BREAKING

Monday, 8 February 2021

WADAU WA MISITU WAIPONGEZA TFS KUPITIA SAO HILL KWA KUGAWA MICHE YA MITI MILIONI MOJA KILA MWAKA

 Katibu wa umoja wa wavunaji miti mkoa wa Iringa (UWASA)Dr Bazir  Tweve akipokea miche ya miti kwa niaba ya wananchi wengine mbele ya Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti la Sao hill Juma Mwita 




Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wadau wa misitu mkoani Iringa wameipongeza wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi kwa kugawa miti milioni moja kila mwaka kwa wananchi na taasisi mbalimbali zinazolizunguka shamba hilo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa miche ya miti ,katibu wa umoja wa wavunaji miti mkoa wa Iringa (UWASA)Dr Bazir  Tweve alisema kuwa uongozi wa shamba la Sao Hill umekuwa ukitoa miti na elimu ya utunzaji wa miti kwa wananchi wanalizunguka shamba hilo.

Alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu ya uhifadhi misitu kwa wananchi na wadau mbalimbali wanajihusisha nawasiojihusisha na zao la miti kwa kuendelea kutunza na kulinda mazingira yasihalibike kwa njia mbalimbali kama vile kuchoma moto au kukata miti hovyo.

Dr Tweve aliongeza kuwa kitendo cha TFS Mufindi kutoa miche milioni moja kunasaidia kuwakumbusha wananchi kupanda miti na kuitunza vizuri hadi pale itakapofika muda wa kuvunwa kutoakana na aina ya mitia ambayo wameipanda.

Alisema kuwa uchumi wa wilaya ya Mufindi na Mkoa wa Iringa kwa ujumla unategemea misiti hivyo zao la miti linachangia kukuza uchumi wa wananchi mmoja mmoja na kueleta maendeleo kwa ujumla kwa wananchi wa mkoa wa iringa nan je ya Iringa.

Dr tweve aliwaomba uongozi wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindikutoa elimu ya uvunaji wa miti ili kuepukana na wananchi kuvuna miti ikiwa bado haijakomaa kuvunwa na kupeleka bidhaa ambayo haihitajiki sokoni.

 “Sasa hizi imezuka tabia ya wananchi wanaomiliki mashamba binafsi kuvuna miti ambayo haijakomaa kuvunwa kutoka na hali ya uchumi hivyo niwaombe mfike kwa wananchi na kutoa elimu hiyo kipindi mnatoa miche na baada ya miche hiyo kupandwa” alisema Dr tweve

 

Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi,Peter Tweve aliwashukuru wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi kwa kazi kubwa wanayifanya ya kutunza maziringa na kutoa elimu ya mazingira kwa wananchi wanaolizunguka shamba hilo.

 Alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Mufindi kwa kiasi kikubwa uchumi wake unategemea Misiti hiyo kitendo cha Sao Hill kutoa miche kwa wananchi kunahamasisha wananchi kuendelea kupanda miti na kutunza mazingara.

Naye Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti la Sao hill Juma Mwita alisema kuwa wameyapokea mawazo ya wadau na kuahidi kuyafanyia kazi ikiwapo swala la kutoa elimu kwa wananchi wanaovuna miti mapema kabla ya muda wake.

 

Alisema kuwa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi wamekuwa wakitoa elimu hiyo na wataendelea kutoa elimu mara kwa mara lengo la wananchi wawe na uelewa wa utunzaji wa mazingira.

 

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube