BREAKING

Monday 8 February 2021

WADAU WA MISITU WAIPONGEZA TFS KUPITIA SAO HILL KWA KUGAWA MICHE YA MITI MILIONI MOJA KILA MWAKA

 Katibu wa umoja wa wavunaji miti mkoa wa Iringa (UWASA)Dr Bazir  Tweve akipokea miche ya miti kwa niaba ya wananchi wengine mbele ya Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti la Sao hill Juma Mwita 




Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wadau wa misitu mkoani Iringa wameipongeza wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi kwa kugawa miti milioni moja kila mwaka kwa wananchi na taasisi mbalimbali zinazolizunguka shamba hilo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa miche ya miti ,katibu wa umoja wa wavunaji miti mkoa wa Iringa (UWASA)Dr Bazir  Tweve alisema kuwa uongozi wa shamba la Sao Hill umekuwa ukitoa miti na elimu ya utunzaji wa miti kwa wananchi wanalizunguka shamba hilo.

Alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu ya uhifadhi misitu kwa wananchi na wadau mbalimbali wanajihusisha nawasiojihusisha na zao la miti kwa kuendelea kutunza na kulinda mazingira yasihalibike kwa njia mbalimbali kama vile kuchoma moto au kukata miti hovyo.

Dr Tweve aliongeza kuwa kitendo cha TFS Mufindi kutoa miche milioni moja kunasaidia kuwakumbusha wananchi kupanda miti na kuitunza vizuri hadi pale itakapofika muda wa kuvunwa kutoakana na aina ya mitia ambayo wameipanda.

Alisema kuwa uchumi wa wilaya ya Mufindi na Mkoa wa Iringa kwa ujumla unategemea misiti hivyo zao la miti linachangia kukuza uchumi wa wananchi mmoja mmoja na kueleta maendeleo kwa ujumla kwa wananchi wa mkoa wa iringa nan je ya Iringa.

Dr tweve aliwaomba uongozi wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindikutoa elimu ya uvunaji wa miti ili kuepukana na wananchi kuvuna miti ikiwa bado haijakomaa kuvunwa na kupeleka bidhaa ambayo haihitajiki sokoni.

 “Sasa hizi imezuka tabia ya wananchi wanaomiliki mashamba binafsi kuvuna miti ambayo haijakomaa kuvunwa kutoka na hali ya uchumi hivyo niwaombe mfike kwa wananchi na kutoa elimu hiyo kipindi mnatoa miche na baada ya miche hiyo kupandwa” alisema Dr tweve

 

Kwa upande wake aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi,Peter Tweve aliwashukuru wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi kwa kazi kubwa wanayifanya ya kutunza maziringa na kutoa elimu ya mazingira kwa wananchi wanaolizunguka shamba hilo.

 Alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Mufindi kwa kiasi kikubwa uchumi wake unategemea Misiti hiyo kitendo cha Sao Hill kutoa miche kwa wananchi kunahamasisha wananchi kuendelea kupanda miti na kutunza mazingara.

Naye Mhifadhi Mkuu wa Shamba la miti la Sao hill Juma Mwita alisema kuwa wameyapokea mawazo ya wadau na kuahidi kuyafanyia kazi ikiwapo swala la kutoa elimu kwa wananchi wanaovuna miti mapema kabla ya muda wake.

 

Alisema kuwa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi wamekuwa wakitoa elimu hiyo na wataendelea kutoa elimu mara kwa mara lengo la wananchi wawe na uelewa wa utunzaji wa mazingira.

 

Monday 1 February 2021

SERIKALI YAPELEKA KIVUKO CHA BILIONI 5.3 MAFIA NYAMISATI

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akikata utepe kuashiria kukipokea rasmi kivuko kipya cha MV. KILINDONI HAPA KAZI TU ambacho amekipokea leo kutoka kwa makandarsi Songoro Marine Transport Boatyard katika hafla fupi iliyofanyika katika kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani. Kivuko hicho kimegharimu shilingi bilioni 5.3 na kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100 na kitakuwa kinatoa huduma kati ya Mafia na Nyamisati.

Kivuko cha MV. KILINDONI HAPA KAZI TU kikielea majini mara baada ya kupokelewa rasmi leo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katika hafla fupi iliyofanyika katika kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani. Kivuko hicho kimegharimu shilingi bilioni 5.3 na kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100 na kitakuwa kinatoa huduma kati ya Mafia na Nyamisati.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akisisitiza jambo wakati wa mapokezi ya kivuko cha MV. KILINDONI HAPA KAZI TU, hafla iliyofanyika katika kisiwa cha Mafia Mkoani Pwani. Kivuko hicho kimegharimu shilingi bilioni 5.3 na kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100 na kitakuwa kinatoa huduma kati ya Mafia na Nyamisati.


Na Mwandishi wetu....


Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), leo imerejesha furaha na matumaini kwa wakazi wa Mkoa wa Pwani wanaoishi kisiwa cha Mafia na eneo la Nyamisati baada ya kutekeleza mojawapo ya ahadi zake iliyowekwa katika ilani ya uchaguzi ya chama tawala ya mwaka 2015-2020 kwa kuwapelekea kivuko kipya cha MV. KILINDONI HAPA KAZI TU. Kwa muda mrefu wakazi wa maeneo hayo hawakuwa na usafiri wa uhakika na hiyo iliwalazimu kutumia boti ndogo na majahazi kwa ajili ya kusafirishia mizigo na abiria na hivyo kuhatarisha maisha yao baharini endapo ingetokea dharura ya ajali.


Kivuko hicho kipya kilichogharimu shilingi Bilioni 5.3 mpaka kukamilika kwake na ambacho ujenzi wake umegharamiwa na Serikali kwa kutumia fedha za ndani, kimejengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Boatyard ya jijini Mwanza katika karakana yake ya kujengea na kukarabati vivuko iliyopo Kigamboni jijini Dar es salaam na kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 ambazo ni sawa na tani 100.


Akizungumza katika hafla fupi ya kupokea kivuko hicho iliyofanyika katika kisiwa cha Mafia na kuhudhuriwa na viongozi kadha wa kadha wa mkoa huo, mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuweza kutoa fedha zote hizo kwa ajli ya kuhudumia wananchi wake na pia aliupongeza Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa kuweza kusimamia ujenzi wa Kivuko hicho hadi kukamilika kwake.


‘’Kama mlivyosikia katika hotuba zilizotangulia Wakala umekamilisha miradi ya ujenzi wa vivuko vipya vya Kayenze – Bezi, Bugolora - Ukara na Chato – Nkome na kufanya vivuko vipya vilivyonunuliwa katika mwaka wa fedha 2019/20 kuwa vinne kikiwepo hiki cha Kilindoni tunachokipokea leo kwa pamoja vikiwa vimegharimu jumla ya Shilingi bilioni 15.3. Haya yote ni matunda ya kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Jemedari wetu Mheshimiwa Dr. John Joseph Pombe Magufuli, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.’’

Alisema Mheshimiwa Ndikilo ambapo aliongeza kuwa  kwa kuwa Kivuko hicho ni rasilimali muhimu ya Taifa na kinahitajiwa na wananchi wa Mafia na Nyamisati, aliuagiza Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kusimamia kwa karibu uendeshaji wake ili wananchi wafaidi matunda mazuri ya Serikali yao kwa fursa ya maendeleo yao binafsi na nchi nzima kwa ujumla wake na pia aliwasisitizia wananchi wa Mafia na Nyamisati kukitunza kivuko hicho na kuwapa ushirikiano wa kutosha wahudumu wake kiweze kuwahudumia kwa kipindi kirefu. 


Naye mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga, Mhandisi Elizabeth Manzi akizungumza katika hafla hiyo, amesema ni dhamira ya Serikali kutaka kutoa huduma iliyo bora yenye kukuza uchumi wa nchi ya Tanzania na Katika mwaka wa fedha 2019/20, Serikali ilitoa jumla ya Billioni 12,245,214,800.00 kwa ajili ya miradi ya vivuko na maegesho ambayo inatekelezwa na Wakala wa Ufundi na Umeme na Fedha hizo zinatokana na Mfuko Mkuu wa Serikali na Mfuko wa Barabara. 

Awali, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle, akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa kivuko hicho alisema, kazi ya ujenzi huo imefanywa kulingana na viwango vinavyokubalika Kimataifa (IMO Standards). 

‘’Kivuko hiki kimefanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ambao walikuwa wakishiriki ukaguzi wakati wa ujenzi ili kuthibitisha viwango vya usalama wa abiria, magari na mizigo.’’ Alisema Mhandisi Maselle ambapo aliongeza kuwa  baada ya ukaguzi wa mwisho TASAC wamefanya usajili wa kivuko hiki kabla hakijaanza kazi kwa jina la MV KILINDONI – HAPA KAZI TU.

‘’Ili kuhakikisha usalama wa kivuko hiki kinapofanya kazi kimefungwa vifaa stahiki vya kuongozea kama vile Radar, GPS, Echo Sounder, vifaa vya mawasiliano (Communication equipment) na vifaa vya uokoaji vya kutosha kwa watu wazima na watoto ambavyo ni makoti ya kujiokoa (life jackets) na maboya (life rafts na life buoys).’’ Alimaliza Mtendaji Mkuu ambapo alishukuru Serikali kwa kuendelea kuuamini Wakala katika kutekeleza miradi hiyo na pia kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya vivuko kwa lengo la kuboresha huduma za usafirishaji katika maeneo mbalimbali nchini na kuahidi kukitunza kivuko hicho kwa kukifanyia matengenezo kama inavyotakiwa ili kiweze kudumu na kutoa huduma bora kwa wananchi kwa wakati wote.

Kukamilika kwa ujenzi wa kivuko cha MV. KILINDONI HAPA KAZI TU kunafanya idadi ya vivuko kote nchini kufikia 33 hadi hivi sasa na hivyo kuifanya serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya usafiri kwa manufaa ya wananchi wengi. 

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube