BREAKING

Thursday, 28 July 2016

PAPA FRANCIS AANGUKA AKIONGOZA IBADA POLAND




Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameteleza na kuanguka alipokuwa akielekea kwenye altare kuongoza ibada ya misa nchini Poland.

Papa Francis alikosa kukanyaga vyema kidato kimoja na akaanguka katika madhabahu matakatifu zaidi nchini humo, madhabahu ya Jasna Gora.

Papa, mwenye umri wa miaka 79, mzaliwa wa Argentina, alionekana akitembea akiwa anatafakari sana, na hakugundua kulikuwa na kidato kimoja kabla ya kufikia altare, shirika la habari la AP limeripoti.

Mapadre waliokuwa karibu naye walikimbia na kumsaidia kuinuka.

Misa iliendelea kama ilivyopangwa na papa alihubiri kwa muda mrefu mbele ya maelfu ya waumini waliokusanyika Jasna Gora katika jiji la Czestochowa, kusini mwa nchi hiyo

Shirika la habari la AFP linasema aliinuka upesi, na hakuonekana kuumia hata kidogo.

Alipoulizwa iwapo Francis aliumia baada ya kuanguka, msemaji wa Vatican Greg Burke ameambia wanahabari “papa yuko salama”.

Papa amewahi kuteleza na hata kuanguka mara kadha awali, na kila mara huwa anainuka peke yake au kusaidiwa na mmoja wa wasaidizi wake, shirika la AP linasema.

Kila mara huenda anaendelea na shughuli zake baadaye kama kawaida.

SIMBA USO KWA USO NA TIMU YA KOCHA WAO WA ZAMANI LOGA...KUTOKA ANGOLA SIMBA DAY


Viongozi na wanachama mbalimbali wa Simba watachangia damu katika hospitali mbalimbali nchini kauli iliyotolewa na Rais wa Simba, Evans Aveva ambapo amesema watafanya hivyo ikiwe ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Simba kwenda kusherekea miaka 80 ya klabu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Aveva amesema Siku kamili ya sherehe itakuwa ni Agosti 8 ikiwa ni kawaida ya klabu hiyo kufanya tamasha la Simba Day ambalo hufanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijiji Dar es Salaamm

Simba wamekuwa wakifanya Tamasha hilo likiwa ni sehemu pia ya kuwatambulisha wachezaji wao wapya waliowasajili kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania bara, utamaduni ambao wamekuwa wakiufanya kila mwaka.

Aveva ameeleza pia katika wiki nzima ambayo watakuwa wakifanya kazi za kijamanii watatumia muda huo kuzngumza na wanachama wao juu ya mstakabali wa timu yao na kuhakikisha inafanya vyema katika msimu mpya unaoaanza mapema mwezi Agosti.


Simba pia itamenyana na timu ya aliyekuwa kocha wao wa zamani anayekinoa kikosi cha Girabola Zdravko Logarusic

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, DK ANGELINA MABULA AAGIZA HALMASHAURI YA UYUI KUKAMILISHA UNUNUZI WA NYUMBA ZA NHC UYUI

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akitembelea nyumba za gharama nafuu Uyui zilizopo Isikizya wilayani Uyui, Tabora ambapo ameiagiza Halmashauri ya Uyui kulipia nyumba zilizojengwa na NHC ili watumishi wake waweze kuhamia. Kushoto kwake ni Meneja wa NHC mkoani Tabora, Dickson Ngonde.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tabora muda mfupi baada ya kutembelea nyumba za gharama nafuu Uyui ambapo ameiagiza Halmashauri ya Uyui kulipia nyumba zilizojengwa na NHC ili watumishi wake waweze kuhamia. PICHA ZOTE ZA KITENGO CHA MAWASILIANO KWA UMMA NA HUDUMA KWA JAMII CHA NHC.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisikiliza taarifa kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora, Bw. Biseko Musiba wakati Waziri huyo alipofanya ziara katika mkoa wa Tabora na kujione hali ya maendeleo ya sekta ya ardhi mkoani humo pamoja na kutembelea miradi ya maendeleo ya taasisi zake.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akimsikiliza Kamishna Msaidzi wa Kanda ya Magharibi, Dorothy Wanzala wakati akikagua masjala ya ardhi ya Tabora.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisoma mojawapo ya mafaili yaliyopo katika masjala ya Ardhi huku Kamishna Msaidizi wa Kanda ya Magharibi, Dorothy Wanzala akishuhudia.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Tabora muda mfupi baada ya kufika katika ofisi hizo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akizungumza na watumishi mbalimbali wa sekta ya ardhi mkoani Tabora.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Tabora muda mfupi baada ya kufika katika ofisi hizo.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,MHANDISI RAMO MAKANI AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA HIFADHI YA TAIFA YA KISIWA CHA RUBONDO.

Naibu Waziri wa Maliasilili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani ,akiviishwa vazi maalum (Boya) ambalo hutumika kujiokoa wakati uafiri wa maji unatumika.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhandisi Ramo Makani akiingia kwenye Boti kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo,Misana Mwishawa akimueleza jambo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani wakati akitembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo.
Mamba ni moja ya vivutio katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo ambayo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani alivutiwa kuwatizama.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akitizama vivutio mbalimbali wakati akizunguka na boti maalumu katika visiwa vilivyoko Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo,Missana Mwishawa akimuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani eneo ambalo ni makazi na mazalia ya ndege katika moja ya visiwa vilivyoko katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi alikuwa ni mmoja wa viongozi walioongozana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani kazika ziara hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizunbgumza jambo mara baada ya kupata maelezo mbalimbali kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo,Misana Mwishawa
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akitia saini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika hoteli ya Asilia Lodge iliyopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa akizungumza wakati wa kikao kifupi cha Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili ,Mhandisi Ramo Makani na viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini,Joseph Kasheku (Msukuma) akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akizungumza katika kikao hicho.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na viongozi wa serikali ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo alipokutana nao katika Hoteli ya Asilia Lodge.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na mmoja wa wageni katika Hoteli ya Asilia Lodge iliyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Ugeni wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani ukipunga mikono kuaga wenyeji wao katika Hoteli ya Asilia Lodge ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
Mwenyekitib wa CCM Dk JohnMagufuli akizunguza
na wafanyakazi wa CCM Makao Makiiu yaCCM mjini
Dodoma leo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mara ya kwanza amekutana na kuzungumza na wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho na baadaye wafanyakazi wa CCM Makao Makuu katika Ofisi za Chama hicho Mjini Dodoma ikiwa ni siku tano tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Tano wa Chama hicho.

Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amekutana na watendaji hao wa CCM kwa lengo la kuwasalimia, kupokea maoni na ushauri wao juu ya utendaji kazi ndani ya Chama.

Katika mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewapongeza watendaji wote wa Chama Cha Mapinduzi kwa kazi kubwa wanayoifanya na kwa namna ya pekee kwa jinsi walivyotoa mchango mkubwa kuhakikisha CCM inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Pia amewataka kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa lengo la kuendelea kukiimarisha Chama hicho ambacho kimebeba dhamana ya kuongoza Serikali kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Dkt. Magufuli amewahakikishia kuwa chini ya uongozi wake atafanyia kazi changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi wa CCM ikiwemo maslahi duni, vitendea kazi na kuondoa utegemezi.

Aidha, Dkt. Magufuli amewataka watumishi wa chama kutoa ushirikiano katika zoezi la uhakiki wa mali za Chama litakalosimamiwa na sekretarieti ya chama na ameahidi kuwa atahakikisha mapato yatokanayo na vyanzo vya mapato vya chama yanatumika ipasavyo.

Kwa upande wao watumishi wa CCM wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdulrahaman Kinana wamempongeza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kwa asilimia mia moja na wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika tarehe 23 Julai, 2016 Mjini Dodoma kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa.
Watumishi hao wamemuahidi kuendeleza utumishi uliotukuka na wameelezea matumaini yao ya kuboreshewa maslahi.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

WAREMBO WANAOWANIA SHINDANO YA MISS TANGA 2016 USIPIME SASA KUFANYIKA IJUMAA MJINI TANGA





 Warembo wanaowania Taji la Mrembo wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016) wakiwa kwenye pozi katika hotel ya Tanga Beach Resort kutakapofanyika shindano hilo Ijumaa Kesho.


Warembo hao wakiwa kwenye picha ya pozi






Warembo wanaowania Taji la Urembo Mkoa wa Tanga(Miss Tanga 2016) ambalo linaandaliwa na Kituo cha Radio cha TK FM cha Mjini Tanga kwa kushirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort wakiwa kwenye picha ya mapozi




Mratibu wa Shindano ya Miss Tanga 2016,Mboni Muya akizungumza na waandishi wa Habari leo kuhusiana na maandalizi ya kuelekea shindano hilo




Baadhi ya Warembo wakimsikiliza Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa nchini Sinza,Beny Kisaka alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kuitembelea kambi ya warembo hao wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Nassoro Makau


Warembo hao wakimsikiliza Mratibu wa Shindano ya Miss Sinza 2016 ambaye aliitembelea kambi hiyo leo


 Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa nchini,Benny Kisaka akitoa nasaha kwa warembo wanaotarajiwa kushiriki kinyang'anyiro cha kumtafuta Mlimbwende wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016 )itakayofanyika Ijumaa kesho  kwenye Ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort.
 Mdau wa Tasnia ya Urembo hapa nchini,Benny Kisaka akisisitiza jambo wakati akizungumza na warembo wanaotarajiwa kushiriki shindano la kumtafuta Mlimbwende wa Mkoa wa Tanga Ijumaa


Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Wednesday, 20 July 2016

WANAHABARI WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA GOMBE.

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika Boti wakielekea Hifadhi ya Taifa ya Gombe,hifadhi maarufu kwa kuwa na mnyama aina ya Sokwe mtu.
Watalii wakielekea Hifadhi ya Taifa ya Gombe .
Eneo mojawapo linalotumiwa na wavuvi katika mwambao mwa ziwa Tanganyika jirani na Hifadhi ya taifa ya Gombe.
Baadhi ya wanahabari muda mfupi baada ya kufika hifadhi ya taifa ya Gombe.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) ,Pascal Shelutete akiwatamburisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini  walipotembelea hifadhi ya taifa ya Gombe.
Kaimu Mhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe,Goodluck Tarimo akizungumza na wanahabari waliotembelea hifadhi hiyo.
Baadhi ya Wahifadhi waongoza wataalii katika Hifadhi ya taifa ya Gombe.
Daktari wa Mifugo katika Hifdhi ya Taifa ya Gombe,Dkt Jane Raphael akizngumza mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kabla ya kuaza safari ya kutembelea hifadhi hiyo.
Mhifadhi Hussein 
Mhifadhi Isaya Mkude akitoa maelezo kwa wanahabari wakati wa kuanza safari ya kwenda kuwatizama Sokwe.
Safari ya kwenda kuwatizama Sokwe ikaanza.
Maeneo mengine Mhifadhi Isaya Mkude aalikua akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali na majibu ya maswali yaliyoulizwa na wanahabari.
Nyani ni miongoni mwa wanyama wanaoonekana kwa urahisi katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Safari ya kuwatafuta Sokwe ili kua ni ya vipando pia.
Wakati mwingine wanahabari walilazimika kupumzika kwa ajili ya kupata pumzi mpya ya kuendelea na safari 
 Baadhi ya Sokwe mtu walioonekana kwa mbaali sana wakiwa katika miti.
Hatimaye safari ya kurudi katika makazi ikaanza kwa kupita katika fukwe ya ziwa Tanganyika inayopakana na hifadhi ya taifa ya Gombe. 

Na Dixon Busagaga wa Michzui Blog.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube