Ronald Selukindo ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko multchoice Tanzania ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Pandatukupandishe...
Kampuni ya Multchoice Tanzania DSTV imezinduzia kampeni yake mpya ya #PandaTukupandishe, ambapo wameeleza hiyo yote ni kuwapa burudani wateja wao katika nyanja mbalimbali kama Soka, Tamthiliya, Filam na Michezo ya watoto.Ronald Selukindo ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko multchoice Tanzania anasema kwamba kama ilivyo kawaida ya DStv inaendelea kuwapa furaha mashabiki wake kupitia ving'amuzi vyao na kuongeza channel zenye burudani..
Amesema wakati Michuano ya Mataifa ya Afrika AFCON ikiendelea nchini Ivory Coast wameendelea kuwapa burudani nyingine watanzania kwa kuhakikisha wasanii mbalimbali nao wanapata furusa ya kuwapa burudani watanzania, ikiwa ni njia mojawapo ya kumuunga mkono Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukuza tasnia ya michezo.
Katika uzinduzi huo Shelukindo amesema DSTV inawaletea burudani nyingine kama Show ya Kijanja Wana wa Town pamoja Tamthilia ya Nuru zitakazoanza mwezi huu wa Februari ulifanyika.