BREAKING

Tuesday, 10 March 2020

TARURA SITISHENI UJENZI WA BARABARA ZA VUMBI HADI MVUA ZITAKAPO SIMAMA

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akizungumza kwenye ziara ya Iringa mpya awamu ya pili alipokuwa anakagua ujenzi wa barabara yaKinyanambo, Pareto,Chumi,Lutherani na Mwamkoa Mbagala iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga akiwataka wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA) kusitisha ujenzi wa barabara hizo kwa kuwa ujenzi huo hauna tija kwa wananchi
 Baadhi ya uharibifu unaondelea kwenye maeneo ambayo ujenzi wa barabara unaendelea hivi sasa kwenye maeneo ya Mji wa Mafinaga Mji.
 Baadhi ya uharibifu unaondelea kwenye maeneo ambayo ujenzi wa barabara unaendelea hivi sasa kwenye maeneo ya Mji wa Mafinaga Mji

NA FREDY MGUNDA,MUFINDI.

SERIKALI ya mkoa wa Iringa imewataka wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA) kusitisha ujenzi wa barabara za vumbi zinazoendelea kujengwa na wakandarasi mbalimbali kutokana mvua kubwa zinazoendelea hivi sasa.

Akizungumza kwenye ziara ya Iringa mpya awamu ya pili alipokuwa anakagua ujenzi wa barabara yaKinyanambo, Pareto,Chumi,Lutherani na Mwamkoa Mbagala iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga,mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi aliwataka wakala wa barabara mjini na vijijini (TARURA) kusitisha ujenzi wa barabara hizo kwa kuwa ujenzi huo hauna tija kwa wananchi.

Kipindi hiki mvua zinanyesha kwa wingi kila kona na zimekuwa zikiharibu miundombinu katika maeneo mengi katika mkoa huu wa Iringa,hivyo kutokana na hali hiyo natangaza kusitisha ujenzi wa barabara hizo hadi pale mvua zitakapo isha.

Hapi aliwataka viongozi wa TARURA kuhakikisha wanawasimamia vilivyo wakandarasi wote wanajenga barabara hizo ili zijengwe katika ubora unatakiwa kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

“Hakikisheni mnawasimamia vilivyo wakandarasi hao kwa kuwa fedha zinazotumika ni kodi za wananchi hao ambao mnawaona hapa,hivyo lazima thamani ya fedha hizo ionekane kwa wananchi hawa” alisema Hapi

Hapi aliwataka TARURA kuongeza kasi ya ujenzi wa mitandao ya barabara za lami katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga na ujenzi wa taa za barabarani ili Halmashauri ya Mji wa Mafinga kuwa Manispaa na hatimaye mkoa wa Iringa kuwa Jiji.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliamu aliwataka TARURA  kujenga mitaro yenye ubora unaotakiwa ikiwa na lengo la kuhakikisha kuwa inamudu maji yote yanayopita na kuzilinda barabara zisiaharibike haraka na zidumu kwa muda mrefu.

“Barabara zetu nyingi za wilaya hii zinaharibika kutokana na kutokuwa na mitaro iliyobora inayohimili maji mengi na ndio maana barabara zinaharibika kila uchwao hizi ni bora kuweni wakali kwa wakandarasi wanaopewa tenda za mitaro kwenye barabara husika” alisema Wiliam

Akijibia hoja za mkuu wa mkoa,mwananchi Inocent Mahanga na mkuu wa wilaya ya Mufindi,meneja wa TARURA Mafinga Tc Injinia Simoni Ngagani alisema kuwa watahakikisha barabara zinajengwa kwenye ubora unatakiwa kulingana na thamani ya fedha za mradi husika.

Tutahakikisha ujenzi wa Mifereji na barabara zinajengwa kwa viwango stahili ili kutumia vilizuri kodi za wananchi


No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube