BREAKING

Saturday, 19 December 2020

AZAM FC YA MSEMAJI ZAKA ZA KAZI NA ILE YA LWANDAMINA INAVYOSHANGAZA....

 


Nelson Mandela, rais wa kwanza wa Afrika Kusini alikuwa wakwanza kuchaguliwa kidemokrasia na hatimaye akaja kuwa Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, ,alifariki 
Desemba 5,mwaka  2013 akiwa na umri wa miaka 95, alikuwa shujaa kila wakati alizungumza kwa staha , alisema maneno kwa adabu na hekima , mafano aliwahi kusema  "I am not a saint, unless you think of a saint as a sinner who keeps on trying.”  akiwa na maana kuwa " Msinihukumu kwa mafanikio yangu, nihukumuni kwa mara ngapi nilianguka na kuinuka tena"Mwisho wa kunukuu, sina maana ya kuzungumza siasa hapa ninachotaka kukizungumza ni kimoja katika soka husuani Msemaji wa Azam FC Zaka za Kazi Vs Lwandamina.... Zaka ni Msemaji hodari, lakini Lwandamina ni Kocha Mahiri wa Azam FC vitendo vya Lwandamina na Zaka ni Mbingu na Ardhi wakati Zaka akituaminisha msimu huu ubingwa unatua ndani ya klabu hiyo kocha wao Mzambia akili yake wala haimsikilizi kwani hadi sasa Azam FC sare zao ni mfanano wa Maua jana Azam FC ilikubali sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Desemba 18, Uwanja wa Azam Complex, ukiwa ni mwendelezo wa matokeo mabovu kwa Lambalamba hao

Katika mchezo wa jana nyota njema ilianzia kwa Nyota wa Azam FC Ayub  Lyanga alikuwa wa kwanza kucheka na nyavu dakika ya 34, bao hilo lilidumu mpaka muda wa mapumziko na kuwafanya vijana wa Charles Mkwasa kwenda vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa nyuma kwa bao moja.

 Kipindi cha pili Iliwachukua dakika 7 Ruvu kuweka mzani sawa kupitia kwa Emmanuel Martin baada ya kipindi kuanza kwa kufunga bao dakika ya 53 ambalo lilidumu kwa muda wa dakika 7 likapinduliwa na Mudahthiri Yahya dakika ya 60.


Ruvu walitumia dakika 10 kusawazisha bao hilo ambapo dakika ya 70 Fully Zully Maganga aliweka mzani sawa na kufanya ubao usome 2-2.

Ni Idd Seleman kwa Azam FC alionyeshwa kadi ya njano huku wajeda wanne walionyeshwa kadi za njano kutokana na nguvu na spidi ndani ya Uwanja wa Azam Complex.


Hii inakuwa ni sare ya pili mfululizo kwa Azam FC ndani ya Uwanja wa Azam Complex baada ya mchezo wao uliopita kufanya hivyo mbele ya Namungo FC na iligawana pointi mojamoja kwa kufungana mabao 2-2.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ibaki nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi 16 kibindoni ina pointi 29 huku Ruvu ikiwa nafasi ya nne na pointi 25 nayo pia imecheza michezo 16.


No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube