BREAKING

Tuesday, 19 April 2016

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA AZINDUA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA 2D NHC MOROGORO


Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya akifunua pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la jengo la biashara na Ofisi la 2D la mjini Morogoro lililojengwa kwa thamani ya Shilingi bilioni 4.3. Jengo hilo ni la ghorofa nne likiwa na eneo la chijni kwa ajili ya maegesho ya magari . Ni mradi wa kwanza kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu mara tuu baada ya kuwashwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa akiupokea kwenge mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.
Meneja wa Shirika la Taifa, Veneranda Seif akiupokea kwenge mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.
Meneja wa Shirika la Taifa, Veneranda Seif akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.
Jengo la Biashara la 2D linavyoonekana leo kabla ya kuzinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya.
Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa akijiandaa kuupokea Mwenge wa Uhuru.
Wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo wakijiandaa kuupokea Mwenge wa Uhuru.
Mwenge wa Uhuru ukiwasili katika eneo la tukio.
Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Issack Peter akiupokea Mwenge wa Uhuru ulipowasili katika eneo mradi wa 2D.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya akizungumza baada ya kuzindua jengo hilo ambapo alilipongeza Shirika hilo kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha wanawapatia wananchi makazi bora na akalitaka Shirika kuendeleza jitihada hizo ili Watanzania wengi zsaidi wafaidike.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya akizungumza baada ya kuzindua jengo hilo ambapo alilipongeza Shirika hilo kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha wanawapatia wananchi makazi bora na akalitaka Shirika kuendeleza jitihada hizo ili Watanzania wengi zaidi wafaidike.
Wafanyakazi wa Ashirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya akizungumza baada ya kuzindua jengo hilo ambapo alilipongeza Shirika hilo kwa kazi kubwa wanayofanya kuhakikisha wanawapatia wananchi makazi bora na akalitaka Shirika kuendeleza jitihada hizo ili Watanzania wengi zaidi wafaidike.

MULTICHOICE TANZANIA WATANGAZA WASHINDI WA "JISHINDIE NA DSTV

bmn2.0-620x308Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akizungumza kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) juu ya droo hiyo pamoja na ofa mbalimbali zinazoendelea kutolewa kwa wateja wa DSTV
DSC_1452Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo akichanganya droo hiyo kwa njia ya kielektoniki kupitia kompyuta. wengine wanaoshuhudia ni maafisa wa MultiChoice Tanzania. Kulia ni mwakilishi kutoka Bahati Nasibu ya Kubahatisha, Bw. Mrisho Millao.
DSC_1453Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akihakiki moja ya majina ambayo yameingia kwenye droo ya ushindi kwa wateja wa DSTV
DSC_1463Droo hiyo ikiendelea
DSC_1451Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionyesha majina ya washindi kwenye 'sreen' kubwa (Haipo pichani) wakati wa tukio hilo
DSC_1484Droo hiyo ya JISHINDIE NA DSTV ikienndelea huku maafisa wa MultiChoice Tanzania na Mwakilishi wa Mchezo wa kubahatisha Tanzania pamoja na wanahabari wakishuhudia tukio hilo mapema leo Aprili 19.2016, Makao makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya MultiChoice Tanzania inayosambaza vifaa vya ving’amuzi vya DSTV hapa nchini mapema leo Aprili 19.2016 imechezesha droo maalum na kuwapata washindi wa “JISHINDIE NA DSTV” katika tukio lililofanyika Makao makuu ya kampuni hiyo Oysterbay, barabara ya Ali Hasan Mwinyi, Jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini.
Awali katika droo hiyo, Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo alieleza kuwa, droo hiyo ilianza tokea mwezi wa kwanza ambapo wateja walitakiwa kuwa na malipo kwenye ving’amuzi vyao vya DSTV bila kukatika kuanzia hiyo Januari hadi mwezi Machi.
Wateja ambao hawajakatiwa ving’amuzi vyao katika promosheni hiyo ya JISHINDIE NA DSTV, waliotangazwa leo ambaoo ni wateja waliojiunga mwezi wa kwanza na kuweza kulipia DSTV zao bila kukatiwa matangazo kwa muda wa miezi mitatu wameweza kujishindia zawadi ya safari ya kwenda Zanzibar wakiwa wao na familia zao.
“Washindi wawili ambao kila mmoja atapata nafasi ya kupelekwa Zanzibar na kukaa huko kwa siku mbili katika hoteli huku akilipiwa kila kitu kuanzia usafiri, malazi, chakula yeye na familia yake ikiwemo baba, mama na watoto wawili. Washini hao ni Mwelly Nyakusaima ambaye ni mkazi wa Igoma-Mwanza na mshindi mwingine ni Evarist Ndambo mkazi wa Tabataa Jijini Dar es Salaam.” Alisema Bi. Hilda Nakajumo.
Aidha, alibainisha kuwa, washindi wengine waliojishindia droo hiyo ambao ni wa kipengele cha pili ni wale wateja ambao tayari walishajiunga na DSTV huku wakitakiwa wasikatiwe malipo yao kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa tatu.
Ambapo wateja 50 wamejishindia DSTV EXPLORA Decoders huku wateja 90 wao wakibahatika kupata kuunganishwa malipo ya bure ya mwezi ikiwemo ya mwezi mmoja, miezi mitatu, miezi sita na miezi 12 bure.
Aidha, washindi hao wote walioshinda MultiChoice ilibainisha kuwa, watapigiwa simu na kuelekezwa namna ya kuchukua zawadi zao hizo kuanzia sasa kwa muda hadi June mwaka huu.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu aliwakumbusha wateja wa DSTV kuendelea kulipia malipo ya ving’amuzi vyao huku wakitoa ofa mbalimbali sambamba na vipindi vizuri ikiwemo vya uhondo wa soka la kimataifa, filamu na muziki..





Wednesday, 13 April 2016

UJUMBE WA MAWAZIRI NA WAFANYABIASHARA WA CZECH REPUBLIC WAFANYA KONGAMANO LA UWEKEZAJI DAR ES SALAAM

 2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Misitu wa Serikali ya Czech Republic Bw. Dusan Benza akizungumza katika kongamano la wafanyabiashara wa nchi hiyo na watanzania lililofanyika leo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Mawaziri wawili Kilimo na Viwanda wa Jamhuri ya Jamhuri ya Czech wakiongozana na wafanyabiashara zaidi ya thelathini wako nchini kwa ajili ya kutafuta na kujionea fursa za uwekezaji nchini Tanzaniam Mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja na Tanzania Investiment Bank (TIB), Ubalozi wa Szech Republic nchini Kenya na Tanzania House Of Business Company Limited (THB).
Ujumbe huo metembelea wizara ya Kilimo na wizara ya Viwanda na Biashara na kusaini mikataba ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji hapa nchini na nchi ya Szech Republic ili kuunganisha masuala ya kibiasha na uwekezaji na kuwezesha wafanyabiashara wa nchi hizi kuwekeza katika masuala ya biashara, Teknolojia na Kilimo kwa ujumla.

Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic hapa nchini John Chaggama akizungumza na mmoja wa viongozi wa ujumbe huo huku Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa Czech akisikiliz kwa makini.
4
Injinia Michal Basovnik wa kampuni ya Impuls akitoa mada kuhusu shughuli mbalimbali zinazotolewa na kampuni yao ambayo ina tawi pia nchini Zambia.
5 7
Injinia Martin Adamuska wa kampuni ya NWT kutoka nchini Czech Republic akifafanua jambo wakati alipokuwa akielezea mambo mbalimbali yanayofanya na kampuni yao lakini pia fursa mbalimbali zinazoweza kuwekezwa.
8
Injinia Petr Pawlica wa wa kampuni ya PAWLICA pia ametoa mada katika kongamano hilo na kuelezea teknolojia ya kampuni hiyo katika masuala ya Kilimo. 9
Bw. Godffrey Kirenga wa SAGCOT CENTER LIMITED akiwaelezea wafanya biashara hao juu ya fursa mbalimbali zilizopo hapa nchini katika uwekezaji wa kilimo.
10
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza katika kongamano hilo kulia ni John Chaggama Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania.
11 12
Kutoka kulia ni Mr Charles Chandika Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania House Of Business Company Limited, Pan Arnold Mturi Charge de Affairs at the Szech Consolate nchini Tanzania, Elipina Makungu na Bahija Salim wakijadiliana jambo wakati wa kongamano hilo la wafanya biashara.
13
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza na Pan Arnold Mturi Charge de Affairs at the Szech Consolate nchini Tanzania wakimsikiliza mmoja wa maofisa kutoka wizara ya mambo ya nje wakati akizungumza nao.
14
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye na John Chaggama Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania wakizungumza na Injinia Vladmir Pikora wa benki ya Czech Export Bank mara baada ya nusu ya kwanza ya majadiliano kati ya wafanya biashara wa Tanzania na Szech Republic katika kongamano lililofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
15
John Chaggama Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ujio wa wafanyabiashara hao.
16
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa ujio wa wafanyabiashara hao na kongamano hilo kwa wafanyabiashara wa Tanzania ya Czech Republic katika masuala mazima ya kibiashara na uwekezaji.
17
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini Czech Republic wakiwa katika kongamano hilo lililofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam
18 19
Baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania wakihudhuria kongamano hilo.
20
Baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali za Tanzania masuala ya biashara na uwekezaji wakiwa katika kongamano hilo.
21
John Chaggama Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania akimsikiliza Pan Arnold Mturi Charge de Affairs at the Szech Consolate nchini Tanzania.
22
Elipina Makungu na Bahija Salim wakifurahia jambo wakati wa kongamano hilo la wafanyabiashara wa Czech Republic na Tanzania kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.

DKT.KIGWANGALLA AKAGUA HOSPITALI YA TAIFA YA KIFUA KIKUU KIBONG'OTO ILIYOPO KILIMANJARO

Dkt.Kigwangalla akagua Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong’oto iliyopo Mkoani Kilimanjaro
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla, ametembelea Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong'oto eneo la Sanya Juu Wilani Siha Mkoani Kilimanjaro.
Dkt. Kigwangalla katika Hospitali hiyo, alipata kitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ya kawaida na ile kali ambapo pia aliweza kutembelea eneo la kituo cha utafiti cha magonjwa hayo pamoja na Maabara.
Kihistoria Hospitali hiyo ya Kibong’oto ilifunguliwa rasmi 29 Oktoba mwaka 1952 na Lady Twining, baada ya miaka saba ya vita ya pili ya dunia chiniya utawala wa Muingereza na imekuwa ikitoa huduma hiyo ya magonjwa ya kuambukiza hususani Kifua Kikuu.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga amemwelezea Naibu Waziri changamoto mbalimbali ikiwemo suala la nyumba za watumishi na mambo mengine ikiwemo suala la bajeti ya vifaa tiba.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo:
DSC_0572Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitia saini kitabu cha wageni katika Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong'oto ilipo Mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake 10 Aprili 2016. Anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga
DSC_0607Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo ya kitaalam kutoka kwa msimamizi wa Maabara ya Hospitali hiyo ya Kibong'oto
DSC_0608Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipatiwa maelezo ya kina namna ya vifaa hivyo vinavyofanya kazi katika upimaji wa kifua kikuu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga
DSC_0612Eneo la Utafiti wa magonjwa ya kuambukiza katika Hospitali hiyo ya KIbong'oto..DSC_0611....Wakitoka katika jengo la Utafiti
DSC_0599Msafara ukielekea upande wa wadi za wagonjwa wa TB sugu..
DSC_0575Moja ya alama zinazoelekeza maeneo ya Hospitali hiyo
DSC_0577Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Kibong'oto, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga akimuongoza Naibu Waziri wa Afya na watendaji mbalimbali kuelekea katika eneo wanalohudumia wagonjwa wenye Kifua kikuu (TB) sugu.
DSC_0581Wafanyakazi wa Hospitali hiyo ya Kibong'oto na wageni wengine wakielekea katika eneo la TB sugu wakati wa ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Afya..DSC_0579Mkuu wa wilaya ya Siha,Dkt Charles Mlingwa (katikati) wakielekea katika eneo hilo la TB sugu wakati wa ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Afya
DSC_0582Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipatiwa maelezo ya kina juu ya wagonjwa wa TB sugu waliopo ndani ya wodi (hawapo pichani) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga
DSC_0586 DSC_0584Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga akionyeshaa namna wodi hizo zinavyofanya kazi na jinsi wanavyotoa huduma.
DSC_0595 DSC_0597
Msafara huo ukirejea katika maeneo mengine wakati wa ukaguzi na Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla.
Pichani wote waliovaa 'mask' maalum ni kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya vijidudu vya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) hasa kwa upande huo wa wagonjwa maalum wa TB sugu.ambao wapo upande maalum. Hivyo kuvaa kifaa hicho kinasaidia kupunguza hali ya maambukizo wakati wa kufika eneo hilo kama sheria na taratibu zilizowekwa kitaalam na uongozi wa Hospitali hiyo.
DSC_0616Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo mafupi kutoka kwa wataalam wa Hospitali hiyo.
DSC_0620Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo mafupi kutoka kwa wataalam wa Hospitali hiyo.
DSC_0631Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa maagizo kwa uongozi wa Hospitali hiyo.
DSC_0637Mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza, wa Hospitali ya Kibong'oto ,Dkt. Stella Mpagama akimkabidhi kitabu chake Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
KAWAIDA: Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla, ametembelea Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong'oto eneo la Sanya Juu Wilani Siha Mkoani Kilimanjaro. Dkt. Kigwangalla katika Hospitali hiyo, alipata kitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ya kawaida na ile kali ambapo pia aliweza kutembelea eneo la kituo cha utafiti cha magonjwa hayo pamoja na Maabara. Kihistoria Hospitali hiyo ya Kibong’oto ilifunguliwa rasmi 29 Oktoba mwaka 1952 na Lady Twining, baada ya miaka saba ya vita ya pili ya dunia chiniya utawala wa Muingereza na imekuwa ikitoa huduma hiyo ya magonjwa ya kuambukiza hususani Kifua Kikuu. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga amemwelezea Naibu Waziri changamoto mbalimbali ikiwemo suala la nyumba za watumishi na mambo mengine ikiwemo suala la bajeti ya vifaa tiba. Tazama MO tv, kuona tukio hilo: Inline image 1 DSC_0572Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitia saini kitabu cha wageni katika Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong'oto ilipo Mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake 10 Aprili 2016. Anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga DSC_0607Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo ya kitaalam kutoka kwa msimamizi wa Maabara ya Hospitali hiyo ya Kibong'oto DSC_0608Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipatiwa maelezo ya kina namna ya vifaa hivyo vinavyofanya kazi katika upimaji wa kifua kikuu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga DSC_0612Eneo la Utafiti wa magonjwa ya kuambukiza katika Hospitali hiyo ya KIbong'oto..DSC_0611....Wakitoka katika jengo la Utafiti DSC_0599Msafara ukielekea upande wa wadi za wagonjwa wa TB sugu.. DSC_0575Moja ya alama zinazoelekeza maeneo ya Hospitali hiyo DSC_0577Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Kibong'oto, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga akimuongoza Naibu Waziri wa Afya na watendaji mbalimbali kuelekea katika eneo wanalohudumia wagonjwa wenye Kifua kikuu (TB) sugu. DSC_0581Wafanyakazi wa Hospitali hiyo ya Kibong'oto na wageni wengine wakielekea katika eneo la TB sugu wakati wa ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Afya..DSC_0579Mkuu wa wilaya ya Siha,Dkt Charles Mlingwa (katikati) wakielekea katika eneo hilo la TB sugu wakati wa ziara hiyo ya Naibu Waziri wa Afya DSC_0582Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipatiwa maelezo ya kina juu ya wagonjwa wa TB sugu waliopo ndani ya wodi (hawapo pichani) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga DSC_0586DSC_0584Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga akionyeshaa namna wodi hizo zinavyofanya kazi na jinsi wanavyotoa huduma. DSC_0595DSC_0597 Msafara huo ukirejea katika maeneo mengine wakati wa ukaguzi na Naibu Waziri wa Afya Dk.Kigwangalla. Pichani wote waliovaa 'mask' maalum ni kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya vijidudu vya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) hasa kwa upande huo wa wagonjwa maalum wa TB sugu.ambao wapo upande maalum. Hivyo kuvaa kifaa hicho kinasaidia kupunguza hali ya maambukizo wakati wa kufika eneo hilo kama sheria na taratibu zilizowekwa kitaalam na uongozi wa Hospitali hiyo. DSC_0616Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo mafupi kutoka kwa wataalam wa Hospitali hiyo. DSC_0620Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akipata maelezo mafupi kutoka kwa wataalam wa Hospitali hiyo. DSC_0631Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa maagizo kwa uongozi wa Hospitali hiyo. DSC_0637Mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza, wa Hospitali ya Kibong'oto ,Dkt. Stella Mpagama akimkabidhi kitabu chake Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog). Attachments area Preview YouTube video Dkt.Kigwangalla akagua Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu Kibong’oto

Wednesday, 6 April 2016

RAIS JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI RWANDA KWA ZIARA YAKIKAZI






 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube