BREAKING

Monday, 4 April 2016

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM, RAJAB LUHWAVI AZUNGUMZA NA MAKATIBU WA MATAWI NA KATA WILAYA YA DODOMA MJINI LEO


 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akiwasalimia baadhi ya viongozi baada ya kuwasili Ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma, leo Aprili 3, 2016, kuzungumza na Makatibu wa CCM wa matawi na Kata katika wilaya ya Dodoma mjini. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, Paulo Luhamo na Katikati ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Salum Kalli.
 Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Salum Kalli akizungumza maneno ya utangulizi kabla ya kuanza kikao hicho
 Makatibu wa matawi na Kata za wilaya ya Dodoma mjini, wakiwa tayari ukumbini kuzungumzana Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi katika Ukumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi (wapili kulia) akiwasili katika ukumbi wa Sekretarieti katika Ofisi ya Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma, leo Aprili 3, 2016, kuzungumza na Makatibu wa CCM wa matawi na Kata katika wilaya ya Dodoma mjini. Kulia ni Katibu wa CCM wa mkoa wa Dodoma, Jamila Yusuph.
 Katibu wa CCM wilaya ya Dodoma mjini akihamasisha, baada ya Luhwavi (katikati) kuwasili ukumbini. kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma Jamila Yusuph
 Wajumbe wakiwa ukumbini
 Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini Paulo Luhamo akimkaribisha Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma ili kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu kuzungumza katika kikao hicho
 Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) kuzungumza katika kikao hicho
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akizungumza na Makatibu wa CCM wa matawi na Kata katika wilaya ya Dodoma mjini, katika Ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Aprili 3, 2016. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Dodoma mjini, Paulo Luhamo
 Maofisa waandamizi wa Chama wakifuatilia kwa karibu kikao hicho
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akizungumza na Makatibu wa CCM wa matawi na Kata katika wilaya ya Dodoma mjini, katika Ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo Aprili 3, 2016. 

Baadhi ya wajumbe wakitoa yao ya moyoni kuhusu kero au changamoto wanazoziona katika utumishi wa Chama. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

WAZIRI MWAKYEMBE AISHUKURU KAMPUNI YA KAMAL STEEL KWA KUTOA VIUNGO BANDIA KWA WALEMAVU

1
Mwenyekiti wa makampuni ya Kama Group , Gagan Gupta wakati wa hafla ilyofanywa na kampuni hiyo ya Kamal Steel Ltd kiwandani hapo wakati wa utoaji wa msaada wa viungo bandia, kwa watu wenye ulemavu 16, vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 80, hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo imefanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akishukuru kampuni hiyo kwa msaada ilioutoa kwa watanzania hao wenye ulemavu wa miguu ambapo yeye ndiye aliyewakabidhi kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta.
3
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akimvisha mguu wa bandia Bw. Siaga Raphael Kiboko mara baada ya kukabidhiwa kutoka kampuni ya Kamal Steel ya jijini Dar es salaam kushoto ni Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw. Gagan Gupta.
4
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na Bw. Siaga Raphael Kiboko kabla ya kumkabidhi msaada wake wa viungo bandia vya mguu.
5
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na Bw. Gagan Gupta ambaye ni mwenyekiti wa kampuni ya Kalam Steel tayari kwa ajili ya kukabidhi msaada huo.
6
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akifurahia jambo na Bw. Siaga Raphael Kiboko mara baada ya kumvisha mguu wake huku Mwenyekiti wa kampuni ya Kamal Steel Bw. Gagan Gupta pamoja na viongozi wengine wa kampuni hiyo wakishuhudia.
7
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na Bw. Joshua Mwamunyange mara baada ya kumvisha mguu wakena kuanza kujaribu kutembea.
8
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akimbidhi Bi Fatuma mguu wake wa bandia ikiwa ni msaada kutoka kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal Steel ya jijini Dar es salaam.
9
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa kampuni ya Kamal Steel na baadhi ya walemavu waliokabidhiwa msaada huo.
10
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mwenyekiti wa kampuni ya Kamal Steel Bw. Gagan Gupta.mara baada ya kukabidhi misaada hiyo katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta na wakuu wengine wa vitengo kutoka kampuni hiyo.
.............................................................................................................
KAMPUNI ya kutengeneza chuma ya Kamal Steel Ltd, imetoa msaada wa viungo bandia, kwa watu wenye ulemavu 16, vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 80.
Akifunga kambi ya kutoa viungo bandia hivyo jijini Dar es Salaam sambamba na kukabidhi vifaa hivyo, Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema, serikali itaendelea kuwawezesha watu wenye ulemavu nchini ili waweze kukabiliana na changamoto zinazowazunguka ikiwa ni pamoja na kuwapatia vifaa bandia.
Alisema, suala la ulemevu linagusa maisha ya kila mwanadamu na kwamba mtu yoyote anaweza kufikwa na tatizo hilo.
Alibainisha, viungo bandia vinauzwa kwa ghalama kubwa ambayo watu wengi wenye ulemavu hawawezi kumudu kununua hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau wake itaendelea kutoa msaada wa vifaa hivyo.
“Jamii iamini kuwa wote ni walemavu watarajiwa. Kupoteza kiungo kimoja cha mwili ni changamoto kubwa. Tunaishukuru kampuni ya Kamal Steel kwa kutoa misaada hii muhimu ambayo tunaamini kuwa inasaidia kupunguza madhira ya ulemavu,”alisema Dk. Mwakyembe ambaye kupitia msaada huo ameweza kuwasaidia watu wenye ulemavu wanne kutoka jimbo lake la Kyela mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa makampuni ya Kama Group , Gagan Gupta, alisema,kampuni yake haijatoa viungo bandia hivyo kama msaada, bali kama wajibu wake kwajamii.
“Tunaamini kwamba, viungo hivi bandia vitawawezesha kumudu kutembea, kufanya kazi mbalimbali zitakazo waletea kipato,”alisema Gupta.
Katika hatua nyingine, Gupta aliahidi kumuajiri mmoja wawatu hao wenye ulemavu mwenye taaluma ya ufundi mitambo, Siaga Raphael ambapo alisema ajira yake itaanza leo.
“Huyu atafundishwa ufundi wa kutengeneza vifaa mbalimbali hasa vya watu wenye ulemavu hapa, ili aweze kusaidia kuwafundisha watu wenye ulemavu wengine.Mradi anataaluma hiyo ataanza kazi kesho asubuhi (leo asubuhi),”alisema Gupta.
Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta, alisema, kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia viungo hivyo bandia kwa watu wenye ulemavu ambapo mpaka sasa imesaidia watu 200.
“Tutaendelea kuwasaidia kila mara ili tuweze kuisaidiana na serikali yetu kuwaondolea changamoto wenzetu hawa. Tunaamini wakipewa viungo hivi bandia wanaweza kushiriki shughuli mbalimbali muhimu zitakazowaingizia kipato,”alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake walio pokea msaada huo, Siaga Raphael, aliipongeza kampuni hiyo kwa masaada wa vifaa hivyo na kuitaka serikali kuwa kumbuka watu wenye ulemavu kwa kuwasaidia pia kuwapa taaluma ya ufundi itakazowawezesha kujimudu kimaisha.

Sunday, 3 April 2016

LUHWAVI ATINGA MAFINGA, AZUNGUMZA NA MAKATIBU WA CCM WA MASHINA NA KATA


 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi akilakiwa na Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Elisha Mwampashi ambaye ni Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Mjini, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Mufindi katika mji mdogo wa Mafinga leo April 2, 2016, akiwa katika ziara ya kikazi, kuzungumza na watumishi wa Chama ili kusikiliza changamoto na kero zinazowakabili. Kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Mufindi, Yohanes Kaguo, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Mufindi katika mji mdogo wa Mafinga leo April 2, 2016, akiwa katika ziara ya kikazi, kuzungumza na watumishi wa Chama ili kusikiliza changamoto na kero zinazowakabili. 
Katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama akisoma taarifa ya wilaya hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi (kulia). katikati ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Yohanes Kaguo
Kaim Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Elishe Mwampashe ambaye pia ni Katibu wa CCM wilaya ya Iringa mjini akisalimia alipotambulisha katika kikao cha ndani baina ya viongozi wa wilaya ya Mufindi na wa mkoa wa Iringa.
Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Mufindi, Yohanes Kaguo akimkaribusha Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi (wapili kushoto), kuzungumza na viongozi waandamizi wa CCM wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa, katika Ofisi ya CCM wilaya ya Mufindi mjini Mafinga leo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi akizungumza na viongozi waandamizi wa CCM katika wilaya ya Mafinga na mkoa wa Iringa, kabla ya kuzungumza na Makatibu wa CCM wa Mashina na Kata katika wilaya ya Mufindi, katika ukumbi wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo, Mafinga  mkoani Iringa, leo Aprili 2, 2016.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akizungumza na viongozi waandamizi wa CCM wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa, kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Mufindi mjini Mafinga leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Yohanes Kaguo na kulia ni Kaim Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Elishe Mwampashe
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akisisitiza jambo alipozungumza na viongozi waandamizi wa CCM wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa, kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Mufindi mjini Mafinga leo
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi, Yohanes Kaguo, wakati akitoka katika Ofisi ya CCM wilaya ya Mufindi kwenda ukumbini kuzungumza na Makatibu wa CCM wa Mashina na Kata katika wilaya ya Mufindi, katika ukumbi wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mkoani Iringa, leo Aprili 2, 2016.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi, Yohanes Kaguo, wakati akitoka katika Ofisi ya CCM wilaya ya Mufindi kwenda ukumbini kuzungumza na Makatibu wa CCM wa Mashina na Kata katika wilaya ya Mufindi, katika ukumbi wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mkoani Iringa, leo Aprili 2, 2016.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi, Yohanes Kaguo, kwenda ukumbini kuzungumza na Makatibu wa CCM wa Mashina na Kata katika wilaya ya Mufindi, katika ukumbi wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mkoani Iringa, leo Aprili 2, 2016.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akiingia ukumbini, kuzungumza na Makatibu wa CCM wa Mashina na Kata katika wilaya ya Mufindi, katika ukumbi wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mkoani Iringa, leo Aprili 2, 2016.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi baada ya kuingia ukumbini, kuzungumza na Makatibu wa CCM wa Mashina na Kata katika wilaya ya Mufindi, katika ukumbi wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mkoani Iringa, leo Aprili 2, 2016.
Wajumbe wakimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi wakati akiingia ukumbini, kuzungumza na Makatibu wa CCM wa Mashina na Kata katika wilaya ya Mufindi, katika ukumbi wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mkoani Iringa,leo Aprili 2, 2016
Makatibu wa Mashina na Kata kutoka wilaya ya Mufindi wakiwa tayari kumsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara, Rajab Luhwavi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wilaya ya Mufindi Malselina Mkini akijitambulisha wakati wa kikao hicho.
Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Elisha Mwampashi ambaye ni Katibu wa CCM wilaya ya Iringa Mjini, akisalimia wajumbe, wakati wa kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Mufindi, Yohanes Kaguo akimkaribusha Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajab Luhwavi(katikati), kuzungumza na Makatibu wa CCM wa Mashina na Kata katika wilaya ya Mufindi, katika ukumbi wa Ofisi ya CCM wilaya hiyo mkoani Iringa, leo Aprili 2, 2016
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi akizungumza na Makatibu wa CCM wa Mashina na Kata katika wilaya ya Mufindi, katika ukumbi wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mkoani Iringa, leo Aprili 2, 2016. 
Mshiriki akinukuu kwa majini, wakati Naibu Kataibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi alipozungumza na Makatibu wa CCM wa matawi na kata katika wilaya ya Mufindi, katika ukumbi wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mkoani Iringa leo, Aprili 2, 2016. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

JK AKUTANA NA AMWAKILISHI KUTOKA TAASISI YA RAIS WA KWANZA WA ANGOLA DK AUGUSTINE NETO

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete katika mahojiano na Ndugu Amarildo Da Conceiacao kutoka Taasisi ya DKt. Agostinho Neto, Mpigania Uhuru na Rais wa Kwanza wa Angola jijini Dar es Salaam jana Na Mwandishi Maalum Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ametembelewa na ujumbe kutoka Taasisi ya Dkt. Agostinho Neto ya Angola jana jijini Dar es Salaam. Ujumbe wa Taasisi hiyo unaoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Amarildo Da Conceicao uko nchini kwa lengo la kufanya mahojiano na viongozi wa Tanzania kwa lengo la kuhifadhi historia ya mpigania uhuru na muasisi wa Taifa la Angola Dkt. Agostinho Neto. Akimuelezea Dkt. Agostinho Neto, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete amemzungumzia mpigania uhuru huyo kuwa mtu mwenye kuzungumza kwa sauti ya upole lakini kiongozi makini, shupavu na mwenye uwezo mkubwa wa kifalsafa na kifikra. Dkt. Kikwete amesema anakumbuka akiwa kiongozi wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, walimualika Dkt. Neto kuja kuzungumza na wanafunzi katika Darasa la Itikadi alipozuru nchini mwaka 1974. Mpigania uhuru huyo aliyembatana na mkewe mwenye asili ya kireno aliulizwa swali na mwanafunzi mmoja, 'iweje yeye ni mpigania uhuru dhidi ya watu weupe ilihali ameoa mwanamke mweupe?'. Katika jibu lake, Dkt. Neto alisema, 'mapambano hayana rangi, hatupambani na watu weupe tunapambana na ukoloni, mtu mweupe anaweza kuungana nasi katika mapambano yetu hali kdhalika wapo wenzetu weusi wanaoungana na kusaidia wakolini dhidi yetu'. ​Rais Mstaafu amewapongeza Taasisi ya Agostinho Neto kwa jitihada inazochukua za kuhifadhi historia ya mpigania uhuru na muasisi wa Taifa la Angola. Amewakumbusha umuhimu wa kuhakikisha kuwa historia hiyo inarithishwa kwa kizazi baada ya kizazi ili watambue tulipotoka, tulipo na tunapotakiwa kwenda. Ujumbe wa Taasisi ya Neto pia umefanya mahojiano kama hayo na Mama Maria Nyerere, Mke wa Baba wa Taifa, Mheshimiwa Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu Mstaafu na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Nchi za Kiafrika (OAU) na viongozi na watanzania mashuhuri ambao walishiriki kwa namna moja au nyingine katika harakati za uhuru wa Angola. Imetolewa na Ofisi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dar es Salaam 2Aprili, 2016

WAZIRI MKUU MSTASAFU WA KENYA RAILA ODINGA AMTEMBELEA RAIS Dkt JOHN MAGUFULI NYUMBANI KWAKE CHATO


. Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwasili kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Chato Mkoani Geita kwa ajili ya kwenda kumsalimia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

...........................
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Raila Amoro Odinga amemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyopo mapumzikoni katika Kijiji cha Kilimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita.

Mheshimiwa Odinga ambaye ameongozana na mkewe Mama Ida Odinga na Binti yake Winnie Raila Odinga, wametua kwa Helkopta katika uwanja wa Shule ya sekondari ya Chato leo tarehe 02 April, 2016 majira ya saa 11 jioni na baadaye kuelekea nyumbani kwa Rais Magufuli ambako wamepokelewa na wenyeji wao Rais Magufuli mwenyewe na Mkewe Mama Janeth Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga nyumbani kwake Chato mkoani Geita mara baada ya Kuwasili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikumbatiana na Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.

Akizungumza mara baada ya kuwasili Chato, Mheshimiwa Raila Odinga amesema yeye na familia yake wapo likizo na wamekuja kumtembelea rafiki wa familia yao, kwa lengo la kumsalimia.

"Nimekuja kupumzika na nimekuja na Mama na Mtoto wangu wa kike, na vilevile kuja kutoa pongezi kwa ndugu yangu kwani tangu achaguliwe sijakuja hapa Chato, na nilisema siendi Dar es salaam nitakuja hapahapa Chato" Alisema Mheshimiwa Odinga.

Pamoja na kukutana na Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Raila Odinga pia amemsalimu Mama wa Rais Bibi Suzana Joseph Magufuli na pia amezulu Makaburi walimozikwa wanafamilia wa Rais, akiwemo Baba Mzazi Mzee Joseph Magufuli.

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada ya kuwasili Chato.
. Waziri Mkuu wa mstaafu wa Kenya Raila Odinga akiwa na Rais John Magufuli, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Raila Odinga Bi. Ida Odinga wakisali kwenye makaburi ya familia ya Mhe. Rais Chato Mkoani Geita.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na mama mzazi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Bi Suzana Joseph Magufuli mara baada ya kuwasili Chato Mkoani Geita.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube