BREAKING

Wednesday, 11 May 2022

TANESCO KUNUNUA NGUZO ZA UMEME NCHINI,WAZIRI ATANGAZA MASHARTI YAKE.


Waziri wa nishati January Makamba akiongea na wadau wa nguzo za umeme mkoani Iringa akiwaondolea sitofaumu iliyokuwepo ya kutonunua nguzo zao
Waziri wa nishati January Makamba akiwasikiliza wadau wa nguzo za umeme mkoani Iringa akiwaondolea sitofaumu iliyokuwepo ya kutonunua nguzo zaoWaziri wa nishati January Makambaakiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga wakati wa majadiliano ya kuondoa sitofaumu iliyokuwepo ya kutonunua nguzo zao

 

Na Fredy Mgunda,Iringa.

WAZIRI wa nishati January Makamba ameliagiza shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuingia zabuni za ununuzi wa nguzo za kusambaza umeme kwa wakandarasi wanaokidhi vigezo,ikiwemo kuthibitisha baadhi ya nguzo zimetoka kwa wazalishaji wadogo wa ndani.

Waziri Makamba alisema kuwa TANESCO inatakiwa kushirikiana na taasisi zinazosimamia ubora wa bidhaa,ikiwepo shirika la viwango nchini (TBS) ili kuhakikisha nguzo zinazonunuliwa zinakidhi viwango vinavyotakiwa na shirika hilo.

Makamba alisema kuwa ili kuondoa changamoto kwa wadau wa nguzo na serikali ataunda kamati y wadau wa nguzo watakaokuwa wanafuatilia namna ya utengenezaji wa nguzo bora za umeme ambao utasaidia kuuza nje ya nchi ambavyo wadau wanguzo nchi nyingine wanafanya kwa ubora unaotakiwa.

“Sasa ipo mifano ya mfumo huu wa uwekezaji wa viwanda vya nguzo,nchi kama Afrika Kusini inamfumo mzuri sana na serikali yenu ipo tayari kuwachukua watu kadhaa kwenye kila wadau na kuwapeleka na kuwalipia mkajifunze kuhusu mfumo wa kudhibiti na kuhusu ubora” alisema makamba

Aidha aliwatoa hofu wadau wa nguzo za Miti za Umeme nchini kwa kuwahakikishia soko la kuuza nguzo zenye ubora kwa Shirika la Umeme nchini( TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini ( REA), hapa nchini.

Makamba alisema kuwa mkutano ulilenga kuondoa sintofahamu pamoja na minong’ono inayoendelea kwa baadhi ya watu wanaopotosha kuwa Serikali haitanunua nguzo za Umeme za ndani na badala yake zitaagizwa kutoka nje ya Nchi.

Katika mazungumzo yake na Wadau hao, Makamba alisema kuwa, Serikali itaendelea kununua nguzo za miti za Umeme kutoka kwa wazalishaji wa ndani ili kulinda viwanda vya ndani kwa kuzingatia ubora wa nguzo uliowekwa.

“Tutakapo toa zabuni ili ufanikiwe kupata zabuni hiyo lazima angalau asilimia Fulani ya nguzo hizo utakazouza ziwe zimetoka ka watu wadogo wadogo na katika nyaraka yako ya kuomba zabuni iwepo ili ufanikiwa angalau asilimia 20 au 10 ya nguzo iwe inatoka kwa wadau wadogo na wawe wamepewa mikataba inayoeleweka” alisema Makamba

Makamba amewataka Wadau hao kuunda chama Cha wazalishaji wa nguzo ili kiweze kudhibiti ubora unaotakiwa na hata kutoa adhabu kali kwa atakayebainika kuzalisha chini ya Kiwango pamoja na kuandaa sheria zitakazoongoza chama hicho.



“Lengo la Serikali ni kukuza uchumi wa wananchi wake kwa kuboresha bidhaa zao kwa kuwasimamia katika kuzalisha kwa vigezo na ubora uliowekwa, ili wananchi hao waweze kunufaika na kukuza uchumi wao na pato la Taifa kwa ujumla” Alisema Makamba.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Maharagwe Change, aliwataka Wadau hao kuwa waaminifu pale nguzo zao zinapotakiwa kupelekwa katika maeneo ya miradi kwa kuweka nguzo halisi zilizokaguliwa na siyo kufanya udanganyifu wa kuweka zisizokuwa na ubora.

Amesema kumekuwa na changamoto ya nguzo kuharibika baada ya muda mfupi kutumika kutokana na kuwa chini ya kiwango na ubora unaotakiwa, huku nguzo hizo zikiwa tayari zimekaguliwa na kuonekana zina ubora unaotakiwa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Said, amewahakikishia Wadau hao kuwa soko la nguzo lipo la kutosha kwani bado miradi mingi ya usambazaji wa Umeme vijijini inaendelea na nguzo nyingi zinahitajika.

Akitoa mfano Mkoa wa Iringa kuwa kuna Mradi wa Ujazilizi ambao unatarajia kuanza hivi karibuni katika Mkoa huo na mikoa mingine.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga amewapongeza wabunge wa Mkoa wa Iringa Kwa kuwa wamoja Katika kutetea ajenda za kimaendeleo zinazohusu Mkoa wa Iringa. 

Alisema kuwa umoja ambao wameonesha kwenye kupigania suala la nguzo za Umeme kuendelea  kununuliwa hapa hapa Nchini wamefanya Jambo la kizalendo sana kwani linaenda kuongeza mapato kwa serikali na Wananchi kwa ujumla. Vivyo hivyo amewataka kuendelea  kufanya hivyo kwenye ajenda nyingine za ki mkoa .

Sendiga Alisema kuwa  Mkoa wa Iringa na Njombe ndio ambao wameuza nguzo zaidi ya asilimia 90 zilizotumika kusambaza Umeme nchini na walishangazwa kusikia hoja ya kuwa nguzo za ndani sio bora wakati tayari nguzo nyingi zimesimikwa Vijijini na zipo imara

"Tukushukuru Mheshimiwa Waziri wa Nishati kwa kufanya maamuzi haya ambayo yana Afya kubwa Kwa uchumi wa mikoa hii miwili na Taifa"

Amewataka Wadau hao kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika na kuwa wasikivu kwa kile watakachokuwa wakielezwa kwa lengo la kupata bidhaa Bora kwa manufaa yao na taifa kwa jumla.

Sendiga alisema kuwa baada ya suala la nguzo kumalizika wabunge hao wana wajibu wa kuendelea kusukuma ajenda ya Mkoa wa Iringa ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha Lami toka Iringa hadi Ruaha Kwa ajili ya kuchochea kasi ya utalii ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha




 

RC SENDIGA ATOA SIKU SABA KWA MKANDARASI PRIPAM KURUDIA UPYA UJENZI WA BARABARA YA ZIZILANG’OMBE NGEREWALA


Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiwa kwenye ukaguzi wa barabara zaTARURA manispaa ya Iringa
Barabara ambazo mkuu wa mkoa wa Iringa alikuwa analalamikia kuwa zimejengwa chini ya kiwango
Barabara ambazo mkuu wa mkoa wa Iringa alikuwa analalamikia kuwa zimejengwa chini ya kiwango

Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiwa kwenye ukaguzi wa barabara zaTARURA manispaa ya Iringa

 Na Fredy Mgunda, Iringa.

 

Mkuu wa mkoa wa Iringa ametoa siku saba kwa mkandarasi Pripam kurudia upya ujenzi wa barabara ya Zizilang’ombe Ngelewala kwa kujenga chini ya kiwango na kusababisha barabara hiyo kuweka nyufa mwezi mmoja tu toka kukamilika kwake.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa barabara za TARURA Manispaa ya Iringa,mkuu wa mkoa Queen Sendiga alisema kuwa hawezi kufarahishwa hata kidogo akikuta barabara imejengwa chini ya kiwango tofauti na thamani ya fedha iliyotolewa kwa mkandarasi.

Sendiga alisema kuwa haiwezekani barabara nyingi za manispaa ya Iringa zimejengwa kwa kiwango kizuri ispokuwa baarabara ya Zizilang’ombe Kitasengwa kwa kuwa imeanza kupasuka mapema jambo ambalo linaashiria kuwa barabara hiyo imejengwa chini ya kiwango.

Aliwataka wataalam Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini wilaya ya Iringa kuhakikisha wanawasimamia vilivyo wakandarasi ambao wanakuwa wamepewa tenda za ujenzi wa barabara wanajenga kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha ambayo imetolewa kutoka serikalini.

Sendiga alisema kuwa baada ya siku saba atafanya ziara kukagua barabara hiyo kama imejengwa kwa kiwango kinachotakiwa kulingana na f thamani ya fedha ambayo imetolewa na serikali la sivyo mkandarasi atachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Sijaridhishwa na ujenzi wa barabara inayotoka Zizi la Ng'ombe kuelekea Ngelewala Manispaa ya Iringa.Nimetoa siku saba kwa mkandarasi kuijenga upya kwa gharama zake na katika ubora unaotakiwa.” Alisema Sendiga

Aliwaambia wataalam wa TARURA wilaya ya Iringa kufanya kazi kwa weredi unaotakiwa ili kuiondolea serikali sitofahamu inayokuwa inaendelea kwenye mitandao ya kijamii juu ya ubovu wa barabara zinazojengwa katika wilaya ya Iringa.

Sendiga alimalizia kwa kuwapongeza viongozi wa TARURA Iringa kwa kazi wanayoifanya isipokuwa mradi mmoja wa barabara ya Zizilang’ombe Ngelewala ambao umeweka doa la mkoa kwa video za nyufa za barabara hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

 

Kwa upande wake meneja wa TARURA mkoa wa Iringa Makori George Kisare alisema kuwa wameyapokea mawazo na maagizo yote ya mkuu wa mkoa na watayafanyia kazi haraka ipasavyo kama alivyo agiza.

Akizungumzia swala la kupasuka kwa barabara ya Zizilang’ombe Ngelewala alisema kuwa mkandarasi anawajibu wa kurudia kwa gharama zake kwa kuwa yeye ndio aliyefanya kosa hilo la kiufundi.

 

Alisema kuwa watahakikisha wanamsimamia ndani ya siku hizo saba anafanya marekebisho yanayotakiwa kwenye barabara hiyo.

 


Friday, 10 December 2021

RAIS UHURU AFANYA ZIARA NCHINI TANZANIA






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, na mgeni wake Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakiwa katika picha yenye waasisi wa Mataifa mawili Tanzania na Kenya Hayati Mwalim Julius Nyerere wa Tanzania na Hayati Jomo Kenyatta wa Kenya wakati Rais Kenyatta alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 2021. Mhe. Rais Kenyatta yupo nchini kwa Ziara ya Kiserikali ya siku moja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mgeni wake Mhe. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alipowasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Desemba, 202. Mhe. Rais Uhuru Kenyatta yupo nchini kwa Ziara ya Kiserikali ya siku moja.

 

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWATUNUKU NISHANI ASKARI 893 ZA MIAKA 60 YA UHURU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitunuku Nishani ya Utumishi mrefu na Tabia Njema Mkaguzi wa Polisi Stahmili Herman Lusatila kati ya watunukiwa 893 ikiwa ni sehemu ya Sherehe ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, katika hafla iliyofanyika leo tarehe 09 Desemba 2021, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitunuku Nishani ya miaka 60 ya Uhuru kwa Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji nchini Kamishna Jenerali Dkt. Anna Peter Makakala kati ya watunukiwa 893 ikiwa ni sehemu ya Sherehe ya Maadhimisho ya kutimiza miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, hafla ya utoaji wa Nishani hizo imefanyika leo tarehe 09 Desemba 2021, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitunuku Nishani ya miaka 60 ya Uhuru kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Simon Nyakoro Sirro kati ya watunukiwa 893 ikiwa ni sehemu ya Sherehe ya Maadhimisho ya kutimiza miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, hafla ya utoaji wa Nishani hizo imefanyika leo tarehe 09 Desemba 2021, Ikulu Jijini Da es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitunuku Nishani ya miaka 60 ya Uhuru kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee kati ya watunukiwa 893 ikiwa ni sehemu ya Sherehe ya Maadhimisho ya kutimiza miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, hafla ya utoaji wa Nishani hizo imefanyika leo tarehe 09 Desemba 2021, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

TANZANIA ILIVYOANDIKA HISTORIA KUBWA DUNIANI,SIKU YA UHURU WA MIAKA 60 MAONYESHO YASISIMUA






















Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kuwapongeza Watanzania kwa kutimiza  miaka 60 ya  Uhuru wa Tanzania Bara, katika Maadhimisho  yaliyofanyika leo tarehe 09 Desemba 2021 katika Uwanja wa Uhuru  Jijini Dar es Salaam.

DC MOYO: AMEPIGA MARUFUKU KUZIBA VICHOCHORO MANISPAA YA IRINGA



Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiona na baadhi ya wananchi wa manispaa ya Iringa wakati wa ziara ya kusikiliza kero za wananchi wa wilaya hiyo
Baadhi ya vichochoro ambavyo vimezibwa kwa kuta na kuhatari maisha ya wananchi wengine endapo itatokea majanga yoyte yale hasa moto
Baadhi ya vichochoro ambavyo vimezibwa kwa kuta na kuhatari maisha ya wananchi wengine endapo itatokea majanga yoyte yale hasa moto
Baadhi ya vichochoro ambavyo vimezibwa kwa kuta na mageti na kuhatari maisha ya wananchi wengine endapo itatokea majanga yoyte yale hasa moto

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ametoa amri ya kuvunjwa kwa kuta zote zilizojengwa kuziba vichochoro katika maeneo ya makazi ya watu Manispaa ya Iringa wavunje mara moja kabla sheria haijachukua mkondo wake kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi.

 

Moyo alitoa amri hiyo baada ya kufanya ziara katika baadhi ya mitaa ya kati kati ya mji wa Iringa na kubaini kuzibwa kwa vichochoro jambo ambalo amelitaja kuwa ni kinyume na sheria za mipango miji.

 

Wakati wa ziara hiyo iliyofuatiwa na mkutano wa hadhara katika kata ya Mivinjeni Moyo amesema kuzibwa kwa vichochoro kunakwamisha jitihada za uokoaji nyakati yanapotokea majanga ya moto hali inayohatarisha usalama.

 

Alisema kuwa kumeibuka tatizo la wananchi kuziba vichochoro vilivyopo mtaani bila kuwa na kibali kutoka katika mamlaka husika.

 

Moyo alisema kuwa wananchi wote walioziba vichochoro watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kuwa wanafanya makosa hayo makusudi hivyo wanapaswa kuvunja mara moja ili kuweka mitaa yote katika hali ya usalama.

 

Alisema wananchi wote wanaofanya shughuli za ujenzi  wanatakiwa kuwa na kibali kutoka katika mamlaka husika la sivyo watakukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa wanakuwa wamevunja sheria kwa makusudi.

 

 

Moyo alisema kuwa vichochoro vyote vilivyopo manispaa ya Iringa vinatakuwa kuwa wazi na marufuku wa idara ya mipango miji kutoa kibali cha kuziba vichochoro kwa ajili ya kulinda usalama wa wananchi wa manispaa ya Iringa na nje ya Iringa.

 

Alisema kuwa ukitokea moto inakuwa vigumu kuuzima kutokana na kuziba kwa vichochoro na kuleta madhara kwa wananchi ambao wanakuwa wamepata majanga hayo kwa kujitakia.

 

Moyo aliwataka wafanyakazi wote wa manispaa ya Iringa kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwa kuwa serikali haijawahi kwenda likizo hivyo wafanyakazi wanatakiwa kuwa kazini muda wote.

 

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo anatoa agizo hilo ikiwa ni siku ya pili mara baada ya kuanza ziara katika manispaa ya Iringa na kubaini kuwepo kwa changamoto ya kuzibwa kwa vichochoro vinavyopaswa kuwapo kati ya jengo moja na jingnine

 

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya Makusudi ya amri hii aliyoitoa ni kuyafanya makazi ya watu katika manispaa ya Iringa kuwa maeneo salama na hasa akieleza kuachwa wazi kwa maeneo hayo kutarahisisha shughuli za uokoaji pindi majanga ya moto yanapotokea

 

Hata hivyo anawageukia maafisa wa Idara ya Mipango miji Manispaa ya Iringa akiwaonya kuwa endapo wamehusika kuruhusu kuzibwa kwa vichochcoro hiyo hatua kali zitachukuliwa huku akiwahusisha na Rushwa

 

Mkuu huyo wa Wilaya anasema ni jambo la kushangangaza kuona wataalam wa Idara ya Mipango miji pamoja na viongozi wa Serikali za mitaa na kata kwa kushindwa kuchukua hatua licha ya kushughudia kila kukicha vichochcoro vikiendelea kuzibwa huku akiwataka kuasha kufanya kazi kwa mazo

Friday, 29 October 2021

HATIMAYE VIBALI VYA NEMC (EIA CERTIFICATE) NDANI YA SIKU 14 BADALA YA SIKU 105



Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Andrea Kundo (Kushoto) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe Hamad Hassan Chande wakati wa kikao kazi cha kujadili kuhusu ufumbuzi wa kero ya ucheleweshwaji wa vibali (Eia Certificate) vinavyotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa NHIF Jijini Dodoma tarehe 28 Octoba 2021



Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Andrea Kundo (Kushoto) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha kujadili kuhusu ufumbuzi wa kero ya ucheleweshwaji wa vibali (Eia Certificate) vinavyotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa NHIF Jijini Dodoma tarehe 28 Octoba 2021.


Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe Hamad Hassan Chande akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha kujadili kuhusu ufumbuzi wa kero ya ucheleweshwaji wa vibali (Eia Certificate) vinavyotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa NHIF Jijini Dodoma tarehe 28 Octoba 2021.


Sehemu ya wajumbe wakifuatilia kikao kazi kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Andrea Kundo (Kushoto) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe Hamad Hassan Chande kujadili kuhusu ufumbuzi wa kero ya ucheleweshwaji wa vibali (Eia Certificate) vinavyotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa NHIF Jijini Dodoma tarehe 28 Octoba 2021.


Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC Dkt Samuel Gwamaka akisisitiza jambo mbele ya Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Andrea Kundo (Kushoto) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe Hamad Hassan Chande wakati wa kikao kazi cha kujadili kuhusu ufumbuzi wa kero ya ucheleweshwaji wa vibali (Eia Certificate) vinavyotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa NHIF Jijini Dodoma tarehe 28 Octoba 2021.


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Andrea Kundo na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe Hamad Hassan Chande kwa pamoja wamekutana na kujadili kuhusu ufumbuzi wa kero ya ucheleweshwaji wa vibali (Eia Certificate) vinavyotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC.

 

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Jijini Dodoma, imebainishwa kuwa kuchelewa kwa upatikanaji wa vibali hivyo kwa kiasi kikubwa imekuwa kikwazo katika miradi ya mawasiliano iliyokuwa ikihitaji Vibali kutoka NEMC.

 

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Andrea Kundo na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe Hamad Hassan Chande katika nyakati tofauti wamewaagiza wataalamu wa Wizara hizo mbili kukaa pamoja na kuunganisha mifumo yao ili iweze kusomana na kuondoa kabisa visingizio vya kutopatikana Vibali kwa wakati.

 

Mhe Kundo amesema kuwa utatuzi huo wa changamoto hiyo iliyopelekea kuchelewa kukamilika kwa miradi ya serikali kwa Zaidi ya miezi saba jambo ambalo lilikuwa likirudisha nyuma utendaji na ufanisi wa kazi za serikali kwa wakati.

 

Amesema kuwa sasa vibali vitaanza kutoka ndani ya siku 14 mpaka 30 kutoka siku 105 za awali ambazo zilikuwa kikwazo kwa wakandarasi waliokuwa wanajenga minara mbalimbali ya mawasiliano.

“Ndugu zangu nimehangika na minara mingi ambayo imebaki viporo ikiwa na visingizio vya kutopatikana Vibali, sasa najua nani ambaye anakwamisha miradi yetu na tutachukua hatua kulingana na uhalisia” Amesisitiza Mhe Kundo

 

Katika kikao kazi hicho, Mhadisi Kundo amemshukuru Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Suleiman Jaffo pamoja na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe Hamad Hassan Chande kwa kufanikisha kikao hiki ambacho kimezaa matunda.


Naibu Waziri Kundo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha Bajeti kwa ajili ya miundombinu ya Mawasiliano ambayo ni moja ya njia kuu za uchumi wa nchi.

 

Naye Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe Hamad Hassan Chande amesema kuwa kikao kazi hicho baina ya Wizara hizo mbili kimezaa matunda ambayo ni manufaa kwa Taifa na vizazi vijavyo kwani kimekuwa na maridhiano makubwa na muhimu.

 

Amesema kuwa pamoja na kuwa na makubaliano hayo yatakayopelekea maendeleo ya uwekezaji lakini ni lazima wananchi kuzingatia umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa sababu ni wazi kuwa bila mazingira hakuna maisha.

 

“Itakuja kuwa ni lawama kubwa sana kwa wajukuu zetu au watoto wetu kama tumewekeza kwenye maendeleo bila kujali mazingira hivyo tumekubaliana kuwa tunaenda kwenye maendeleo lakini maingira lazima tuyatazame kwa jicho la tatu” Amesisitiza Mhe Chande

 

Naibu Waziri Chande amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ambaye ameamua kuleta na kuwakaribisha wawekezaji na kuzifanya sera kuwa rahisi zinazowafanya wawekezaji kutokuwa na kigugumizi katika kuwekezaji nchini Tanzania.

“Ushirikiano huo unapaswa kuwa sababu ya mahusiano ya karibu ya ujenzi wa Taifa kwa pamoja kwani kufanya hivyo Taifa litafaidika na matunda ambayo yatakuwa ni endelevu wakati wote” Amekaririwa Mhe Chande

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC Dkt Samuel Gwamaka ameahidi kufanya kazi na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote nchini UCSAF ili kuweka mazingira mazuri ya kufanya kazi hizo.

 

Asema kuwa atatekeleza maelekezo yaliyotolewa na Naibu Mawaziri hao ikiwemo kutoa vibali kwa wakati kama ilivyotakiwa kutolewa ndani ya siku 14 mpaka 30.

 

Naye Mkuu wa Uendeshaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote nchini Mhandisi Albert Richard amesema kuwa kikao kazi hicho kimekuwa na tija kwa kiasi kikubwa kwani serikali inadhamiria kufikisha huduma mawasiliano kwa wananchi wa mijini na vijijini ambapo hakuna mvuto wa kibiashara.

 

Mhandisi Richard amesema kuwa ili kufanikisha miradi hiyo ni lazima kupata vibali mbalimbali kwa wakati ikiwemo cha Mazingira ili kurahisisha na kutatua tatizo la kuchelewa kwa vibali hivyo.


 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube