BREAKING

Tuesday, 24 August 2021

WAZIRI MKENDA ALIVYOONGOZA MAMIA YA WANANCHI MAZISHI YA BASIL MRAMBA//ANENA MAZITO


Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akitoa salamu za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan wakati akiaga mwili wa marehemu Mhe Basil Mramba katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo katika Wilaya ya rombo Mkoani Kilimanjaro.
Mwili wa marehemu Mhe Basil Mramba katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo katika Wilaya ya rombo Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya ibada ya mazishi.

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda (Kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Stephen Kagaigai (Wa pili kulia) wakiwa katika ibada maalumu ya kuaga  mwili wa marehemu Mhe Basil Mramba katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo katika Wilaya ya rombo Mkoani Kilimanjaro.


Sehemu ya familia ya Marehe Mhe Basil Mramba wakiwa katika ibada maalumu ya kuaga  mwili wa marehemu Mramba katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo katika Wilaya ya rombo Mkoani Kilimanjaro.


Sehemu ya viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika ibada maalumu ya kuaga  mwili wa marehemu Mramba katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo katika Wilaya ya rombo Mkoani Kilimanjaro.


Mwakilishi wa Askofu wa jimbo katoliki la moshi Padre Deogratius Matiika akiendesha misa katika viwanja vya Sabasaba katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro wakati wa ibada ya mazishi ya Mhe Basil Pesambili Mramba.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Stephen Kagaigai akitoa salamu za wananchi wa mkoa huo wakiwa katika ibada maalumu ya kuaga  mwili wa marehemu Mhe Basil Mramba katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo katika Wilaya ya rombo Mkoani Kilimanjaro.


Geofrey Mramba ambaye ni mtoto wa kwanza wa marehemu Mhe Basil Mramba, akisoma wosia wa marehemu baba yake katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo katika Wilaya ya rombo Mkoani Kilimanjaro wakati wa ibada ya mazishi.


Mamia ya wananchi wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro na kwingineko nchini wamejitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo na kushika wadhifa mkubwa akihudumu wakati huo kama waziri wa fedha, Mhe Basil Pesambili Mramba.


Katika shughuli hiyo ya kuaga mwili huo iliyofanyika katika viwanja vya sabasaba vilivyopo katika Halamshauri ya wilaya ya Rombo kwa niaba ya serikali, iliongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda aliyemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan.


Mhe Mramba ambaye alifariki Agosti 17, mwaka huu katika hospitali ya Regency iliyopo mkoani Dar es salam ameagwa katika uwanja wa sabasaba na kisha kuzikwa kijijini kwake Shimbi wilayani Rombo.


Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais Samia,  Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda ambaye amesema Taifa litamkumba Basil Mramba kwa uzalendo na juhudi zake alizozifanya wakati akiwa katika nyadhifa mbalimbali za uwaziri serikali na kusema ameacha alama kubwa kwa Taifa inayopaswa kutambuliwa ipasavyo.


Waziri Mkenda amesema kuwa, Mramba ameacha alama ambazo hazitafutika kamwe katika wilaya ya Rombo hasa katika suala la barabara na kilimo cha ndizi na maparachichi ambacho ndio uchumi mkubwa na tegemezi kwa wananchi wa wilaya hiyo.


"Wananchi wa Rombo kamwe hatutamsahau Mramba kwa mambo makubwa aliyoyafanya wakati wa ubunge wake,wakati anaingia kwenye ubunge kwa mara ya kwanza Rombo ilikuwa na shule nne pekee za Sekondari na mpaka anaondoka kwenye nafasi hii ya ubunge alicha shule zaidi ya 40 kutokana upambanaji wake," Amekaririwa Profesa Mkenda


Waziri huyo wa Kilimo Mhe Profesa Mkenda amewaahidi wananchi wa Jimbo hilo kuwa ataendeleza yale yote ambayo Mramba alitamani kuyakamilisha lakini hayakukamilika wakati alipouwa madarakani.


Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro, Ndg Patrick Boisafi amesema kifo cha Mramba ni pigo kubwa kwa wanachi na wakazi wa Rombo na Taifa kwa ujumla kwani alikuwa ni mtu aliyetumikia Taifa kwa upendo na kulipenda jimbo lake.


"Mramba ameacha alama hapa Rombo na Taifa kwa ujumla, maisha yake yanajieleza na alifanya kazi kubwa kwenye nchi hii na sisi sote ni mashahidi, aliipenda Rombo na Kilimanjaro kwa ujumla tuna cha kujifunza  kupitia kwake, alitumia nafasi aliyopewa na serikali kuwatumikia wananchi wake," Amesema Boisafi


Akizungumza wakati wa ibada ya mazishi, Mwakilishi wa Askofu wa jimbo katoliki la moshi, Padre Deogratius Matiika amesema Mramba ameandika historia katika jimbo hilo na kwa kanisa katoliki na kwamba atakumbukwa kwa mengi kwani alikuwa ni kimbilio la wengi.


"Tutaendelea kumuenzi ndugu yetu Mramba amekuwa ni mti mzuri uliozaa matunda kwani alimpenda Mungu na alimtumikia ipasavyo, alishiriki nasi katika maeneo mbalimbali pale ambapo kulikuwa na msaada kanisani alitusaidia, ameandika historia ambayo haitafutika Kilimanjaro, hakuna anayeweza kupinga hili kwamba aliweka historia wilaya ya Rombo," Amesisitiza Padre Matiika


Mramba alihudumu katika nyadhifa mbalimbali za uwaziri ikiwemo Waziri wa Fedha, Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye pia alikuwa mwanzilishi wa viwanda vidogo vidogo nchini (SIDO)


Wednesday, 18 August 2021

MAAFISA UGANI NI MBONI YA JICHO LA WIZARA YA KILIMO-WAZIRI MKENDA



Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na maafisa ugani wa Wilaya ya Kongwa wakati apokutana na kuzungumza nao katika kikao kazi wilayani humo katika Mkoa wa Dodoma, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kongwa Leo tarehe 17 Agosti 2021. Wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Antony Mtaka (Kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Renidius Mwema. 


Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na maafisa ugani wa Wilaya ya Kongwa wakati apokutana na kuzungumza nao katika kikao kazi wilayani humo katika Mkoa wa Dodoma, 


Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Antony Mtaka wakimkabidhi zawadi ya Televisheni Afisa Ugani Kata ya Ng'humbi Ndg Charles Mujule kama kielelezo cha kufanya kazi kwa ufanisi wakati alipokutana na kuzungumza na maafisa ugani wa Wilaya ya Kongwa katika Mkoa wa Dodoma, 



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Antony Mtaka (Kulia) akizungumza na maafisa ugani wa Wilaya ya Kongwa katika kikao kazi wilayani humo katika Mkoa wa Dodoma, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kongwa Leo tarehe 17 Agosti 2021. Wengine pichani ni Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Renidius Mwema (Kushoto).


Sehemu ya maafisa Ugani wa wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) wakati wa kikao kazi kilichofanyika Leo tarehe 17 Agosti 2021 katika ofisi za Halamshauri ya Wilaya ya kongwa.


Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Kulia), 


Sehemu ya maafisa Ugani wa wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) wakati wa kikao kazi kilichofanyika Leo tarehe 17 Agosti 2021 katika ofisi za Halamshauri ya Wilaya ya kongwa.


Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) amesema kuwa Wizara ya Kilimo ilifanya utafiti ikagundua kuwa ili iweze kupiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta ya kilimo ni wazi kuwa lazima kuwatumia maafisa ugani kwa umuhimu na ufanisi mkubwa.

Amesema kuwa maafisa ugani ndio mboni ya jicho la Wizara ya Kilimo hivyo ili nchi iweze kuwa na kilimo bora kinachokidhi matakwa ya tija na wingi wa uzalishaji na kuwa na kilimo kitakachokidhi matakwa ya soko ni wazi kuwa elimu ni muhimu itolewe kwa wakulima.

Waziri wa Kilimo ameyasema hayo leo tarehe 17 Agosti 2021 wakati akizungumza kwenye kikao kazi na maafisa ugani wa Wilaya ya Kongwa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja wilayani hapo mkoani Dodoma.

Amesema kuwa serikali imeandaa mafunzo rejea kwa maafisa ugani wote nchini ili kuimarisha sekta ya kilimo na kila afisa ugani katika mikoa kielelezo ya Dodoma, Singida na Simiyu atakabidhiwa Pikipiki kwa ajili ya kurahisisha huduma zao kwa kuwafikia wakulima wengi kwa siku.

Ameongeza kuwa pamoja na pikipiki hizo kwa maafisa ugani, pia serikali itawapatia simu za mkononi kwa ajili ya kurahisisha huduma za mawasiliano na wakulima ikiwa ni pamoja na kuzitumia kwa ajili ya taarifa za utendaji kazi wao.

Pia, ameongeza kuwa maafisa ugani wote wanapaswa kuwa na mashamba ya mifano ambayo serikali itaandaa mfumo mzuri kwa ajili ya kuwasaidia pembejeo ili wawe kielelezo kizuri kwa wakulima katika maeneo yao.

“Mimi nikitaka kujua kama kweli afisa ugani anafanya kazi yake inavyotakiwa nikienda kwenye eneo lake si nitaomba tu kuona shamba lake alilolima kisha nitajiridhisha kwamba anafaa” Amekaririwa Waziri Mkenda

Kuhusu kilimo cha alizeti Waziri Mkenda amesema kuwa maafisa ugani wengi wamekuwa wakifanya kazi zisizohusiana na kilimo lakini serikali ipo katika mkakati wa kuwarejesha kwenye majukumu yao ili kuongeza kasi ya kukuza kilimo nchini.

Sunday, 15 August 2021

KAMATI YA KUDUMA YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI YAPONGEZA UWEKEZAJI WA MAZAO YA MBOGAMBOGA, MATUNDA NA MAZAO YA MIZIZI



Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TAHA Dkt Jacqueline Mkindi walipotembelea shamba la kampuni ya uzalishaji wa ndizi pamoja na karanga aina ya Macademia ya Macjaro Ltd iliyopo eneo la Machame katika Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kikazi ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji. Tarehe 14 Agosti 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)



Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni inayohusika na uzalishaji wa vikonyo vya maua  ya Vasso Agroventures ltd Ndg Fons Nijenhuis akitoa ufafanuzi kuhusu uzalishaji wa maua mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakati wa ziara ya kikazi katika shamba hilo lililopo Kijiji cha Mkoringa kilichopo Kata ya Kibosho Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro. Tarehe 14 Agosti 2021.

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akimsikiliza kwa makini 
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akishiriki palizi kwenye migomba alipotembelea shamba la kampuni ya uzalishaji wa ndizi pamoja na karanga aina ya Macademia ya Macjaro Ltd iliyopo eneo la Machame katika Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kikazi ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji. 
Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TAHA Dkt Jacqueline Mkindi (Kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Almas Maige (Kulia) walipotembelea shamba la kampuni ya uzalishaji wa ndizi pamoja na karanga aina ya Macademia ya Macjaro Ltd iliyopo eneo la Machame katika Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kikazi ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji. 

Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Meneja Ubora wa Kampuni inayohusika na uzalishaji, ununuzi na usafirishaji wa maharage Machanga ya African Vegetable Limited liyopo eneo la Machame katika Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kikazi ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji. Tarehe 14 Agosti 2021.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe Dkt. Christine Ishengoma ameipongeza Wizara ya Kilimo pamoja na Taasisi Kilele inayojihusisha na ulimaji wa mbogamboga, maua na mazao ya bustani TAHA kwa uwekezaji mzuri nchini.

Dkt Ishengoma ametoa pongezi hizo tarehe 14 Agosti 2021 mara baada ya kutembelea na kukagua shamba la kampuni ya African Vegetable Limited, Shamba la Macjaro Limited lililopo Machame Wilayani Hai na Shamba la Vasso Agroventures Ltd lililopo katika kijiji cha Mkoringa kata ya Kibosho Wilaya ya Moshi Vijijini.

Mhe Ishengoma ameahidi kuzisimamia na kuhakikisha kuwa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo nchini zinatatuliwa na serikali kupitia Wizara ya kilimo ili kuongeza uwekezaji na ajira kwa watanzania wengi.

Akizungumza katika ziara hiyo Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa sekta ya mbogamboga, maua na mazao ya bustani haina changamoto ya soko hivyo wananchi wanapaswa kuuona umuhimu wa kuwekeza katika sekta hiyo.

Amesema kuwa sehemu kubwa ya mazao mengi nchini wakulima hulima bila kujua soko lilipo lakini katika sekta hiyo mkulima anaweza kulima huku akiwa na uhakika wa soko la ndani nan je ya nchi.

Amesema kuwa serikali inatambua umuhimu wa zao la ndizi hivyo tayari imejipanga kufanya mkutano maalumu kwa ajili ya kuweka mikakati ya kilimo cha zao hilo ikiwa ni pamoja na kufungua maabara ya utafiti ili kuongeza uzalishaji wa mazao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Kilele inayojihusisha na ulimaji wa mbogamboga, maua na mazao ya bustani-TAHA Dkt Jacqueline Mkindi amesema kuwa sekta hiyo imeendelea kupata ushirikiano madhubuti kutoka serikalini jambo ambalo linaimarisha uhusiano wa kiutendaji.

Amesema kuwa ziara hiyo ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imetoa fursa ya kuimarisha sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza uwekezaji utakaotoa fursa kubwa ya ajira kwa vijana ikiwa ni pamoja na kuimarisha kipato cha wananchi.

Amesema Tanzania ina ardhi yenye rutuba nzuri, uwepo wa maji ya kutosha hivyo matarajio yake ni kujipanga vizuri kwenye mifumo na miundombinu ya kufikia masoko ili kutengeneza mapato kwa mwaka kwa zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 6.


 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube