BREAKING

Tuesday, 22 November 2016

MAJALIWA AMJULIA HALI BABA MZAZI WA WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo kati yake na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda baada ya kuwasili kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma ambako alikwenda kumjulia hali baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Xavery Kayanza Pinda Novemba 22, 2016. Kulia ni Paroko wa Kanisa Kuu Katoliki la Dodoma , Padri Wisi Onesmo na wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kaasim Majaliwa  akiongozana na  Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kuelekea wodini wakati alipokwenda kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma kumjulia hali Mzee Xavery Kayanza Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Novemba  22, 2016. Mzee Pnda amelazwa kwenye hospitali hiyo kwa matibabu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kaasim Majaliwa  akiteta  na  Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda  wakati alipokwenda kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma kumjulia hali Mzee Xavery Kayanza Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Novemba  22, 2016. Mzee Pinda amelazwa kwenye hospitali hiyo kwa matibabu.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Monday, 21 November 2016

MAJALIWA AZUGUMZA NA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII NA WAKUU WA MAPORI YA HIFADHI ZA MISITU


Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akizungumza katika Mkutano ulioitishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  kati yake na Watendaji Wakuu wa  Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakuu wa Mapori  ya Hifadhi za Misitu, Ofisini kwake mjiniDodoma Novemba 21, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


 Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akizungumza katika Mkutano ulioitishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  kati yake na Watendaji Wakuu wa  Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakuu wa Mapori  ya Hifadhi za Misitu, Ofisini kwake mjiniDodoma Novemba 21, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya Watendaji Wakuu  wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Misitu  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao Ofisini kwake mjini Dodoma, Novemba 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya Watendaji Wakuu  wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Misitu  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao Ofisini kwake mjini Dodoma, Novemba 21, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Sunday, 20 November 2016

ATLETICO MADRID WALIVYOLAMIMBISHWA HALUA YA MABAO 3-0 NA REAL MADRID ,CRISTIANO RONALD AKIPIGA HAT - TRICK


Cristiano Ronaldo celebrates after completing his hat-trick in Real Madrid's emphatic derby win against their bitter rivals
Ushangiliaji wa Cristiano Ronaldo ulivyowaacha hoi Atletic Madrid baada ya kufunga mabao 3 (hat-trick) PICHA ZAIDI GONGA HAPA......

WENGER NA MOURINHO KILA MMOJA USO WA MBUZI TAZAMA WALIVYOPEANA MIKONO

Manchester United na Arsenal zimetoshana nguvu sawa katika mchezo wao baada ya kutoka sare ya bao 1-1, lakini mchezo huo licha kuwa wa kuonyesha unaupinzani mkubwa uwanjani,upinzani mwingine bado upo kwa mameneja wa tyimu zote hizo mbili.

Jose Mourinho na Arsene Wenger wanaonekana bado hawaivi chungu kimoja tangu walivyoanza kurushiana maneno miaka kadhaa iliyopita.


Katika mchezo wa leo mara baada ya mechi ya o kumalizika makocha hao walipeana mkono kila mmoja akiwa ameangalia upande mwingine kabisa inshara inayoashiria kuwa mambo si mazuri

walipeana mkono kama sehemu ya kutimiza kile kinachoweza kuitwa bora liende huku kila mmoja akitazama nanapopajua.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1,Arsenal wakilazimika kusawazisha bao likifungwa kwa kichwa na Mfaransa Olvier Giroud akitokea benchi.





Friday, 18 November 2016

NDUGU WA TCHETCHE OUT AZAM FC.....


Timu ya Azam FC imeamua kuachana na kiungo wake wa Kiamataifa kutoka Ivory Coast  Kipre Bolou .

Azam FC, imeachana na nyota huyo baada ya mkataba wake kumalizika na sasa familia ya wawili hao ndugu imeisha kabisa baada ya awali  ndugu yake Kipre Herman Tchetche kuondoka na kuelekea ughaibuni.

Bolou alitua Azam FC akiwa na ndugu yake Tchetche ambaye sasa yupo nchini Oman anakocheza soka la kulipwa.

Thursday, 17 November 2016

QATAR AIRWAYS YAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI KWA KUCHANGIA MADAWATI KISARAWE



Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kumaliza tatizo la madawati mashuleni, Shirika la ndege linalotoa huduma ya usafirishaji wa anga la Qatar Airways nchini Tanzania limechangia msaada wa madawati 100  kwa Shule ya Msingi ya Chanzige B, iliyopo  Kisarawe mkoani Pwani.
Msaada huo wa Qatar Airways  ni sehemu ya mradi wa kusadia juhudi za Serikali kupitia mpango wa kuondoa uhaba wa Madawati nchini hasa shule za msingi ambapo pia  kwa shirika hilo imefanya hivyo kama moja ya kurudisha shukrani kwa jamii.
Akipokea madawati hayo 100, Mbunge wa Kisarawe na Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh.Suleiman  Jafo ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo,  ameshukuru kwa msaada huo kwani umewezesha kupunguza kero kwa wanafunzi waliokuwa wakikaa chini  huku akiomba uongozi wa shule hiyo kuangalia uwezekano wa kugawa madawati hayo shule jirani pale wanapoona panafaa kutokana na uhitaji uliopo.
Aidha, Mh. Jafo ameliomba Shirika hilo la  Qatar Airways kuangalia  uwezekano wa kupiga tafu shule ikiwemo huduma zingine ikiwemo ujenzi wa Maktaba kama watakuwa tayari kwani tayari shule ina eneo la uwanja mkubwa wa ujenzi huo.
“Sisi watanzania. Tunafarijika na utendaji wenu  Qatar Airways wa kazi hapa nchini Tanzania. Ndio maana sasa hivi tunaboresha miundombinu ya uwanja wetu wa ndege hapa nchini. Tunaamini kupitia ndege zenu tutapata watalii mbalimbali ambao watakuwa chachu ya uchumi wa Tanzania” alieleza Mh. Jafo.
Kwa upande wake  Meneja wa Qatar airways Tanzania, Bw. Basek Haydar ameeleza kuwa, wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuchangia huduma za kijamii pamoja na kuimalisha usafiri wa anga  kwa kuwa na safari zake mbalimbali kutokea hapa nchini Tanzania.
Tukio hilo limefanyika Novemba 14.2016 katika viwanja vya shule hiyo ya Chanzige B,  ambapo pia viongozi  mbalimbali walihudhuria  wakkiwemo wafanyakazi wa Qatar na wawakiishi kutoka ofisi ya Doha pamoja na Dk. Amon Mkoga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Amon Mkoga Foundation, bodi ya wakurugenzi, walimu wa shule hiyo, wazazi na wanafunzi.

ai2a0462Mbunge wa Kisarawe na Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh.Suleiman  Jafo akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa tukio hilo la kukabidhiwa madawati.
ai2a0842Baadhi ya madawati hayo
dsc_0733Mwalimu Mkuu wa shule hiyo akisoma hotuba kwa mgeni rasmi.
dsc_0752Meneja wa Qatar airways Tanzania, Bw. Basek Haydar akisoma taarifa ya Shirika hilo namna linavyosaidia jamii pamoja na shughuli zake za usafiri hapa nchini
dsc_0765Mbunge wa Kisarawe na Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh.Suleiman  Jafo akitoa neno la shukrani wakati wa tukio hilo.
dsc_0771Mbunge wa Kisarawe na Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh.Suleiman Jafo, Meneja wa Qatar airways Tanzania, Bw. Basek Haydar na k. Amon Mkoga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Amon Mkoga Foundation wakiwa wameshika cheti maalum katika tukio hilo la ukabidhiwaji wa madawati.
dsc_0783Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Suleima n Jaffo akikata utepe wakati akipokea msaada wa madawati hayo 100.  Anaye fuatia ni Meneja wa Qatar Tanzania Basel Haydar
ai2a0750Meneja wa Qatar Tanzania, Basel Haydar akiwa amekaa katika moja ya dawati katika hafla hiyo.
ai2a0596Picha ya pamoja baada ya kukabidhi madawati hayo
ai2a0766
QATAR TANZANIANaibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mh.  Suleiman  Jaffo na Meneja wa Qatar Tanzania Basel Haydar, wakipokea zawadi kutoka kwa Wanafunzi wa shule ya Msingi Chanzige B, mara baada ya Naibu Waziri Jafo kupokea msaada wa madawati 100 yaliyotolewa na Shirika la Ndege la Qatar Airways.
ai2a0681Mwalimu Mkuu akipokea zawadi kutoka shirika la Qatar 
ai2a0902ai2a0892Baadhi ya wafanyakazi wa Qatar wakifurahia kwa pamoja na baaddhi ya watoto wa shule ya hiyo ya Chanzige B, mara baada ya tukio la kukabidhiwa madawati.
ai2a0526Meneja wa Qatar Tanzania, Basel Haydar akiwa amekaa katika moja ya dawati ndani ya darasa pamoja na wanafunzi 
ai2a0576Moja ya madarasa yakiwa na madawati hayo huku watoto wakiwa wamekalia
QATAR TANZANIANaibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mh.  Suleiman  Jaffo na Meneja wa Qatar Tanzania Basel Haydar, wakipokea zawadi kutoka kwa Wanafunzi wa shule ya Msingi Chanzige B, mara baada ya Naibu Waziri Jafo kupokea msaada wa madawati 100 yaliyotolewa na Shirika la Ndege la Qatar Airways.

HAPI ATAJA MAENEO YA MAGULIO KINONDONI

Na Bashir Nkoromo
Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, imeainisha maeneo ya magulio kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuzitaka mamlaka zinazohusika kutenga maeneo ya wafanyabiashara hao kabla ya kuwatimua katika maeneo yasiyoruhisiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Salum Hapi, ameyataja maeneo hayo kuwa yapo katika kata za Kinondoni, Bunju, Msasani,  Mabwepande,  Kunduchi na Kata ya Wazo.

Hapi amesema, vitu vitakavyoruhiswa kuuzwa kwenye magulio hayo ni bihaa za sokoni, vyombo vya nyumbani,  nguo mpya na mitumba, viatu, urembo, na kwamba kwa ujumla ni bidhaa ambazo hutumiwa na watu katika maisha ya kila siku.

Ametaja mpangilo unaotakiwa kwenye magulio hayo kuwa ni, kupangwa eneo moja bidha zinazofanana, viwepo vyoo vya muda,  na uafi wa eneo la gulio ambao utasimamiwa na Mtendaji Mwenyewe wa eneo husika.
MPANGILIO NA RATIBA  KAMILI YA MAGULIO HAYO



 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube