BREAKING

Friday 22 March 2019

DSTV YATOA ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHEN YA TIA KITU PATA VITUZ!

 Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo akichezesha droo ya kupata washindi wa huku Afisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Humudi Semvua  (kulia) akifuatilia kwa makini. Kushoto ni Benson Urio wa kitengo cha Teknohama cha DStv. Promosheni hiyo ni kwa wateja wanaolipia kwa wakati kabla vifurushi vyao havijakatika hivyo kupata fursa ya kushinda kifurushi cha miezi miwili. Promosheni hiyo itaendelea kwa wiki 8 ambapo jumla ya washindi 120 watapatikana.

z!


Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo (Katikati) Akizungumza kwa ismu na moja ya washindi wa promosheni hiyo.  Kulia ni Afisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Humudi Semvua  na kushoto ni Afisa Uhusiano Grace  Mgaya  Promosheni hiyo ni kwa wateja wanaolipia kwa wakati kabla vifurushi vyao havijakatika hivyo kupata fursa ya kushinda kifurushi cha miezi miwili. Promosheni hiyo itaendelea kwa wiki 8 ambapo jumla ya washindi 120 watapatikana.
 Kampuni ya inayoongoza kwa huduma bora za vinga’muzi nchini, DStv  imetangaza washindi 15 wa  droo ya 4 ya  Promosheni hiyo ya wiki nane inayoendelea  nchi nzima maarufu kama “ Tia Kitu pata vituz”.

Promosheni hiyo ni ya wazi kwa wateja wote wa DStv ambao watalipia vifurushi vyao kabla havijakatika. “Mteja yeyote wa DStv atakayelipia kifurushi chake kabla hakijakatika moja kwa moja anaingia katika droo na fursa ya kujishindia kifurushi chake kwa muda wa miezi miwili.” Alisema Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo wakati wa kufanya droo ya wiki ya nne ya promosheni hiyo.

Akizungumza  baada ya kufahamishwa juu ya ushindi wake huo Bw. Issa Mohammed ambaye ni mteja wa DStv aliyepo mkoani Dar es Salaam alisema kuwa amefurahi sana kuibuka mshindi na kuongeza kuwa anaishukuru sana DStv na kuwaasa kuwa waendelea kuwajali wateja wake hivyo hivyo.


No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube