BREAKING

Sunday 23 July 2023

KINANA : MSHIKAMANO, MOJA NI SILAHA YA USHINDI KUELEKEA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.








MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana, amewashauri viongozi wa Chama hicho katika ngazi zote kuendeleza umoja ili kwenda katika Uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 wakiwa wamoja na kuibuka washindi pamoja.

Kinana ameyasema hayo leo Julai 23, 2023 wakati akizungumza na viongozi wa CCM katika kikao cha ndani cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kondoa mkoabi Dodoma.

"Napongeza kazi kubwa inayofanywa na viongozi wa CCM hususan katika ngazi kitongoji, Kijiji, mtaa na Kata kwa kazi nzuri mnayoifanya. Mwakani ni mwaka wa Uchaguzi, hivyo naamini wana CCM tutakwenda kwenye uchaguzi wa Serikali za Mtaa mwaka 2024 tukiwa kitu kimoja, tukifanya kampeni wamoja na tutaibuka na ushindi tukiwa wamoja, hivyo hivyo katika uchaguzi mkuu mwaka 2025," amesema Kinana.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kwamba Chama pia kinatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotelewa na viongozi wa CCM katika ngazi za kata, vitongoji, vijiji, wilaya na mkoa kwani wao ndio wanaokutana na wananchi na wakati wa uchaguzi ndio wanaokwenda kuomba kura.

Pia, amewapongeza madiwani wanaotokana na CCM ambao wamekuwa wakisimamia ngazi ya Kata na wamekuwa wakifanya hivyo bila ya kuwa na mshahara.

Saturday 15 July 2023

KATIBU MKUU WA CCM DANIEL CHONGOLO AWASILI MBEYA...




 







Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akisalimiana na wajumbe Mbeya mara baada ya kuwasili Mbeya ikiwa ni Ziara yake ya Siku moja yenye lengo la Kuzungumza na Wananchi pamoja na Wana CCM kutoka Baadhi ya Mikoa ikiwemo Songwe, Iringa, Rukwa pamoja na Njombe

Wednesday 12 July 2023

WIZARA YA NISHATI YATENGA BILIONI TANO KUCHANGIA UTOAJI ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA KULINDA MABWAWA

 Wizara ya Nishati imetenga Sh bilioni tano katika bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya kuchangia utoaji elimu ya kutunza mazingira ili kulinda mabwawa yanayozalisha umeme nchini.

Waziri wa Nishati January Makamba amesema hayo katika ziara ya viongozi wa dini kutoka baraza Kuu la waislam Tanzania lililofanya ziara katika mradi ya kufua Umeme,wa Julius Nyerere .




Waziri wa Nishati January Makamba 




 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube