Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Mafinga Reginant Kivinge akiongea madiwani,watendaji na wananchi waliohudhuria ufunguzi wa baraza hilo.
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini na mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve wakiwa kwenye uzinduzi wa baraza hilo la madiwani
MADIWANI wa
Halmashauri ya mji wa Mafinga mkoani Iringa wametakiwa kufanya kazi kwa
ushirikiano mkubwa ili kureta maendeleo kwa wananchi waliwachagua na kuwapa
dhamana ya kuwepo madarakani mara baada ya uchaguzi mkuu
Akizungumza mara
baada ya kuzinduliwa kwa baraza jipya la madiwani wa Halmashauri ya mji wa
Mafinga,mwenyekiti wa halmashauri hiyo Reginant Kivinge alisema kuwa wananchi
wanamatumaini makubwa ya kimaendeleo kutoka kwa madiwani hao hivyo wanapaswa
kwenda kuchapa kazi kwa nguvu zao zote.
Kivinge alimuomba
mkurugenzi wa halmashauri hiyo Saada Mwaruka pamoja na watendaji wote
kuhakikisha wanashirikiana kwa ukaribu ili kuhakikisha wanatatua na kumaliza
kero zote zinazowakabili wananchi.
Alisema kuwa
halmashauri hiyo bado inakabiriwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa
zikikwamisha juhudi za kureta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini
hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa umoja wao ili kuleta maendeleo kwa wananchi
yanayotarajiwa.
"Natambua
uchaguzi huu ulioisha tulipitia mambo mengi sana,lakini sasa uchaguzi
umekwisha ni mwendo wa kuchapa kazi sasa twende kuchapa kazi ili
turudishe ile heshima muliyopewa na wananchi wetu kwa kutuchagua " alisema
Kwa upande wake mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi wa (CCM) wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa Daudi Yasini
amewataka madiwani wa halimashauri ya Mji Mafinga kwenda kushungulika na
kutatua kero za wananchi kwani chama hicho hakitasita kumchukulia hatua diwani
yoyote asiyetimiza majukumu yake ipasavyo .
Kauli hiyo
imetolewa wakati wa kikao cha kwanza cha madiwani wa halmashauri hiyo baada ya kula
kiapo cha utii wa kuwatumikia wananchi kwa kufuata kanuni za maadili ya
utumishi wa umma
Daudi alisema kuwa
wananchi wamekuwa na imani kubwa na chama cha mapinduzi hivyo hivyo wanapaswa
kuheshimu na kuthamini nafasi waliyopewa kwa kufanya kazi kwa weredi na
ushirikiano kuhakikisha wanatatua kero za wananchi wa halamshauri hiyo.
"Tumekuwa na
uchaguzi nyingi ila uchaguzi wa mwaka huu tumeweka historia kwa wilaya ya
Mufindi kwa baraza letu lote ni CCM na hii ni kwa sababu ya kazi kubwa
iliyofanywa na mh Rais Magufuli hivyo naamini hamtatuangusha mkatumikie nafasi
muliyopewa kwa weredi uliotukuka"
Daudi alitoa onyo
kali kwa madiwani wote wanaodhani wamepewa nafasi hiyo kwa ajili ya
kujinufaisha wao au kujipatia mali katika Halmashauri hiyo,chama cha mapinduzi
kitapita kata kwa kata kuhakikisha kuwa viongozi waliochaguliwa wanatatua kero
za wananchi la sivyo hatua kali zitachukuliwa kwa Diwani husika.
“Niwaonye wale wote
ambao mnadhani mmepata nafasi ya kwenda kupiga dili halimashauri hapa ni kazi
tu na endapo tutakuja kwenye kata yako na kukuta wananchi wanalalamika kero
nyingi hazitatatuliwa basi hawatasita kuwachukulia hatua” alisema Daudi
Hata hivyo Daudi
alimtaka mkurugenzi pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo kushirikiana vyema
na madiwani hao ili kutatua kero za wananchi zinazowakabili na sio kupishana
kwenye maamuzi ya vikao ambavyo lengo ni kupunguza mzigo wa kero kwa wananchi
Naye katibu wa CCM
wilaya ya Mufindi James Mgego aliwashukuru madiwani hao kwa uvumilivu na
ushindi waliopata kwenye uchaguzi uliopita kwani walipita kwenye viunzi na
vikwanzo Vingi mpaka kufika hapo walipo
Mgego alisema kuwa
wananchi wamemaliza kazi yao na wajibu wao hivyo sasa ni wakati wa madiwani hao
kurudisha dhamana na heshima waliyopewa kwa kwenda kuwatumikia na kutatua kero
za wananchi
Alisema chama hicho
kinatambua dhamana kubwa waliyopewa na wananchi hao kwa kuonyesha imani kwa
chama hicho hivyo wanadeni kubwa la kurudisha maendeleo ya kweli kwa
watanzania wote bila kujali itikadi ya vyama kwani uchaguzi umekwisha na
sasa ni muda wa kuchapa kazi
Lakini pia Mbunge wa jimbo la Mafinga Cosato Chumi alissema
kuwa anataka kupeleka mapendekezo bungeni ili kuweza kupata kibali na
kubadili sheria ili kufanya biashara kwa mji wa Mafinga masaa 24 kwani wilaya
hiyo inapitiwa na barabara kuu hivyo itakuwa ni fursa ya kukuza uchumi kwa
wakazi wa Mafinga na kuongeza pato la halimashauri hiyo endapo watu watafanya
biashara masaa 24
Mkurugenzi wa halmashauri
ya Mji wa Mafinga Saada Mwaruka alisema kuwa watendaji wote wa halmashauri
hiyo wapo tayari kujitolea na kuonyesha ushirikiano kwa madiwani wote ili
kuhakikisha wanatatua kero za wananchi na kuleta maendeleo katika Jimbo la
Mafinga Mjini.