa Madini, Doto Biteko (pichani) amefanya uzinduzi wa Soko Kuu la Madini Mwanza na kutumia fursa hiyo kuwahimiza wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kutumia soko hilo kuuzia madini yao na kuachana na tabia ya utoroshaji wa madini.

Uzinduzi wa soko hilo unganishi Kanda ya Ziwa umefanyika Mei 08, 2019 katika jengo la Rock City Mall ambapo Biteko amebainisha kwamba uanzishwaji wa masoko ya madini nchini umesaidia ongezeko la kiwango cha uuzaji madini tofauti na hapo awali ambapo yalikuwa yakiuzwa kiholela na hivyo kuikosesha Serikali mapato.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akitoa salamu za tume kwenye uzinduzi huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akitoa taarifa ya hali ya uanzishwaji masoko ya madini nchini ambapo amebainisha kwamba zaidi ya mikoa 10 tayari imeanzisha masoko hayo.
Mfanyabiashara wa madini, Kakono Kaniki akitoa salamu kwa niaba ya wafanyabiashara wa madini mkoani Mwanza.

Mongella ajivunia Soko Kuu la Madini Mwanza "tunataka nchi ifaidike"

DC KASESELA: MARUFUKU KUFANYA BIASHARA IRINGA KAMA HULIPI KODI AU HUNA KITAMBULISHO CHA MACHINGA

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizunguza na wafanyabiashara wa bidha za kusindika walikuwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali
 Wafanyabiashara wa bidha za kusindika wakiwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali na wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa bidhaa za kusindika

 NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Wafanyabiashara wa wilaya ya Iringa wametakiwa kufanya biashara wakiwa wamelipa kodi au wanatakiwa kuwa na kitambulisho cha wafanyabishara wadogo wadogo maarufu kama kitambulisho cha machinga.

Akizungumza na wajasiliamali waliokuwa wamekusanyika katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Iringa,mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema ni marufuku kwa sasa kufanya biashara yoyote wilaya ya Iringa bila kulipa kodi na zile ambazo hazijafikia hatua kodi zitalipa tozo

“Sasa tunaanza kufanya mchakato wa kuchunguza kujua wafanyabiashara wangapi wanafanya kazi hizo bila kulipa kodi na tutawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria za nchi zinavyosema” alisema Kasesela

Kasesela aliwataka wafanyabiashara wadogowadogo wote wa wilaya ya Iringa kuhakikisha wanapata kitambulisho cha kwa shilling elfu ishirini ambacho kinatamruhusu kufanya biashara sehemu yoyote hapa nchini kwa mujibu wa Rais

“Jamani ili ufanye biashara kwa uhuru katika wilaya ya Iringa ni lazima uwe na kitambusho cha wafanyabisahara wadogo au uwe umelipia leseni kutoka katika mamlaka husika la sivyo huwezi kufanya biashara hiyo wilaya ya Iringa” alisema Kasesela

Kasesela aliwataka wananchi wote wanaopenda kufanya biashara kuhakikisha wanafanyabiashara kwa kufuata taratibu zilizowekwa na nchi ili wasipate usumbufu wowote ule kutoka kwa mamlaka za wilaya ya Iringa.

“Jamani wananchi wa Iringa changamkieni kuchukua vitambulisho vya wafanyabishara wadogo wadogo ili kufanya biashara zenu mkiwa na uhuru wa kutosha ila mkikahidi mkono wa sheria utawahusu” alisema Kasesela

Aidha Kasesela aliwashauri wafanyabishara ya bidhaa za kusindika kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa kufuata kanuni za kisheria kwa kuhakikisha wanalipa kodi kama inavyostahili.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo walimuadi mkuu wa wilaya hiyo kuwa watahamasishana kuhakikisha wote wanakuwa na vitambulisho hivyo ili wafanye biashara kwa uhuru na haki.

“Mkuu tunakuhakikishia kuwa tutafanyabiashara huku tukiwa tumevaa vitambulisho hivi kwa kuwa Rais wetu katupa uhuru wa kufanya biashara zetu mahali popote pale bora mradi tuwe na vitambulisho hivyo” walisema wafanyabiashara hao

Friday, 12 April 2019

DSTV YAWASHA MOTO KUELEKEA AFCON U17 2019

 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Omar Singo (aliyevaa koti) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa (Taifa Stars) na maafisa waandamizi wa MultiChoice Tanzania wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni maalum ya DStv Inogile ambayo pia inalenga kuhamasisha umma kwa ajili ya mashindano ya AFCON U17 yanayoanza mwisho wa wiki hii. kutoka kushoto (waliasimama) ni Dua Said, Lubigisa Madata, Edibily Lunyamila, Amri Kiemba, Mohammed Hussein na Fikiri Magoso. Kwa waliokaa  ni Sekilojo Chambua, Ronald  Shelukindo na Salum Salum.


Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Omar Singo (aliyevaa koti) akimkabidhi mchezaji wa zamani wa Taifa Stars Amri Kiemba mpira wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni maalum ya DStv Inogile ambayo pia inalenga kuhamasisha umma kwa ajili ya mashindano ya AFCON U17 yanayoanza mwisho wa wiki hii. Wengine wachezaji wa zamani wa Taifa Stars na maafisa waandamizi wa MultiChoice Tanzania. Miongoni mwao ni  Dua Said, Lubigisa Madata, Edibily Lunyamila, Amri Kiemba, Mohammed Hussein na Fikiri Magoso na Sekilojo Chambua.

Katika kuhakikisha kuwa Tanzania inaendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya kimataifa na Watanzania kushuhudia mubashara timu yao DStv imetangaza rasmi kuwa itarusha mubashara michuano ya kombe la AFCON U17 2019 na hivyo kutangaza kampeni maalum ya kuhamasisha ushindi kwa timu yetu ya Serengeti Boys!

Akizungumza katika hafla ya kuzindua kampeni hiyo ya DStv ijulikanayo kama ‘DStv Inogile’, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Baraka Shelukindo amesema kuwa katika kuunga mkono kampeni ya kuifanya nchi yetu ifanye vizuri katika michezo mbalimbali, DStv imehakikisha kuwa michuano mbalimbali ya kimataifa inarushwa mubashara tena katika kifurushi cha chini kabisa cha DStv Bomba cha Sh. 19,000 tu - hivyo kuwawezesha mamilioni ya watanzania kuziona timu zetu na hivyo kuongeza ari ya kuziunga mkono kwa hali na mali.

Kwa upande wa michuano ya AFCON ya vijana inayoana mwishoni mwa wiki hii, Shelukindo amesema DStv itakuwa ikifanya kampeni kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa njia ya mitandao na matangazo mbalimbali kuhamasisha na kuitia nguvu timu ya taifa ili iweze kufanya vizuri

“Hili ni swala la kitaifa, hivyo tunataka watanzania popote walipo waweze kushuhudia timu yetu ikipambana kwa ajili ya sifa ya nchi yetu” alisema Shelukindo na kuongeza kuwa DStv inaonekana kote barani Afrika hivyo kitendo cha kuonyesha michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini kitaufanya ulimwengu kuyashuhudia mashindano hayo na pia kuitangaza nchi yetu. “Kwa michuano hii kuonekana DStv, ina maana kubwa sana kwa nchi yetu, hii ni njia moja wapo pia ya kuitangaza nchi yetu na Afrika na dunia nzima itambue kuwa na sisi tuna uwezo siyo tu wa kuandaa mashindano haya bali pia wa kuyaonyesha”

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Dr. Omar Singo amesema kuwa kitendo cha DStv kuonyesha mubashara michuano hiyo ni cha kupongezwa kwani ni sifa kubwa kwa nchi yetu. Pia amesema mchango mkubwa unaotolewa na MultiChoice Tanzania katika sekta ya michezo umechangia sana katika kukuza michezo na kuliletea taifa sifa kubwa.
“Serikali inathamini sana michango ya aina mbalimbali inayotolewa na wadau kama DStv katika kukuza michezo hapa nchini. Tunaamini kuwa kwa ushirikiano huu mafanikia haya ambayo tumeanza kuyapata yataendelea na tutafikia azma yetu ya kuwa taifa kubwa kimichezo duniani” alisema Dr. Singo

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake waliowahi kuichezea timu ya Taifa – Taifa Stars ambao walishiriki katika hafla hiyo, mchezaji machachari Amri Kiemba moja kati ya wachezaji nguli waliowahi kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania kwa miaka ya nyuma aieleza kuwa , “Kwa mara ya kwanza Tanzania imepewa heshima kubwa kuyaandaa mashindano haya makubwa hivyo ni wajibu wetu sisi watanzania kuonyesha uzalendo na kuwatia moyo vijana wetu ili kuhakikisha wanashinda katika michuano hii na kupata tiketi ya kwenda kwenye mashindano ya dunia nchini  Brazil”. Wanasoka wengine nguli walioshiriki katika hafla hiyo ni Fikiri Magoso, Dua Said, Lubigisa Madata, Amri Kiemba, Edibily Lunyamila na Sekilojo Chambua

Mbali ya michuano ya kombe hili la vijana wa chini ya miaka 17 itakayoanza hivi karibuni, wateja wa DStv pia wataendelea kufurahia maudhui mbalimbali zikiwemo sinema na tamthilia mbalimbali kutoka nje na hapa nyumbani kama vile msimu mpya wa vichekesho vya Kitimtim, tamthilia ya HUBA, Rebeca kipindi maarufu cha Shilawadu Xtra na bila kusahau kipindi kipya cha Maisha Yangu kinachoelezea maisha na mapito ya watu mashuhuri kutoka hapa nyumbani Tanzania vyote vikiwa vinapatikana kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo iliyopo katika kifurushi cha Bomba.

Wednesday, 3 April 2019

DC KASESELA: MARUFUKU AKINA MAMA KUJIFUNGULIA NYUMBANI


Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka viongozi wa sekta ya afya katika halmauri ya Iringa vijijini kuendelea kutundika bendera nyekundu kwa wananchi ambao hawana vyoo bora ili kutumisha usafi na afya kwa wananchi wote.Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akimpongeza mwenyekiti wa halmshuri ya wilaya ya Iringa Vijijini Stephen Mhapa kumpa tuzo ya ngao kwa kufanya vizuri katika utunzaji wa mazingira pamoja na kuwa na vyoo safi na bora.
 Baadhi ya washiriki waliofika katika kikao hicho cha utoaji tuzo kwa utunzaji bora wa mazingira na kuwa na vyoo bora
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa sambamba na mkurugeni wa halmashauri ya Iringa vijijini Robert Masunya wakinywa maziwa ya asas

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka viongozi wa sekta ya afya katika halmauri ya Iringa vijijini kuendelea kutundika bendera nyekundu kwa wananchi ambao hawana vyoo bora ili kutumisha usafi na afya kwa wananchi wote.

Akizungumza wakati wa utoaji tuzo kwa wananchi,viongozi,taasisi na jumuiya mbalimbali kwa kutekeleza vizuri kampeni ya kuwa na vyoo bora ambavyo vimeipa ushindi halmasahuri ya Iringa Vijijini kwa kupata tuzo ya usafi hapa nchini.

Kasesela alisema kuwa ofisi ya afya katika halmasahuri ya Iringa Vijijini wamekuwa wakisimamia vizuri swala la afya na kuwa na vyoo bora ambapo wanataraji kuwa halmashauri ya kwanza kwa kuwa na vyoo bora kuliko halmashuri zote za mkoa wa Iringa hadi taifa.

“Nampengeza bibi afya wa hapa amekuwa mkali kuhakikisha hakuna mtu anayeweza kukwamisha zoezi lolote la kuboresha sekta ya afya na kuhakikisha afya za wananchi wa wilaya hii wanakuwa na afya njema” alisema Kasesela

Aidha Kasesela amepiga marufuku wa wazazi kujifungulia majumbani kwa kuwa sio sehemu salama kwa uzazi wa mtoto wakati serikali imefanikiwa kuboresha sekta ya afya ambayo ndio kipaumbele cha serikali ya awamu ya tano.

“Jukumu la kwanza kwa baba ni kuhakikisha amempeleka mama kliniki kupata huduma ili kuwa na malezi mazuri ya mtoto,hivyo tutaondoa ile njia ya akinamama kujifungulia majumbani kwa kuwa tayari baba atakuwa anajua wajibu wake” alisema Kasesela

Kasesela amewataka watendaji wa kata,vijiji na maafisa tarafa kuhakikisha hakuna mama anajifungulia nyumbani na nitamshughulikia mtendaji yeyeto Yule ambaye hata wachukulia hatua akibaba watakao fanikisha mama kujifungulia numbani.

Awali akitoa hutuba kwa mgeni rasmi mkurugenzi wa halmasahuri ya Iringa Vijijini Robert Masunya aliwataka  watendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha wameendeleza juhudi hiyo ya kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na vyoo bora ili kupunguza na kumaliza tatizo la milipuko ya magonjwa.

“Niwaombeni tena tuendelee kushirikiana vyema katika kuhakikisha halmasahuri ya Iringa Vijijini inaongoza kwa kuwa na mazingira bora na safi kuliko halmashuri zote hapa nchini kwa kuwa tuna mikakati ambayo ni bora sana” alisema Masunya

MKAZI WA MTWARA ALAMBA MAPESA YA VODACOM TUZO POINTS

 Meneja wa Vodacom Tanzania (PLC), mkoani Mtwara, Charles Minungu (kushoto) akiwa na meneja wa vodashop Mtwara, Frank Daud wakimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi 500,000/-mmoja wa washiriki wa kampeni ya Vodacom M-Pesa Tuzo Points, Eladius Lutha mkazi wa Naliendele katika hafla iliyofanyika Mtwara. Kupitia kampeni hii wateja 140 wa Vodacom walizawadiwa shilingi 25,000/-kila mmoja na baada ya kampeni kumalizika wateja 10 wa Vodacom nchi nzima watazawadiwa shilingi 500,000/-kila mmoja
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube