BREAKING

Monday, 7 December 2015

MKUU WA MAJESHI MSTAAFU,JENERALI GEORGE WAITARA AONGOZA TIMU YA MAAFISA 24 WA JESHI KUPANDA MLIMA KILIMANJARO.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Fulgence Mponji akizungumza katia hafla fupi ya kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa maofisa 24 wa jeshi la wananchi Tanzania .kulia ni Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali George Waitara na kushoto ni Mnadhimu mkuu wa Jeshi la wananchi ,Luteni Jenerali ,Samweli Ndomba.
Baadhi ya washiriki wa zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa majeshi Mstaafu,Jenerali George Waitara akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wapandaji.
Mhifadhi Mkuu ,Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,( KINAPA) akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Washiriki.
Afisa Masoko wa KINAPA,Antypas Mgungusi akieleza jambo wakati wa hafala hiyo.
Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii,Balozi Charles Sanga ni mingoni mwa washiriki wa zoezi hilo la kupanda mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi mkuu KINAPA,Erastus Lufunguro akiongozana na mgeni rasmi kwa ajili ya kukabidhi bendera kwa wapandaji mlima hao.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi,Fulgence Mponji akikabidhi bendera kwa Mkuu wa majeshi mstaafu ,Jenerali George Waitara ambaye ndiye kiongozi wa msafara huo.
Washiriki wakijiandaa kuanza safari.
Safari ya kuelekea kilele cha Mlima Kilimanjaro ikaanza kwa maafisa 24 wa JWTZ .

Wednesday, 2 December 2015

CHAMA CHA AFYA YA JAMII TPHA WATEMBELEA HOSPITALI YA UTAFITI WA MAGONJWA NA TIBA YA "THE BENJAMIN MKAPAULTAMODER HOSPITAL"!!

DSC_2982

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (Tanzania Health Public Association-TPHA) wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wa Hospitali ya Utafiti wa magonjwa na Tiba ya "The Benjamin Mkapa Ultra modern Hospital" iliyopo ndani ya viunga vya Chuo kikuu cha Dodoma UDOM. Ziara hiyo imefanyika jana Desemba Mosi

[DODOMA] Chama cha Afya ya Jamii Tanzania ( Tanzania Health Public Association-TPHA) kipo katika mkutano wake mkuu wa 32 wa mwaka unaofanyika mjini hapa huku ukishirikisha wanachama mbalimbali kutoka 'Chapter' za mikoa zaidi ya 10 nchini.

Mkutano huo wa mwaka ulioanza Novemba 30 mwaka huu na kufunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Chiku Gallawa na viongozi wengine mbalimbali wa mkoa huo umeweza kuwa wa matumaini kwa Serikali kwani imepongeza juhudi zinazofanywa na TPHA hapa nchini ikiwemo kuhakikisha wananchi wote wanapata afya na elimu sahihi ya tiba.

Siku ya pili ya Mkutano huo wa TPHA, Desemba Mosi, Wanachama wameweza kutembelea Hospitali ya Utafiti wa magonjwa na Tiba ya "The Benjamin Mkapa Ultra modern Hospital" iliyopo ndani ya viunga vya Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) na kujionea mambo mbalimbali hi ni kuhakikisha mambo ya msingi katika sekta ya afya yanafanikiwa kama ilivyo dira ya Chama hicho.

Aidha, mada mbalimbali za kitaalamu kuhusiana na masuala ya afya na kisayansi zaidi ya 10 zimeweza kuwasilishwa hiyo jana. 

DSC_3084

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania ( Tanzania Health Public Association-TPHA) wakipata maelezo kutoka kwa Mkandarasi wa jengo hilo la Hospitali ya Utafiti wa magonjwa na Tiba ya "The Benjamin Mkapa Ultra modern Hospital" (aliyekunja mikono katikati).

DSC_3065

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania ( Tanzania Health Public Association-TPHA) wakiwa katika moja ya maeneo ya jengo hilo la Hospitali ya Utafiti wa magonjwa na Tiba ya "The Benjamin Mkapa Ultra modern Hospital" iliyopo ndani ya viunga vya Chuo kikuu cha Dodoma UDOM. 

DSC_2939
DSC_2976

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (Tanzania Health Public Association-TPHA) wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wa Hospitali ya Utafiti wa magonjwa na Tiba ya "The Benjamin Mkapa Ultra modern Hospital".

DSC_2958

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania  (Tanzania Health Public Association-TPHA) wakiongozwa na mwenyeji wao (mwenye koti jeusi mbele) katika Hospitali ya Utafiti wa magonjwa na Tiba ya "The Benjamin Mkapa Ultra modern Hospital".

DSC_3037
DSC_3015

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania ( Tanzania Health Public Association-TPHA) wakiwa katika moja ya chumba cha maabara cha Hospitali ya Utafiti wa magonjwa na Tiba ya "The Benjamin Mkapa Ultra modern Hospital".

DSC_2996

Baadhi ya wanachama wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania ( Tanzania Health Public Association-TPHA) wakipata maelezo ya Hospitali ya Utafiti wa magonjwa na Tiba ya "The Benjamin Mkapa Ultra modern Hospital".

DSC_3082
DSC_2984
DSC_3088
DSC_3066
DSC_2951
DSC_2969
DSC_2976
DSC_2932

Wanachama wakipata picha ya ukumbusho wakati wa kutoka katika jengo hilo
DSC_2924

Administrator wa TPHA, Eric akipiga picha ya ukumbusho katika jengo hilo.. 

CCM ITAMPA USHIRIKIANO MKUBWA DK. MAGUFULI ATEKELEZE ILANI KIKAMILIFU

Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation Ltd, Absalom Kibanda akimkarbisha Karibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, alipotembelea Ofisi za kampini hiyo leo, Sinza jijini Dar es Salaam
 Karibu sana
 Karibu sana hapa ni ofisini kwako
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mhariri wa Habari wa gazeti la Mtanzania, Bakari Kimwanga
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CCM, Godfrey Chongolo akisalimiana na Kibanda
 Wakienda ukumbini

 Wakiwa katika mazungumzo
 Kimwanga akinukuu dondoo za mazungumzo
 Khamis Mkotya akiuliza swali
 Nape akijibu swali
 Mazungumzo yakiendelea
 Asha Bani akiandika dondoo za mazungumzo
 Nape na Hussein Bashe wakifurahia jambo katika mazungumzo
 Naam hayo ndivyo yalivyo.....
 Mkurugenzi wa New Habari Corporation  Erasto Matasya akizungumza






 Mazungumzo baada ya mazungumzo
Nape akiwa na Absalom Kibanda na Asha Muhajj
 Nape akiwa na Asha Bani

Nape akiagana na Bashe kabla ya kuondoka. Picha zote na Bashir Nkoromo

HABARI KAMILI
NA BASHIR NKOROMO
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema, kitampa ushirikiano mkubwa, Rais Dk. John Magufuli, ili aweze kwa ufanisi zaidi mapambano yake dhidi ya mafisadi na mikakati mingine ya kuinua uchumi wa Watanzania.

Kimesema, kitampa ushirikiano huo Rais Dk. Magufuli, kwa sababu, aliyoanza kuyafanya na atakayoyafanya baadaye katika uongozi wake wa Urais anatekeleza yale yaliyomo katika ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020.

Hayo yalisemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akijibu maswali kadhaa yaliyoulizwa na baadhi ya wahariri, aliokuwa akizungumza nao, katika ziara aliyofanya leo, katika Kampuni ya New Habari Corporation, Sinza jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wahariri, waliohoji ni kwa nini CCM haijitokezi kumpongeza Dk. Magufuli katika juhudi ambazo ameanza kuonyesha katika kupambana na ufisadi ikiwemo kubana fedha za walipa kodi ambazo zingepotea bure katika masuala yasiyo ya lazima na wakati huohuo kuanza kuwabana wafanyabiashara wanaodaiwa kukwepa kulipa ushuru.

"Yapo mengi tuliyoanisha katika ilani yetu ya Uchaguzi, na yote yahahusiana sana na haya mnayoyaona yanafanywa na Rais Dk. John Magufuli, tena Ilani hii tumeitunga hata kabla ya kumteua kugombea Urais, Sasa anachofaya ni kuitekeleza ilani hii, isipokuwa mbinu anazotumia ni ubunifu wake na hili hatuna tatizo nalo kama Chama maana kiongozi wa aina hii ndiye tuliyemtaka", alisema Nape.

"Najua wapo wanaojaribu kutengeneza magingira ya kumtaka kumtenganisha Dk. Magufuli na CCM, nawambieni Dk. Magufuli ni zao la CCM na mwana CCM Kindakindaki, hivyo ni upotoshaji wa hali ya juu kujaribu kuuaminisha umma kwamba anayofanya Dk. Magufuli hayana uhusiano na maelekezo ya CCM", aliongeza Nape.

Alisema, baada ya kutengeneza ilani yake, CCM, ilidhamiria kwamba, awamu hii ya tano ni ya kutafsiri uchumi katika nyanja za huduma za Jamii, ikiwemo miundomboni, maji, afya na elimu.

"Ni kutokana na lengo hili, ndiyo sababu tukakaa kwa makini na kuhakikisha ilani hii ya sasa tunamkabidhi mwana CCM ambaye utekelezaji wake hautakuwa wa mashaka mashaka, Ndiyo huyo Dk. Magufuli, bila shaka sasa na ninyi ni mashahidi mmeanza kuuona utekelezaji wake wa ilani", alisema Nape.

Akizungumzia kuhusu Rais Dk. Magufuli kuchelewa kutangaza Baraza lake la Mawaziri, Nape alisema, Chama Cha Mapinduzi kimeshaunda serikali kwa kumpata Rais, kilichobaki sasa ni kwa Rais mwenyewe kuteua watendaji wake, lakini katika kufanya hivyo hakuna mda aliopangiwa kuanza kufanya hivyo na hashurutishwi na Chama wala sheria.

Nape alisema, Dk. Magufuli hachelewi kuteua Baraza la Mawaziri kwa sababu anakosa wakuwateua, isipokuwa, anayo namna na mda ambao mwenyewe Kama Rais amejipangia, na mda huo ukijiri wa kuamua kufanya hvyo atafanya.

"Tatizo hapa ni kwamba mnayo kiu kubwa ya kutaka kujua nani atawateua, sasa kiu yenu imepita kiasi, ndiyo maana mnaanza kuhoji, lakini mimi naamini Dk. Rais Magufuli ataikata kiu yetu, wala msipate taabu ya kuhoji kila kukicha", alisema Nape.

Nape alisema, mbali na Chama kutengeneza ilani ambayo italeta mageuzi makubwa ya kiuchumi hapa nchini, pia Watanzania watarajie kuona mageuzi makubwa ndani ya CCM, kwa sababu yapo njiani kuwadia.

"Kama ilivyo kawaida yetu, kila baada ya uchaguzi mkuu huwa tunafanya tathmini, baada ya tathmini hiyo, huwa lazima tufanye mageuzi kwa yale ambayo tumebaini kuwa ni kikwazo kwa uhai na maendeleo ya Chama katika nyanja mbalimbali, na mageuzi haya tunayafanya kuzingatia mahitaji ya sasa na wakati ujao", alisema Nape.

Kuhusu Mwenyekiti wa sasa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kumwachia Ueneyekiti Rais Dk. Magufuli, Nape alisema, hayo si mambo mageni kwa CCM, imekuwa ikifanyika katika awamu zote za Urais, hivyo Kikwete anaweza akaamua kumwachia kabla ya uchaguzi mkuu wa CCM utakaofanyika mwaka 2017 au kabla ya hapo akiona inafaa.

Zanzibar
Akizungumzia mgogoro wa Zanzibar uliotokana na kufutwa uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar, Nape alikiri kamba ni mbaya na unaitia doa Tanzania, akisema, lakini akasisitiza kwamba njia pekee ya kuumaliza ni kwa mazungumza baina ya viongozi wa ndani bila kushirikishwa mataifa ya nje.

Alisema, msingi wa mgogoro uliojitokeza Zanzibar, si wa kisheria, bali ni wa kisiasa zaidi, hivyo juhudi ziwekwe kwenye mazungumzo kuutatua, na baada ya kuutatua yaendelee kufanyika mazungumzo ambayo yataleta suluhisho la kudumu kwa kuwa imekuwa ni kawaida kwa Zanzibar kuzuka migogoro kila baada ya uchaguzi mkuu jambo linaloonyesha kuwa tatizo ni la asili zaidi kuliko inavyodhaniwa.

Katika mazungumzo yake na wahariri hao wa New Habari Corporation Ltd, Wachapishaji wa magazeti ya Rais, Mtanzania na Dimba, alivitaka vyombo vya habari nchini, sasa kushirikiana na Serikali kulijenga taifa.

"Tunajua wakati wa kampeni kulikuwa na mambo mbalimbali ambayo wakati mwingine vyombo vya habari vililazimika kukampenia vinaowaona kuwa wanafaa kutokana na sababu mbalimbali, lakini kama tulivyokuwa tukisema, kwamba baada ya uchaguzi maisha yataendelea, sasa umefika wakati wa kuendelea na maisha tuwe kitu kimoja", alisema Nape.

Alivitaka vyombo vya habari, kusaidia kuishari Serikali na CCM, katika kutekeleza yaliyo bora kwa taifa na hata pale vyombo hivyo vitakapoona kwamba Chama au serikali vinaenda kinyume, visihofii kukosoa.

Kwa upande wao, Mtariri Mtendaji wa Habari Corporation, Absalom Kibanda akimpongeza Nape kwa ushirikiano ambao amekuwa akivipa vyombo vya habari, na kumtaka aendelee kuwacha milango wazi kwa waandishi wa habari kama ambavyo amekuwa akifanya.

Ziara hiyo ya Nape aliyoianza jana, kwenye vyombo vya habari inatarajiwa kuendelea kesho kwa kutembelea vyombo vingine vya habari vyenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube